Fahamu mambo mbalimbali kuhusu Kilimo cha Korosho

HABARI,
"mnyikungu,
Sawa hongera sana Tena kwa Iringa mna fulsa nyingine ambayo maeneo mengi hakuna fulsa ya kilimo cha parachichi kwenye wilaya ya kilolo na mkoa wa Njombe nakutakia kila jema Comrade.

LUMUMBA
Nashukuru mkuu, hiyo plan ya palachichi nataka nianze mwaka huu nina eneo wilaya ya mufindi nimeambiwa inafaa. Kwahiyo haya maarifa uliyomwaga hapa nitayatumia pia kwa parachichi. Asante sana
 
Nashukuru mkuu, hiyo plan ya palachichi nataka nianze mwaka huu nina eneo wilaya ya mufindi nimeambiwa inafaa...kwahiyo haya maarifa uliyomwaga hapa nitayatumia pia kwa parachichi...asante sana

HABARI,
"mnyikungu,
Safi sana omba niulize heka moja wanauzae.

LUMUMBA
 
HABARI,
"Shark's Style,
Hongera sana kwa juhudi zako kwenye kilimo cha korosho nina uhakika utafanikiwa na ukiweza kufata ushauri mzuri unauhakika wa kuvuna tani 1 kila heka hilo nina uhakika nalo.Na tani moja ni zaidi ya milioni 3 kwa sasa,
Kuhusu msimu wa kupanda nikwambie tu korosho hazina msimu wa kupandwa ila inaitaji maji tu kama huna chanzo kizuri cha maji basi subiri msimu wa mvua ukianza unapanda.Kuhusu shamba darasa hapo jaribu kuwasiliana na Naliendele wanajua mashamba darasa yote Na ninauhakia maeneo ya pwani mkuranga lazima kutakuwa na shamba darasa maeneo hayo au nenda ofisi za mkoani pwani ukiulizia wanajua wapi shamba darasa lilipo.

LUMUMBA

Asante mkuu, nina swali la ziada kutoka kwenye hizo video nimezifuatilia kwa umakini sana na nimeelewa kifanyikacho physically ila chemically kuna vitu huenda sijaelewa vizuri au sababu zake au mibadala yake, ni kuhusu hiyo plastic film anayozungushia nimeangalia video nyingi sana wengine wanatumia kitu kama gundi ya sellotape ambayo ina dark color wengine wanatumia hizo plastic film ambazo ni transparents halafu wana cover kikonyo kizima kilichobebeshwa kuprevent kisikauke kimsingi nataka kujua mazingira sahihi na vifaa vya kazi haswa kwa sie ambao tunatarajia kufanya kienyeji enyeji ili kupata matokeo sawa na anaebebesha kisasa na kuweza kupunguza gharama ikiwezekana.
 
HABARI,
"jombezi,
Asante nawe pia,Usijali hujatoka nje ya mada,Hizo habari ni za kweli ila sio duniani kote sisi msimu wetu tunavuna sawa na msumbiji ila kipindi hicho nchi kama India na Africa magharibi wanakuwa hawavuni hiyo ndio sababu kubwa inayofanya korosho yetu kuwa na bei kubwa na sio kuwa kubwa ila ni kuwa katika kipindi hicho kwenye soko la dunia korosho huwa bei iko juu kwani mahitaji ni makubwa Supply ni ndogo.Sasa sisi ni Nchi ya 8 kwa duniani na ya 4 kwa Africa kwa uzalishaji wa korosho sasa Nchi kama India ambayo ni ya 3 Kwa uzalishai duniani na Nchi ya 1-3 kwa uzalishaji kwa africa Nigeria,Ivory coast,Guinea Bissau ambazo zinaongoza kwa africa zinakuwa nje ya msimu lazima korosho iwe bei juu kipindi hicho.Lingine Tanzania tuna mbegu za korosho ambazo zinasifika sana kwa ukubwa Nayo hiyo inachangia sana Korosho zetu kuwa na soko zuri.Hapo utakuwa umenipata kidogo Comrade.


LUMUMBA
Niko na takriba

Ni ekari 20 za miparachichi ambazo nimeanza kupanda kuanzia mwaka jana na mwaka huu shughuli zinaendelea,tamaa ya moyo wangu ni kuwa pia na shamba la mikorosho ktk maeneo Morogoro au Iringa.

Lkn ipo hofu kidogo juu ya haya mazao ambayo soko lake asilimia mia ni la nje,je kinini kimesibu zao la mbaazi ufuta ,choroko.nk kuporomoka bei kwa kiwango hicho?na je changamoto hii haiwezi kutokea kwa korosho?

