Nasikia Malalamiko Kanda ya ziwa

Nasikia Malalamiko Kanda ya ziwa

Mkuu, umesema watu wa kanda ya ziwa wanakosa upendo kwa ndugu zao lakini naona hoja yako imejikita sana kwa mkoa wa Kagera peke yake, ebu tuambie watu wa Mwanza, Shinyanga, Tabora, then itakuwa vizuri ukatueleza watu wa wapi wana upendo na ndugu zao na uweke vielelezo kama ulivyoweka

ndugu Dume ukisoma mada vizuri utaona pale mwisho nimeeleza kuwa bado sijagusia mwanza,mara,shinyanga na kwingineko. Ukweli ni kwamba mada mleta mada kaweka wazi kuwa kanda ya ziwa wanasahau hali ya ndugu zao. No research no right to speak,kwa iyo sijagusia musoma au mara kwa kuwa sijaizunguka nzima naongea ninachokijua,sitaki kujadili nisichojua,hata ivo apo juu mchangiaji kashauliza kuhusu mikoa kama tabora ambayo ina viongoz wa juu kama spika wa zaman lakini bado hamna cha maana,Tabora ina mchumi wa kimataifa,ndugu Prof.Haruna Lipumba,lakini safiri leo uione Tabora!utalia machozi,nenda kule Sokomatola kwa ndugu Waziri mkuu Pinda,hata taa zilizowekwa barabarani zina miezi kadhaa kwa kukosa uwezo wa kulipa bill ya umeme! Iyo inakufurahisha?achana na iyo,kuna vituo vya afya hata juz Tbc1 walionesha vifaa vya hospital vinachemshwa kwa kuni,magunzi na wengine uambiwa waende hospital na kopo moja la mkaa la kuchemsha vifaa ya upasuaji,apo Pm Pinda uenda kuhutubia akiwa ndani ya V8 ya sh.200mil. Alaf ndo mtoto wa mkulima. Masilingi alishawahi kumsema Prince Bagenda ambaye ana ofisi pale London,juzi amerudi ccm,uyu mtu kwao shamba limegeuka kichaka,nduguze wanaishi kwa kuuza miogo na viazi jumapili pale soko la Rubya,iyo ni akili,upendo au uchumi? Twende shinyanga,pale wilaya ya kishapu imedaiwa mkurugenzi kafisadi karibu mil200,yan mpaka wilayani ni vumbi ambalo hutimuka kama kuna mtu anaswaga ng'ombe,huduma za kibenk kama crdb mpaka ufanye safari ya kuja uku shinyanga. Juzi tu watu wameanza kufa kwa njaa na ukame umeshika kasi,yan ata mifugo kama ng'ombe wamekonda na wengine wanakufa. Tunaitaji nini mpaka walau hata ngombe wa shinyanga wapate kuishi ili tupate nyama,maziwa mbolea na ngozi?tutafute wazungu wawekeze au? Leo hii watu wa Zanzibar wanalipiwa na bodi ya mikopo kuanzia certificate,diploma,digrii,mpaka masters,leo hii mtoto wa mzee wa karibu na mgodi wa Barrick anajilipia mpaka cheti,wanawatega fom6,wapate div.3 wakose mkopo warudi makwao. Huu ni uuaji na usaliti kielimu. Jaman tuelewane kuwa kanda ya Ziwa inahitaji special attention imesahaulika!
 
Mkuu Gsana, tukianza kutaja sehemu walizotoka viongozi wa Tanzania hakuna mwenye nafuu, nashukuru kwa hoja zako kuna sehemu kubwa kuna ukweli
 
GreatThinkers,

Kimbunga hiki si kwamba watu wanataka ukanda la hasha, ni jambo la muhimu sana kwa Mtu wa Nguruka na Bangwe Kigoma aanze kujifikiria hivi amefaidika nini na mto Maragarasi na ziwa Tanagnyika,Hifadhi za taifa Mahale na wingi wa Mawese!

Vili vile si vibaya Uyui,Kaliua na Puge Tabora kujiuliza kwa nini viongozi wao hawafikirii kuweka kiwanda cha Sigara kwao licha kulima Tumbaku kwa wingi?

Wanavijiji wanategemea sana usomi wenu na uelewa wenu ili kuwaamsha, CDM inafanya hivyo kwa mikutano YES lakini hata sisi wasomi ni wakati muafaka sasa.

Kuna faida gan Mtu kluzaliwa nyumba ya tope, ukakulia nyumba ya tope huku kodi unalipa, hadi leo hakuna uwezekano wa kufika kwenu hata kwa bajaji, hakuna zahanati, hakuna viwanda, kule si lolote si chochote.

Ndio maana nasema, kila mtu akomae na atokako ili Tanzania ya kweli isiwe na tabaka.

Nchi hii inakoelekea sehemu baadhi zinaendelea zingine zinasaidia maeneo flani kuendelezwa.

IT IS NOT FAIR.
 
Mwanza ni international airport mkuu, unless kama hufahamu maana ya international airport!

Sijawahi kusikia ikiitwa wala kuona bango au mahali popote pale palipo andikwa Mwanza International Airport (MIA), umetumwa vibaya. Majengo ya uwanja yenyewe yanatia aibu licha ya pesa nyingi kutumika kujenga lakini huwa wanakarabati hovyohovyo na zingine zinapitia timbo street!

Mizigo huwa inarushwa hovyo hovyo kwenye sakafu iliyochimbika chimbika mpaka mabegi mengine yanaharibika na kujaa vumbi na mchanga.
 
Nyambala,

Hebu fikiria jasho jasho letu linavyotumika vibaya.

Unadhubutu kumsahau mjomba na shangazi yako kijijini ili kukilinda kichaka cha wezi.
  • TICTS
  • RADAR
  • NDEGE YA RAIS
  • SAFARI ZA NJE YA NCHI-UTADHANI YEYE NI WAZIRI WA MAMBO YA NJE
  • TWIN TOWERS BOT
  • MIKATABA ISIYO NA TIJA KWA NCHI(Madini)
  • KAGODA(EPA)
  • MEREMETA
  • RICHMOND/DOWANS
  • WAKUU WA MIKOA na WILAYA(Hao ni Watumishi wa CCM)
  • IPTL
  • KIWIRA COAL MINES
  • NETGROUP SOLUTIONS
  • MISAMAHA YA KODI(Nchi inakosa mapato)
  • ALEX STEWART
  • BEI YA BIDHAA ie. UMEME (watanzania ndiyo wanaofidia misamaha ya kodi)
  • RITES
  • ALLIANCE AIR
  • KUJENGA BARABARA KUPITIA MBUGA YA SERENGETI(Matumizi mabaya ya kodi zetu)
  • LOLIONDO
  • BARABARA YA KILWA NA MANDELA KAZI KURUDIWA
Hivi nyie tuwavumile mpaka lini, mikataba yote mmetuingiza Mkenge na sasa inatuumiza sie na ninyi mnaishi kwa ile twenty percent mliyopata.

NO WAY, Kimbunga bora kianzie Kanda ya Ziwa kanda zingine zitaamka.

Hicho kichaka ni cha wezi.
 
Nyie endereeni tu kulalamika hamjui kuwa wakoroni wenu wanatumia hao wenzenu kama vibaraka ili mwenderee kunyonywa.msomi gani mhaya anaishi bukoba kama siyo dsm.hao hao ndo wanapewa ongo eti ni posho wanasahau walikotoka. Ondoa mafisadi wenye midomo na matumbo yenye njaa kila siku, eti karamagi anashirikiana kuiba na rowasa, rowasa anajenga kwao karamagi anajisahau matokeo yake aliyapata.
 
Nyambala,

Hebu fikiria jasho jasho letu linavyotumika vibaya.

Unadhubutu kumsahau mjomba na shangazi yako kijijini ili kukilinda kichaka cha wezi.
  • TICTS
  • RADAR
  • NDEGE YA RAIS
  • SAFARI ZA NJE YA NCHI-UTADHANI YEYE NI WAZIRI WA MAMBO YA NJE
  • TWIN TOWERS BOT
  • MIKATABA ISIYO NA TIJA KWA NCHI(Madini)
  • KAGODA(EPA)
  • MEREMETA
  • RICHMOND/DOWANS
  • WAKUU WA MIKOA na WILAYA(Hao ni Watumishi wa CCM)
  • IPTL
  • KIWIRA COAL MINES
  • NETGROUP SOLUTIONS
  • MISAMAHA YA KODI(Nchi inakosa mapato)
  • ALEX STEWART
  • BEI YA BIDHAA ie. UMEME (watanzania ndiyo wanaofidia misamaha ya kodi)
  • RITES
  • ALLIANCE AIR
  • KUJENGA BARABARA KUPITIA MBUGA YA SERENGETI(Matumizi mabaya ya kodi zetu)
  • LOLIONDO
  • BARABARA YA KILWA NA MANDELA KAZI KURUDIWA
Hivi nyie tuwavumile mpaka lini, mikataba yote mmetuingiza Mkenge na sasa inatuumiza sie na ninyi mnaishi kwa ile twenty percent mliyopata.

NO WAY, Kimbunga bora kianzie Kanda ya Ziwa kanda zingine zitaamka.

Hicho kichaka ni cha wezi.

Hapo kwenye Wakuu wa Mikoa na Wilaya kwa kweli mimi sioni faida ya hawa jamaa;

Mkoani; kuna mkuu wa mkoa, kuna RAC toa Mkuu wa mkoa bakisha RAC
Wilayani: kuna mkuu wa wilaya, kuna mkurugenzi, toa Mkuu wa wilaya abaki DAS

sasa punguza mishahara ya hao jamaa, posho zao, magari ( manunuzi,mafuta na matengenezo) fikiria ni pesa ngapi itapatikana

pia sio kila Wizara inahitaji naibu Waziri kuna wizara kama tano tu ndio zinahitaji naibu waziri, kama kuna makatibu wa wizara na wakurugenzi kwa nini unaweka utitili wa wanasiasa!
 
CCM wanatumia msemo wa "Mfinyanzi hulia gaeni" , maana yake wakiwaruhusu Kanda ya Ziwa wapate mgao mkubwa kulingana na wanacho zalisha, watashindwa kuwatawala kwa kuwahonga khanga na chumvi. Ikizingatia Kanda ya Ziwa ndilo eneo lenye kutoka kabila kubwa Tanzania, liajiimarisha na litakuwa linatoa rais kila awamu.

CCM inafurahia umasikini wa watanzania ili iendelee kubaki madarakani, inajitahidi sana kuhakikisha watu wanaendelea kubaki masikini kwa kugawa rasilimali za Taifa kwa wageni. Jinsi watu wanavyokuwa masikini zaidi ndiyo inakuwa rahisi zaidi kuwatawala, kwani watatumia muda mwingi kuhangaika kutafuta chakula na washindwe kufikiri zaidi ya hapo!
 
Nakumbukia kauli mbiu ya Mtikila akipambana na magabachori
"Saaa ya ukombozi ni sasa"
 
Kiusalama ili ndege itue inahitaji runway ya kutosha, kwa mfano kama ndege inahitaji 1km kutua yaani kukimbia mpaka kufunga brake, inatakiwa iwepo 1km ya ziada kama ndege hiyo itahitaji kuruka kwa dharura baada ya kutua, Mwanza airport hauna kiwango hicho na hata hizo ndege kubwa zinazotua zinatua kwa kulazimisha tu,

Mkuu mara ya mwisho kufika Mza airport ilikuwa lini?

Airport Code : MWZ
Airport Name : Mwanza
Runway Length : 10830 ft. = 3.3KM
Runway Elevation : 3763 ft.

City : Mwanza
Country : Tanzania
Country Abbrev. : TZ
Airport Guide : Unavailable

Longitude : 32° 56' 0" E
Latitude : 2° 27' 0" S
GMT Offset : +3.0
 
Sisi wa-Mwanzanyika tumeliona hilo na yote uliyoyasema ni kweli kabisa.
Ndio maana tunajiandaa na 2015, lazima tuwe na serikali yetu wenyewe.
Tutapambana mpaka mwisho. Lazima kieleweke. Dhahabu tunayo, Almasi tunayo, Samaki tunao, wasomi tunao, 60% ya GDP inatoka Kanda ya Ngosha, Uranium tunayo, nia tunayo, sababu tunayo na uwezo tunao.
Chadema tupo pamoja mpaka kielewe 2015.
 
Haya yote nshayaona, nabaki kutoa macho tu nkisubiri mustakabari wa hii nchi!
 
Greatthinkers,

Unapotoa Comments zingatia kuwa;
Mgodi wa Dhahabu Resolute- Nzega-Tabora-Kanda ya ziwa
Mgodi wa dhahabu Tulawaka-Biharamuro-Kagera-kanda ya ziwa
Mgodi wa dhahabu Geita-Geita-Mwanza-Kanda ya ziwa
Mgodi wa dhahabu Nyamongo-Tarime-Mara-Kanda ya ziwa
Mgodi wa dhahabu Buzwagi-Kahama-Shinyanga-Kanda ya ziwa
Mgodi wa dhahabu Bulynhulu-Kahama-Shinyanga-Kanda ya ziwa
Mgodi wa Almasi Williamson-Mwadui-Shinyanga-Kanda ya ziwa
Usisahau minofu ya sangara ktk ziwa Victoria-Kanda ya ziwa pia
 
Mkuu Gsana, tukianza kutaja sehemu walizotoka viongozi wa Tanzania hakuna mwenye nafuu, nashukuru kwa hoja zako kuna sehemu kubwa kuna ukweli

Labda Moshi ambako nchi hii wanaogopa kuwapa uongozi kwani wanajua wale watu hawana mchezo na masuala ya maendeleo lakini cha ajabu hawa watu ukienda kwao wanamaendeleo. Ukiangalia kwa makini utagundua kuwa watu wa Kilimanjaro maendeleo yao yanatokana na kutotegemea sana serikali. Wanakumbuka nyumbani tofauti na watu wengi wa kanda ya ziwa ambao wakitoka ndio mwisho wa kurudi kwao, sijui wanaogopa uchawi manake kanda hii nayo......!
 
maendeleo huletwa na wenyeji nyie mnasubiri wangine wawaletee mandeleo? endeleeni kusubiri! Nawashauri Watz badilisheni uongozi wa nchi ccm kishakuwa chama cha wachache wanaofaidi nchi yenu la sivyo mtaendelea kunyonywa mpaka damu yote ikauke
 
mkuu unaongelea International airport, wakati watu hawana hata uhakika wa kupata mlo mmoja kwa siku..., hawana uhakika wa kipato chochote.., in short hili ni janga la Taifa Tanzania is so wealthy while people are sooo poor....., kwa kweli inasikitisha na kutokana na vitega uchumi vya nchi hakuna hata mkoa mmoja unaoweza kujivunia...., Kama tungekuwa na busara maliasili za kanda ya ziwa pekee zingeweza kuendesha Tanzania yote na sio mifuko ya wachache
 
CCM INA SHULE ZAKE (hasa za sekondari).....CHAMA GANI KINGINE KINA SHULE HATA MOJA.....? HATA YA CHEKECHEA....? ILI TUNAPOONGEA TUWE NA FIRM GROUND.......!
Tuache porojo tujenge nchi kwa vitendo
acha uduanzi hizo shule CCM ilizijenga lini kama sio kipindi cha chama kimoja! kiustaarabu zinabidi zitaifishwe na serikali nyie ngojeni CHADEMA ishike dola!
 
There are currently 19 users browsing this thread. (7 members and 12 guests)
Narubongo Geza Ulole fazili mwabaluhi mfereji maringo Dr.W.Slaa marwacha

nakuona dr tupo pamoja, yasome haya machozi yetu sisi watu wa kanda ya ziwa 2015 utuokoe baba.. tupo pamoja captain, tunakupenda sana dr wasimamie vizuri vijana wetu huko bungeni. 2015 tunakuunga mkono zaidi ya 2010
 
Back
Top Bottom