Waasisi wa CHADEMA ambao hadi leo wapo kwenye chama ni akina nani? Je, ni kweli ni chama kikuu cha upinzani?

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,866
5,742
Nawakumbuka Wachache tu ambao ni Waasisi wa Chama cha Demokrasia na Maensdeleo (CHADEMA)
Wazee namkumbuka Mtei pekee. Wengine wote Wakiongozwa na Prof. Baregu hana sifa hata moja ya kuitwa CHADEMA asili, hawa ni watu wamekwenda tu huko kwa shida shida tu. Labda wengine ambao sasa nao wanaweza kuitwa wazee ambao tunaweza kuwapa sifa ya waasisi wa CHADEMA ni Mbowe mwenyewe na Tundu Lissu.
Vijana waasisi wa CHADEMA ni pamoja na Zitto Kabwe (Hayumo), John Mnyika(bado yumo) , Halima Mdee (bado yumo). Wengine ni akina nani?
Hii Orodha hii (Wazee kwa Vjana) ilikipaisha sana chama hiki lakini kamwe hawakuwa , hawana na hawatakuwa wawe na sifa za kuitwa waasisi wa CHADEMA. Wamehangaika sana huku na kule mwisho wake wakajikuta wanatua CHADEMA . wengine wameendelea kuwemo huku wakibebwa na sifa kadha wa kadha. Wengine wanusa na kuondoka tena wakishika pua huku maneno yakiwatoka kuwa huko hakufai jambo ambalo wajuzi wa masuala ya siasa wanaaamini wanachokisema ni cha kweli maana sababu zao hazitofautiani hata kidogo (Hili ni doa kubwa sana kwa Chama kinachotaka. kushika dola). Hata wale waliomo bado wamo kama hawamo (wamo jina tu), Chama kimebaki kuwa chake mwenyewe, chao wenyewe , chetu wenyewe (Nadhani mnawafahamu hawa ninaowasema)
1. Waled Kaburu​
2. Dr. Wilbrod Slaa​
3. Prof. Baregu​
4. Wakili Mabere Nyaucho Marando​
5. Edward Lowassa​
6. Fredrick Tluwaye Sumaye​
7. Juma Duni​
8. Lawrence Masha​
9. Samson Mwigamba​
10. Prof. Kitilla Mkumbo​

kwa kifupi, CHADEMA hakijawahi kuwa maarufu kwa kutumia waasisi wake hata siku moja.
Maswali ya kujiuliza ni
a) Matunda ya CHADEMA kupata umaarufu kwa kutumia wakuja ni kupanda kwa ruzuku ambayo hata hivyo nayo inalalamikiwa kutumbuliwa naye , na wao, na sisi au kitakuja kushika madaraka kwa kubahatisha bahatisha watu maarufu kiasi hiki?
b) kwanini wanaoondoka CHADEMA ni wale wale na wanaobakia ni wale wale (mnanielewa lakini?
c) Hivi tuko serious kabisa na kwa ujasiri tunatamka kuwa CHADEMA ni chama kikuu cha Upinzani? (Binafsi vyama vya upinzani naona kama ni CUF, NCCR-Mageuzi ambavyo naona kama vimekuwa na waaisisi wake muda mwingi angala0)

d) wanaofaidi umaarufu wa kushtukiza wa CHADEMA ni wachache au ni wanachama wote na baadaye Watanzania wote watafaidi?
e) Tukisema leo Ruzuku kwa vyama zimefutwa na Mungu akajalia CHADEMA kikapata wafuasi wengi hata wa kukiwezesha kuunda SerikaLI yeye, Wao na sisi wachache tuko tayari kuiishi hali hiyo ya Ukata wa pesa lakini utajiti wa wafuasi (Tutakuwa Confortable na kufurahia kuwa sisi ni Chama kikuu cha Upinzani?)

Binafsi naona kama kuna Maigizo makubwa sana huku.

Nini Maoni yako? tufanye nini? au ndo tuendelee na kale kawimbo ketu kwamba CHAMA KINAMHITAJI KIPINDI HIKI KULIKO KIPINDI CHOCHOTE KILE?
 
hivi mzee Victor Kimesera na yule mzee aliyekimbilia Chadema baada ya kukosa nafasi ya kugombea jimbo la ubunge la ubunge kushindwa sijui wako wapi ni mzee kutoka kigoma na aliwahi kuwa waziri nimemsahau jina lake si unajua ukienda Chadema unasahaulika katika ulingo wa kisiasa
 
Yaani maelezo yako yote yamebeba ujumbe wa kutaka mbowe ang'atuke, sijui akitoka wewe utafaidika na nini!?
 
Nyie ndio maana hamteuliwi, badala yake wanateuliwa watu kutoka upinzani, kwasababu hamna kitu kichwani, na Mwenyekiti wenu anawadharau. Ameshawaona hamna kitu kichwani.
 
Nawakumbuka Wachache tu ambao ni Waasisi wa Chama cha Demokrasia na Maensdeleo (CHADEMA)
Wazee namkumbuka Mtei pekee. Wengine wote Wakiongozwa na Prof. Baregu hana sifa hata moja ya kuitwa CHADEMA asili, hawa ni watu wamekwenda tu huko kwa shida shida tu. Labda wengine ambao sasa nao wanaweza kuitwa wazee ambao tunaweza kuwapa sifa ya waasisi wa CHADEMA ni Mbowe mwenyewe na Tundu Lissu.
Vijana waasisi wa CHADEMA ni pamoja na Zitto Kabwe (Hayumo), John Mnyika(bado yumo) , Halima Mdee (bado yumo). Wengine ni akina nani?
Hii Orodha hii (Wazee kwa Vjana) ilikipaisha sana chama hiki lakini kamwe hawakuwa , hawana na hawatakuwa wawe na sifa za kuitwa waasisi wa CHADEMA. Wamehangaika sana huku na kule mwisho wake wakajikuta wanatua CHADEMA . wengine wameendelea kuwemo huku wakibebwa na sifa kadha wa kadha. Wengine wanusa na kuondoka tena wakishika pua huku maneno yakiwatoka kuwa huko hakufai jambo ambalo wajuzi wa masuala ya siasa wanaaamini wanachokisema ni cha kweli maana sababu zao hazitofautiani hata kidogo (Hili ni doa kubwa sana kwa Chama kinachotaka. kushika dola). Hata wale waliomo bado wamo kama hawamo (wamo jina tu), Chama kimebaki kuwa chake mwenyewe, chao wenyewe , chetu wenyewe (Nadhani mnawafahamu hawa ninaowasema)
1. Waled Kaburu​
2. Dr. Wilbrod Slaa​
3. Prof. Baregu​
4. Wakili Mabere Nyaucho Marando​
5. Edward Lowassa​
6. Fredrick Tluwaye Sumaye​
7. Juma Duni​
8. Lawrence Masha​
9. Samson Mwigamba​
10. Prof. Kitilla Mkumbo​

kwa kifupi, CHADEMA hakijawahi kuwa maarufu kwa kutumia waasisi wake hata siku moja.
Maswali ya kujiuliza ni
a) Matunda ya CHADEMA kupata umaarufu kwa kutumia wakuja ni kupanda kwa ruzuku ambayo hata hivyo nayo inalalamikiwa kutumbuliwa naye , na wao, na sisi au kitakuja kushika madaraka kwa kubahatisha bahatisha watu maarufu kiasi hiki?
b) kwanini wanaoondoka CHADEMA ni wale wale na wanaobakia ni wale wale (mnanielewa lakini?
c) Hivi tuko serious kabisa na kwa ujasiri tunatamka kuwa CHADEMA ni chama kikuu cha Upinzani? (Binafsi vyama vya upinzani naona kama ni CUF, NCCR-Mageuzi ambavyo naona kama vimekuwa na waaisisi wake muda mwingi angala0)

d) wanaofaidi umaarufu wa kushtukiza wa CHADEMA ni wachache au ni wanachama wote na baadaye Watanzania wote watafaidi?
e) Tukisema leo Ruzuku kwa vyama zimefutwa na Mungu akajalia CHADEMA kikapata wafuasi wengi hata wa kukiwezesha kuunda SerikaLI yeye, Wao na sisi wachache tuko tayari kuiishi hali hiyo ya Ukata wa pesa lakini utajiti wa wafuasi (Tutakuwa Confortable na kufurahia kuwa sisi ni Chama kikuu cha Upinzani?)

Binafsi naona kama kuna Maigizo makubwa sana huku.

Nini Maoni yako? tufanye nini? au ndo tuendelee na kale kawimbo ketu kwamba CHAMA KINAMHITAJI KIPINDI HIKI KULIKO KIPINDI CHOCHOTE KILE?
Sababu za kuondoka kwao haziwezi zikatofautiana kwa sababu ni wimbo waliofundishwa na kukaririshwa katika ofisi za Lumumba.
 
Inashangaza sana wasio na chama (CCM) wanalalamika zaidi ya wenye chama (CDM), ujinga ujinga tu.
 
Back
Top Bottom