Natafuta mtu wa Kuniloga.

Natafuta mtu wa Kuniloga.

Acha kelele rudi tena zenji mtafute jamaa anaeitwa adui chongo(kwao donge) gegeda/tongoza waifu/binti yake halafu mjulishe then ndio tutasikiliza vizuuri hadith zako!wewe unafikiri mungu anaweza akakataza kitu kisicho kuwepo?
Hivi hajasikia jamaa aliwekewa dushelele hapo kwenye paji la uso? Chezea uchawi!!!
 
Unapatikana wapi? Ushawahi kusikia kijiji cha Kwamsisi? Kifupi attach hapa jina lako kamili na la mama yako mzazi kamili.
 
we kijana acha dharau wewe! kwa hiyo unajiamini hatukuwezi eh? ngoja tukugoogle ili tujue pa kuanzia!
`Kesho mtoto wako ataugua sana to the point of death'
 
Kuamini au kutoamini kulogwa ndiyo msingi wa kuweza kulogwa au kutoweza kulogwa.

Ni nguvu ya kuamini au kutoamni inayowezesha hali yeyote, tukio au mazingira unayopitia maishani
.
Matokea yatategemea kama unaamini kuwa unaweza kulogwa au hapana.

Uchawi ni matokeo ya nguvu ya imani. Huwa unawashangaza watu kwa kutojua nguvu ya imani.

Imani hufanya kazi kama msumeno. Kama unaamini kuwa kuwa unaweza kulogwa na ukalogeka ni sawa utalogeka vizuri sana lakini kama una amini uwezi kulogeka ni sawa pia uwezi kulogeka.

Unapoamini kuwa hauwezi kulogeka alaf ukaingia shaka kuwa unaweza kulogeka utalogeka vizuri tena mchana kweupe. Matokeoyakulogwa au kutologwa lazima yaumbwe na imani, hakuna kinyume na hapo.

Wazo lakulogwa linakuwepo/linakuja,halafu inategemea nini kiko kwenye imani zako. Mfano; unaposema sala zako hazijibiwi inaweza kuwa ni suala la kukinzana kwa kile unachoamini kwenye mawazo ya kina na unachotaka kiwe kwenye mawzo yako ya kawaida au imani haikuwa imara. Ukiwa na wazo lakulogwa na kulogeka, wazo hilo huzaa hisia, ambazo husema nini kitatokea. Hisia zilizotengenezwa nyuma zaweza kuharibu nia au lengo la leo.


Baada ya kutoa hizo dondoo naona sasa nielezee kidogo kuhusu hicho kinaitwa uchawi. Hakuna ajuaye uchawi ulianza lini. Lakini, katika kujiuliza maswali binadamu aligundua nguvu zenye kumzunguka.
Lakini, miaka mingi kabla ya Yesu kuja watu walianza kutambua nguvu nyingi kamauchawi,zenye kuweza kudhuru.

Baadaye uchawi ulianza kutumiwa kamakisingizio, ambapomatajiri walituhumiwana kuhukumiwa, kwamba, ni wachawi. Kijicho na uadui mwingine vilitekekelezwa kupitia uchawi. Walioouwawa zaidi hasa ulaya na Marekani walikuwa wanawake (asilimia 90). Kisa, Kanisa liliamini Ibilisi anaweza kuwashawishi kirahisi zaidi wanawake kupitia uchawi.

Hivi sasa wanaokubali kuwepo kwa uchawi wanaugawa katika makundi mawili-Mweupe na Mweusi.

Nadharia kuhusu uchawi Mweupe na Mweusi

-Ni kwamba uchawi mweupe au mweusi, wote ni uchawi bali ule mweusi ndiyo wenye lengo la kudhuru. Hata dini zinapozungumzia uchawi zinazungumzia huu mweusi.

-Wengine wanaamini kwamba, uchawi unakuwa uchawi wenye madhara ( mweusi) kama tu kuna vitu kama nywele, damu, au nguo za anayeunuiziwa zinazotumika katika kufanya hivyo.

-Wengine wanasema hakuna uhusiano kati ya uchawi mweusi na mweupe kwani kila mmoja unatumia njia na mbinu zake kufanya kazi. Wengine wanasema uchawi mweupe na mweusi ni sawa, ingawa matokeo ndiyo yanayotofautiana. Kama ni manuizi ni yaleyale, bali nani analengwa na kwa lengo gani, ndicho kitaleta matokeo, ambayo yatakua tofauti.

Sheria/amri kuu za uchawi.

Mchawi yeyote anayejua kwamba, analoga anajua kuhusu sheria hizi, hata kama hajui kuwa ni sheria au hata kama hatazijua kwa njia ya moja kwa moja.

1.Sheria ya uzao wa utatu Hii ina maana tutavuna tulichopanda. Tunachopanda kitaota na kutupa mazao mara tatu zaidi. Kama ni mazao ya maumivu, umasikini, utaturudia mara tatu. Watu wa Wicca wanatishwa sana na kanuni hii.

2.The wiccan rede Mchawi anahusiwa kufanya chochote kupitia nguvu za uchawi, mradi tu hajiumizi mwenyewe wala kumuumiza mwingine. Kwa wale wa wicca, hili wanalifuata sana pia.

