Natafuta mke lakini sina kazi!!!!

mume eti..ha ha!! kweli unawaangusha wanaume wenzio, hata soni huna!!

Huenda ni ajira tu imegoma mambo mengine muhimu kwa maisha ya binadamu amekamilisha na isitoshe huenda alishafanya kazi kipindi cha nyuma hivyo mafao yake yapo NSSF yamezuiliwa na SSRA muda si mrefu atakua njema kama marekebisho ya sheria ya fao la kujitoa ikifanyika vinginevyo bado kidogo afike miaka 55 hivyo mke avumilie
 
Cjaelewa elewa!anatafuta
mme ama mke?kazi ya mwanaume ni kumlisha,kumvisha na kutake care vyote
vinavyohusiana na mkeo na hata kama ana kazi usitegemee mshahara
wake,,hapo ndo utapata heshima yako kama mwanaume,,haya endelea kutafuta
niliona ktk gazeti moja la udaku wanatafuta wenza nafikiri litakufaa
maana mabinti wa JF wapo juu wanataka mtu responsible.kwanza una
qualification gani?

Apo chacha,a-e-i-o-u
 
Mkuu kwani ni kazi ndiyo
inaoa au wewe
Kitu si kina fanya kazi tafuta mchumba fanya process zingine kwa
expirience yangu ukisubiri hadi upate kazi nzuri muda unasogea na naona
age ya kuoa inakutupa mkono
Ukiendele kukaa single pengine hujishughulishi sana ila uliwa let's say
family kazi utapata tu

sio swala la kazi nzuri mkuu,soma maelezo yake hata iyo kazi mbaya hana.
 
Daaaah!! Kweli ukistaajabu ya Musa,.......... ya filauni!!. Leo nimeyaona lol.
Yaani huna kazi halafu unataka kuoa? Au nimesoma maneno yako vibaya, unamaanisha unataka kuolewa?
 
Ileza CV yako ili uwavutie. KUNAKO SHUGHULI, KIWANGO CHAKO CHA KUJITUMA KIKOJE? NAHISI UKILIWEKA WAZI HILI, WATAKUTAFUTA WENYEWE NA UTATUZWA. WAPO WENGI TU, KAZI HAWANA, WANAKULA VIZURI, KUNYWA NK. KWENYE SHOW SASA................. UGOI GOI NI TIKETI YA TALAKA.
 
Mimi kama mwanamke sione kama mnyella umewahaibisha wanaume kama wengi wa wanawake wenzangu wanavyochonga,sijui kwanini wana jf mnashangaa,kitu gani cha kushangaza kama mnazaliwa leo,mwanaume kutokuwa na kazi na mwanamke kuwa na kazi mnashangaa!,naona nyinyi hamjui dunia,dunia ina siri kubwa,hiyo kawaida tu mnyella achana nao,mijitu kama kina mnyella ukiwachukua na kuwapa dili ni watu wa kupambana sana,mm binafsi nakufikiria mnyella,nina kuPM sasa hivi na najua nikikupa dili utanitoa kwasababu najua una hasira,husikonde tupo wanawake tunaoelewa maisha,maisha ya kusema mwanaume lazima umuhudumie mwanamke yamepitwa na wakati acheni ushamba tuacheni sisi madada tuliozaliwa mjini tunaelewa maisha yakoje,maisha ya sasa hivi ni kusaidiana unaweza ukamchukua mnyella mkapanga nae akaja akakutoa.
 
nimependa ushauri wenu mwingi anachotakiwa aseme kuwa hana sehemu ya kupata mshahara kuhusu mke kazi anayo ndo mana katangaza kuoa.
 
Jamani kina dada/mama,mimi ni mwanaume mwenye umri wa miaka 42,NAITAJI MKE lakini jamani sina ajira/kazi yoyote ile,yule mwanamke ambae atarizia na atakaekubaliana na hali hii tafadhali naomba tuwasiliane kwa email address ifuatayo mnyella@ovi.com

Kama umesubiri hadi 42, vuta subira tu....utapata mke mwema lkn uwe pia na kipato kama kichwa cha nyumba. Kila la kheri.
 
Hivi kuoa lazima uwe na kazi au mapenzi yanatazama kama una kazi au huna? Hii inaonesha mtazamo wa watz wengi kuhusu maisha ukoje
 
Kazi ipo lol, sasa utaoaje na mahali unatoa wapi? khaa, kwani kazi mpk uajiriwe? si ujiajiri mwenyewe
 
Hii inawezekana tu kwa jamii ya wafugaji kama kule kwa ndugu zetu Wakurya mwanaume anaoa wanawake hata wanne na kila mwanamke anachacharika mwanaume kazi yake kukusanya mapato toka kwa kila mwanamke na kukaa na wanaume wenzake wanapiga story BUT hata hao wana kianzio hata ng'ombe mmoja kwa kila mke mwisho wa siku wake zake wanaleta mabadiliko

kazi nayozungumzia namaanisha ni shuhuli pevu atakayo pata baada ya kuoa na kukaa na uyo mwanamke under the same roof.
Imagine Nelson Mandela alikaa mika 27 jela bila wasiwasi ila baada ya kurudi kwa mkewe akaishi naye miezi kadhaa na kuamua kuvunja ndoa, sasa pata picha jinsi mke alivyokua ni kazi kubwa kuliko.
 
Mimi nikushauri ubadilishe hii thread " Natafuta kazi" ..... Ukishapata kazi automatically umepata pesa.... Ukipata pesa.. Women (wives) will chase you... proved!!!! .... Don't chase women, chase money automatically.... Umenipata!
 
Huenda ni ajira tu imegoma mambo mengine muhimu kwa maisha ya binadamu amekamilisha na isitoshe huenda alishafanya kazi kipindi cha nyuma hivyo mafao yake yapo NSSF yamezuiliwa na SSRA muda si mrefu atakua njema kama marekebisho ya sheria ya fao la kujitoa ikifanyika vinginevyo bado kidogo afike miaka 55 hivyo mke avumilie

hahaha mke mtarajiwa amsubirie afikishe miaka 55 kisa ilhali sisi tupo
 
Hivi kuoa lazima uwe na kazi au mapenzi yanatazama kama una kazi au huna? Hii inaonesha mtazamo wa watz wengi kuhusu maisha ukoje

mahali utapata wapi wewe?tena siku hizi naona zimepanda bei mahali hadi kilo 7,,sasa ukishindwa kuzitoa hizo unategemea nini sasa?labda kama wewe ni mtoto wa tajiri sawa baba ako atakulipia mahali
 
mahali utapata wapi wewe?tena siku hizi naona zimepanda bei mahali hadi kilo 7,,sasa ukishindwa kuzitoa hizo unategemea nini sasa?labda kama wewe ni mtoto wa tajiri sawa baba ako atakulipia mahali

Ukiwa mtoto wa tajiri hata kama huna kazi utasema ni mfanyabiashara japokuwa BRELA huna kumbukumbu kwani mdingi anatoa pocket money za kutosha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom