Siku 470 nikiwa na hofu ya kuambukizwa virusi vya Ukimwi

Mr George Francis

Senior Member
Jun 27, 2022
186
212
SIKU 470 NIKIWA NA HOFU YA KUAMBUKIZWA VIRUSI VYA UKIMWI.
[Sehemu Ya 1 ]

Tarehe 1 mwezi wa 12 ya kila huwa tunaadhimisha siku ya UKIMWI duniani.

Katika kutambua umuhimu wa siku hii kwa jamii na taifa letu kwa ujumla, naomba tupate funzo kupitia historia yangu na jinsi nilivyoishi siku 470 nikiwa na hofu ya kuwa na virusi vya UKIMWI.

Miaka kadhaa nyuma niliangukia katika huba la mapenzi na Binti mmoja wa Kizanzibari ambaye tulikutana chuoni.

Alikuwa ni Binti mzuri sana wa sura, shepu na hata tabia zake zilinivutia pia. Hivyo, haikuwa ngumu kwangu kumpenda na kumuamini.

Tulianza kama marafiki lakini mwisho wa siku tukajikuta katika mahusiano ya kweli na yasiyo na kificho.

Kabla ya dating yetu ya kwanza, nakumbuka aliwahi kuniambia kuwa yeye ni muathililika tangu kuzaliwa kwake.

Lakini kwa jinsi alivyo, uzuri na umbile lake, sikuweza kabisa kumuamini bali nilidhani ni mtu ambaye hataki tu kudate na mimi.

Nusrat alinishauri basi tukapime lakini niliona tu kama ananizingua.

Kwakuwa alikuwa ananipenda sana, hakutaka kunipoteza hatimae alikubali tudate bila kupima na kujua Afya zetu, japo alisisitiza sana juu ya matumizi ya condoms.

Baada ya kuzoeana tukajikuta wote hatukumbushani tena matumizi ya condoms.

Tukiwa mwaka wa mwisho chuoni Nusrat, alibeba ujauzito. Sikuwa na wasiwasi hatakidogo kwani tulipanga kuoana, baada ya kumaliza masomo.

Lakini ili kuanza kliniki ya uzazi ilitakiwa mama mjamzito na baba mtarajiwa wa mtoto ambaye ni mimi tukapime kwa usalama wetu na usalama wa mtoto aliye tumboni.

Kupima HIV haikuwa desturi yangu. Nilikataa katakata kupima. Nikamwambia "kapime mwenyewe bwana!"

Sijui alijitetea vipi hospitali lakini alikubaliwa kupima peke yake nakurudi na majibu.

Nilisoma kikaratasi cha majibu nikiwa natetemeka, jasho linanitoka. Majibu yalionesha kuwa Nusrat alikuwa ni HIV positive.

"Mungu wangu! Nimeshakufa mimi!!" Nilijisemea huku nabubujikwa na machozi. Lakini yeye wala hakuonesha wasiwasi wowote, nadhani kwakuwa alikuwa anaifahamu hali yake tangu zamani.

Nilibadilisha kabisa mtazamo wangu juu ya maisha. Tangu siku ile nilijua tu itakuwa nimeshaathirika mimi ni wa kufa leo ama kesho.

#No_Learning_No_Earning
So we have to Learn.

NAME : Mr George Francis
📩 mr.georgefrancis21@gmail.com

Inaendelea.....
IMG_20231130_134454_043.jpg
 
Kosa ni lako maana alikupa habari mapema na hukuamimi, nenda kapime Kama umenasa kula njugu
 
SIKU 470 NIKIWA NA HOFU YA KUAMBUKIZWA VIRUSI VYA UKIMWI.

Sehemu Ya II

Nikiwa nimekata tamaa ya kuishi kutokana na hofu ya kuambukizwa virusi vya UKIMWI, Nusrat alikuwa akinifariji kama sio yeye yule ambaye majibu yake yalikuwa ni HIV positive.

Sikutaka kuendelea kumsikiliza, niliamua kuondoka huku akili yangu ikiniambia "ni heri nife kuliko kuendelea kuishi na virusi vya UKIMWI."

Nikiwa nimekaa natafakari nitumie njia gani ya kuniondoa duniani haraka ili niepuke fedheha, nikawa nategea sikio kipindi kimoja cha redio.

Hata sikumbuki ni redio gani lakini nakumbuka ni kipindi kilichokuwa kinaelezea kuhusu mambo ya UKIMWI.

Daktari alikuwa akielezea jinsi ambavyo mgonjwa wa HIV anavyoweza kuishi kwa muda mrefu.

Moja ya njia hizo ni
(i). kutumia dawa za kufubaza makali ya virusi vya UKIMWI kwa usahihi.

(ii). Kula mlo kamili ikiwemo na ulaji wa matunda na mboga za majani.

(iii). Kufanya mazoezi marakwamara kwa kuzingatia kanuni za afya.

(iv). Kuhepuka kuwa na msongo wa mawazo na kupata muda mzuri wa kupumzika baada ya kazi.

Kimsingi haya ni miongoni mwa mambo ambayo yalinipa tumaini la kuishi kwa muda mrefu, lakini kuhusu matumizi ya ARV hili lilikuwa mithani mkubwa kwangu.

Ulikuwa mtihani kwasababu nilikuwa sitaki kupima. Mimi nilishajiona tu mwenyewe kuwa tayari nina maambukizi.

Nilijiwekea mikakati ya kufanya mazoezi na kula vizuri lakini kuhusu kupima nilisema siwezi.
"mimi afya yangu naijua, hivyo siwezi kupima."

Nilitaka kuachana na Nusrat lakini nilijiuliza,
"Kama kuathirika nimeshaathirika, sasa kwanini nimuache!!?

Nusrat alijifungua mtoto wa kiume miezi miwili baada ya kuhitimu elimu yetu ya chuo kikuu.

Mtoto alizaliwa bila maambukizi ya virusi vya UKIMWI na hadi leo hana maambukizi.

Basi niilikamilisha taratibu kadha wa kadha na kuanza kuishi na Nusrat kama mume na mke.

Yeye aliendelea kutumia vidonge vyake vya ARV kwa uaminifu lakini mimi sikutaka kuonekana huko kwenye foleni za dawa.

Kuna kipindi niliumwa sana, mke wangu na hata mimi mwenyewe tukajua tayari virusi vimeanza kufanya kazi katika mwili wangu.

Inaendelea...

#No_Learning_No_Earning
So we Have To Learn.

NAME: Mr George Francis
📩 mr.georgefrancis21@gmail.com

IMG_20231130_165037_991.jpg
 
Sehemu Ya III

Hali ilikuwa mbaya sana. Nilikimbizwa hospitali nikiwa hoi bin taabani. Mke wangu alilia sana alijua kuwa sitaweza kupona.

Kutokana na hali yangu, Daktari aliyekuwa akinipatia huduma alishauri nipimwe vipimo vyote ikiwemo vipimo vya HIV na hapo nilikubali.

Sikuwa na hofu kabisa kuhusu majibu ya vipimo, kwani teyari nilishakuwa nimejikatia tamaa muda mrefu sana.

Majibu mengine yote sikuwa na shaka nayo lakini, majibu ya vipimo vya HIV yalinishangaza sana.

Sikuweza kuamini, niliomba Madaktari warudie vipimo vya HIV lakini sasa wanipime pamoja na mke wangu kipenzi Bi Nusrat Kareem.

Majibu yalikuja vilevile. Baada ya siku 470 za kuishi nikidhani naishi na virusi vya UKIMWI, majibu haya yalikuwa ya kustaajabisha sana.

Majibu yalionesha kuwa sina maambukizi ya virusi vya UKIMWI lakini mke wangu ni HIV positive.

"Oh! My God! How is it possible!!" Nilijiwazia mwenyewe.

Nikajikuta nimepata nguvu ghafla, nikainuka kitandani na safari hii nilisema kwa sauti
"How is it possible!!"

Ndipo Daktari alipoona kuwa sasa tunahitaji kuolewa elimu zaidi.

Daktari alisema,
"Ni kweli inawezekana kushiriki tendo la ndoa na mtu mwenye maambukizi ya virusi vya UKIMWI na wewe usiupate.

Kitendo cha Nusrat kutumia dawa za ARV kwa muda mrefu na kwa usahihi pengine kumesaidia kufubaza makali ya virusi kiasi cha kupunguza uwezekano wa kumwambukiza mtu mwingine."

Nilimsimulia Daktari jinsi nilivyoishi siku 470 nikidhani kuwa nimeathirika.

Daktari alinishauri na leo napenda kushare na wewe,
"Usimwamini mtu kwa macho, mkiwa na mahusiano, kabla ya sex hakikisha kwanza mnapima na kufahamu afya zenu.

Tendo la ndoa la dakika mbili linatosha kabisa kukupa virusi vya UKIMWI. Matumizi ya condoms kwa ushahihi ni muhimu sana.

MWISHO, kama jamii, tushirikiane kukumbushana na kupiga vita unyanyapaa dhidi ya waathirika wa virusi vya UKIMWI."

MUHIMU = Pamoja na mambo mengine yote, tusiache kumwomba Mwenyezi MUNGU juu ya ulinzi wa afya zetu na wapendwa wetu.

Nusrat aliyekuwa mke wangu na mama wa mwanangu, kwa sasa hayupo tena duniani.

Alifariki mwaka huu tarehe 6 June kwa ugonjwa wa kichaa cha mbwa ma wala sio kwasababu ya ugonjwa wa UKIMWI.

Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema peponi.
AMEN. 🙏

#No_Learning_No_Earning
So we have to Learn.

Kauli mbiu 2023 =
#jamiiiongozekutokomezaukimwi

NAME: Mr George Francis
📩mr.georgefrancis21@gmail.com
 
Back
Top Bottom