Nataka kugombea ubunge Karatu 2015

moseskwaslema

Member
May 3, 2012
92
13
attachment.php


JINA-Moses K. Lorri
NATIONALITY-Tanzanian
EDUCATION-BED PSYCHOLOGY 2008 UDSM
CURRENT POSITION-College tutor
PLACE OF BIRTH-Endallah village in Karatu district.
POLITICAL PARTY-CHADEMA.
AGE----31 years old

Ndugu zangu watanzania, naomba kuchukua nafasi hii kuwajulisha kwamba nimeamua kuchukua uamuzi mgumu kugombea ubunge katika jimbo la karatu kupitia chama cha demokrasia na maendeleo. Lengo hasa ni kuwatumikia wananchi wa karatu kwa uadilifu.

Nimeamua kufanya hivi kwa kuwa kwanza ni haki yangu kikatiba na pili nina uwezo wa kutosha kwa kushirikiana na wananchi wa karatu ili tuweze kuleta maendeleo kwa pamoja. Naomba vijana wote wa kitanzania kuniunga mkono kwa hili ninalotaka kufanya.

AHSANTENI SANA
 

Attachments

  • baba prosper.JPG
    baba prosper.JPG
    481.4 KB · Views: 543
HONGERA sana ila hapo si kuna mbunge au?na ana mapungufu gani na uliwasiliana na uongozi kabla ya kusema haya?na je unaona ni muda sahihi wa kusema hayo kwa sasa?na je hauna njia nyingine ya kulisaidia jimbo lako zaidi ya kugombea ubunge?
NIJIBU
 
Umeamua gombea kupitia cdm .... je umeshapitishwa na chama kwa taratibu husika ?... je kwa taratibu za chama huu Ndiyo muda muafaka? ..... je ni mwaka gani unategemea kugombea 2015, 2020, 2025?
 
Mkuu Pamoja na kwamba ni haki yako kikatiba nataka kufahamu mchango wako kwa jamii ya kitanzani, Pili kusema unataka kugombea ubunge maana yake unaitaka na si unaonekana unafaa. Kama kweli wewe ni mwana CDM je unafahamu taratibu za kuwa kiongozi ndani ya CDM?, Mimi nadhani hizi nafasi za kuwaongoza wananchi ni wananchi wenyewe wakiamua na wakaona una sifa ndiyo wakusukume si busara hata kidogo kulala na kuamka kusema unasema unataka kugombea ubunge.

Kwa jinsi unavyosema ni kama watoto wa vigogo wanaogombania vyeo mle ndani ya CCM, Je hao wanaojiyolea na kupigwa mabomu kila kukicha watasema nini?
 
Hayo maswali hapo juu atujibu kwanza ndio tuamue kumsupport au tumshauri aende ccm ndio kuna watu wa aina yake
 
Hadi leo umekisaidia nini CHAMA au jamii unayoishi nayo, ukiacha Kugawa pesa au kufundisha?
 
Kawaambie wananchi wa jimbo la karatu wao ndo wataamua wengne haituhusu,kwani karatu hawana mbunge? We ni mwalimu kwa nini usiwafundishe uwaondolee maradhi ya ujinga,kuwasaidia wananchi wa karatu si lazma uwe mbunge. WENYE NIA ZA KUTAKA UBUNGE MSIJE KUZITOLEA HAPA JF
 
View attachment 63521

jina-moses k. Lorri
nationality-tanzanian
education-bed psychology 2008 udsm
current position-college tutor
place of birth-endallah village in karatu district.
Political party-chadema.
Age----31 years old

ndugu zangu watanzania,naomba kuchukua nafasi hii kuwajulisha kwamba nimeamua kuchukua uamuzi mgumu kugombea ubunge katika jimbo la karatu kupitia chama cha demokrasia na maendeleo.lengo hasa ni kuwatumikia wananchi wa karatu kwa uadilifu. Nimeamua kufanya hivi kwa kuwa kwanza ni haki yangu kikatiba na pili nina uwezo wa kutosha kwa kushirikiana na wananchi wa karatu ili tuweze kuleta maendeleo kwa pamoja.naomba vijana wote wa kitanzania kuniunga mkono kwa hili ninalotaka kufanya.

