Natafuta mtu wa Kuniloga

NGULI

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2008
Posts
4,801
Reaction score
652
Wakuu,

Nina miaka 4 sasa nafanya utafiti kuhusu kuwepo kwa uchawi sijapata kujiridhisha kihalisia kuwepo kwa ushirikina.Nimetembelea maeneo yote yanayosemekana ni maarufu kwa ushirikina kama Tanga, Sumbawanga, Pemba na Bagamoyo. Huko pemba nimefika maeneo ya wete kuna kamsitu wanasema ndio hatari kwa wachawi kukaa na kufanya matambiko kuna makaburi ya zamani sana walisema tukifukua tutakufa kwa vile tutachokoza 'wazee' tumefanya excavation vizuri tukakuta artifacts na masufuria ma hirizi na mavitambaa mekundu na meusi na manyoa, ni mwaka sasa na mpaka sasa hata mafuta hakuna aliye pata kwenye team yetu. Tulilala hapo hapo makaburini kwa kutumia tent hata mbu hakutun'ata.

Sasa swali ni kwamba mtu anasema ooh nimelogwa na kukimbilia kwa hawa watumishi fake wa Mungu na kusema wamepona, wamenpona nini? Mimi nimeomba wazee waniloge wakasema wameniloga sitozaa kabisa kwa sasa na miaka 28 na watoto 6 na wana afya nzuri na nimepima DNA ni wa kwangu.

Kama kuna mtu amelogwa au anaweza kuniloga atoe fact hapa.
Mzizi mkavu Asprin Bujibuji Nyani Ngabu faiza Fox Yericko Nyerere

 
Tafuta mwanamke wa uswahilini, muonyeshe kama una gari nyumba na mali. Anzisha mahusiano

kisha utakuja kusema mwenyewe kama kurogwa kuko

Tena hao ndio hawalogi kabisa sema wanajua kumtuliza mwanaume kumpa..... kisawasawa refer to my last thread... kuwa watoto wa imani ya.... ni noma. Sasa mwanaume anakuwa zuzu akiambiwa mguu pande na mguu sawa anaenda. So hakuna uchawi
 
Okay, fanya jaribio la mwisho kabisa. Nenda Sumbawanga, ulizia wale wazee wenye sifa ya kuwa ni walozi wa ukweli halafu wafanyie moja kati ya haya:-

i. Tembea na mwanae halafu umpe mimba kisha ukimbie, au
ii. Kawatukane, uone kama watakupeleka polisi, wasipokupeleka polisi, subiri majibu
iii. Au ukawaombe tu wakuroge.
 
Kuna Mtanzania mmoja alisema kuwa yoyote atakayemgusa kwa lengo la kumdhuru atawaangamiza ukoo wake wote kwa uchawi, hata PANYA hawatabakia.

Kama uko serious, mtafute huyo Rais umdhuru utajua kama uchawi upo au lah.
 

kwenye blue hapo ndio umenifanya nianze kutilia mashaka uhalisia wa post yako.najua inawezekana lakini haileti mantiki kwa ''mtafiti'' kama wewe..
 
NGULI, umenikumbusha mbali sasa, umenikumbusha ule mwembe mkubwa ambao ulikuwa unageuka kuwa mamba.
Pia unanikumbusha yale maji taka yaliyokuwa yakikutwa kwenye kabati bovu jirani na ule mwembe.
Safari yenu ya Pemba imenikumbusha giLESi wangu wa moyo, ngoja nimtafute.
 
Last edited by a moderator:
Ninapata mashaka kidogo kwa umri ulionao na idadi ya watoto ulionao! Hata hivyo labda nikuulize swali unaamini uchawi upo?
 
Ninapata mashaka kidogo kwa umri ulionao na idadi ya watoto ulionao! Hata hivyo labda nikuulize swali unaamini uchawi upo?

Hilo la watoto naomba mliache kwa sasa. Siko kuelezea maisha yangu binafsi naulizia uchawi. Kuna member wanaonijua uhalisia wangu na hao watoto kwa mfano Bujibuji na @aspirin. Nikielezea nilivyopata hawa watoto itakuwa thread maisha yangu ni muujiza tosha kaka.
 
Last edited by a moderator:
Yaani miaka 28 watoto sita? Si ndo kurogwa kwenyewe ukifikisha 35 utakuwa na watoto 18 na utashindwa kuwalea na kuwasomesha kipato chako kitakuwa duni! Utajaribu kila kitu hutafanikiwa hakika umerogwa
 
Tena hao ndio hawalogi kabisa sema wanajua kumtuliza mwanaume kumpa..... kisawasawa refer to my last thread... kuwa watoto wa imani ya.... ni noma. Sasa mwanaume anakuwa zuzu akiambiwa mguu pande na mguu sawa anaenda. So hakuna uchawi

Umenena vyema, hilo halina ubishi.
 

Akuroge nani wewe? apoteze wakati wake? mwenyewe hapo ulipo upo hoi bin taabani, ungekuwa mzima ungeota mchana (hallucinate) kuwa Kikwete ni baba'ko mzazi?
 
Akuroge nani wewe? apoteze wakati wake? mwenyewe hapo ulipo upo hoi bin taabani, ungekuwa mzima ungeota mchana (hallucinate) kuwa Kikwete ni baba'ko mzazi?

Kama huna cha kujibu bora ukae kimya. Wanasema bora kukaa kimya nakuonekana unajua kuliko kufungua mdomo na kuthiirishia umma ulivyo mtupu. Kila nacho post ndio jibu hilo hilo unatoa. Inaonekana wewe mjane na unaendeshwa kwa hisia zaidi ya reasoning. Kuna tiba nitakuponya kisaikolojia kwa vile kila jamii ina watu kama nyie na mko ili sisi tujione ni kiasi gani tumebarikiwa na Mungu.
 
Nilikutana na padri mmoja aliyekuwa anafanya utafiti kwa ajili Phd yake.
Anasema alizunguka kwa waganga wote maarufu nchini, mpaka nchi za jirani kujalibu kupata taafa zake ila kati ya mambo ambayo alisema hayapo ni "UCHAWI". Anasema kuna sumu, na mazingaombwe lakini uchawa kama ule wa kudai mtu kuruka na ungo ni uongo na kwamba hakuna anayeweza.
Ni mchango wangu tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…