Ushauri kwa CHADEMA: Tumeshindwa uchaguzi, Mbowe beba mzigo

G4N

JF-Expert Member
Apr 6, 2014
1,429
3,532
Ni wazi kwamba CHADEMA ilianzishwa ili kuwa tofauti na CCM na vyama vingine. Tofauti hii lazima iwe dhahiri na ya kivitendo. CHADEMA iendeshwe kama vyama vya wenzetu kule Ulaya. Chama kikifanya vibaya ktk chaguzi kiongozi anawajibika. Uwajibikaji wa jumla " collective accountability".

Baada ya uchaguzi na michakato yake yote kukamilika chadema imepata nafasi ya pili, huku ikipata wabunge na madiwani kiduchu sana ukilinganisha na harakati, matarajio na nguvu iliyotumika.

Sasa nilitarajia na bado ninatarajia kuona vikao vya tathmini vikikaa na kufanya upembuzi wa kina kubaini sababu ya kushindwa kwenda ikulu na kuambulia wabunge na madiwani kidogo kiasi hiki.

Ni dhahiri kuwa kuna uzembe wa kupanga mikakati ya kupata ushindi mnono uliofanywa na viongozi wa ngazi zote. Hapa ndipo Kamanda Mbowe anabeba gunia la lawama kama kiongozi wa juu wa chama.

Alikuja na mbinu ya kubadili gia angani sawa Lakini je, mbinu hii ya kubadili gia angani imeleta athari gani chanya na hasi kwenye chama? Ukiziweka kwenye mizania athari hizi chanya na hasi, zipi zina uzito kuliko nyingine? Chama bado kina kasi ya kupendwa ama sasa kimefifishwa na mbinu ya kubadili gia angani?

Watu wengi huko mitaani wanaona CHADEMA ina wenyewe, na wenyewe ni akina Mbowe waliokaa Kitako wakamkaribisha Lowassa kisha mkutano mkuu ukaitishwa kama bosheni tu kuja "kuthibitisha" kilichoamriwa na "wakubwa".

Hii imepunguza ari ya kuibeba CHADEMA moyoni kama mwanzo. Maana wameona mpambanaji mwenzao Dr. Slaa aliyeumia ktk harakati za kukijenga chama na mkewe aliyevuja damu walivyopuuzwa na kutoswa kwa udhalili. Hii INA madhara makubwa kwa chama.

Sasa kamanda Mbowe jiuzuru ili aje mwingine na timu yake wafanye mikakati mipya ya kurudisha misingi ya chadema. Ikibidi hata kwa kuwafukuza waliokuja kufifisha nuru ya chama.

Aingie mtumbua majipu ndani ya chadema asafishe na kujenga matumaini mapya kwa wanachama. Vinginevyo chama kimekwama kwenye tope.
 
Hiv chadema si ingeongoza nchi kama tunge kuwa na tumehuru ya uchaguz.
 
Hivi unajua namba ??

Kwa mujibu wa namba chadema imekua chini ya mbowe.

Ila kwa mujibu wa ujinga wako chadema imekufa chini ya mbowe.
 
Ni kawaida duniani vyama vingi vikishindwa kwenye uchaguzi viongozi wa juu hujiuzulu kupisha timu ingine.Kwa CHADEMA nina uhakika Mbowe angejiuzulu tena chap chap kama chama kushindwa kwake kungekikosesha ruzuku.Lakini as long as ruzuku bado ipo Mbowe hatoki.Ombeni serikali ifute ruzuku mfano leo hii tamko likitolewa tu la kufuta ruzuku Mbowe dakika hiyo hiyo ataitisha press conference kujiuzuru na kusema kaongoza muda mrefu anahitaji kupisha wengine yeye abaki kama mshauri tu.
 
Hiv chadema si ingeongoza nchi kama tunge kuwa na tumehuru ya uchaguz.

Haya malalamiko ya tume huru yapo miaka yote. Na ktk uchaguzi uliomalizika tuliaminishwa na wanachama wakahamasika kuwa haitaibiwa kura hata moja. Isije ikawa tume huru ni uchochoro wa kuficha udhaifu wa chama ktk chaguzi. Tuambiwe tena kwa ushahidi ni vipi kura ziliibiwa?
 
Haya malalamiko ya time huru yapo miaka yote. Na ktk uchaguzi uliomalizika tuliaminishwa na wanachama wakahamasika kuwa haitaibiwa kura hats moja. Isije ikawa time huru ni uchochoro wa kuficha udhaifu wa chama ktk chaguzi. Tuambiwe tena kwa ushahidi ni vipi tuliibiwa?

Hiv tume ambayo inagemea chama kimojs kama hii ya lubuva inayopokea maelekezo toka ccm ,matokeo yenyewe hayahojiwi mahakaman...
 
Mkuu huku kulialia bila ya kutafutakutafuta ufumbuzi kutakatisha watu tamaa na kuwafanya wajiondoe kwenye vyama vya upinzani. Kuna haja gani ya kusimamisha mgombea ili hali tunajua atashindwa?
Nini kifanyike?
 
CCM wapinzani wakisusa ndo kabisa wataendelea kutawala hata hao wabunge wachache wa upinzani hawatakuwepo.....
 
hoja dhaifu sana,na wewe ulikuwa na ndoto ya kuwa tajiri japo hujafanikiwa kufika hata robo yake unaonaje familia ikakuwajibisha?
 
Mkuu hapa unakaribisha usultani. Ukishakuwa baba hutaweza tena kuwa mtoto. Ni tofauti sana na vyeo vya kisiasa. Mbowe ajiuzuru kwa kushindwa kufikia malengo ya chama na wanachama. Aje mtu mpya mwenye mawazo mapya kusukuma gurudumu ktk staili mpya
 
Adui wa Chadema kwa sasa sio CCM tena, ni chama chochote kinachokua na kuonyesha kuwa mbadala wa Chadema ya miaka ya nyuma.
 
Ni wazi kwamba CHADEMA ilianzishwa ili kuwa tofauti na CCM na vyama vingine. Tofauti hii lazima iwe dhahiri na ya kivitendo. CHADEMA iendeshwe kama vyama vya wenzetu kule Ulaya. Chama kikifanya vibaya ktk chaguzi kiongozi anawajibika. Uwajibikaji wa jumla " collective accountability".

Baada ya uchaguzi na michakato yake yote kukamilika chadema imepata nafasi ya pili, huku ikipata wabunge na madiwani kiduchu sana ukilinganisha na harakati, matarajio na nguvu iliyotumika.

Sasa nilitarajia na bado ninatarajia kuona vikao vya tathmini vikikaa na kufanya upembuzi wa kina kubaini sababu ya kushindwa kwenda ikulu na kuambulia wabunge na madiwani kidogo kiasi hiki.

Ni dhahiri kuwa kuna uzembe wa kupanga mikakati ya kupata ushindi mnono uliofanywa na viongozi wa ngazi zote. Hapa ndipo Kamanda Mbowe anabeba gunia la lawama kama kiongozi wa juu wa chama.

Alikuja na mbinu ya kubadili gia angani sawa Lakini je, mbinu hii ya kubadili gia angani imeleta athari gani chanya na hasi kwenye chama? Ukiziweka kwenye mizania athari hizi chanya na hasi, zipi zina uzito kuliko nyingine? Chama bado kina kasi ya kupendwa ama sasa kimefifishwa na mbinu ya kubadili gia angani?

Watu wengi huko mitaani wanaona CHADEMA ina wenyewe, na wenyewe ni akina Mbowe waliokaa Kitako wakamkaribisha Lowassa kisha mkutano mkuu ukaitishwa kama bosheni tu kuja "kuthibitisha" kilichoamriwa na "wakubwa".

Hii imepunguza ari ya kuibeba CHADEMA moyoni kama mwanzo. Maana wameona mpambanaji mwenzao Dr. Slaa aliyeumia ktk harakati za kukijenga chama na mkewe aliyevuja damu walivyopuuzwa na kutoswa kwa udhalili. Hii INA madhara makubwa kwa chama.

Sasa kamanda Mbowe jiuzuru ili aje mwingine na timu yake wafanye mikakati mipya ya kurudisha misingi ya chadema. Ikibidi hata kwa kuwafukuza waliokuja kufifisha nuru ya chama.

Aingie mtumbua majipu ndani ya chadema asafishe na kujenga matumaini mapya kwa wanachama. Vinginevyo chama kimekwama kwenye tope.

"If you'd kept your mouth shut, we would have thought you were clever."

Similar Discussions

Back
Top Bottom