Natafuta mume anayeishi na virusi vya UKIMWI

Natafuta mume anayeishi na virusi vya UKIMWI

Tafuta dawa za kuponyesha huo ugonjwa; kuna watu humu wanajitangaza kuwa wanatibu tatizo na linakwisha kabisa, yaani unakuwa -ve. Ila uwe makini kuna MATAPELI humu.
 
Dada nimependaa ushujaa wako utampata wakoo tena utaishi maisha marefu zaidi ya uwajuaoi hawana...all the best swithat
 
ila usuof kutoa namba kwan itarahishisha zaid, kikubwa kuwa makin ktk kuonana au kuweka picha Whatsap au unaweza kuwa na namba kwa ajul hiyo tu hata ukipatikana usiku tu,
nb haya mavitu ni matamu ni ngumu kuacha jumla.
 
Hongera kwa ujasiri uliotukuka....be strong, stay strong
 
mtanganyika wa kweli kama wewe hauna hizo sifa basi pita tu usianze kutoa kashfa,wewe kama una afya bora na ukae na afya bora milele,usije ukapata hata upele wala chunusi,God is watching u

Achana nae huyo hajielewi..
 
May God grant your hearts desire. Una ujasiri mkubwa sana ila usijiweke kuwa ni lazima uolewe na mtu mwenye VVU , tumepata shuhuda nyingi humu za watu kuonana mmoja ana maambukizi na mwingine hana maambukizi. Muombe Mungu neema ya kukutana na mtu atakayekufariji. Na pia mdogo wangu, please don't compromise furaha na afya yako kwa sababu tu unahitaji mume. Wengine watakuja na mizigo mikubwa kwako na watakudrain your happiness. You know better what you desire , mlilie Mungu na kamwe hatakuacha.

May God bless you.
 
Habari wana jukwaa,

Mimi ni binti mwenye umri kati ya miaka 25 hadi 30 na mwaka 2010 wakati niko kwenye maandalizi ya ndoa na aliyekuwa mchumba wangu tuliambiwa tukapime, na ndipo nilikutwa nikiwa na maambukizi wakati mchumba wangu alikuwa mzima, tulipanga kuachana kwa siri bila kutoa sababu halisi na kiukweli iliniathiri sana kisaikolojia, lakini baadae nilipata ushauri kutoka kwa wataalamu wa afya na kuendelea na maisha, mwaka mmoja baadae mchumba wangu alipata binti mwingine na kufunga ndoa.

Mwanzoni nilihisi mwisho wa maisha yangu umefika na sitaweza kuolewa tena lakini kadri muda unavyokwenda sasa ni miaka 5 naona niko vizuri kabisa,sijawahi kuwa na afya mgogoro wala kuumwa mara kwa mara maana nilianza dawa mapema na ninazingatia maagizo ya daktari, nafanya kazi zangu vizuri na maisha yanakwenda.

Sasa nimekuja kwenye jukwaa hili kutafuta endapo kuna mtu ambae anaishi na virusi na anafikiri we can make a good couple na awe tayari kufunga ndoa takatifu kanisani, awe mrefu kwa sababu mimi ni mrefu na awe anajituma kutafuta fedha kwa kuajiriwa au hata kujiajiri maana pesa ndo itafanya tuishi muda mrefu na tuwe na afya bora lakini mtu mvivu asiefanya kazi simtaki maana atafanya tukose lishe bora na kupunguza maisha yetu, kwa wale ambao walifiwa na wenzi wao pia wanakaribishwa.

Kumbuka kupata VVU SIO MWISHO WA MAISHA, life goes on, alie tayari ani pm email address yake.

Thanks
NB:Hii ni issue serious sio utani wala drama kwaiyo naomba wanaotuma pm wawe serious na usitoe namba ya cm tafadhali mimi ninahitaji email address tu,wengine wanataka watoe namba ili nikipiga wapate namba yangu then what for?namba tutapeana tukishafika kwenye level fulani za mawasiliano na ikibidi tukishaonana,Ahsanteni
 
Hakika wewe ni mfano mzuri wa kuigwa. Usishangazwe sana na wale wenye mitizamo hasi kwa kila jambo kwakuwa ukweli ni kwamba hawajieliwi vyakutosha na hata afya zao pia hawazielewi.

Kila la kheri na Mungu ni mwema atakupa mume bora na mwenyekuthamini utu wako pamoja na vile vizuri unavyovithamini wewe mwenyewe.
 
Hongera kwa kuwa muwazi, Mungu atakupatia hitaji la moyo wako.
Baadhi ya sifa ninazo ila hiyo ya urefu imekuwa kikwazo kwangu.
 
Back
Top Bottom