Nasita kuikubali hii ofa ya Mwananchi Communications!

tang'ana

JF-Expert Member
Apr 3, 2015
11,814
15,105
Wadau,
Nipo mahali ambapo gross salary yangu ni 1.1 milion, hawa Mwananchi wamenipa ofa kubwa kidogo ya gross 1.52 milion lakini kituo cha kazi kitakua Dodoma.

Sasa hivi niko Arusha na maisha ya Arusha nimeyazoea sana as napata kila kitu ninachohtaji kwa bei nafuu. Naona kama Dodoma maisha yataniwia vigumu kidogo.

Je nikubali hyo ofa au niipotezee?
 
Wadau,nipo mahali ambapo gross salary yangu ni 1.1 milion,hawa mwananchi wamenipa ofa kubwa kidogo ya gross 1.52 milion lakini kituo cha kazi kitakua dodoma.sasa hvi niko arusha na maisha ya arusha nimeyazoea sana as napata kila kitu ninachohtaji kwa bei nafuu.naona kama dodoma maisha yataniwia vigumu kidogo.je nikubali hyo ofa au niipotezee?
kukubali ofa mpya inabidi uangalie vitu vingi na sio tu mshahara.
 
Wadau,nipo mahali ambapo gross salary yangu ni 1.1 milion,hawa mwananchi wamenipa ofa kubwa kidogo ya gross 1.52 milion lakini kituo cha kazi kitakua dodoma.sasa hvi niko arusha na maisha ya arusha nimeyazoea sana as napata kila kitu ninachohtaji kwa bei nafuu.naona kama dodoma maisha yataniwia vigumu kidogo.je nikubali hyo ofa au niipotezee?
Kwani kwenye maisha yako wewe nini ni priority? Pesa au furaha? Ukiweza kujijibu hili wala uwezi kuomba ushauri kwa jambo dogo kama hili.
 
Uliomba ulitegemea mshahara mkubwa? au ni kazi ulikuwa unaipenda kuifanya?.. kama unapenda kazi nenda ukapate experience mpya na ubadili mazingira. Hata na hivo gross ya 1.5 sio mbaya mkuu ukiondoa tax na makato mengine bado itakuwa above 1.1
 
Haiwezi kubaki hela hyo mkuu
 
Usije ukahama Chugga Jombii.
Hiyo tofauti ya mshahara ni ndogo sana kukufanya uhame mahali poa kama Arusha.
 
Njoo PM nikushauri nimewahi kupita hapo, hapa wanaweza kusema ni majungu
 
Kwani kwenye maisha yako wewe nini ni priority? Pesa au furaha? Ukiweza kujijibu hili wala uwezi kuomba ushauri kwa jambo dogo kama hili.
Daaah we kijana wewe yaani unakubali kazi mpya kwa adition ya laki nne tena wanakutoa kwenye comfort zone yako aise aaa wapi usiende Dodoma huko, huko waachie wenye chama na serikali
 
Unaweza ukalipwa mshahara mkubwa ila ndio unakuwa wa kunasubiri mwisho wa mwezi tu.

Na unaweza ukawa unalipwa pesa ndogo ila karibu kila siku unakuwa unapata michongo ya pesa. Mwisho wa siju unakuwa unatengeneza pesa za kutosha kuliko mwenye mshahara mkubwa.
 
Back
Top Bottom