Natanguliza shukurani comredi!
 
Nina heka 20 lindi nimeanza kulisafisha ikiwezekana msimu ujao nianze kupanda korosho inabidi nije PM kuchukua namba yako comrade Lumumba waweza kuwa msaada kwenye hatua zangu za awali za hili zao.
 
Niko na takriba
ni ekari 20 za miparachichi ambazo nimeanza kupanda kuanzia mwaka jana na mwaka huu shughuli zinaendelea,tamaa ya moyo wangu ni kuwa pia na shamba la mikorosho ktk maeneo Morogoro au Iringa

Lkn ipo hofu kidogo juu ya haya mazao ambayo soko lake asilimia mia ni la nje,je kinini kimesibu zao la mbaazi ufuta ,choroko.nk kuporomoka bei kwa kiwango hicho?na je changamoto hii haiwezi kutokea kwa korosho?

Natanguliza shukurani comredi!

HABARI,
"jombezi,

Hongera Sana kuthubutu heka 20 za Parachichi ni uwekezaji mkubwa sana, kwa zao la korosho nashauri kama ukipata kwa morogoro Itakuwa vema sina taarifa za utafiti wa kina kama umefanyika Iringa na pia wakulima mkiwa wachache hakuna mnunuzi atakaye kuja kununua kiasi kidogo ni lazima kuwa wengi. Hilo la korosho nakushauri ungeliacha kwa sasa wewe wekeza zaidi kwenye parachichi ukikaa sawa na kuanza kurudisha pesa sasa unaweza kuangalia uwezekano hata wa kwenda mkoa wa pwani ukapata heka 200 uhakika upo kama unapesa ukaanzisha korosho.

Kwenye swala la mbaazi, ufuta, choroko, dengu shida ya hii ni kwamba soko kubwa lilikuwa India na wengi wanaopeleka kule ni wahindi wa hapa tanzania na walikuwa wanafaidika sana kwa kuwalalia wakulima tofauti na soko la korosho vietnam.Na pia ni kweli mnunuzi mkubwa alikuwa ni Manji sasa toka naye apate matatizo ya kesi sasa hakuna mnunuzi mwingine, ila kama tungekuwa na watanzania wenzetu wenye uwezo wakatafuta masoko nje na kununua mazao yetu na kuyapeleka huko ingekuwa Tiba kubwa kwa tatizo hili. Mfano mdogo ni zao la muhogo mikoa mingi zao la muhogo linastawi na kuna mbegu nzuri ziko kutoka kwenye vituo vya utafiti na china wanahitaji sana muhogo kwa matumizi mengi ila hakuna mtu wa kupeleka kule ila soko lipo. Hapa comrade kunatatizo kubwa sana.

Kwa korosho tatizo hili ni gumu kwakuwa soko kubwa lakorosho lipo marekani hata Vietnam wakinunua wao wanapeleka marekani na ulaya pia muda wa sisi kuvuna korosho nchi nyingi msimu unakuwa umekwisha hivyo mahitaji yake yanakuwa juu sana kama ilivyo parachichi inaweza kutokea ila pana ugumu sana hilo lisitukatishe tamaa Tupande.

LUMUMBA
 
HABARI,
"jombezi,

Hongera Sana kuthubutu heka 20 za Parachichi ni uwekezaji mkubwa sana,Kwa zao la korosho nashauri kama ukipata kwa morogoro Itakuwa vema sina taarifa za utafiti wa kina kama umefanyika Iringa na pia wakulima mkiwa wachache hakuna mnunuzi atakaye kuja kununua kiasi kidogo ni lazima kuwa wengi.Hilo la korosho nakushauri ungeliacha kwa sasa wewe wekeza zaidi kwenye parachichi ukikaa sawa na kuanza kurudisha pesa sasa unaweza kuangalia uwezekano hata wa kwenda mkoa wa pwani ukapata heka 200 uhakika upo kama unapesa ukaanzisha korosho.

Kwenye swala la mbaazi,ufuta,choroko,dengu shida ya hii ni kwamba soko kubwa lilikuwa India na wengi wanaopeleka kule ni wahindi wa hapa tanzania na walikuwa wanafaidika sana kwa kuwalalia wakulima tofauti na soko la korosho vietnam.Na pia ni kweli mnunuzi mkubwa alikuwa ni Manji sasa toka naye apate matatizo ya kesi sasa hakuna mnunuzi mwingine,Ila kama tungekuwa na watanzania wenzetu wenye uwezo wakatafuta masoko nje na kununua mazao yetu na kuyapeleka huko ingekuwa Tiba kubwa kwa tatizo hili.Mfano mdogo ni zao la muhogo mikoa mingi zao la muhogo linastawi na kuna mbegu nzuri ziko kutoka kwenye vituo vya utafiti na china wanahitaji sana muhogo kwa matumizi mengi ila hakuna mtu wa kupeleka kule ila soko lipo.Hapa comrade kunatatizo kubwa sana.

