Natafuta Mwekezaji katika biashara yangu

Kama hujipendi basi weka mtaji wako kwa mtu mweusi hasa Mtanzania umeisha.

Nimechoma Mil 17 with 4 months.. tena usijaribu kabisa, huwa wanaanza na lugha nzuri sasa weka hela yako uone kazi.
Umechoma m17 within 4minth katika biashara Gani mkuu
 
Kama ni wakala wa MNOs na Banks, maana yake una leseni zote na TIN
Weka vizuri dhamana zako nenda bank uombe mkopo.
Uzuri bank riba zake ni nafuu na mifumo yake ya kurudisha pesa inaeleweka
 
Kwa mwanzo inaweza ikaanza hata milioni 2 hadi 3, jinsi unavyoendelea kufanya inakuwa inapanda kwasababu wateja wAkishaju wakala una mTAJI wa kutosha waanza kufanya biashara na wewe hivyo inaendelea kupanda kwa kasi hapo ukiachana na wale wanaopita njia. Pia kipindi cha misimu ya ada za shule na sikukuu ndo kamishen inapanda balaa tokana na uhitaji wa miamala kwa wateja ni MKUBWA SANA
Malipo ya ada yana kamisheni ? Unayalipa kwa kutumia nini? Kulipa ada sio bure ?
 
zakuambiwa changanya na zako ikitokea yani mtaji utaopata, wazee wa kazi majambazi wamekuja wameondoka nao vipi inakuaje hapo? biashara inakua imeisha au tutaweka mlinzi, tutakata na bima au, lakiini una dhamana gani wewe? au ndio huo mlango tu huna hata nyumba, kiwanja jieleze vizuri ndugu usitafute mwekezaji kihuni, kweli jamani line za mpesa ziwe dhamana hii nchi uhuru umepita mipaka kweli yani line tu ndio dhamana, mi nadhani IFIKE WAKATI KUTAFUTA MWEKEZAJI KWA NAMNA HII IWE KOSA LA JINAI.

Una point nzuri sana mkuu, japo umeweka utani mwingi
 
Habari Zenu Wakuu, Mimi ni Mfanyabiashara wa Biashara ya UWAKALA ( Electronic Money Transactions ), nina uzoefu nayo sana toka mwaka 2018.

Ipo miamala ya simu kama; Tigo Pesa, M-Pesa, Airtel Money, T-Pesa, HaloPesa na Azam Pesa

Pia miamala ya Bank kama; CRDB, NBC, NMB, TCB, UBA, ACB, AMANA, EXIM, EQUITY, AZANIA, MKOMBOZI na STANBIC

Nachohitaji ni Mwekezaji wa Mtaji ( CASH ) ili tuweze kutengeneza faida na kugawana kwa makubaliano maalum. Fremu ya Biashara ipo Barabarani kituo cha mwendokasi, sehemu ambayo ni njia panda kwenye mzunguko mkubwa wa Biashara. Nilichokosa ni mtaji tu ila vitendea kazi vyote vipo na wateja ninao wengi sana changanya na wapita njia Kwasababu ni kitua cha abilia, lete mtaji tugawane faida na nguvu kazi mimi mwenyewe. Tunaandikishiana Mbele ya Mashahidi pande zote mbili na ikibidi mbele ya Mwanasheri, Siku unaamua kutoa Mtaji wako, unauchukua kama ulivyo haipungui hata senti moja kwasababu hii sio biashara ya kununua bidhaa.

Na Upigaji Wa Hesabu ni mwepesi kwasabu nadili na miamala tu hivyo ukiweka pesa yako inabidi isipungue bali iongezeke kutokana na kamisheni tutazotengeneza.

Faida (kamisheni) ikitoka haina kificho kwasabu wanakutumia.

ujumbe wa faida yako (Kamisheni) mwisho wa mwezi. Bahati mbaya sms imefutika, tunapiga simu mtandao husika na wanakutajia kamisheni yako.

Mawasiliano 0768 828082, hii Namba ina WhatsApp pia
Unataka mwekezaji awekeze shilingi ngapi?
 
Back
Top Bottom