Nasisitiza; Binti usizae kabla hajakuoa(Epuka kuwa single Mother)

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,341
51,907
NASISITIZA; BINTI USIZAE KABLA HAJAKUOA "EPUKA KUWA SINGLE MOTHER"

Na, Robert Heriel

Elewa kuwa jukumu la kubeba mimba Kwa mwanamke ambaye hajaolewa ni lake mwenyewe sio la mwanaume.

Sisi wanaume hatuna muda wa kuwaza mambo ya mimba ambayo hayatuhusu Kwa watu ambao hatujawaoa.
Ndio maana hata nyumbani wazazi huwezi sikia akimuambia mtoto wa kiume kuwa ajizuie asitie mimba mabinti za watu Bali wazazi huwachunga mabinti zao wasije kupewa Mimba.

Hata Malaika alivyoleta ujumbe wa kuzaliwa Kwa Kristo Yesu alimfuata moja Kwa moja Bikra Mariam Kwa sababu Hakuwa ameolewa Bali alikuwa mchumba wa Mtu. Hivyo jukumu la mimba halikuwa juu ya Yusufu(mchumba wa Mariam) bali lilikuwa jukumu la Bikra Mariam.

Hii ni tofauti na Malaika waliokuja kutoa ujumbe wa kuzaliwa Kwa Isack, walimfikishia moja Kwa moja Ibrahimu mumewe Sarah Kwa sababu tayari kulikuwa na ndoa baina yao. Hivyo mwenye wajibu na jukumu la masuala ya mimba ndani ya ndoa ni Mwanaume.

Binti yangu, jiepushe na ngono zembe, haijawahi tokea tangu dunia kuumbwa ngono zembe ikawa sifa Kwa Mwanamke. Hii ni tofauti na Sisi wanaume, Sisi wanaume hatuna kitu kinaitwa ngono zembe. Bali yunakitu inaitwa Urijali na ushababi. Historia na Asili ya ulimwengu inaeleza hivyo.

Taikon kuwa na majike kumi kwangu ni sifa na wala sio tatizo,
Taikon kuwa na Watoto katika wanawake tofautitofauti hiyo kwangu sio tatizo Kwa sababu Mimi ni Mwanaume.
Hiyo iko hivyo Daima na itadumu hivyo.

Binti yangu, Kama amri hiyo ya kuacha ngono zembe itakushinda basi kuwa na akili hata kidogo basi, usibebe mimba kabla hajakuoa. Kuna hatari kubwa ya kuwa single mother endapo utazaa kabla hajakuoa. Niamini Mimi, usisome Kwa mihemko ukadhani nakukandia, au labda nakuchukia.
Mimi ni Mwanaume najua vile wanaume tulivyo.

Elewa kuwa ukishashika mimba akili ya mwanaume hugeuka na kuwaza mambo mengi hasa kama alikuwa hakupendi.

Wakati wewe upendo ukizidi kutokana na tayari huna option Kwa sababu unamimba, mwenzako anafikiria namna ya kukuacha alafu anaweza majukumu ya kukuhudumia wewe na mtoto. Hapo Kama ndio uchumi wake ni wakuungaunga ndio Kabisa umekwisha.

Elewa kuwa unapobeba mimba alafu alikuficha kuwa anamtu wake, elewa kuwa ndio anakuona Kama huna akili na umekuja kuyavuruga maisha yake na Mpenzi wake ampendaye, hapo ndio anaweza kukuambia umejichukulia maamuzi ya kujibebesha mimba bila ya kumshirikisha.

Na kamwe usijemuambia mambo ya kwamba Kama alikuwa hataki mtoto angetumia kondomu au angetoa nje, hapo ndio atakuona wewe ni popoma wa mwisho Kabisa. Jukumu la mimba sio lake, jukumu la mimba ni lako wewe mwenyewe.

Kama angekuwa amekuoa automatically wanaume tulivyo lazima angekuwa anafuatilia hizo ishu za siku zako kwani anamipango na wewe ya muda mrefu.

Binti yangu, ukiwa single mother elewa unajipa mzigo mzito sio wewe tuu Bali hata mtoto utakayemzaa.
Elewa kuwa wewe ni mwanamke mzuri ambaye unatakiwa uwe unafikiriwa na Mwanaume muda wote, sasa unapozaa na mtu ambaye hajakuoa na hakupendi elewa kuwa Mwanaume huyo hajawahi na hatawahi kuja kukufikiria, ndio maana single mother ndio mnaowapigia simu Wanaume. Nadra Sana mwanaume kukupigia simu kujua hata hali ya mtoto.

Hii ni Kwa sababu mwanaume haoni umuhimu wako licha ya kuwa ulimzalia Mtoto. Ninachokuambia ni ukweli Kabisa.

Tena atakuona msumbufu katika maisha yake ndio maana ninakuambia Epuka kuwa single mother ili uepuke kuwa msumbufu Kwa watu wengine.

