Nasikia Malalamiko Kanda ya ziwa

Mwanza ni international airport mkuu, unless kama hufahamu maana ya international airport!

Mkuu nilisafiri kwa ndege hadi Mwanza mkoa baba na mama wamezaliwa uwanja ulikuwa umejaa maji wasafiri tulioopolewa na coaster za airport. Aibu tupu, Pinda amewahi kukaa masaa kadhaa airport.
 
Usinichekeshe maana nakumbuka siku jengo la NSSF Bukoba (Jengo pekee lenye lift mkoa wa Kagera ambako asilimia 70 ya maprof wametokea) wali walivyoshinda kwenye lift kwenda juu na kutelemka bila kutoka mchana kutwa. Kweli kanda ya Ziwa yahitaji Mabadiliko. Ni kanda ambayo madukani huwezi kuta price tag kwenye bidhaa watu hununua kwa majadiliano kama mnadani tu aahh balaaa

Inachekesha ingawa kuna hali fulani ya ukweli.
 
Nyambala,

Uwanja una uzio? kwa nini mifugo inalisha pale?

Je unajua wananchi wa Igombe wanakatisha Uwanjani kwenda makwao, kiusalama ni sawa?

Unajua ni njia moja tuu ya ndege kupaa na kutua?

Unajua ule uwanja ni wa jeshi?

Unajua pale hata watu hamsini hawawezi kukaa katika viti kwa wakati mmoja, halafu AC haifanyi kazi?

Unazifahamu vizuri shule za kata, zimejengwa kuridhisha tu watunzania ila si kweli kwamba ni kwa dhati ya kukuza elimu tanzania.

Ndio uwanja wa mwanza ulivyo.

Mkuu hapo umefananisha vizuri Mwanza airport vs shule za kata (walimu wawili).
 
Nyambala,

Uwanja una uzio? kwa nini mifugo inalisha pale?

Je unajua wananchi wa Igombe wanakatisha Uwanjani kwenda makwao, kiusalama ni sawa?

Unajua ni njia moja tuu ya ndege kupaa na kutua?

Unajua ule uwanja ni wa jeshi?

Unajua pale hata watu hamsini hawawezi kukaa katika viti kwa wakati mmoja, halafu AC haifanyi kazi?

Unazifahamu vizuri shule za kata, zimejengwa kuridhisha tu watunzania ila si kweli kwamba ni kwa dhati ya kukuza elimu tanzania.

Ndio uwanja wa mwanza ulivyo.

asante mkuu kuna siku mtasikia gari limegongana na ndege! Yaani mabasi yaendayo Igombe yanapita mita 40 mkiani mwa ndege zinazotua na kuondoka
 
Hii hoja imenikuna sana kamanda mwanzishaji big ups sana mkuu. Dah; what a great thinking. Same same idea should be applied to other zones in the country if not regions and districts. Watu wa Namtumbo kunamadini huko balaa, Mbinga, Ludewa, Kiwira, Bahi, Manyoni...jamani, bado watu wanaimba CCM ilituzaa...lakini pole pole hii kitu brothers inakufa. CCM is dying hata wao wanajua. Inatafuta tu mtu/watu wa kufa nayo.
 
2Mine umesema kweli,

CDM wana sera ambayo mi naikubali-Majimbo kujitawala kiuchumi.

Huu mpango wa kupeleka kila kitu Pwani unaumiza sana maeneo mengine.
 
Habari ndo hiyo wakuu,

Malalamiko kwa kweli ni mengi.

mengine nimeyaacha tu ila nitakuwa naongeza kadri ninavyoona kuwa inafaa.
 
Wabunge wa Mkoa Kagera Mmewaadalia Mpango gani wa Maendeleo wananchi wa Mkoa wa KAGERA?Naomba kuwauliza wah,Wabunge wetu wa mkoa wa Kagera hasa mbunge wa Bukoba Vijijini (v) ni mpango gani wa maendeleo ambao mmetuandalia wananchi wa mkoa wetu ukizingatia Tayali mapendekezo yenu ya ongezeko la posho Spika wa Bunnge la jamuhuri amelikubali ingawa sisi mabosi wenu hatujatia Sahihi mapendekezo yenu kwa vile hamjaonyesha nia thabiti ya kuwatumikia wananchi waliowapa ridhaa ya kwenda pale Mjengoni Dodoma. Nimezaliwa miaka 57 iliyopita na ninatoka katika moja ya majimbo ya Mkoa wa Kagera jimbo la Bukoba vijijini kilomita 25 kutoka Mjini Bukoba miaka nenda rudi wananchi wa eneo hilo tumekuwa tukisubiri wabunge wetu wanaochaguliwa kwa kishindo kuwaonyesha njia ya maendeleo bila mafanikio ukiondoa miradi wanayojitolea Wananchi kwa nguvu zao kama ujenzi wa shule Zahanati ofisi za Vijiji na wanasiasa kudandia miradi yao ya kwamba miradi hiyo wameileta wao.Katika barabara ya Kashozi Road miaka 50 ya Uhuru barabara ya Lami haijavuka katika mlima wa NSHAMBYA mlima mbaya sana hasa wakati wa masika unahatarisha maisha ya wananchi Eneo hilo kama serikali ingelipa kipau mbele angalau ingefika njia panda ya kwenda shule ya Ihungo Secondary, Umeme tangu mkoloni upo pale Kashozi Dispensary miaka 50 iliyopita haujavuka Kibengwe mahitaji ya kuupata umeme huo kwa wananchi wa tarafa ya Bugabo ni kubwa lakini hadi leo wananchi wamekata tamaa lakini kipindi cha uchaguzi wabuge hao kutwa wakiomba kura toka kwa wananchi wa maeneo hayo. namalizia nini tukitegemee toka kwenu wabunge wetu ? na maeneo mengine ya mkoa huo. ukizingatia zao la migomba, Kahawa, vyote havileti matumaini kwa watu wa mkoa wa kagera ziwa letu hilo ndio kabisa sijawahi kusikia wabunge wetu wakihoji serikali kiasi gani la pato wananufaika nalo. Anatory Mujwahuzi
 
Wakati wa Nyerere Wahaya walinyimwa nafasi japo walikuwepo wasomi, Akaja Karamagi kwenye Wizara akaleta Ufisadi tu. Kanda Hii haiwezi kuendelea kwa kuja Imejaa watu wabinafsi wanaoangalia Maslahi yao na Familia zao. Tazama akina Sarungi au Igogo wamefanya nini Rorya? Bora hata yule mbunge wa Ukerewe aliwapelekea Feri Ukara, Hadi tuache Ubinafsi na Kuweka Mbele maslahi ya Kanda, tutaendelea kubaki vile vile....
 
acha basi umesahau wabunge wa ccm watu wazima waliwazomea cdm siku ya kwanza wanatoka bungeni? mpaka naibu spika akawaambia ni kawaida bunge zote hufanya hivyo looo acha bana


Achana na John Marwa, ni Kagamba mtoto hako. Hakaoni wala hakasikii. Mtoto wa familia ya Fisadi mmoja mkubwa wa siku nyingi!!!
 
Kanda ya ziwa imeumizwa sana na CCM, acheni tuwapige chini.
 
Sababu tunayo, Nia tunayo na Nguvu tunayo


Mkuu, yaani we acha tu!! Aibu!! Ila nina imani tukishikamana vizuri tutashinda. Hapa mimi ninaongeza juhudi ktk kubeba box ili 2014 niwe na nguvu ya kuzunguka Bk vijijini nikimwaga sumu, nina uhakika hawa wazee wetu waliolala kwenye mibuni wataamka tu!!

Juzi nimeongea na Rwakatare anasema kuna "operation amsha wazee vijijini" iko karibu kuanza!! Na vitendea kazi vi njiani kuja Bk, tusikate tamaa, nina imani na Wahaya wenzangu tutaizika CCM soon!!

NB: kunamkutano leo Bk mjini tafadhari turushie updates, mie niko mbali kidogo!!
 
... itakua ni kosa kubwa ajabu IKULU kudhani kumnyanganya Kamanda Lema ubunge kupitia mahakama huenda ikawa ni suluhisho.

Kamanda Lema endelea kuonyesha TALANTA yako ya kupendwa na vijana wa Tanzania kwa kuhamisha Vijiji vyote nchini toka CCM na kujiunga na CDM.

Kamanda Lema, onyesha UWEZO wa 'Nguvu ya Umma' kote nchini kupitia hiki chombo mahiri cha M4C huku ukiambatana na Jenerali na Dokta wa ukweli, Dr Slaa, kwa kutetemesha mafisadi katika kila jimbo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom