Natafuta mume anayeishi na virusi vya UKIMWI

Cutie M

Member
Nov 9, 2015
14
2
Habari wana jukwaa,

Mimi ni binti mwenye umri kati ya miaka 25 hadi 30 na mwaka 2010 wakati niko kwenye maandalizi ya ndoa na aliyekuwa mchumba wangu tuliambiwa tukapime, na ndipo nilikutwa nikiwa na maambukizi wakati mchumba wangu alikuwa mzima, tulipanga kuachana kwa siri bila kutoa sababu halisi na kiukweli iliniathiri sana kisaikolojia, lakini baadae nilipata ushauri kutoka kwa wataalamu wa afya na kuendelea na maisha, mwaka mmoja baadae mchumba wangu alipata binti mwingine na kufunga ndoa.

Mwanzoni nilihisi mwisho wa maisha yangu umefika na sitaweza kuolewa tena lakini kadri muda unavyokwenda sasa ni miaka 5 naona niko vizuri kabisa,sijawahi kuwa na afya mgogoro wala kuumwa mara kwa mara maana nilianza dawa mapema na ninazingatia maagizo ya daktari, nafanya kazi zangu vizuri na maisha yanakwenda.

Sasa nimekuja kwenye jukwaa hili kutafuta endapo kuna mtu ambae anaishi na virusi na anafikiri we can make a good couple na awe tayari kufunga ndoa takatifu kanisani, awe mrefu kwa sababu mimi ni mrefu na awe anajituma kutafuta fedha kwa kuajiriwa au hata kujiajiri maana pesa ndo itafanya tuishi muda mrefu na tuwe na afya bora lakini mtu mvivu asiefanya kazi simtaki maana atafanya tukose lishe bora na kupunguza maisha yetu, kwa wale ambao walifiwa na wenzi wao pia wanakaribishwa.

Kumbuka kupata VVU SIO MWISHO WA MAISHA, life goes on, alie tayari ani pm email address yake.

Thanks
NB:Hii ni issue serious sio utani wala drama kwaiyo naomba wanaotuma pm wawe serious na usitoe namba ya cm tafadhali mimi ninahitaji email address tu,wengine wanataka watoe namba ili nikipiga wapate namba yangu then what for?namba tutapeana tukishafika kwenye level fulani za mawasiliano na ikibidi tukishaonana,Ahsanteni.
 
mmmmmmmmh,pole sana na hongera sana kwa ushujaa kwani wengi sana hua hawasemi wanazidi kuumiza wenzao..
 
kwanza hongera kwa kuikubali hali yako Cutie M pole kwa yaliyokukuta na mwisho i wish you all the best.
 
Last edited by a moderator:
Mungu akubariki kwa kuwa muwazi Dada,utampata humu wa hitaji ulolisema,barikiwa sana
 
Cutie M

Pole sana kwa hali hiyo,hata hivyo wewe ni strong woman Mungu akujalie upate mume mwema
 
Last edited by a moderator:
Mungu anampango wake, utapata mume mumeo na tena mume bora na siyo bora mume. Nitaomba kwa ajili yako ila isiwe ushigongo tu
 
Back
Top Bottom