Natafuta Mwekezaji katika biashara yangu

Nikiweka 20m faida ni kama ngapi kwa mwezi.
Kwa mwanzo inaweza ikaanza hata milioni 2 hadi 3, jinsi unavyoendelea kufanya inakuwa inapanda kwasababu wateja wAkishaju wakala una mTAJI wa kutosha waanza kufanya biashara na wewe hivyo inaendelea kupanda kwa kasi hapo ukiachana na wale wanaopita njia. Pia kipindi cha misimu ya ada za shule na sikukuu ndo kamishen inapanda balaa tokana na uhitaji wa miamala kwa wateja ni MKUBWA SANA
 
Ilikuwa siku zile. Kamishine za sasa ni ndogo sana na unagawana na serikali, mtandao/bank, withholding tax, kodi. Halafu malipo kibao ya serikali hayana kamisheni hata cent.
Kikubwa ni Kuweka Mtaji wa kutosha na mitando na mabank makubwa yote uwe nayo. Pia location ya Biashara iwe iliyochangamka. Mimi bado nafanya ila mtAji ndo sina. Kuna siku zingine zinachangamka unahudumia wateja hadi unawKimbia ilimladi ukale kwanza chakula. LOCATION*MTAJI*EXPERIENCE
 
Anaweka maneno na Laini zake pamoja na eti location kwamba kuna flow ya watu nzuri tena karibu na mwendokasi mbona mtaji wake ulikata kama angekua anatengeneza faida?. Hii ni ngumu kumeza hata mwenye mtaji akiweka apimwe vizur akili.

Kasema kila kitu atakua anasimamia yeye wakati mara ya kwanza biashara imekufa..jamaa janja sana huyu..unajikuta mtu kaweka 10M faida ya miamala yote anambiwa 400k na maneno kibao sijui chuma ulete, sijui kaja mtu kutoa kumbe n mwizi, mara kuna shoti imeingia.
Hapo mtu anaweza geuka mbogo!
Unachoongea ni kweli lakini jua kabisa sio watu wote ni Matapeli, Nimechanganua vizuri sana, nimefanikuwa kuwa na vitendea kazi na bahati ya kuwa sehemu nzuri ya mzunguko wa Biashara ila nimekosa mtaji. Kupata mtaji sio ishu lelemama, mawakala wangapi unatAka toa pesa nyingi anakwambia sina cash, sio kwamba hataki kukuhudumia mtaji tatizo. Ukimkuta wakala ana mtaji kubwa muheshimu sana kwasabu anapatA faida kubwa sana. Sisi tusion na mtaji tunatAfuta tu pesa Ya kodi, pesa ya kula. Naona bora nigawAne na mwenzangu mwenye mtaji kuliko miaka inaenda faida ndogo. Ningekopa BANK ila sina dhamana ya kupata mkopo mkubwa. Kuaminiana peke yake hakutoshi bali na mwekezaji kufuatilia mahesabu ya pesa yake. Nina Experience ya mda mrefu hivyo hasara za kijinga jinga hakuna na nina CCTV Camera, mashine ya kuhesabu pesa. Nipo Serious Tufanye biashara, kuja jamii forum kuomba Mwekezaji ni jibu jepesi NIMEKWAMA MTAJI BOSS
 
Maana aliona kama anakupa hela bure eeh
Ndio ivo ...watanzania tulio wengi tuna changamoto kubwa sana ya kukosa uaminifu yaani huyu dogo angenifata kistaarabu tukaongea akanipoza kiasi fulani akawa mmiliki wa ofisi kwa 100%

Ila ndio ivo akaamua kutaka kunidhulumu ila nilienda nae sawa nikachukua baadhi ya vifaa muhimu vya kufanyia kazi.
 
Ndio ivo ...watanzania tulio wengi tuna changamoto kubwa sana ya kukosa uaminifu yaani huyu dogo angenifata kistaarabu tukaongea akanipoza kiasi fulani akawa mmiliki wa ofisi kwa 100%

Ila ndio ivo akaamua kutaka kunidhulumu ila nilienda nae sawa nikachukua baadhi ya vifaa muhimu vya kufanyia kazi.
Eeh sasa aliona we huwezi mfanya chochote maana ushakula laki mbili zako.
 
Mtaji kwa vijana ni changamoto sana, hongera mkuu umethubutu kutoa kilicho moyoni japo wachangiaji wanakuona mpigaji lakini kwa wajuzi wa iyo kazi they are with you.

Keep it up mkuu usikate tamaa mpaka kieleweke usikubali kukatishwa tamaa kwa kutoa mawazo yako huru. Pambana na Mungu atakupambania pia, kumiliki mtaji sio jambo rahisi

Ushauri wangu kwako endelea na ulicho nacho hata kama una lak5 na mavitu ulionayo yote(vitendea kazi) jipe muda na bana matumizi kata mipango yako yote weka nguvu katika kukuza mtaji unaweza jipa hata mwaka mzima mpaka pale utakapojiridhisha kimtaji ndio utaendelea na mipango mingine

Nakutakia mapambano mema
 
Habari Zenu Wakuu, Mimi ni Mfanyabiashara wa Biashara ya UWAKALA ( Electronic Money Transactions ), nina uzoefu nayo sana toka mwaka 2018.

Ipo miamala ya simu kama; Tigo Pesa, M-Pesa, Airtel Money, T-Pesa, HaloPesa na Azam Pesa

Pia miamala ya Bank kama; CRDB, NBC, NMB, TCB, UBA, ACB, AMANA, EXIM, EQUITY, AZANIA, MKOMBOZI na STANBIC

Nachohitaji ni Mwekezaji wa Mtaji ( CASH ) ili tuweze kutengeneza faida na kugawana kwa makubaliano maalum. Fremu ya Biashara ipo Barabarani kituo cha mwendokasi, sehemu ambayo ni njia panda kwenye mzunguko mkubwa wa Biashara. Nilichokosa ni mtaji tu ila vitendea kazi vyote vipo na wateja ninao wengi sana changanya na wapita njia Kwasababu ni kitua cha abilia, lete mtaji tugawane faida na nguvu kazi mimi mwenyewe. Tunaandikishiana Mbele ya Mashahidi pande zote mbili na ikibidi mbele ya Mwanasheri, Siku unaamua kutoa Mtaji wako, unauchukua kama ulivyo haipungui hata senti moja kwasababu hii sio biashara ya kununua bidhaa.

Na Upigaji Wa Hesabu ni mwepesi kwasabu nadili na miamala tu hivyo ukiweka pesa yako inabidi isipungue bali iongezeke kutokana na kamisheni tutazotengeneza.

Faida (kamisheni) ikitoka haina kificho kwasabu wanakutumia.

ujumbe wa faida yako (Kamisheni) mwisho wa mwezi. Bahati mbaya sms imefutika, tunapiga simu mtandao husika na wanakutajia kamisheni yako.

Mawasiliano 0768 828082, hii Namba ina WhatsApp pia
Niuzie hiyo nafasi kisha utapata mtaji ukafungue kwingine.
 
Kwa nini usiweke hapa mkuu kila mtu akaona. Unataka mwekezaji, ingekuwa vyema ukataja na kiasi unachotaka.

Tangazo umeleta jukwaani, ila ukiulizwa maswali unataka watu waje Whatsapp, hii maana yake nini?. Halafu maswali unayoulizwa ni rahisi sana.
Hata mm nashangaa wakati ni kiasi cha kutaja lest say 5milion nk
 
zakuambiwa changanya na zako ikitokea yani mtaji utaopata, wazee wa kazi majambazi wamekuja wameondoka nao vipi inakuaje hapo? biashara inakua imeisha au tutaweka mlinzi, tutakata na bima au, lakiini una dhamana gani wewe? au ndio huo mlango tu huna hata nyumba, kiwanja jieleze vizuri ndugu usitafute mwekezaji kihuni, kweli jamani line za mpesa ziwe dhamana hii nchi uhuru umepita mipaka kweli yani line tu ndio dhamana, mi nadhani IFIKE WAKATI KUTAFUTA MWEKEZAJI KWA NAMNA HII IWE KOSA LA JINAI.
Anakaa na wahuni wanachora raman mara ofisi imevamiwa wahuni wanapita na hela ndio hela yako inakua imeishia hapo au?
 
Haya na mimi nataka mwekezaji wà hardware, m5 tuweke tiles thamana ya pesa yake nampa kadi ya gari na kila mwezi nampa faida kama kuna aliye tayari njoo tuyajenge--!-------
Heri wewe umekua muwazi dhamana ni kadi yako ya gari
 
Mkuu kwako ilikuaje mtaji ukapotea wakati unasema una uzoefu wa hio kazi?,mbona hapa nahisi harufu mbaya....
 
Back
Top Bottom