CHADEMA inapokea Ruzuku ya Tsh. Millioni 107 kwa mwezi sawa na Tsh. Billion 1 na Millioni 284 Kwa mwaka!

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
18,081
12,235
Ndugu zangu Watanzania,

Chama kikuu cha upinzani hapa Nchini CHADEMA kinapokea Ruzuku kutoka serikalini ya takribani Millioni 107 kwa Mwezi ambayo ni sawa na Billion 1 na Millioni 284 kwa mwaka. Yaani:

107,000,000 x 12= 1,284,000,000/=.

Ambapo hata hivyo CHADEMA inasema kiasi hicho ni kidogo sana ukilinganisha na mahitaji na matumizi ya chama. Hiyo ni kwa mujibu wa John Mrema ambaye anasema pesa hiyo haitoshi na haiwatoshi.

Anasema ni ndogo kwa sababu chama kina ofisi ya makao makuu Dar es salaam, makao makuu ndogo Zanzibar pamoja na ofisi 10 za kanda ambazo zina waajiriwa rasmi wanaolipwa mishahara.

Swali linalokuja kwangu na ambalo ningependa kuwauliza CHADEMA ni kuwa kama Million 107 kwa mwezi ni ndogo. Je, CHADEMA walitaka walipwe shilingi ngapi ambazo ndio wataona ni nyingi? Mbona wakati wanapokea nyingi hususani 2015-2020 walipokuwa na wabunge wengi napo hawakuwahi kusema kuwa wanapokea nyingi na badala yake tuliona ofisi za chama huku mikoani zikiwa zimechoka sana na hali mbaya sana.

Hali ambayo ilionyesha na kutoa ishara ya kuwa ofisi hizi zilikuwa hazipati pesa au pesa zilikuwa hazifiki katika ofisi hizi. Lakini ikumbukwe kuwa pamoja na kupokea kwake Ruzuku kubwa bado wabunge wake nao walikuwa wakikatwa pesa kila Mwezi kuchangia chama. na ajabu zaidi ikifika wakati wa uchaguzi wagombea wake wa ubunge wamekuwa wakikabiliwa na ukata mkubwa sana wa kifedha na kupelekea kusuasua kwa kampeni.

Lakini pia kama CHADEMA inaona pesa hizo ni ndogo jambo ambalo linaweza kuwa kweli katika kujiendesha kitaasisi. Je, imefanya mikakati gani na mipango gani kuwekeza katika miradi ya chama itakayokiingizia na kukiongezea chama kipato? Miradi ya chama ipo wapi? Kwanini chama hakina miradi wakati kimepokea pesa nyingi sana kwa miaka kadhaa iliyopita?

Ikumbukwe ya kuwa pamoja na kupokea pesa kwa wingi lakini chama hakina hata tu kituo cha Tv au hata redio .yaani CHADEMA nzima inazidiwa maarifa na uthubutu na wasanii kama Diamond aliye na kituo cha Tv pamoja na Redio. Inazidiwa hadi na Millard Ayo.

Unaweza kuona udogo wa mawazo kiliyo nayo chama hiki. Maana jambo kubwa linaanza kujengwa katika fikira kwanza yaani kichwani. Lakini chama hiki cha CHADEMA hakina fikira kubwa kichwani mwake za kujiongezea kipato kupitia miradi na vitega uchumi vyake na badala yake kinategemea kikinge mikono kutoka kwa serikali hii hii ya Jemedari wetu shupavu na imara Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan.

Ili sasa wakalipane mishahara na posho nene nene halafu wanarudi wanasema pesa ni kidogo na wakati mwingine wanaitukana na serikali inayowapa shibe na jeuri. CHADEMA hata wapewe kuongoza nchi kwa wiki moja kazi wanayoweza kuifanya ni kukomba na kukausha pesa zote hazina kama nyasi zilizopigwa dawa ya glamakisoni.

CHADEMA ni chama kisicho na ubunifu wala mikakati wala mbinu, wala njia ya kukiongezea na kutunisha mfuko wa pesa. Na lazima ifahamike ya kuwa siasa inahitaji uchumi ,chama kinahitaji kiwe na misuli ya kiuchumi na kifedha kwasababu huwezi kueneza chama kama huna pesa.

