Nasikia Malalamiko Kanda ya ziwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nasikia Malalamiko Kanda ya ziwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by spencer, Jun 7, 2011.

 1. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #1
  Jun 7, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,792
  Likes Received: 1,337
  Trophy Points: 280
  GreatThinkers,

  Naskia kuna malalamiko kuwa Kanda ya ziwa licha ya kuwa Migodi yote ya Dhahabu iko kule hakuna hata international airport, Mwanza airport ni kama shule ya kata ni kweli?

  Nasikia kuna Malalmiko Rocky City Mwanza, Kikwete hadi December 2011 hajaleta hata Sh. kumi ya ruzuku ktk Jiji wakati hadi leo alitakiwa awe ameshatoa 40Bilioni ili kuwakomoa kwa kuwapiga chini ktk Uchaguzi ni kweli?

  Nasikia kuna malalamiko, yakuwa lile Jiwe maarufu la Bismack pale Kamanga Ferry lililokuwa ktk noti ya Tsh. 1000 likiwa na sahihi ya Mramba na Balali pia wameiondoa na kuweka kilima cha pale Gairo kikiwa na sahihi ya Mkulo na Ndulu, ni kweli?

  Naskia kuna malalamiko kanda ya ziwa kuwa licha ya kuwa na watu 16mil kati ya 45mil Tz, Katiba imejadiliwa Dodoma, Dar na Zanzibar, hawataki kabisa kuwashirikisha kisha wanataka CCM muwapiguie kura, ni kweli?

  Naskia Kuna malalamiko kuwa kanda ya ziwa licha ya kuwa asilimia hamsini ya wasomi wote tanzania wanatoka kule hakuna hata chuo kikuu hata kimoja cha serikali ni kweli?

  Naskia kuna malalamiko kuwa kanda ya ziwa licha ya kuwa na madini yanayoweza zalisha Cement yako pale Shinyanga hakuna hata mpango wa kujenga kiwanda licha ya kuwa 2005 mliahidiwa ni kweli?

  Naskia kuna malalamiko kuwa kanda ya ziwa mkoa mpya wa Simiyu umeomba ile barabara inayopita serengeti mmeomba ipitie Lamadi, bariadi kuja Hydom na kuunga Babati naskia wamekataa ni kweli?

  Naskia kuna malalamiko kuwa kanda ya ziwa kuna hakuna viwanda licha ya kuwa mna bidhaa nyingi lakini vinajengwa vyote pwani eti msafiri mkaombe vibarua Kibaha na bagamoyo ni kweli?

  Nasikia kuna malalamiko kanda ya ziwa kuwa ili bandari ya nchi kavu Isaka-Shinyanga vijijini nayo imekufa ili kuimalisha ajira ya pwani na kuanzisha bandari mpya ya nchi kavu Chalinze ni kweli?

  Naskia kuna malalamiko kuwa wilaya nyingi za zamani kama Musoma vijijini,Shinyanga Vijijini hazina hata makao makuu lakini baadhi ya zilizoteuliwa juzi juzi tuu zimejengwa vizuri ile mbaya ni kweli?

  Sasa kama ni kweli mnangoja nini- Hameni wote Si Si EM inaonekana wanachumia kwenu halafu wanawekeza kule Chalinze
   
 2. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #2
  Jun 7, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,847
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  Kanda ya ziwa hakuna CCM tena ilishakufa baada ya uchaguzi.kwa mkoa wa shinyanga mbunge wa CCM ni Masele tu. wengine wanatumikia upinzani.

  Tunasubiri 2014 tusimike serikali za mitaa zote CDM na UDP kwa Bariadi.Siku hizi hata sare za CCM wanavalia ukumbini hawana ubavu wa kutembea kifua mbele wanajua ni ngome ya CDM.

  Siku hizi Shinyanga hakuna ugomvi wa kisiasa kwani CCM kilishageuka kuwa chama cha upinzani, chama tawala ni CDM, hilo liko wazi hata kwa wana-ccm wenyewe ndiyo maana hakuna vurugu
   
 3. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #3
  Jun 7, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,057
  Likes Received: 3,084
  Trophy Points: 280
  Point yako ya pili ni kweli kabisa,kanda ya ziwa inakosa hata chuo kikuu 1 cha serikali kitu ambacho ni mkakati wa wazi wa viongozi wetu

  Ni ajabu na kweli kanda yenye kuwa na ziwa kubwa barani Afrika,kanda yenye migodi mingi ya madini tokea mkoloni,kanda yenye idadi kubwa ya watu kupita kanda zote,kanda yenye hazina ya wasomi maarufu Duniani kote,kanda yenye kiasi kikubwa cha maji eti leo ukitaka kusoma upolisi,ujeshi,uhasibu,udaktari,uinjinia,chuo kikuu, unalazimika kusafiri kwenda pwani,kask n.k

  Ndo maana CDM tunataka tuweke serikali za kanda ili kudecentralise madaraka na maamuzi yafanywe na serikali za kanda kuliko kuongoza kwa upendeleo,fitina na majungu kama ilivyo sasa


  Inauma sana.
   
 4. Muangila

  Muangila JF-Expert Member

  #4
  Jun 7, 2011
  Joined: Feb 24, 2010
  Messages: 1,854
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  kanda ya ziwa tulikuwa tunategemea zaidi reli ya kati lakini mpaka sasa ndo hivyo tenqa reli imekufa,migodi iliyopo kketu imeajiri watanzania wa kanda zote bila kubagua watokako wakati wanachi asilia wa maeneo hayo wakizidi kuwa mackini.
  Mkoa wa kagera ulikuwa unaongoza kielimu kwenye miaka yas 80 lkn toka wamepandishiwa pass mark eti kunyanyua maeneo yaliyokuwa nyuma kielimu hata uliposhuka kielimu:confused2: bado pass mark hazijashushwa INAUMA SANA.
   
 5. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #5
  Jun 7, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Yote uliyosema ni kweli, mimi ni mojawapo ya waathirika wananchi wa kanda ya ziwa. Napenda kuogezea
  1. Zaidi ya asilimia 99 ya watu wa kanda ya ziwa hawana maji ya bomba licha ya kuzungukwa na ziwa la pili kwa ukubwa duniani
  2. zaidi ya asilimia 99 hawana umeme
  3. Asilimia >90 ya watu hawajawahi kuona barabara ya rami
  4. Shule za msingi watoto hawapewi chakula, wanakaa chini, madarasa yameezekwa kwa nyasi.
  5. Shule za secondary za kata hazina umeme, walimu, vyoo, mabweni nk
  Unaweza kuongezea pia, CCM NI MAAFA YA KANDA YA ZIWA.
   
 6. Mkuu wa chuo

  Mkuu wa chuo JF-Expert Member

  #6
  Jun 7, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,255
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  CCM ni wadwanzi, tumeshaamua kuachana nao!
   
 7. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #7
  Jun 8, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,792
  Likes Received: 1,337
  Trophy Points: 280
  Kanda ya ziwa;

  Hongereni sana, sasa naamini mmeshaamka toka usingizi fo-fo-fo,

  hili wala si jambo la kujiuliza Si Si Em ni chama cha Upinzani.

  Poleni na hongereni,

  Mtawaona kina Nape watakavyozomewa wakitia timu.

  2011 hali ni hii, 2014-15 itakuwaje, Si Si Em itakuwa zile zile familia

  zinazolala na kuamka ktk nyumba zilizojengwa kwa ufisadi
   
 8. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #8
  Jun 8, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  hivi ni mpaka 2014...
   
 9. W

  WAMURUBHERE JF-Expert Member

  #9
  Jun 8, 2011
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  unachosema ni kweli mimi nimetokea wilaya ya musoma vijijini,hakuna makao makuu ya wilaya tangu nazaliwa hadi sasa nina umri zaidi ya miaka 40,mwaka 1984 majengo yalijengwa Kiabakari sehemu moja inaitwa busaraga lkn hadi sasa hayajafunguliwa na nakumbuka tofali tulisomba sisi vichwani,pia ni wilaya kubwa sana ambayo inatakiwa igawanjwe au kuwe na majimbo 2 ya uchaguzi,nakumbuka mwaka 1995 mbunge alitoka upinzani NCCR-mageuzi balozi mstaafu Ndobho ingawa naye nasikia karudi ccm! hakuna,makao makuu yapo musoma mjini kwa hiyo inatupatia taabu sana kufuata huduma zote wilaya nyingine,wilaya hii ndo inajumuisha na sehemu ya butiama,na mbunge wake ni Mh. mkono,pia nimekaa shinyanga na kufanya kazi huko,nako hakuna tofauti na musoma vjjn,hakuna makao makuu ya wilaya!
   
 10. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #10
  Jun 8, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mwanza ni international airport mkuu, unless kama hufahamu maana ya international airport!
   
 11. bullet

  bullet JF-Expert Member

  #11
  Jun 8, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 959
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  mhh Mwanza International airport!!!
   
 12. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #12
  Jun 8, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,057
  Likes Received: 3,084
  Trophy Points: 280
  Kanda ya ziwa tunadai utajiri wetu urudishwe kwa watu wake vinginevyo uvumilivu hauko tena rohoni mwetu
   
 13. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #13
  Jun 8, 2011
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  CCM INA SHULE ZAKE (hasa za sekondari).....CHAMA GANI KINGINE KINA SHULE HATA MOJA.....? HATA YA CHEKECHEA....? ILI TUNAPOONGEA TUWE NA FIRM GROUND.......!
  Tuache porojo tujenge nchi kwa vitendo
   
 14. Avater1971

  Avater1971 Member

  #14
  Jun 8, 2011
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 13
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Usinichekeshe maana nakumbuka siku jengo la NSSF Bukoba (Jengo pekee lenye lift mkoa wa Kagera ambako asilimia 70 ya maprof wametokea) wali walivyoshinda kwenye lift kwenda juu na kutelemka bila kutoka mchana kutwa. Kweli kanda ya Ziwa yahitaji Mabadiliko. Ni kanda ambayo madukani huwezi kuta price tag kwenye bidhaa watu hununua kwa majadiliano kama mnadani tu aahh balaaa
   
 15. WISDOM SEEDS

  WISDOM SEEDS JF-Expert Member

  #15
  Jun 8, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 782
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Internationa airport kwa kigezo gani?
   
 16. WISDOM SEEDS

  WISDOM SEEDS JF-Expert Member

  #16
  Jun 8, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 782
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  nonsense!
   
 17. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #17
  Jun 8, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,792
  Likes Received: 1,337
  Trophy Points: 280
  GreatThinkers,

  Naskitika kusema si muda mrefu hasira zilinipanda uwanja wa ndege Mwanza nikiwa nimesimama zaidi ya saa tatu kwa kukosa siti watu wakiwa kama 60 ivi, kuna ndege ilichelewa.

  hainingii kchwani kabisa.

  Kama kuna kila kigezo cha kuwa na int. airport na hakuna sasa wa nini hao tuwajali?

  Chapa lapa.

  CDM Moto chini hadi kieleweke
   
 18. J

  John Marwa JF-Expert Member

  #18
  Jun 8, 2011
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 275
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Chadema na Falsafa ya Kuzomea! Ujinga ndani ya Wajinga!
   
 19. m

  mmakonde JF-Expert Member

  #19
  Jun 8, 2011
  Joined: Dec 26, 2009
  Messages: 967
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  I feel mapinduzi ya haki yatatoka Mikoa ya Ziwa!Na mikoa hii ndiyo itaikomboa Tanzania kutoka kwa mkoloni mweusi.

  Shinyanga wameanza,Mwanza wanachuchua !Tabora wamelala
  Wanyatunzu wa Bariadi ni hypocrites wakiongozwa na Cheyo na Vijisenti.

  Ukisoma historia ya Tanganyika,upinzani wa Nyerere ulikuwa Tabora(Chief Fundikira,Kasela Bantu,James Mapalala etc)
  Shinyanga ilikuwa na Chief Makwaia.

  Bila ya SAUT,credit to Catholic church,kusingekuwa na chuo cha maana kanda ya ziwa.

  Rais anayekuja aone hili,watu wako tired na propaganda za kisiasa.
  Shinyanga ina pamba,almasi,dhahabu,mchele etc,lakini wananchi wako duni sana.
   
 20. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #20
  Jun 8, 2011
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,668
  Likes Received: 21,901
  Trophy Points: 280
  CCM in a shule zake? Nenda kapime malaria! Hizo shule zilikuwa za TAPA (Jumuia ya wazazi ya CCM) unajua nani walizijenga? Ni sawa na CCM kujisifu kuwa wanaviwanja Kama Kirumba,Jamhuri,majimaji nk, wakati hizo ni nguvu za wananchi tena kwa kulazimishwa na hata wengine walifungwa kwa kukaidi amri ya kuchangia. Hivyo vyote vinapaswa kurudishwa kwa wananchi kupitia halmashauri zao.
   
Loading...