Habari za asubuhi wana jukwaa.
Mie ni mtumishi wa umma na niliajiriwa mwaka 2013.Nina watoto wawili wa kiume,Nina viwanja vitatu ambapo kimoja nimejenga nyumba iliyoishia kwenye linta.
Toka aingie mkulu maisha yamekuwa magumu Sana,si furahii kazi yangu hata kidogo naenda tu kazini kuonekana nipo.Na siyo kuwa ni mpiga madili Wala,zamani tulikuwa tunapata hata viextra duty vinatuboost mwezi unaisha,ila saivi Nina mwaka wa tatu siijui posho.Tulikuwa tunaenda kazini hadi jmos angalau tupate chochote tulishe family.
Nimejaribu kuuza kiwanja kimoja at least nimalizie nyumba nihamie,manake Kodi inanitesa Sana huku nilikopanga ila nimekosa mteja.wanangu wanasoma mmoja baby class na mwingine class one.Bado mfanyakazi kumlipa hapo hujasaidia ndugu wanao ona nalipwa mamilioni ilihali mwisho wa mwezi napokea laki mbili na ishirini(220,000) ambayo haikidhi mahitaj yote.
Am a single parent kwahiyo mimi ndiyo baba na mama kwa wanangu.Baba yao tuliachana akaoa,na alitaka wachukua watoto ila sikuwa tayari kuacha wanangu wa under 7 years walelewe na mama wa kambo,hivyo kawasusa hatoi hata Senti tano kwaajili yao,so am their only hope.
Naona napoteza muda,nimeshafikiria hata kujirusha ghorofan ili nitoweke duniani ila nikiwafikiria wanangu roho inauma naona sitawatendea haki.So nimewaza nikaona si bora niache kazi,niuze Kila nilichonacho ingawa wateja wanakuwa tabu,nihame mji,nende sehemu nyingine nikaanze upya.Nimewaza pia kufanya nite business at least watoto wale na nipate Kodi ya nyumba,sema dhamira inakataa.
Mkuu hata Kama tulikuudhi tusamehe,tunadhalilika na familia zinateseka.Binafsi sioni faida ya kuitwa mtumishi wa umma ilhali Kuna wakati nakosa hadi nauli ya daladala kwenda kazini.Pia toka nimeajiriwa sijawahi panda cheo.
Naombeni ushauri wadau nifanyeje?je niache kazi?then niende wapi ama nifanye Nini baada ya kuacha kazi,Ningekuwa Sina watoto ningeshaondoka kitambo,tatizo mustakabali wa maisha ya wanangu utakuwaje,nikiwaza Hilo nachoka,naishia kumwaga machozi kama mtoto.
Teh teh teh wangejua nimepigika hadi najichukia,naichukia hata kazi yanguHuu uzi pm zitakuwa nyingi sana ..wapenda miteremko tunawaona tu[emoji134]
AminaVumilia ndugu yangu kamwe usikate tamaa muombe sana mungu ipo siku atajibu maombi yako
Acha tu,nilikuwa na ndoto nyingi nzuri tuHivi mtu unamaliza shule unaenda kuajiriwa na SERIKALI?
Hakuna majitu dhalimu na system dhalimu dunia hii kama kitu kinachoitwa SERIKALI!
Ni dude linaloendeshwa kwa matakwa ya wanasiasa!
It is a murder engine!
Tatizo wateja hamnaWakati wengine wanatafuta ajira wengine wanataka kuacha, uza kiwanja kimoja malizia nyumba na kazi usiache
Teh teh teh wangejua nimepigika hadi najichukia,naichukia hata kazi yangu
Laiti ningalijua nisingeajiriwa serikalin,nilikuwa private Kwa mwaka mmoja ,walipotangaza ajira kiherehere nikajitosa,kumbe naingia pori la miiba
Halafu plot zenyewe ni potential sema hamna wanunuzi,kimoja Cha makazi nilichojenga,kingine nilipanga kujenga mjengo wa kustaafia sema naona dream zi ebadilika na upepo,na Cha mwisho ni industrial plot hiki,nilipanga nipate mwekezaj tuingie partinership sema disko limeingia mmasai.
Sijawah cheza game ofisin kamweKwani shida iko wapi unalipwa mshahara ambao huufanyii kazi effectively? Unafika ofcn unacheza gemu kwa komputa mwisho wa mwezi unaenda ATM kutoa mshiko, shida iko wapi?
Acha tu tumekuwa wanyoonge hadi basiNi vile nchi yetu maskini tu..mie mdogo wangu anasema anajuta hata kupeleka cv huko...ovyo sana...alafu watumishi wamekuwa wanyoooongeee..tena mwez huu qwngine mshahara umechelewa sana sana kutoka..shenzy kbs
Pole sana kusoma sio kuwa na maisha rahisiTatizo wateja hamna
Kazi nataka acha manake siioni job satisfaction,Kila nikifika ofisin nawaza miaka 4 nilopoteza chuo nabak najiinamia tu
Ngoja nijitafakari upya mamiiCHOMA MOTO MELI WEWE
Sijataka maisha rahisi ila nataka nione matunda ya elimu yangu na sio kuwa kama ambaye hajakanyaga darasanPole sana kusoma sio kuwa na maisha rahisi
Viwanja viko mkoa gani? Mimi ni single father napenda sana watoto.Wateja hakuna kila unayemgusa hana hela,nishatumia hadi madalali,na viko sehemu nzuri tu
Kila la heri karibu mtaaniSijataka maisha rahisi ila nataka nione matunda ya elimu yangu na sio kuwa kama ambaye hajakanyaga darasan
That's y nataka niondoke,niwaachie ofisi yao
Ngoja nikitafuteNunua kitabu cha mzee mengi cha I must,I will and I can ....am sure utapata majibu na uelekeo maisha yapo kwenye taarifa sahihi...
Sitaki mume nataka nipate kipato Cha kujisimamia na wanangu tu baassiViwanja viko mkoa gani? Mimi ni single father napenda sana watoto.