Kama huna pesa utashindwa hata kulipia ofisi wilayani na kwenye kata huko, kama ambavyo tumeshuhudia CHADEMA ikikosa ofisi ngazi hizo na pale ambapo zipo unakuta zimefungwa na kubaki maandishi nje tu, kwa sababu ya kukosa kodi ya nyumba ambayo unakuta ni ndogo tu lakini chama kimeshindwa kulipia, mpaka wenye nyumba wanaamua kuweka makufuri juu ya makufuri.

Naweka kalamu yangu chini.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Uchaguzi haramu wa mwendakuzimu 2020 ccm walikwapua mabilioni ya walimu kupitia cwt mwekahazina wa cwt alikuwa mohamed utali baada ya kufanikisha ule wizi wa hela za cwt akapewa asante ya kuwa mkuu wa wilaya ya mvomero kilipo kiwanda cha mtibwa kilicholipuka jana ambacho pia ni kiwanda cha ccm kupitia familia ya mkapa.
 
Mnapokea mamillioni ya Ruzuku halafu bado haieleweki hata mnafanyia nini zaidi ya kuzitafuna tu. Maana ofisi tu huku chini mnashindwa kulipa kodi mpaka zinafungwa.
 
Uchaguzi haramu wa mwendakuzimu 2020 ccm walikwapua mabilioni ya walimu kupitia cwt mwekahazina wa cwt alikuwa mohamed utali baada ya kufanikisha ule wizi wa hela za cwt akapewa asante ya kuwa mkuu wa wilaya ya mvomero kilipo kiwanda cha mtibwa kilicholipuka jana ambacho pia ni kiwanda cha ccm kupitia familia ya mkapa.
Weka ushahidi wa huo ukwapuaji wa pesa za cwt.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Chama kikuu cha upinzani hapa Nchini CHADEMA kinapokea Ruzuku kutoka serikalini ya takribani Millioni 107 kwa mwaka ambayo ni sawa na Billion 1 na Millioni 284 kwa mwaka. Yaani:

107,000,000 x 12= 1,284,000,000/=.

Ambapo hata hivyo CHADEMA inasema kiasi hicho ni kidogo sana ukilinganisha na mahitaji na matumizi ya chama. Hiyo ni kwa mujibu wa John Mrema ambaye anasema pesa hiyo haitoshi na haiwatoshi.

Anasema ni ndogo kwa sababu chama kina ofisi ya makao makuu Dar es salaam, makao makuu ndogo Zanzibar pamoja na ofisi 10 za kanda ambazo zina waajiriwa rasmi wanaolipwa mishahara.

swali linalokuja kwangu na ambalo ningependa kuwauliza CHADEMA ni kuwa kama Million 107 kwa mwezi ni ndogo ,je CHADEMA walitaka walipwe shilingi ngapi ambazo ndio wataona ni nyingi? Mbona wakati wanapokea nyingi hususani 2015-2020 walipokuwa na wabunge wengi napo hawakuwahi kusema kuwa wanapokea nyingi na badala yake tuliona ofisi za chama huku mikoani zikiwa zimechoka sana na hali mbaya sana.

Hali ambayo ilionyesha na kutoa ishara ya kuwa ofisi hizi zilikuwa hazipati pesa au pesa zilikuwa hazifiki katika ofisi hizi. Lakini ikumbukwe kuwa pamoja na kupokea kwake ruzukt kubwa bado wabunge wake nao walikuwa wakikatwa pesa kila Mwezi kuchagua chama .na ajabu zaidi ikifika wakati wa uchaguzi wagombea wake wa ubunge wamekuwa wakikabiliwa na ukata mkubwa sana wa kifedha na kupelekea kusuasua kwa kampeni.

lakini pia kama CHADEMA inaona pesa hizo ni ndogo jambo ambalonlinaweza kuwa kweli katika kujiendesha kitaasisi. Je imefanya mikakati gani na mipango gani kuwekeza katika miradi ya chama itakayokiingizia na kukiongezea chama kipato? Miradi ya chama ipo wapi? Kwanini chama hakina miradi wakati kimepokea pesa nyingi sana kwa miaka kadhaa iliyopita?

Ikumbukwe ya kuwa pamoja na kupokea pesa kwa wingi lakini chama hakina hata tu kituo cha Tv au hata redio yaani CHADEMA nzima inazidiwa maarifa na uthubutu na wasanii kama Diamond aliye na kituo cha Tv pamoja na Redio. Inazidiwa hadi na Millard Ayo.

Unaweza kuona udogo wa mawazo kiliyo nayo chama hiki. Maana jambo kubwa linaanza kujengwa katika fikira kwanza yaani kichwani. Lakini chama hiki cha CHADEMA hakina fikira kubwa kichwani mwake za kujiongezea kipato kupitia miradi na vitega uchumi vyake na badala yake vinategemea vikongwe mikono kutoka kwa serikali hii hii ya Jemedari wetu shupavu na imara Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan.

ili sasa wakalipane mishahara na posho nene nene halafu wanarudi wanasema pesa ni kidogo. CHADEMA hata wapewe kuongoza nchi kwa wiki moja kazi wanayoweza kuifanya ni kukomba na kukausha pesa zote hazina kama nyasi zilizopigwa dawa ya glamakisoni.

CHADEMA ni chama kisicho na ubunifu wala mikakati wala mbinu,wala njia ya kukiongezea na kutunisha mifuko wa pesa. Na lazima ifahamike ya kuwa siasa inahitaji uchumi chama kinahitaji kiwe na misuli ya kiuchumi na kifedha.kwasababu huwezi kueneza chama kama huna pesa.

Kama huna pesa utashindwa hata kulipia ofisi wilayani na kwenye kata huko ,kama ambavyo tumeshuhudia CHADEMA ikikosa ofisi ngazi hizo na pale ambapo zipo unakuta zimefungwa na kubaki maandishi nje tu ,kwa sababu ya kukosa kodi ya nyumba ambayo unakuta ni ndogo tu lakini chama kimeshindwa kulipia.moaka wenye nyumba wanaamua kuweka makufuri juu ya makufurri.

Naweka kalamu yangu chini.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
CCMinapokea Ruzuku kiasi Gani kwa mwezi?
Na fedha hizo zinatumika kufanya KAZI Gani na wapi?
Kwanini wengi ni wapigaji na ruzuku wanapokea?
 
Na tozo zetu siku hizi hatuambiwi zinaenda wapi kufanya nini.
Tozo zimefanya kazi kubwa sana katika maeneo mbalimbali.mfano ni kupitia tozo vilijengwa vituo vya afya 234 maeneo mbalimbali hapa nchini. Vipi embu niambie huwa mnafanyia na kupeleka wapi pesa za Ruzuku ninyi CHADEMA?
 
CCMinapokea Ruzuku kiasi Gani kwa mwezi?
Na fedha hizo zinatumika kufanya KAZI Gani na wapi?
Kwanini wengi ni wapigaji na ruzuku wanapokea?
Achana kabisa na CCM Chama kiongozi barani Afrika chenye maendeleo chungu nzima na miradi ya kila aina kwa kutumia pesa zake halali. CCM Ina shule kibao,vyombo vya habari,fremu au vibanda vya biashara,viwanja vya michezo n.k.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Chama kikuu cha upinzani hapa Nchini CHADEMA kinapokea Ruzuku kutoka serikalini ya takribani Millioni 107 kwa mwaka ambayo ni sawa na Billion 1 na Millioni 284 kwa mwaka. Yaani:

107,000,000 x 12= 1,284,000,000/=.

Ambapo hata hivyo CHADEMA inasema kiasi hicho ni kidogo sana ukilinganisha na mahitaji na matumizi ya chama. Hiyo ni kwa mujibu wa John Mrema ambaye anasema pesa hiyo haitoshi na haiwatoshi.

Anasema ni ndogo kwa sababu chama kina ofisi ya makao makuu Dar es salaam, makao makuu ndogo Zanzibar pamoja na ofisi 10 za kanda ambazo zina waajiriwa rasmi wanaolipwa mishahara.

swali linalokuja kwangu na ambalo ningependa kuwauliza CHADEMA ni kuwa kama Million 107 kwa mwezi ni ndogo ,je CHADEMA walitaka walipwe shilingi ngapi ambazo ndio wataona ni nyingi? Mbona wakati wanapokea nyingi hususani 2015-2020 walipokuwa na wabunge wengi napo hawakuwahi kusema kuwa wanapokea nyingi na badala yake tuliona ofisi za chama huku mikoani zikiwa zimechoka sana na hali mbaya sana.

