Nataka kufunga ndoa tatzo sijui nijipangeje?

Akili Pesa

JF-Expert Member
Jun 18, 2014
616
854
Jamani habari za humu ndani? Naamin mpo vizuri.
Sasa naomba mnishauri mm ni kijana nina umri wa miaka isyopungua 30 ninampango wa mwakani kuoa kwa maana ya kufunga ndoa, tatzo langu ni dogo sana nashindwa kujua nianzie wapi kujipanga ili lengo langu litimie kwa mwakani miezi kama hii niwe nimemuoa tayari mchumba angu.
Asnten sana Naomba mnishauri kwa uaminifu sana ili nipate mawazo mazuri.
 
Kuna mengi ya kujiuliza
1.kwa nn unataka kuoa
2. Huyo ulienae yupo tayar kaolewa.
3.je pesa ya mahar ipo kumbuka hata kama ni material things vinahtaji hela
4.mshenga unaye tayar hapa familia yako lazma ishirkishe
5.ndoa c sherehe na si lazma ili kupunguza madeni watu wachache kwa dinner itakuwa bora
6.ndoa njema mkuu
 
Kwanza naamini huyo mchumba wako nayee yuko tayari kwa hili la Kama hujamwambia kaa NAYE chini muelezee mpango wako kwake. ningeijua dini ingependeza zaid . Kisha hapo

Nikuwaeleza tu wazaz au walezi wako wao watakwambia taratibu zote kipi kianze nini kifate.
 
Achana na kuoa kwanza....kamilisha malengo mengine huku ukiwa na hiyo mchuchu wako...then badae mtabarik ndoa hata mkiwa na watoto kumi si mbaya...
Zinaa mbaya unataka achezee mtoto wa watu mpk lini kesho akimtia Binti wa watu mimba lawama zote zinamwangukia mwanamke
 
Raha za MMU... cha kwanza kabisa wasiliana na wazazi wako juu ya kusudio lako hili... Kisha washirikishe ndugu na jamaa... JF iwe ya mwisho!
BTW mchumba mwenyewe umeshampata?
JF iwe ya kwanza mkuu, huku kuna shule safi.

Tuna Imani Na Magufuli
 
Hata kwenye vitabu vya dini wapo watakatifu waliozini sembuse ww ulie Tz..chamsingi ni life kwanza....imani zipo tu.

Unasema Maisha kwanza maisha ni nini ?

Mpaka uwe na Gari, nyumba, kazi nzuri au Pesa Ndio Maisha hayo ! Wangapi wanavyo vyote na hawana raha wala amani ?

Wewe utakuwa mvulana Kwaheriiii
 
Ni kama vile bado haupo tayari. Haiwezekani usijue pa kuanzia na umri huo.
 
Shirikisha familia yako swala hilo nawe utapata utaratibu mzima kuendana na mila na desturi zenu
 
Unasema Maisha kwanza maisha ni nini ?

Mpaka uwe na Gari, nyumba, kazi nzuri au Pesa Ndio Maisha hayo ! Wangapi wanavyo vyote na hawana raha wala amani navyo?

Wewe utakuwa mvulana Kwaheriiii
Ndo ujiulize kwenye jamii aneheshimika zaidi ni aliefunga ndoa au mwenye Mali...Hata mashuleni ambapo ndo tunatumia mda mwingi wa maisha yetu kujifunza , hatufundishwi kufunga kuoana.....tunafundishwa jins gani ya kujitegemea ili hata badae uyo utakaemuoa asipate shida...

Hivyo basi tafuteni kwanza kuweza kujitegemea ndiposa utafute wa kukutegemea .

Pia nashkuru kwa kuniaga, ingawa sikukukaribsha...
 
Raha za MMU... cha kwanza kabisa wasiliana na wazazi wako juu ya kusudio lako hili... Kisha washirikishe ndugu na jamaa... JF iwe ya mwisho!
BTW mchumba mwenyewe umeshampata?



Akifanya akamaliza hayoo nguvu lazima zimuishe ata siredi hataanzisha tena.
 
Jamani habari za humu ndani? Naamin mpo vizuri.
Sasa naomba mnishauri mm ni kijana nina umri wa miaka isyopungua 30 ninampango wa mwakani kuoa kwa maana ya kufunga ndoa, tatzo langu ni dogo sana nashindwa kujua nianzie wapi kujipanga ili lengo langu litimie kwa mwakani miezi kama hii niwe nimemuoa tayari mchumba angu.
Asnten sana Naomba mnishauri kwa uaminifu sana ili nipate mawazo mazuri.
Kwanza hongera mkuu kwa kufikiria hili jambo ni LA Baraka katika maisha,mambo muhimu ya mwanzo kabisa kabla hata ya kutaarifu familia Kama wewe na mwenzi wako mjadiliane mnatakata ndoa ya aina gani?Mara nyingi wanaume huwa wanataka kitu simple tu ika wadada kichwani mwao huwa wanataka kitu cha kihistoria kitakachoacha gumzo mjini au mtaani ukilinganisha na zilizopita,hili ni jambo LA muhimu sana kukubaliana mwanzo kabisa aina ya ndoa mnayotaka baada ya hapo sasa ndo utajua namna ya kujipanga kwa sababu utapata roughly idea kwamba kwa maongezi haya nahitaji kuwa na amana nono au ya kawaida.Jambo kubwa LA kujua ni kwamba kuna issue ya mahari hili ni lako mkuu ukipata wakwe wanaomuuza binti utalia maana utapangiwa mahari kubwa bila kujali uwezo wako lakini wazazi wengine wanamuuliza binti uwezo wako kisha wanapanga mahari kulingana na uwezo wako hili ni lako halina michango,kama wazazi wa binti ni wa mkoa wa mbali na ulipo jipange kwa nauli wewe na utakaoambatana nao kwenye mahari,lingine ni kwamba gharama karibu zote za vifaa vya harusi vya binti wewe ndo utaingia mfano gauni LA sendoff,Viatu,pete ya engegament na vingine vya ndani,ukija kwenye harusi pia wajibu wako kwenye shela,Viatu,vyupi,pete ,saloon,na mambo mengine ni yako hayana michango haya,la mwisho sasa ni kkujipanga na ndugu na jamaa kuona namna gani wanaweza kukusaidia kwa hali na Mali kukamilisha issue yako kumbuka kama wewe mgumu wa kuchangia watu na wewe utachangiwa kwa shida,hayo ni baadhi ya mambo unayotakiwa kujiweka sawa. Wengine wataongezea maana hapo mengi sana.Kila la heri mkuu umeamua jambo jema
 
Back
Top Bottom