Kwa korosho tatizo hili ni gumu kwakuwa soko kubwa lakorosho lipo Marekani hata Vietnam wakinunua wao wanapeleka marekani na ulaya pia muda wa sisi kuvuna korosho nchi nyingi msimu unakuwa umekwisha hivyo mahitaji yake yanakuwa juu sana kama ilivyo parachichi inaweza kutokea ila pana ugumu sana hilo lisitukatishe tamaa Tupande.

LUMUMBA
Asante sana comredi,umenitia nguvu za kusonga mbele, barikiwa sana kwa ufafanuzi mzuri, wewe mi mtu mhimu sana kwangu nitazidi kukusumbua usipojali
 
Asante sana. Kuna mtu kanishawishi niingie kwenye hiki kilimo kulikuwq na fursa ya kununua mashamba mkoa wa Lindi kwa sh 50,000 kwa heka nimeshalipia eka 20, wiki ijayo nataka niende huko nikaone eneo na nianze matayarisho.

Tuendelee kujuzana kuhusu hili suala.
 
Asante sana comredi, umenitia nguvu za kusonga mbele, barikiwa sana kwa ufafanuzi mzuri, wewe mi mtu mhimu sana kwangu nitazidi kukusumbua usipojali

HABARI,
"jombezi,
Asante nawe pia. Amen ubarikiwe nawe pia usijali Karibu sana kama unaswali lolote muda wowote nitakujibu kwa kiwango cha juu cha uelewa wangu.

LUMUMBA
 
Brother Lumumba Ubarikiwe kwa maarifa unayo tupa hapa nimejifunza mengi mimi mwaka huu ndiyo ninataka nianze kupanda korosho maeneo ya kisarawe ila sina uzoefu wowote. Kuna mbegu ametuambia ni ya miaka mitatu naomba kujua kama unauelewa nayo nijue faida zake na asara zake ili nijipange mapema pia naomba kujua uzaaji wa hizi korosho pia nitashukuru sana.
 
Brother Lumumba Ubarikiwe kwa maarifa unayo tupa hapa nimejifunza mengi
mimi mwaka huu ndiyo ninataka nianze kupanda korosho maeneo ya kisarawe ila sina uzoefu wowote
kuna mbegu ametuambia ni ya miaka mitatu naomba kujua kama unauelewa nayo nijue faida zake na asara zake ili nijipange mapema pia naomba kujua uzaaji wa hizi korosho pia nitashukuru sana

HABARI,
"baba2,
Asante ubarikiwe nawe pia Samahani nilichelewa kujibu swali lako majukumu yalibana kidogo, Hongera kwa kuweka mkazo kwenye kilimo ndiyo Ninauelewa na hizo mbegu kwa uelewa wangu ni kweli kuna mbegu ziko za miaka mitatu hizo ni zile zilizofanyiwa utafiti na kuboreshwa Hasa kutoka kituo cha naliendele na hasa ubora wake unakuja kwanza zinaanza kutoa mazao ndani ya miaka mitatu ila muda unavyozidi kwenda ndio mavuno yanaongezeka na pia mbegu hizo zinahimili sana magojwa mavuno yake ni mengi ukifananisha na zile za kienyeji unaweza kukuta hizi za kisasa mti wa miaka 10 ukavuna kilo 30 kila mtu wakati zile za kienyeji zitachelewa kutoa mazao na mti wa miaka 10 ukavuna kilo 10. Pia hizi unaweza kupanda maramoja na nusu idadi kwenye heka moja tofauti na ile za kienyeji hizo ni faida mama zinazohitajika, kwenye hasara naomba nisitumie hilo neno huwa hakuna hasara ila kuna faida hasi ila ni za lazima kufata kwa kila mkulima mbegu hizi huwa zinahitai mbolea ya kupandia inashauriwa ili kuipa nguvu mimi naweza kusema hilo ndio kubwa.

LUMUMBA
 
Kaka Lumumba Nashukuru sana hapa umechochea kitu ndani yangu nitakuacha kwa sasa ila nitakuwa nakuatafuta Mara kwa Mara ili kile Mungu alicho weka ndani yako tukifaidi wote kaka.
 
Kaka Lumumba Nashukuru sana hapa umechochea kitu ndani yangu nitakuacha kwa sasa ila nitakuwa nakuatafuta Mara kwa Mara ili kile Mungu alicho weka ndani yako tukifaidi wote kaka
HABARI,
"baba2,
Asante nimefarijika sana kama nimeweza kutoa kitu na kikawa msaada kwa wengine wewe nitafute majukumu hayaishi mimi nimejitolea muda wowote wakati wowote uliza swali nitalitengea muda wa kulijibu wala usihofu hakuna kuniacha ukikaa kimya na mimi kuna mambo yatapotea kichwani uliza hata mje 100 nitajibu kila swali kwa muda wake kama litakuwa nje ya upeo wangu kuna wengine watajibu hakuna muda wa kupoteza tena.

Natamani kuona Tanzania ambayo hakuna kipande cha aridhi kikiota nyasi na vichaka mbadala iwe ni mazao ya biashara ya kutuletea fedha za kigeni na kupaisha uchumi wetu kuna nchi jirani tu hawana aridhi wanahangaika sisi tunayo tunaichezea alafu tunalia umasikini hata mbele za mungu ni dhambi kwasababu kila kaya ikiwa hata na mikorosho 100 hao sio masikini tena hii kitu inanipa shida sana"baba2,

LUMUMBA
 
Mkuu Lumumba asante sana kwa taarifa kwa kweli nimekuwa nafuatilia sana mada zako especially kwenye zao la korosho na nimekuwa interested sana najaribu kukusanya data maana nataka nifanye uwekezaji mkubwa sana kwenye hilo zao kwa kuanzia kama heka 100 swali langu je kwa tanga kama nitapata eneo na nikafanikiwa kulima wanunuzi wanakuja maeneo hayo au ndio mpaka tusafirishe kupeleka kusini au pwani na calcurated risk ya hili zao ni zipi.
 
HABARI,
"fungafunga,

Ndugu Hongera Tena kwa kuwa na kiasi hicho cha shamba kwani kama ukifanikiwa kupanda shamba lote unauhakika wa kuwa na miti sio chini ya elfu 3 ambacho ni kiasi kikubwa sana kwa kuanzia.
Nakushauri upande mikorosho iliyo bebeshwa kwani unaweza kupanda idadi kubwa kwenye shamba dogo pia inauvumilivu mkubwa wa magonjwa na inatoa mazao mapema.

Kwa kuandaa shamba ukisha safisha nivema kama mengi ni majani itakuwa vema kama ukiyachoma moto huwa inasaidia kuangamiza magojwa mbalimbali yaliyokuwa kwenye mimea hiyo ya mwanzo.

Umbali kati ya shimo na shimo unaweza kuweka kati ya mita 5-6 na umbali kati ya mstari unaweza kuweka mita 6-7,
kwa vipimo hivyo unaweza kuwa na mashimo 100-120 kwa heka moja.

Na uchimbaji wa mashimo unaweza kuchimba sentimeta 50 kwenda chini na upana wa sentimeta 50,Ni vema udongo wa juu nusu ya shimo yani sentimeta 25 ukautenga na ule wa chini wa sentimeta 25,Huu udongo wa juu utautumia kuchanganya na mbolea ya samadi wakati wa kupanda mmea.

Inashauriwa kupanda mmea wakati wa mvua na kabla ya kupanda changanya ule udongo na mbolea na kuacha kwa wiki mbili ili kuwezesha samadi kuchanganyika vizuri na udongo ndipo upande mmea.

Wakati wa kupanda unashauriwa kuweka ule udongo uliochanganya na samadi ujae robo ya shimo ndipo upande mmea wako na na wakati wa kufukia fukia nusu ya shimo kwa utaratibu huo utakuwa umefukia shimo lako na mmea kwa robotatu hiyo itasaidia kuacha eneo la maji kutuama wakati wa mvua au wakati wa kumwagilia na pia mmea kupumua vizuri,

Hii nimekupa picha kidogo juu ya maandalizi hayo ila nakushauri nenda Kituo cha naliendele Nimeweka post zake kadhaa hapa na anuani zake pale utapata maelekezo mengi juu ya magojwa na tiba zake kwakuwa mradi wako unaonekana ni mkubwa huna budi kufika pale.

Contact
Zonal Director (South),
Naliendele Agricultural Research Institute (NARI),
10 Newala Road, P. O. Box 509, Mtwara.
Tel.: +255 732 934 035
Fax.: +255 732 934 103
e-mail: utafiti@iwayafrica.com


LUMUMBA
Ubarikiwe sana mkuu.
 
Back
Top Bottom