Hali ambayo ilionyesha na kutoa ishara ya kuwa ofisi hizi zilikuwa hazipati pesa au pesa zilikuwa hazifiki katika ofisi hizi. Lakini ikumbukwe kuwa pamoja na kupokea kwake ruzukt kubwa bado wabunge wake nao walikuwa wakikatwa pesa kila Mwezi kuchagua chama .na ajabu zaidi ikifika wakati wa uchaguzi wagombea wake wa ubunge wamekuwa wakikabiliwa na ukata mkubwa sana wa kifedha na kupelekea kusuasua kwa kampeni.

lakini pia kama CHADEMA inaona pesa hizo ni ndogo jambo ambalonlinaweza kuwa kweli katika kujiendesha kitaasisi. Je imefanya mikakati gani na mipango gani kuwekeza katika miradi ya chama itakayokiingizia na kukiongezea chama kipato? Miradi ya chama ipo wapi? Kwanini chama hakina miradi wakati kimepokea pesa nyingi sana kwa miaka kadhaa iliyopita?

Ikumbukwe ya kuwa pamoja na kupokea pesa kwa wingi lakini chama hakina hata tu kituo cha Tv au hata redio yaani CHADEMA nzima inazidiwa maarifa na uthubutu na wasanii kama Diamond aliye na kituo cha Tv pamoja na Redio. Inazidiwa hadi na Millard Ayo.

Unaweza kuona udogo wa mawazo kiliyo nayo chama hiki. Maana jambo kubwa linaanza kujengwa katika fikira kwanza yaani kichwani. Lakini chama hiki cha CHADEMA hakina fikira kubwa kichwani mwake za kujiongezea kipato kupitia miradi na vitega uchumi vyake na badala yake vinategemea vikongwe mikono kutoka kwa serikali hii hii ya Jemedari wetu shupavu na imara Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan.

ili sasa wakalipane mishahara na posho nene nene halafu wanarudi wanasema pesa ni kidogo. CHADEMA hata wapewe kuongoza nchi kwa wiki moja kazi wanayoweza kuifanya ni kukomba na kukausha pesa zote hazina kama nyasi zilizopigwa dawa ya glamakisoni.

CHADEMA ni chama kisicho na ubunifu wala mikakati wala mbinu,wala njia ya kukiongezea na kutunisha mifuko wa pesa. Na lazima ifahamike ya kuwa siasa inahitaji uchumi chama kinahitaji kiwe na misuli ya kiuchumi na kifedha.kwasababu huwezi kueneza chama kama huna pesa.

Kama huna pesa utashindwa hata kulipia ofisi wilayani na kwenye kata huko ,kama ambavyo tumeshuhudia CHADEMA ikikosa ofisi ngazi hizo na pale ambapo zipo unakuta zimefungwa na kubaki maandishi nje tu ,kwa sababu ya kukosa kodi ya nyumba ambayo unakuta ni ndogo tu lakini chama kimeshindwa kulipia.moaka wenye nyumba wanaamua kuweka makufuri juu ya makufurri.

Naweka kalamu yangu chini.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
CCM wanapokea sh ngapi? Act wanapokea sh ngapi? Hebu niwekee data kwanza na kazi yake ni Nini kama siyo kulipana posho. Au unadhani hatuwaoni au hatuishi nao? Unapotoa hoja watu wachangie use your common sense.
 
Na vyama vingine vinapokea RUZUKU kiasi gani kwa mwezi ikiwa vyote ni vyama vya siasa?!
Ukizingatia CHADEMA kama chama kikuu kinapata mil. 107 kwa mwezi ambayo ni sawa na jumla ya bil. 1.284 kwa mwaka! 🤔
 
Mimi kwa sasa nimejielekeza kukishukuru CHADEMA kutusaidia kujua kinakubalika kwa kiasi gani kupitia michango ya kununua V8 la Lissu. Kimsingi CHADEMA kimesuswa na wapiga kura. Kwenye 500m za kununua gari la kifahari la Lissu zimepatikana 20m tu.
 
Na vyama vingine vinapokea RUZUKU kiasi gani kwa mwezi ikiwa vyote ni vyama vya siasa?!
Kizingatiwa CHADEMA kama chama kikuu kinapata mil. 107 kwa mwezi ambayo ni sawa na jumla ya bil. 1.284!
Kaa kwa kutulia ukitaka hivyo vingine vya upinzani tulia tu hapa hapa.
 
Back
Top Bottom