Ahsanteni sana

nadhani jimbo hlo ndilo aliloliwakilisha slaa, na kumwachia kijiti mch. Natse. Kama kuna majimbo mawili, gombea hilo la pili, hili liache kwani tayari ni letu
 
Mkuu awali ya yote hebu tuambie utaifanyia ni Karatu, wana-Karatu, na Tanzania ambacho unadhani watangulizi wako wameshindwa kukifanya?
 
Kwani mchungaji aliepo pale Karatu ana shida gani, fafanua hilo kabla ya kuomba kura za wananchi
 
Mkuu kwa umri wako wa miaka 31 kuna lolote ambalo umewahi kufanyia wananchi wa karatu,kama kujitolea???anyway nafikiri karatu kuna mbunge wa chadema na anaheshimika sana,sio lazima kuwa mbunge ndio uwatumikie wananchi kuna mambo mengi ya kufanya,labda kama unahitaji hiyo mihela yao!
 
View attachment 63521

JINA-Moses K. Lorri
NATIONALITY-Tanzanian
EDUCATION-BED PSYCHOLOGY 2008 UDSM
CURRENT POSITION-College tutor
PLACE OF BIRTH-Endallah village in Karatu district.
POLITICAL PARTY-CHADEMA.
AGE----31 years old

Ndugu zangu watanzania,naomba kuchukua nafasi hii kuwajulisha kwamba nimeamua kuchukua uamuzi mgumu kugombea ubunge katika jimbo la karatu kupitia chama cha demokrasia na maendeleo.Lengo hasa ni kuwatumikia wananchi wa karatu kwa uadilifu. Nimeamua kufanya hivi kwa kuwa kwanza ni haki yangu kikatiba na pili nina uwezo wa kutosha kwa kushirikiana na wananchi wa karatu ili tuweze kuleta maendeleo kwa pamoja.Naomba vijana wote wa kitanzania kuniunga mkono kwa hili ninalotaka kufanya.

AHSANTENI SANA
tueleze mapungufu ya Natse na jinsi ulivyo jipanga kukabidhiana nayo.Au nia ni kukimbia mshahara mdogo?
 
Napata wasiwasi kama kweli wewe ni mwalimu, anyway kwa kuwa ni saikolojia ya kitandani " bed psychology" pengine ndo maana hujui kanuni za kichama. Nakushauri wakati ukifika gombea ila usitumie hiyo picha maana macho yamevimba kama mtu anaetumia dawa muda mrefu.
 
Jf watakusaidiaje? Nenda kwa wananchi husika kwa kuwa wao ndio wapiga kura na uende kwa wakati mwafaka. Usijekuta una tamaa tu ya madaraka. Anyway ni haki yako kikatiba kugombea uongozi.
 
Hakuna shida. Ila muda wa kutangaza nia nadhani bado. Otherwise, mimi nadhani itakuwa ni kukua kwa chama.
 
Wewe ni college tutor wapi! huko unapofundisha hakuna vyeo vya kugombea, uanze kuomba kura huko.... Najua ulisoma pale DUCE, but mbona hata kwenye harakati ndogo ndogo huko chuoni hukuwahi kusikika.....?
 
Ameona mwanga wa radi nje akadhani kumekucha!ahaaahaa rudi kalale dogo,kukikucha utaamshwa tu,tutakwenda pamoja,hatuwezi kukuacha bwana mdogo sawa eeh?
 
Ameleta uzi alafu badala ajibu hoja amebaki kuzichungulia tu .
sijui alidhani ukishakuwa mweupe kama kikwete kura ni za kufikia
 
Back
Top Bottom