Nasubiri mshahara wa Octoba 2017

Nasubiri mshahara wa Octoba 2017

Ukitaka hata mbwa wako akuheshimu basi wewe mlishe vizuri tu hakika kila utakalomwambia atafanya ila ukimlaza njaa usishangae akihamia kwa jirani au akawa anashinda dampo,ni upuuzi kutimiza wajibu wakati muajiri hatimizi majukumu yake.
mutual responsibilities
 
HAhaahaaa Njoo Kamanda...,Saiv Nipo napata mbuzi choma na Windhoek baridi kusuuza koo
Hahhaha Best................. hiyo kata kiu yako inaniongezea hasira tu usawa huu............ kwanza ni haja ndogo ya mende wala si maji ya dhahabu (Maneno ya mkosaji mwe Kaka Magu hebu legeza kidogo bana😀😀😀)
 
Wanabodi, kwa kuwa mshahara wa mwezi Septemba ulitoka tarehe 22 ya mwezi huo, na pia kwa kuwa mwezi uliotangulia mshahara ulitoka tarehe hizo hizo, maana yake mwisho wa mwezi sasa ni tarehe 22, yaani ukifika tarehe 22 ni tayari mwezi umekamilika tokea mshahara uliotangulia.

Kwa kuwa mpaka sasa hivi niandikapo, tarehe 24 Oktoba, mshahara wa mwezi Oktoba haujatoka bado (labda kwa wanajeshi na wengine wateule), maana yake ni tayari siku 32 tokea mshahara uliopita. kwa hiyo kimsingi leo ni tarehe 02 Novemba 2017 kwa hesabu za kimshahara, kwa kuwa siku 30 zilikamilika toka majuzi, na mwezi huu una siku 31. kwa hesabu hizo, mshahara tayari umechelewa. sasa hii ni mara ya kwanza tokea Awamu hii imeingia madarakani, mshahara kuchelewa. kwa kweli tokea enzi za unaibu waziri wa fedha wa Mwigulu Nchemba, sekta ya mishahara iliimarishwa. Sasa tujadili, kabla hatujasikia sababu "sahihi" kutoka Serikalini.

Inawezekana sababu ikawa ni kutokana na mahesabu ya nyongeza za mishahara za wale wafanyakazi 59,000+ ambao tuliambiwa mishahara yao itapanda kutokana na kupandishwa madaraja nk. kwa hiyo katika kuyakokotoa, inachukua muda wa ziada. na kwa kuzingatia kuwa serikali hii haielekei kutoa malipo ya ziada kwa wahasibu watakaolazimika kufanya kazi za ziada kuweka mambo sawa, ni wazi kazi itachukua muda mrefu kwa kufanywa katika muda wa kawaida wa kazi. Lakini pia hiyo isingekuwa tatizo kama jambo hili lingefanyiwa kazi kwa utaratibu wa kawaida, sema tu zile tambo za serikali, maana Rais alijikanyaga, mwanzo kasema haongezi mishahara, baada ya kusikia watu wanachambua kauli hiyo, na kuhoji kama alimaanisha nini wakati kwenye kampeni aliahidi kuboresha mishahara, ikabidi atoe kauli hii ya kupandisha madaraja "mwezi huu huu wa oktoba". kwa hiyo hata kama serikali haikuwa imejipanga kulitekeleza hilo kwa mwezi huu, itabidi litekelezwe kwa udi na uvumba ili alichoahidi mkuu kitimie. maana kama ni kuchelewa serikali ilishachelewa sana tu. hii ni ahadi ya tokea mwezi Julai mwaka jana. sasa kuna haraka gani ya kufanya mwezi huu huu?

Lakini pia inawezekana Zitto yuko sahihi kwamba mambo siyo shwari. maana haiwezekani tuone TRA wameacha kutoa takwimu, BoT nao wanasitisha kutoa takwimu. halafu visingizio vinatolewa. halafu mshahara unachelewa. hapo inawezekana kuna harufu ya mzoga ambao unafichwa sana, na kupigwa pafyumu.

Ukiangalia Press Conference ya Mbowe kuhusu Uchumi, na data anazotumia Zitto Kabwe kujenga hoja zake, wote wanatumia data za serikali. na ndio maana hoja zao zinakuwa kali sana. Njia pekee ni JPM aagize tu kwamba marufuku kutoa data sasa hivi, au data ziwe zinaandaliwa na kitengo maalum cha data, na siyo idara ya Takwimu wala BoT wala TRA. wachukuliwe vijana wazuri wapewe kompyuta na watapika kila kitu na kupakua. shida itabaki mifukoni, kwenye ajira, na uhalisia wa kiuchumi utakuwa unaongea lugha tofauti. lakini angalau serikali itajificha hapo ambapo watu hawataweza kutumia data za serikali kuikaanga serikali hiyo hiyo.

Vinginevyo, Rais JPM hajajibu kabisa hoja za Zitto Kabwe kuhusu uchumi, ila kamtisha tu. kazi kwa IGP. atatumia kifungu gani, uchochezi? Kama ni hivyo, basi hata mimi nisemaye kwamba mishahara imechelewa, ni mchochezi!
 
Kama uko CRDB au kwingine, vumilia. wale NMB hoyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Back
Top Bottom