Nataka kufunga ndoa tatzo sijui nijipangeje?

Nataka kufunga ndoa tatzo sijui nijipangeje?

Achana na kuoa kwanza....kamilisha malengo mengine huku ukiwa na hiyo mchuchu wako...then badae mtabarik ndoa hata mkiwa na watoto kumi si mbaya...
Zinaa. Nasema hivo sbb hata mimi nipo kama huyu jamaa sa hivi mshenga nishatuma ila kichwa kimejaa mambo ambayo hata hamu ya mapenzi sina hongeren mliooa. Ikimbie zinaa kabisa ni mbaya huyu Mungu msidhan hayupo
 
Ndo ujiulize kwenye jamii aneheshimika zaidi ni aliefunga ndoa au mwenye Mali...Hata mashuleni ambapo ndo tunatumia mda mwingi wa maisha yetu kujifunza , hatufundishwi kufunga kuoana.....tunafundishwa jins gani ya kujitegemea ili hata badae uyo utakaemuoa asipate shida...

Hivyo basi tafuteni kwanza kuweza kujitegemea ndiposa utafute wa kukutegemea .

Pia nashkuru kwa kuniaga, ingawa sikukukaribsha...[emoji12] [emoji12]
Kaka unaishi kwa mapenzi ya watu na si ya Mungu mtegemee Mungu mtii yupo anatisha utaheshimika dunian mbingun ukibisha hodi utaambiwa wewe si wangu
 
Raha za MMU... cha kwanza kabisa wasiliana na wazazi wako juu ya kusudio lako hili... Kisha washirikishe ndugu na jamaa... JF iwe ya mwisho!
BTW mchumba mwenyewe umeshampata?
Hahah.... Eti jf iwe ya mwisho. Yeye kaenda vice versa kabisaa
 
Jina lako ni Akili pesa, vyote kwa pamoja ungekuwa navyo wala usingekuja kuomba ushauri sana sana ungekuja kugawa kadi za harusi bureee....
 
Unataka kuoa mkuu aisee kuna watu mnapenda kuchezea moto
 
We mtoroshe tu ndo gharama na saiv watu ni wagumu kuchanga balaa
 
messi na utajiri wake wote amebariki ndoa mwaka jana baada ya kuishi na mpenzi wake miaka 10 na watoto wawili.. ronaldo hadi leo hajaoa...

sisi maskini tunachoma hela harusini ujanani.na baadae tunalia hatuna mitaji

Achana na kuoa kwanza....kamilisha malengo mengine huku ukiwa na hiyo mchuchu wako...then badae mtabarik ndoa hata mkiwa na watoto kumi si mbaya...
 
km ww ni muislam tatzo liko wp?? sukari kilo moja, maziwa lita 2 , mchele kilo 5, nyama kilo 3, ngano kilo 3, mshenga na mawalii vinakushinda hivyoo??? au unataka uanze kusumbua watu na michango wa left kwenye magroup na wasipokee sim zako.
 
Huku unazunguka tuu,ivi kweli huna ndugu jamaa au rafiki ukamuliza unafanyaje? hapa utapata basic sana,ila nenda kwa wazazi wako kama wapo hai washirikishe wao watafanya kila kitu,huna basi ndugu atafaa,sababu wengine wanafanya ki mila wengine kawaida na hata dini yako pia itachangia sanaa..
 
Jamani habari za humu ndani? Naamin mpo vizuri.
Sasa naomba mnishauri mm ni kijana nina umri wa miaka isyopungua 30 ninampango wa mwakani kuoa kwa maana ya kufunga ndoa, tatzo langu ni dogo sana nashindwa kujua nianzie wapi kujipanga ili lengo langu litimie kwa mwakani miezi kama hii niwe nimemuoa tayari mchumba angu.
Asnten sana Naomba mnishauri kwa uaminifu sana ili nipate mawazo mazuri.
sawa sawa. Kwanza katoe mahari. Then urudi
 
Una miaka 30 kweli wewe? Tafta mtu wako wa karib mwenye hekma zake atakusaidia michakato yote
 
Kabla ya ndoa je huyo anayetaka kumuoa umemridhia na anakukubali jinsi ulivyo? Usioe kisa umri unaenda, usioe Kwa sifa, usioe kisa nyege maana bora ukosee kwingine kote kuliko ndoa
 
Jamani habari za humu ndani? Naamin mpo vizuri.
Sasa naomba mnishauri mm ni kijana nina umri wa miaka isyopungua 30 ninampango wa mwakani kuoa kwa maana ya kufunga ndoa, tatzo langu ni dogo sana nashindwa kujua nianzie wapi kujipanga ili lengo langu litimie kwa mwakani miezi kama hii niwe nimemuoa tayari mchumba angu.
Asnten sana Naomba mnishauri kwa uaminifu sana ili nipate mawazo mazuri.
Kama unatafuta ushauri muhimu namna hii mtandaoni badala ya ndugu zako na wazazi wako basi wewe umeamua kujipoteza mwenyewe. ina maana kwenye ukoo wenu hamna wazee na watu walioa hadi unakuja kuomba ushauri kwa vijana wa shule.
Inaonekana kijana huko kwenu wamekushindwa na huwaheshimu kabisa ndugu zako
 
Ushauri wa kipagani
Paulo alikuwa mtume wa Mungu lakini hakuoa na hata kwenye maandiko ameandika kuwa anapenda watu wasioe kama yeye...Mbona msiseme ni mpagani....Acheni mambo yenu.....kwanza kufunga ndoa ni ushamha.....watu kama mmeelewana fresh mnaanzisha maisha yenu tu....tena mtaishi maisha mazuri kuliko hao wanafk wanaofunga ndoa alaf kesho kila mtu anamsliliti mwenzie.
 
Back
Top Bottom