Nataka kuigeuza Tsh. 2,000 itengeneze zaidi ya Tsh. Million 1 kila mwezi

stevhinoz

JF-Expert Member
Jun 15, 2021
228
488
Nimewaza kutafuta biashara nitayopata faida sh 2000 kwa kila item. Nimepiga hesabu nitatengeneza million na zaidi kwa mwezi.

Hesabu ipo hivi, niweze kuuza bidhaa 500 ndani ya mwezi, nipate shilingi 2,000 faida kwa kila bidhaa. Kwa siku niuze bidhaa 20 na kila bidhaa niuze kwa faida ya Tsh 2000.

Location maeneo yaliyochangamka haswa kwenye junctions kama Mbagala, Mbezi Kimara, Tegeta, Gongolamboto.

Goli liwe kati ya laki 2 hadi laki 2.5. Sasa hapa naumiza kichwa ni bidhaaa ipi naweza zungusha ikakubaliana na hesabu zangu.

Naomba tupeane mawazo wadau ni bidhaa ipi yoyote naweza iuza inayozunguka fasta na ina faida ya buku 2 kwa kila item.
 
Nimekaa siti ya mbele kwenye uzi huu, màana usiku silali nawaza nn cha kufanya.

Ila ushauri wangu, faida ya elfu 2 uuze bidhaa 20 hiyo faida ni kubwa kwann tusitafute faida ya jero alafu tuangalie mzunguko ndio uwe mkubwa wa kuleta total ya 40000 km mwanzo
 
Wewe ukiwa unawaza ushawai kuwaza kuuza kitu gani?

Faida ya jero mkuu unaweza kata tamaa kabisa na biashara maana utakuwa unalaza laki 3 kwa mwezi ambayo hauwezi hata kulipia ubao.

Ushawai waza lolote kuhusu vipodozi na urembo?
Viatu fake za kina mama?

Vitafunwa?

Ebu tuendelee kuchakata inawezekana tukaapta idea
 
Mkuu ulishwahi kufikiria biashara ya kuuza mashati ya mtumba ila wewe unaongeza quality ktk sehemu ya kuuzia tofauti na wamachinga wengi ,it means unakuwa na frame nzuri na ya kuvutia pamoja na mpangilio mzuri wa kuweka item zako

Mzigo wako wa mashati ya mtumba unachukulia kariakoo na tandika kwa kusample shati moja moja kutoka katika minada inayofanyika maeneo hayo na sio kuchukua Belo zima na lengo ni kupata mzigo wenye quality nzuri

Pia unaweza kuagiza Belo za mashati ya mtumba kutoka Uganda,kule ndo kunatoka mizigo yenye quality nzuri tena kwa bei nzuri na affordable

Mashati utayapata kwa bei ya Tsh.2000/= na ikizidi sana Tsh.3000/=..………na wewe unakuja kuuza Tsh.5000/= na utakuwa umepata faida yako ya Tsh.2000/=kwa kila item yako

Maeneo yenye mkusanyiko mkubwa wa watu uliyoyasema hapo juu hasa Mbagala,Kimara,Mwenge na maeneo yanayofanana na hayo unaweza kureach target yako ya kuuza item 20 kila siku

Changamoto kwenye kila biashara zipo sana hasa unapoanza biashara mpya chamsingi ni kuyavumilia mawimbi yake wakati biashara yako ikiendelea kuwa stable hadi kuja kusimama kwenye malengo yako

Naleta wazo lingine la biashara kutokana na faida unayohitaji kwa kila item
 
Jaribu pia kufikiria biashara ya Biashara ya kuuza Mkaa

Ukipata eneo zuri ukaweka banda lako la mkaa,kwa target yako ya kupata faida ya Tsh.40,000/= kwa siku,kupitia biashara hii pesa hiyo inapatikana

Biashara ambayo uhitaji wake ni mkubwa sana hasa kwa watu wengi wenye maisha ya kati na ni hitaji la lazima

Mkaa huo utakuwa unauza kwa gunia zima,Debe,pamoja na kipimo cha chini kabisa cha Tsh.1000=

Ni biashara ambayo watu wengi wanaidharau sana,ila ni moja kati mambo ambayo watu wanayoifanya hupata faida kubwa zaidi,ukipata eneo zuri faida yake ni zaidi ya milioni moja kwa mwezi

