wakuu heshima mbele sana
kwa mnaojua,nisaidieni kunipatia vigezo ambavyo vinaweza kumfanya mtanzania kufanya kazi usalama wa taifa.mtaani nimesikia wakisema hizi kazi huwa unachaguliwa tangia ukiwa shule ya msingi au sekondari huwezi kujipeleka mwenyewe kuomba hizi kazi.je ni kweli?je ni kweli ni lazima upitie mafunzo ya kijeshi kabla ya kujiunga usalama wa taifa?
mimi napenda sana kufanya kazi na usalama wa taifa je siwezi kujiunga uko baada ya miaka 2 nikimaliza masomo yangu(nina miaka 28,nafanya masters sasa).
Mkuu p53 heshima mbele.
Kazi ya kukusanya taarifa za siri (intelligence gathering ni pana kidogo), hasa kwenye karne hii ambapo kuna mpaka kuangalia mitandao au "cyberspace"
Inategemea upo uraiani, jeshini, polisi, Ikulu au nje ya nchi lakini lengo ni moja kupata data ambazo zitatumika kupata ama faida juu ya mshindani wako kwenye maeneo kama uzalishaji viwandani, siasa, vita baina ya nchi na nchi na maeneo mengine.
Kuna maeneo mengi tu ambayo ofisa usalama anaweza kuajiriwa na akafanya kazi yake kulingana na elimu yake kama vile kutafsiri mawasiliano ambayo yanatumia lugha mbalimbali ama mitandaoni kwenye simu au internet.
Bila kueleza sana, idara za kijasusi zinapenda kuajiri watu wa kutoka rika zote na kabila mbalimbali ili kuleta uwiano kwenye suala zima la ajira kwa wananchi na pia kuhakikisha hawaonekani kuwa ni wabaguzi na wenye kutoa nafasi kwa upendeleo.
Sasa idara ya usalama Tanzania sifahamu imekalia vipi suala la ajira na muelekeo mzima wa kuwa na watu hata wa aina yako mkuu ambao wapo tayari kujitoa mhanga kutetea na kulinda nchi yao.
Nasema hivi kwasababu katika nchi zilizoendelea kwa mfano, idara za usalama hutoa matangazo katika magazeti, internet na hata kujipenyeza kwenye michezo ya video kwenye internet au online games kuchagua wanafunzi.
Kwakweli kwa sisi watanzania sifahamu wanapitia wapi ila nafikiri bado watakuwa wanatumia zile njia zao za asili ambazo ni shuleni, jeshini, vyuoni na pengine ukibahatika hata mitaani.
Ni kazi nzuri ukiwa mtaalam (specialist) hasa kwenye computer, hesabu, lugha (multilingual ) ambae unazungumza lugha nyingi na umahili mwingine kama wa James Bond.
Jitahidi kaka unaweza kupata.