Nasikia Malalamiko Kanda ya ziwa

Nasikia Malalamiko Kanda ya ziwa

GreatThinkers,
Kama siyo wewe nani?

Kama siyo leo lini?

Ni sisi
Wake up kanda ya ziwa.
Mali ya madini yenu yote inajenga Int. Airport Bagamoyo na Kigamboni New City
 
Kweli kazi iko....poleni wana sisiemu wa mwanza ambao bado mpo usingizini japo mnaamshwa alakini bado tu......
 
GreatThinkers,

Naskia kuna malalamiko kuwa Kanda ya ziwa licha ya kuwa Migodi yote ya Dhahabu iko kule hakuna hata international airport, Mwanza airport ni kama shule ya kata ni kweli?

Nasikia kuna Malalmiko Rocky City Mwanza, Kikwete hadi December 2011 hajaleta hata Sh. kumi ya ruzuku ktk Jiji wakati hadi leo alitakiwa awe ameshatoa 40Bilioni ili kuwakomoa kwa kuwapiga chini ktk Uchaguzi ni kweli?

Naskia kuna malalamiko kanda ya ziwa kuwa licha ya kuwa na watu 16mil kati ya 45mil Tz, Katiba imejadiliwa Dodoma, Dar na Zanzibar, hawataki kabisa kuwashirikisha kisha wanataka CCM muwapiguie kura, ni kweli?

Naskia Kuna malalamiko kuwa kanda ya ziwa licha ya kuwa asilimia hamsini ya wasomi wote tanzania wanatoka kule hakuna hata chuo kikuu hata kimoja cha serikali ni kweli?

Naskia kuna malalamiko kuwa kanda ya ziwa licha ya kuwa na madini yanayoweza zalisha Cement yako pale Shinyanga hakuna hata mpango wa kujenga kiwanda licha ya kuwa 2005 mliahidiwa ni kweli?

Naskia kuna malalamiko kuwa kanda ya ziwa mkoa mpya wa Simiyu umeomba ile barabara inayopita serengeti mmeomba ipitie Lamadi, bariadi kuja Hydom na kuunga Babati naskia wamekataa ni kweli?

Naskia kuna malalamiko kuwa kanda ya ziwa kuna hakuna viwanda licha ya kuwa mna bidhaa nyingi lakini vinajengwa vyote pwani eti msafiri mkaombe vibarua Kibaha na bagamoyo ni kweli?

Nasikia kuna malalamiko kanda ya ziwa kuwa ili bandari ya nchi kavu Isaka-Shinyanga vijijini nayo imekufa ili kuimalisha ajira ya pwani na kuanzisha bandari mpya ya nchi kavu Chalinze ni kweli?

Naskia kuna malalamiko kuwa wilaya nyingi za zamani kama Musoma vijijini,Shinyanga Vijijini hazina hata makao makuu lakini baadhi ya zilizoteuliwa juzi juzi tuu zimejengwa vizuri ile mbaya ni kweli?

Sasa kama ni kweli mnangoja nini- Hameni wote Si Si EM inaonekana wanachumia kwenu halafu wanawekeza kule Chalinze

Duh! hata mimi nasikia malalamiko kwamba Mwanza Airport ilikua ijengwe kwa kiwango cha kimataifa ila Mh. mmoja ambaye hivi karibuni amerejea toka India akachakachua funds zikaenda kujenga Songwe Airport! nasikia malalamiko......
 
GreatThinkers,

Naskia kuna malalamiko kuwa Kanda ya ziwa licha ya kuwa Migodi yote ya Dhahabu iko kule hakuna hata international airport, Mwanza airport ni kama shule ya kata ni kweli?

Nasikia kuna Malalmiko Rocky City Mwanza, Kikwete hadi December 2011 hajaleta hata Sh. kumi ya ruzuku ktk Jiji wakati hadi leo alitakiwa awe ameshatoa 40Bilioni ili kuwakomoa kwa kuwapiga chini ktk Uchaguzi ni kweli?

Naskia kuna malalamiko kanda ya ziwa kuwa licha ya kuwa na watu 16mil kati ya 45mil Tz, Katiba imejadiliwa Dodoma, Dar na Zanzibar, hawataki kabisa kuwashirikisha kisha wanataka CCM muwapiguie kura, ni kweli?

Naskia Kuna malalamiko kuwa kanda ya ziwa licha ya kuwa asilimia hamsini ya wasomi wote tanzania wanatoka kule hakuna hata chuo kikuu hata kimoja cha serikali ni kweli?

Naskia kuna malalamiko kuwa kanda ya ziwa licha ya kuwa na madini yanayoweza zalisha Cement yako pale Shinyanga hakuna hata mpango wa kujenga kiwanda licha ya kuwa 2005 mliahidiwa ni kweli?

Naskia kuna malalamiko kuwa kanda ya ziwa mkoa mpya wa Simiyu umeomba ile barabara inayopita serengeti mmeomba ipitie Lamadi, bariadi kuja Hydom na kuunga Babati naskia wamekataa ni kweli?

Naskia kuna malalamiko kuwa kanda ya ziwa kuna hakuna viwanda licha ya kuwa mna bidhaa nyingi lakini vinajengwa vyote pwani eti msafiri mkaombe vibarua Kibaha na bagamoyo ni kweli?

Nasikia kuna malalamiko kanda ya ziwa kuwa ili bandari ya nchi kavu Isaka-Shinyanga vijijini nayo imekufa ili kuimalisha ajira ya pwani na kuanzisha bandari mpya ya nchi kavu Chalinze ni kweli?

Naskia kuna malalamiko kuwa wilaya nyingi za zamani kama Musoma vijijini,Shinyanga Vijijini hazina hata makao makuu lakini baadhi ya zilizoteuliwa juzi juzi tuu zimejengwa vizuri ile mbaya ni kweli?

Sasa kama ni kweli mnangoja nini- Hameni wote Si Si EM inaonekana wanachumia kwenu halafu wanawekeza kule Chalinze

Inauma sana.Ila ccm ndiyo nitolee huku.haturudi nyuma kamweeeee
 
mi mzaliwa wa kanda ya ziwa na ni mkazi wa mwanza, kiukweli ulichoandika hakina uongo yote ni kweli kabisa, inauma sana but ndo mwisho wa ccm uku, chuki waliyonayo wakazi wa kanda ya ziwa juu ya huu utapeli wa ****** na jopo lake umeongezeka mara mbili za ilivyokuwa wakati wa uchaguzi wa mwaka jana, u just wait n c, kama 2015 kutakuwa na mdudu anaitwa ccm kanda ya ziwa.
 
hata mbunge wa kahama mhe.LEMBELI alishawambia CCM kuwa wasipokua makini 2015 majimbo yote ya mkoa wa shinyanga yataenda upinzani.....
 
Nasikia malalamiko kanda ya ziwa eti watu wanakula mapanki aka mabaki ya samaki huku minofu inasafirishwa kwenda Ulaya.
 
hapa tu huwa ndipo ninapochoka na wale wanaompigia chapuo Mwandosya.....huyu alipeleka uwanja wa ndege wa maana nyumbani kwao Mbeya mpaka leo najiuliza ni kwa nini na sipati sababu.Mwanza mbali ya kuwa na madini kama ilivyotajwa hapo juu kuna samaki ambao wanakuwa exported kupitia uwanja huo na bado pia ni base ya ndege za UN kwa ukanda wetu wa maziwqa achilia mbali kuwa kiungo na nchi zote za hapa jirani..... ninapata hasira hata kuandika tena siwezi
 
Na Chuo cha madini kiko Moshi
Monday, 27 September
Na Kizitto Noya

SEKTA ya madini ni miongoni mwa sekta chache zinazokua kwa kasi nchini. Lakini kwa muda mrefu baadhi ya wafanyakazi migodini, wamekuwa wakifanya kazi bila utalaamu wala mikataba maalumu ya ajira.

Tatizo hilo limeifanya serikali kwa kushirikiana na wadau wengine wa sekta ya madini nchini kuanzisha mradi wa kuwaandaa watalaamu wa kufanya kazi migodini unaojulikana kama Integrated Mining Technical Training Project, (IMTT).

Wazo la kuanzisha mradi huo wenye lengo la kuwapata mafundi sanifu, lilianza mwaka 2008 baada ya wadau kubaini hasara kubwa waliyokuwa wakiipata baada ya kuajiri watu wasiokuwa na sifa migodini.


Serikali, Kituo cha Nishati na Madini (TCME), African Barrick Gold (ABG), ambayo zamani ilikuwa ikijulikana
kama Barrick na Aglo Ashanti
, ndio walikuwa wadau wa kwanza kufikiri na kukubali kuchangia mradi huo.