Pia ukizingatia kwasasa bei ya Mkaa imechangamka sana huku mtaani
 
Mkuu ulishwahi kufikiria biashara ya kuuza mashati ya mtumba ila wewe unaongeza quality ktk sehemu ya kuuzia tofauti na wamachinga wengi ,it means unakuwa na frame nzuri na ya kuvutia pamoja na mpangilio mzuri wa kuweka item zako

Mzigo wako wa mashati ya mtumba unachukulia kariakoo na tandika kwa kusample shati moja moja kutoka katika minada inayofanyika maeneo hayo na sio kuchukua Belo zima na lengo ni kupata mzigo wenye quality nzuri

Pia unaweza kuagiza Belo za mashati ya mtumba kutoka Uganda,kule ndo kunatoka mizigo yenye quality nzuri tena kwa bei nzuri na affordable

Mashati utayapata kwa bei ya Tsh.2000/= na ikizidi sana Tsh.3000/=..………na wewe unakuja kuuza Tsh.5000/= na utakuwa umepata faida yako ya Tsh.2000/=kwa kila item yako

Maeneo yenye mkusanyiko mkubwa wa watu uliyoyasema hapo juu hasa Mbagala,Kimara,Mwenge na maeneo yanayofanana na hayo unaweza kureach target yako ya kuuza item 20 kila siku

Changamoto kwenye kila biashara zipo sana hasa unapoanza biashara mpya chamsingi ni kuyavumilia mawimbi yake wakati biashara yako ikiendelea kuwa stable hadi kuja kusimama kwenye malengo yako

Naleta wazo lingine la biashara kutokana na faida unayohitaji kwa kila item
Shati zuri la mtumba grade A ni 5000 na yeye anauza 7000 haya atauza kwa haraka kuliko shati la buku tatu

Ila pia angewaza sandle sijui kwa nn hii biashara nimekuja kuijua baada ya mtaji wangu kukata dah
 
Nimewaza kutafuta biashara nitayopata faida sh 2000 kwa kila item.

Nimepiga hesabu nitatengeneza million na zaidi kwa mwezi.

Hesabu ipo hivi, niweze kuuza bidhaa 500 ndani ya mwezi, nipate shilingi 2,000 faida kwa kila bidhaa.

Kwa siku niuze bidhaa 20 na kila bidhaa niuze kwa faida ya Tsh 2000.

Location maeneo yaliyochangamka haswa kwenye junctions kama Mbagala, Mbezi Kimara, Tegeta, Gongolamboto.

Goli liwe kati ya laki 2 hadi laki 2.5

Sasa hapa naumiza kichwa ni bidhaaa ipi naweza zungusha ikakubaliana na hesabu zangu.

Naomba tupeane mawazo wadau ni bidhaa ipi yoyote naweza iuza inayozunguka fasta na ina faida ya buku 2 kwa kila item.
Kuingiza million 1 kwa mwezi sio habari kubwa, habari kubwa nikuaitahitaji capital ya maana Sana hadi kugenerate kias hicho chafaida.
Maybe watu wawili/ watatu washare rent nawagawane muda wakukaa dukani, kila mtu awe nabidhaa yake moja ilazote zitakaa dukani at the same time

Mfano mmoja biashara ya huduma zauwakala, wapili hayo mashati yamitumba watatu trey zamayai.
 
Mimi ntamuuzia mayai ya kienyeji
IMG_20220603_192901.jpg
IMG-20220610-WA0006.jpg
 
Biashara mazee, daah halafu bado hicho chamtoto mi nahitaji uwekezaji wa faida hiyo hiyo kwa mwezi.
 
Kuingiza million 1 kwa mwezi sio habari kubwa, habari kubwa nikuaitahitaji capital ya maana Sana hadi kugenerate kias hicho chafaida.
Maybe watu wawili/ watatu washare rent nawagawane muda wakukaa dukani, kila mtu awe nabidhaa yake moja ilazote zitakaa dukani at the same time

Mfano mmoja biashara ya huduma zauwakala, wapili hayo mashati yamitumba watatu trey zamayai.
Duka moja lina uza mayai, pembeni kuna mashati alafu kuna mpesa nawaza tu linavyooneka 😅😅😅
 
Back
Top Bottom