Wakuu,
Nina miaka 4 sasa nafanya utafiti kuhusu kuwepo kwa uchawi sijapata kujiridhisha kihalisia kuwepo kwa ushirikina.Nimetembelea maeneo yote yanayosemekana ni maarufu kwa ushirikina kama Tanga, Sumbawanga, Pemba na Bagamoyo. Huko pemba nimefika maeneo ya wete kuna kamsitu wanasema ndio hatari kwa wachawi kukaa na kufanya matambiko kuna makaburi ya zamani sana walisema tukifukua tutakufa kwa vile tutachokoza 'wazee' tumefanya excavation vizuri tukakuta artifacts na masufuria ma hirizi na mavitambaa mekundu na meusi na manyoa, ni mwaka sasa na mpaka sasa hata mafuta hakuna aliye pata kwenye team yetu. Tulilala hapo hapo makaburini kwa kutumia tent hata mbu hakutun'ata.
Sasa swali ni kwamba mtu anasema ooh nimelogwa na kukimbilia kwa hawa watumishi fake wa Mungu na kusema wamepona, wamenpona nini? Mimi nimeomba wazee waniloge wakasema wameniloga sitozaa kabisa kwa sasa na miaka 28 na watoto 6 na wana afya nzuri na nimepima DNA ni wa kwangu.
Kama kuna mtu amelogwa au anaweza kuniloga atoe fact hapa.
Mzizi mkavu
Asprin Bujibuji Nyani Ngabu faiza Fox
Yericko Nyerere