NaamSwali: Hii leo kumeenea mialiko na fatwa zinazojuzisha kumuoa mwanamke mjamzito ambaye si mke wa mtu. Ni mamoja anayemuoa ni huyohuyo aliyempa ujauzito au mtu mwengine. Mambo haya yameenea na tunataraji kutoka kwako muheshimiwa utatuzi, kuwazindua watu juu ya ukhatari wake na ubainifu wa hukumu ya Shari´ah juu yake. Allaah akujaze kheri.
Jibu: Haijuzu kumuoa mjamzito mwenye ujauzito unaotokana na uzinzi au usiotokana na uzinzi mpaka kwanza atwahirike. Allaah (Ta´ala) amesema:
وَأُولَاتُ الْأَحْمَالِ أَجَلُهُنَّ أَن يَضَعْنَ حَمْلَهُنَّ
“Na wenye mimba muda wao [wa eda] watakapojifungua mimba zao.” (65:04)
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Yeyote anayemwamini Allaah na siku ya Mwisho basi asimwagilie maji juu ya mazao ya mwingine.
Bi maana manii yake.
“… mazao ya mwingine.
Bi maana ujauzito wa mwingine.
Ikiwa ujauzito huu ni wa mwanamke aliyeachika au ambaye amefiliwa, basi haijuzu kwake kumuoa mpaka kwanza ajifungue.
Ikiwa mimba hiyo inatokana na uzinzi, haifai vilevile kumuoa – si mwanamke huyu mzinzi wala mwenginewe – mpaka azae. Kwa sababu mimba hii ni yenye utata kwa tone la manii ambalo halinasibishwi si kwa yule mwanamme mzinzi wala mwengine. Mtoto huyo atanasibishwa kwa mama yake. Mtoto hanasibishwi kwa yule mwanamme mzinzi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mtoto ni wa kitanda na mzinzi anastahiki [kupigwa] jiwe.”
Mtoto ni wa mama akiwa ni wa nje ya ndoa na yule mwanamme mzinzi anastahiki kusimamishiwa adhabu ya ki-Shari´ah.
Mwanamke akishika ujauzito na bado hajaolewa basi haijuzu kumuoa kabisa katika nchi yoyote ile mpaka kwanza ajifungue. Akishajifungua basi itafaa kumuoa. Hayo yafanyike baada ya kutubia, kurejea na kutujia kwa Allaah. Basi hapo itafaa kwa muislamu kumuoa baada ya kutubia.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Nuur ´alaad-Darb
Watu manashangaza sana et bakwataHapa kwenye haya makundi ondoa shiya na ahmadia haya hayafai kabisa kwenye uisilamu na sio miongoni mwa waisilamu.
Ahl sunna na Salafi hawa ndio huitwa Wahabi kwq pmj.
Sufii ndio bakwata ambao ni waisilqmu pia ila kuna madhaifu yao lkn yanarekebishika na hayajawatoa kwenye uisilamu kwa maana mapungufu yao wengi ni kuzusha tu baadhi ya mambo kwenye dini kwa kukosa tu elimu
Mf suni na salafi anaweza kuswali nyuma ya sufi lkn si nyuma ya shia wala ahmadia
Naweza kuwa nimekosea kwenye uwasilishaji lakini maana ikawa imeeleweka ila kwa kuwa uko kwajili ya kubishna,basi utatafuta kasoro hata iwe ndgo ili kuendeleza ubishiNaam
Watu manashangaza sana et bakwata
Kwani bakwata ni dini? mpka useme sufi ndio bakwata haya hiyo bakwata ipo nchi ipi na ipi?
Sina nia ya kubishana na ww ni basi tu baadhi ya watu hili neno bakwata wanalitumia vibaya kana kwamba ni diniNaweza kuwa nimekosea kwenye uwasilishaji lakini maana ikawa imeeleweka ila kwa kuwa uko kwajili ya kubishna,basi utatafuta kasoro hata iwe ndgo ili kuendeleza ubishi
Karibu mkuuSina nia ya kubishana na ww ni basi tu baadhi ya watu hili neno bakwata wanalitumia vibaya kana kwamba ni dini
Anyway ninekuelewa sana ila naomba nikuulizr kitu
Kuna jamaa anajiita busu la kenge huyu kwa mujibu wa ma bandiko yake ni shiyah au ahmadiyah?Karibu mkuu
Kwa mujibu wa mabandiko yake ni shiaKuna jamaa anajiita busu la kenge huyu kwa mujibu wa ma bandiko yake ni shiyah au ahmadiyah?
SawaKwa mujibu wa mabandiko yake ni shia
Kwa hiyo mrs none nisubir had liniSawa
Hadi nijufungueKwa hiyo mrs none nisubir had lini
Lkn now umeipinga nguvu hoja ya ndoa baada ya kujifunguaHadi nijufungue
S umenifahamisha nimeelewa haiswihiLkn now umeipinga nguvu hoja ya ndoa baada ya kujifungua
Manhaj Salaf ni njia, misingi, na mwenendo wa kufahamu, kuamini, na kutenda mambo ya dini ya Kiislamu kwa kufuata mwendo wa Salafus-Saalih — yaani Waislamu wa mwanzo waliokuwa na uelewa sahihi wa dini:Unaijua Manhaj Salaf?
Sawa tutayajengaS umenifahamisha nimeelewa haiswhi
InshallahSawa tutayajenga
Huyo mkaldayo ni mkristo wala hakuna shia wala ahmadiyah pale.Kuna jamaa anajiita busu la kenge huyu kwa mujibu wa ma bandiko yake ni shiyah au ahmadiyah?
Hahaah mnanifurahisha mjue.Kwa hiyo mrs none nisubir had lini
Nilitaka nikuite, njia ipo wazi😅😅Pole sana watakuja
Mmh kweli? Kivip?Huyo mkaldayo ni mkristo wala hakuna shia wala ahmadiyah pale.