Wakati serikali ikichangia mradi huo kwa kutoa chuo cha VETA Moshi, kitumike
kama
kituo cha mafunzo, AGB na Anglo Ashanti wamechanga fedha kwa ajili ya uwekezaji wa awali katika mradi huo.

Meneja Uhusiano wa ABG Teweli Teweli, anasema kabla ya mradi huo, migodi ilikuwa ikiajiri watu na kuwapa mafunzo wakiwa kazini, jambo ambalo sio tu lilikuwa likiwaletea hasara, bali pia lilipoteza muda mwingi wa uzalishaji.

"Utaratibu huo ulionekana kupoteza hela na muda kabla kampuni haijaanza kunufaika na mfanyakazi. Hivyo wadau wakaamua kuchanga fedha kwa ajili ya kuanzisha mradi huo ili kuwaandaa watalaamu.

"Tunaamini IMTT itasaidia kupunguza gharama hiyo kwa kiasi kikubwa,"anasema Teweli na kubainisha kuwa wakufunzi wa mafunzo hayo wanatoka nchini Afrika Kusini.


Mratibu wa mafunzo katika mradi huo, Yan Kleinhans anataja baadhi ya masomo yanayofundishwa chuoni hapo kuwa ni ufundi mitambo, uchomeaji vyuma, ufundi wa magari makubwa, umeme wa viwandani, umeme mdogo na umeme wa magari.

Anasema mafunzo hayo yanatolewa kwa muda wa miaka mitatu na mhitimu ambaye anapata cheti cha kimataifa cha ufundi sanifu, anaweza kufanya kazi migodini katika nchi yoyote duniani.



Kwa mujibu wa Kleinhans baadhi ya kampuni na migodi inayofatoa ufadhili kwa wanachuo hao ni African Barrick Gold (ABG), Mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM), Sandvick Mining, Pan African, mgodi wa dhahabu wa North Mara na African Mining Service.


Anaeleza kuwa nchini
Tanzania
mradi huo umeanza katika kipindi muafaka kwani nchi nyingi duniani zimekuwa zikihangaika kutafuta watalaamu wa ufundi sanifu na kuwalipa fedha nyingi.

Hata hivyo Kleinhans anasema katika kuuendesha mradi huo, anakumbana na changamoto nyingi lakini kubwa ni kubadilisha fikra za wakufunzi wazalendo ambao wengi wao wanachukuliwa kutoka vyuo vya Veta.


"Nimekuwa pia nikikabiliana na changamoto ya walimu kuwawekea alama za ufaulu wanafunzi wakati uwezo wao ni mdogo. Wanafunzi wengi pia wana uelewa mdogo wa lugha ya Kiingereza ambayo ndio inayotumika kufundishia."anasema.

Mmoja wa wakufunzi wa chuo hicho, Michael Kimambo anaeleza changamoto wanazokumbana nazo wakufunzi kuwa ni pamoja na mishahara isiyoendana na ugumu wa kazi
yao
.

"Mimi nimeingia kwenye mradi wa IMTT nikitokea VETA. Nilichogundua ni kwamba nimeongezewa majukumu lakini mshahara haujabadilika," anasema na kubainisha kuwa sasa analazimika kufika kazini saa 12 asubuhi na kuondoka saa 12 jioni badala ya saa moja asubuhi na saa tisa na nusu jioni.

Mkufunzi mwingine Hassan Mhavile anasema, kazi ni ngumu na malipo ni kidogo. "Hali hii haitii moyo,"anasema na kuongeza kuwa amefanya kazi na VETA kwa takriban miaka 30 sasa, lakini majukumu aliyonayo sasa ni tofauti na magumu zaidi kuliko alivyokuwa VETA

"Mimi nimefika hapa nikitokea Morogoro, kazi ni nzuri lakini malipo hayaridhishi. Hapa ninabanwa na majukumu muda wote," anaeleza.

Henry Peter naye analalamikia kipato akisema ni kidogo na hakidhi mahitaji hivyo kuitaka serikali na wadau walioanzishwa mradi huo kuwafikiria zaidi.

"Kazi kama unavyoiona, ni nzuri na tunaendelea vizuri lakini tunaomba watufikirie kidogo maana hali ya kipato sio nzuri,"anaeleza Peter.

Anasema mbali na kuongeza watalaamu, sababu nyingine ya kuanzishwa mradi huo ni kupunguza majeruhi wanaopatikana kutokana na kazi za migodini.

"Mafunzo haya ni kwa ajili ya kuongeza uzalishaji lakini usalama kazini ni jambo la muhimu zaidi. Tumelenga kupunguza majeruhi watokanao na kazi za migodini,' anasema.


Mwanachuo, Yasin Msangi anaitaka serikali kukiendeleza chuo hicho kwa vifaa na wakufunzi ili mradi huo uwe endelevu na uweze kulisaidia taifa.

"Kwa mafunzo haya, naarajia kuwa mtu makini kazini na kuongeza umaarufu nitafanya kazi kwa nguvu na bidii zangu zote ili nijenge jina na niwe soko la kimataifa,"anasema.

Anaendelea, "Wito wangu kwa serikali na wadau wote wa sekta ya madini ni kuwataka wakiendeleze chuo hicho. Wasiishie kwenye mradi wa majaribio tu
kama
huo bali mafunzo hayo yasambazwe kwenye vyuo vya VETA nchini ili watanzania wengi waweze kuyapata."

Mkuu wa chuo cha VETA Moshi, Daniel Komba anasema pamoja na changamoto mbalimbali, anaamini mradi wa IMTT umekuja wakati muafaka kutokana na sekta ya madini kukua kwa kasi nchini.

"Zamani tulikuwa tunafundisha tu na mwanafunzi alikuwa anajaribiwa kokote, lakini sasa IMTT inatupa fursa mpya ya kuwapeleka wanafunzi kufanya mazoezi kwa vitendo kwenye makampuni ya madini hasa migodini," anasema.
 
Kama vipi dawa ni kujikata tu. Inawezekanaje ujenge uwanja wa kimataifa bagamoyo wakati kanda ya ziwa na kanda ya magharibi hakuna uwanja wa kimataifa?! Kuna watawala nchi hii wana roho mbaya kuliko hata ya shetani mwenyewe.
 
Huyu ndugu yetu mwandosya naye bure kabisa.Hatutaki hata kuoana Mamvi yake huku Mwanza.Ni mnafiki mkubwa.Na hao CCM huku hawana chao tena,Huku kila kitu ni CDM.Hatutaki kusikia CCM wala UDP na NCCR.
 
Barabara za mwanza ni mbovu, pamba road, karuta, barabara ya kwenda butimba, kwenda kiseke, kwenda busweru, kilimahewa, kiloleli, nyasaka, lumala na nyingine nyingi lakini barabara za bagamoyo, chalinze kwenda msoga zinatengewa mabilion ya ukarabati kila mwaka, nasikia malalamiko.
 
Nasikia malalamiko kanda ya ziwa eti watu wanakula mapanki aka mabaki ya samaki huku minofu inasafirishwa kwenda Ulaya.
utamu wa samaki uko kwenye mifupa ndo maana zamani ni wazee tu waliruhusiwa kula kichwa cha samaki. kama unatoka kanda ya ziwa thamini na rudia utamaduni wako. pia kumbuka kuwa samaki ambaye anasafirishwa ni sangara ambaye kwa wakazi wa kando kando ya ziwa walioota meno yote si mali kitu.
 
Yan hawa CCM wanatulostisha saana kanda ya ziwa lakn poa dawa yao tunaendelea kuindaaa tulianza 2010 lakn nadhan 2015 kitaeleweka u
 
Kama vipi dawa ni kujikata tu. Inawezekanaje ujenge uwanja wa kimataifa bagamoyo wakati kanda ya ziwa na kanda ya magharibi hakuna uwanja wa kimataifa?! Kuna watawala nchi hii wana roho mbaya kuliko hata ya shetani mwenyewende.
ndege zenyewe ziko wapi?sema kitu ambacho kinahitjika kweli kwa watu wa kawaida
 
Mimi ni mzaliwa wa kanda ya ziwa.kweli hatuna viongozi,waliopo wanajali maslai yao binafsi.Angalau Ngeleja na diwani billionea Joseph kando mkama wamewekeza kanda ya ziwa.lakini pia tunasikia tetesi kuwa mnadhulumu nyumba za watu.kama ni kweli rudisheni mnakipaka matope chama chetu.ninyi ni viongozi muwe mfano bora ktk jamii.tusitumie vyeo kudhurumu watu
 
Chadema na Falsafa ya Kuzomea! Ujinga ndani ya Wajinga!

acha basi umesahau wabunge wa ccm watu wazima waliwazomea cdm siku ya kwanza wanatoka bungeni? mpaka naibu spika akawaambia ni kawaida bunge zote hufanya hivyo looo acha bana

 
Back
Top Bottom