Binti yangu, ukiwa single mother mwanaume atakayekuoa muda wote atakuwa na pressure, hatakuwa anakuamini licha ya kuwa atajitahidi kuonyesha anakuamini(Kama atakuwa na busara)
Yaani utampa msalaba mwanaume mwingine mzigo mzito ambao hataweza kuubeba.

Binti yangu, elewa kuwa utakapokuwa single mother, mwanaume atakayekuoa atakuwa anadharauliwa mpaka na Mama yake aliyemzaa na ndugu zake kisa kuwa na wewe. Just imagine, unaweza kupuuzia Kwa sababu kila mwamba Ngoma huvutia kwake, hivyo wewe utaangalia maslahi yako na sio maslahi ya mwanaume aliyekuoa.

Nataka nikuambie kuwa ukiwa single mother mwanaume atakayejitokeza kukuoa yeye mwenyewe kuna wakati akikaa pekeake anaingia katika uhasama wa kinafsia na kuona alifanya makosa au hakutumia akili kukuchagua wewe.

Nataka nikuambie ukiwa single mother, migogoro yenu mingi ndani ya ndoa itakuwa sababu ya u-single mother wako aidha kuhusu mtoto au kuhusu mzazi mwenza.

Kwani utampa mwanaume huyo mzigo usiowake wa Kulea na kumtunza Mtoto asiye damu yake. Na asipofanya hivyo ninakuhakikishia wewe kama mama huwezi kukubali utamuona hafai na hakupendi.
Ndio maana nikakuambia Epuka kuwa single mother.

Binti yangu, elewa kuwa kila binadamu ni mbinafsi, na ubinafsi ndio ubinadamu wenyewe. Mwanaume atakayekuoa hatataka mtoto wa mwanaume mwingine awazidi watoto wake kimaarifa au Kwa sifa yoyote njema.

Binti yangu, elewa kuwa wanaume wanaolala na watoto wao Asilimia kubwa hulala na watoto wakufikia, yaani hapo Baba amekula kuku na mayai yake.

Binti yangu bado hujanielewa au unataka nisikilize mihemko yako.

NINI CHAKUFANYA ENDAPO UTAJIKUTA KATIKA HALI YA U-SINGLE MOTHER

1. Usikubali kuolewa na kijana Mdogo ambaye hajawahi kuwa na Familia.
2. Hakikisha unakuwa Stable kiuchumi ili usimpe mzigo huyo mwanaume aliyeamua kuunda familia na wewe licha ya usingle mother wako.

3. Mtoto/watoto wako wasiishi kwenye nyumba ya huyo mwanaume aliyekuoa. Sio salama na haiwezi kuwa nzuri Kwa furaha ya Mapenzi yenu.
Wapeleke Kwa Bibi au Kwa Baba Yao.

4. Olewa na Mwanaume mkubwa ambaye tayari alikuwa na familia. Itapendeza akiwa mjane.

5. Usikubali kuolewa na Mwanaume ambaye anandoa ambayo iko hai. Kamwe usivuruge familia za watu. Haiwezi kukusaidia.

Kama utaweza unaweza kumfuata mke mwenzako mkazungumza kuwa unataka uwe mke mwenzake, Kama akikataa basi achana nao. Yaani mtongoze mke mwenza.

6. Kubali wewe ndiye mwenye makosa Kwa kushindwa kufanya uchaguzi sahihi, na sio kumlaumu muda wote aliyekuzalisha. Elewa kuwa Upendo sio lazima. Kama alikudanganya ni Sawa lakini nawe ulikubali kudanganywa hivyo wote mnamakosa.

7. Usikubali kuzaa zaidi ya Mababa wawili. Yaani usifanye makosa zaidi ya mara mbili. Utaonekana ulikuwa hamnazo. Au unalaana kama sio mikosi.

8. Usiolewe na Mwanaume asiye na akili za kutosha kwani tayari ukishazalishwa na kuachwa unakuwa na akili mara mbili ya zile ulizokuwa nazo. Hivyo unahitaji mwanaume mwenye akili za kutosha ku-deal sio tuu na Dunia Bali pamoja na wanawake. Yaani awe anajua Woman Psychology

9. Usiache kuomba toba mara Kwa mara na kuondoa huo mkosi wa u-single mother usiwakute watoto watakaotoka katika tumbo lako na tumbo la mabinti zako.

Hata kama utafanikiwa kuishi maisha ya furaha na Mumeo mpya elewa kuwa hiyo ni bahati yako tuu kwani wengi WA Aina yako wanateseka, hivyo ni vizuri kumuomba Mungu aondoe huo mkosi wa u-single mother.

10. Wape watoto wako wakiume Wosia wasioe single mother hata kama wewe ulikuwa single mother. Wape na sababu ya vile ulivyokuwa unajihisi na usiwadanganye Kwa kutaka wawaonee huruma.

Hata hivyo wasisitize kuwa wasiwatie mimba mabinti za watu ili kuepuka kuwafanya masingle mother. Ingawaje wajulishe kuwa wapo wanawake wanaweza kujibebesha mimba Kwa makusudi. Hivyo Kama itatokea wasiwaoe kama hawawapendi, yaani wasiowaoe Kwa sababu ya huruma

Kufikia hapo sina la ziada.
Ni Yule Baba yenu, masalia wa Wazee wakale.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Kama binti ana kazi na anaweza kumlea mtoto wake mwenyewe asizae asubirie kuja kuolewa anaweza akazekea nyumbani.

Vijana wa siku hizi hawa ambao role model wao ni akina Diamond na Harmonize? wapenda Singeli ndio waje kuoa?

Kila mtu aishi anavyotaka ili mradi asiwe kikwazo kwa wengine
 
Kuwa single mother hauna pesa ni mtihani Sana ,

Elimu ya darasani huna
Elimu ya Maisha huna
Pesa huna
Kazi au Biashara iloyosimama huna

Sasa hapo ukijichanganya ukawa single mother tegemea dharau kutoka Pembe zote za dunia


Single Mothers wapewe moyo na kutiwa Faraja life goes on
 
Kuwa single mother hauna pesa ni mtihani Sana ,

Elimu ya darasani huna
Elimu ya Maisha huna
Pesa huna
Kazi au Biashara iloyosimama huna

Sasa hapo ukijichanganya ukawa single mother tegemea dharau kutoka Pembe zote za dunia


Single Mothers wapewe moyo na kutiwa Faraja life goes on

Sisi Kama wazazi wa kizazi hiki ni jukumu letu kuiunda jamii Bora Kwa kuhakikisha Wana na binti zetu tunawajengea misingi mizuri sio tuu ya kielimu na kiuchumi Bali pia misingi ya kimaadili ya kimahusiano
 
Kama binti ana kazi na anaweza kumlea mtoto wake mwenyewe asizae asubirie kuja kuolewa anaweza akazekea nyumbani
Vijana wa siku hizi hawa ambao role model wao ni akina Diamond na Harmonize? wapenda Singeli ndio waje kuoa?

Kila mtu aishi anavyotaka ili mradi asiwe kikwazo kwa wengine

Kwani anaharaka Gani?
Haraka ni yashetani Mkuu.
Mwendokasi unaua.
Mwenye subira yuna Mungu.

Mnaowaharakisha dada zetu ndio mnawaingiza kwenye matatizo.

Unafikiri maishani kuwa na kazi pekeake.
Kuna kufukuzwa kazi, kuna kupata matatizo,

Kanuni za Asili ni zilezile hazibadiliki,
 
wanaume nao watunze magobore yao hadi hapo watakapofikia wakati wa kuoa .. wako ndoani ndo watumie risasi zotee kwa mwanamke wa ndoa na si vinginevyoo haaaa
 
pigia Mbuzi gitaa
FB_IMG_1661784196480.jpg
 
Kwani anaharaka Gani?
Haraka ni yashetani Mkuu.
Mwendokasi unaua.
Mwenye subira yuna Mungu.

Mnaowaharakisha dada zetu ndio mnawaingiza kwenye matatizo.

Unafikiri maishani kuwa na kazi pekeake.
Kuna kufukuzwa kazi, kuna kupata matatizo,

Kanuni za Asili ni zilezile hazibadiliki,
Ni mwili wake mwenyewe na kama anaweza kumtunza mwenyewe hana deni na mtu akiamua kuzaa na anayemtaka..hii ni 2022 sio 1960
 
Kama binti ana kazi na anaweza kumlea mtoto wake mwenyewe asizae asubirie kuja kuolewa anaweza akazekea nyumbani
Vijana wa siku hizi hawa ambao role model wao ni akina Diamond na Harmonize? wapenda Singeli ndio waje kuoa?

Kila mtu aishi anavyotaka ili mradi asiwe kikwazo kwa wengine
Hatukukatazi uishi unavyotaka lakini kumbuka unawajibika kwa jamii unayoishi. Hivi unafikiri chanzo cha hawa panya road ni nini kama siyo family failures?
 
Hatukukatazi uishi unavyotaka lakini kumbuka unawajibika kwa jamii unayoishi. Hivi unafikiri chanzo cha hawa panya road ni nini kama siyo family failures?
Family failures inaletwa na single mother pekee? Failures zinaletwa na wazazi irresponsible, wanaume na wanawake
Ndio maana nikasema kama mwanamke anajiweza kiuchumi na anaweza kumtunza mwanae yupo huru kuzaa...kuna familia ya single mother zinafanya vizuri kuliko za wazazi wawili
 
Back
Top Bottom