3.ULOGAJI:kuna matumizi ya nguvu nyingi. Mawazo ndiyo chanzo kikuu. Ile nia ya kudhuru. Laana:Hapa kuna aina kadhaa kama vile gypsy🙁kunuiza:mfano; utakua mtu wa kutangatanga kwenye uso wa dunia milele, hutalala mara mbili kwenye kitanda kimoja, hutakunywa maji mara mbili toka kisima kimoja na hutavuta mto huohuo zaidi ya mara mbili kwa mwaka).

-Siyo kila neno au maneno yanaweza kuwa na nguvu ya kuathiri. Kama ingekuwa hivyo, wengi tungeshakufa ua kuumia kupindukia. Utaalamu wa maneno ni muhimu pia, kwani unaweza kuwa unampa mtu baraka badala ya kumloga.

-Maneno yasiyo maalumu sana huleta tu mikosi na yale maalumu huweza kudhuru afya au kipato.

Ishara
; Mtu anachukua hata toi, analivisha nywele za anayetaka kumdhuru au kipande cha nguo yake ama damu yake. Halafu mchawi hutumia pini kumchoma huu mdoli akiwa ameweka uzingativu kiakili kwa anayemloga. Hii hutumika sana kwenye uchawi wa voodoo wa Carbbean.

Kunuia: kunakuwa na seti maalumu ya aya, kanuni, kitendo au aya na kitendo. Mchawi hunuizia kwa aya au aya na kitendo akimnuia mtu. -Anaweza hata kwenda kwa mtu akafanya kitu mlangoni mwa nyumba yake. Mfano, mfano punje za mchele na sarafu akazitupa mlangoni mwa mtu kwa kunuizaa kwamba asipate kipato…alafu….!!!! -Kwa mfano, Oborojino wa Australia wanaamini kwamba, ukimnyooshea mtu mfupa wa kangaroo na kunuiza jambo baya, anaweza kudhurika. -Kaburi la Farao Tutankhamen wa Misri lina historia hii. Ni aya ya zamani ambayo ilisemwa na Mfalme huyo na kubandikwa nje ya kaburi hilo. -Mrusi Rasputin alitamka maneno Fulani wakati akikata roho dhidi ya Utawala wa Kifalme wa Urusi enzi zake, kufuatia kupigwa kwake risasi na kuasiwa na mtoto wa Mfalme. …..!!!! …
 
Hamna uchawi wala nini, ni mazingaombwe madogo madogo tu.
 
Ni jambo jema na lakushangaza...
Nitafute,kuna dawa inaitwa weja.Hii ukichimbia nyumbani kwa mtu kila kiumbe hai kitakufa kwa mda wake kuanzia vifaranga hadi mwenye mji..

Hata a lump of radiactive material may have the same effect.

Mengine ni sayansi tu hatujaijua.

Unataka kuua mtu, unaenda kwa mchawi, anakupa a chemical ambayo ni sumu chemically, unamlisha mtu, anakuca.

Kisha unasifia uchawi!
 
Mkuu, mi naamini suala la uchawi liko akilini zadi na si physical hasa. wazungu walipokuja afrika waafrika waliamini kuwa wasingefika mbali. waliwagawia maeneo aliyosadikiwa kuwa hatari.hatari haikuonekana. kina kinjekitile waliwashawishi wafuasi wao wanywe dawa iliyochanganya na maji na risasi za mjerumani zingegeuka maji. haikuwa hivo. kama ulisoma Things Fall Apart utakuwa umeona haya. kimsingi ni kuwa watu wanaoamini sana uchawi hawawezi kabisa kuendelea bali wale wanaowaaminisha wengine wataendelea maana watakula kupitia hofu za wanaoamini uchawi.
 
Kuna nyumba za ibada ambazo kila siku mapepo huwaangusha waumini yaani mapepo hayaishi humo. kwingine hakuna kitu kama hicho na watu wamechanganyika katika nyumba na mitaa lakini mapepo yanawachagua tu baadhi na kuwaacha wengine. imani kuhusu uchawi ni hatari kuliko uchawi wenyewe. anayeamini uchawi sana ataogopa kila kitu hadi macho ya mama yake au baba yake. kanda ya ziwa huwaua sana vikongwe kwa imani za uchawi. kaskazini hakuna kitu kama hicho.
kwa hiyo mkuu amini tu kuwa hakuna uchawi na huna haja ya kuwaambia watu hilo na hata siku moja hutaona kitu uchawi.
 
weka jina lako halisi nikutumie mzigo uangaike nao kuanzia sasa
 
Nina idea moja ambayo kama serikali ikiamua kuifanyia kazi
a. Itainua jina la Utalii wetu
b. Itaingiza fedha za kigeni kuliko mahali popote Afrika
c. Na itaifanya Tanzania kuwa katika hadhi ya pekee yake kila watu wanapozungumzia utalii duniani.

I would like though to patent it. Sijawahi kuisikia mahali popote, haipo katika sera zetu za utalii, na siyo mawazo ya mtu mwingine (I didn't plagiarize). How can a Tanzanian patent an idea that will affect the tourism industry and earn him some good money?

Can I patent an Idea in US that will affect another foreign country? I'm willing to share that idea with someone who knows architecture, drawing, and marketing.....Believe me, once you hear it, It'll blow you mind!!!!!!



Tunajua kuwa uhalisia wa thread yako ni kuwa wewe ni mganga wa kienyeji uliyejidhatiti dhidi ya kirogwa na waganga wenzio sasa hapa unafuta kuhakiki ukali wa dawa ulizojiwekea ili kujua ikiwa zinafanya kazi au la
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom