Nasikia Harufu Kali na Mbaya ndani ya CHADEMA

Nasikia Harufu Kali na Mbaya ndani ya CHADEMA

Tena nyie drs ndo mnaochangia,
hivi inakuwaje kila dr ana duka la dawa za binadamu
na zahanati yake?
Unategemea huko hosptalini kuna kitu kitasalia kweli
Heri angerudi nyerere awafungie hizo maduka na hosp
tuone kama tutanunua glov. (Azimio la Arusha)

kichwa chako hakipo timamu wewe,Kina mama huko vijijini wanatafuta maji kwa kubeba kichwani zaidi ya kilomita 10 wewe unaleta ujinga hapa!
 
mleta mada atakuwa anaskia harufu ya MSALANI namshauri amkumbushe kwenda kutawaza!
 
Sio kwamba mkeo hajaoga siku tatu kwa sababu ya ubahili wako wa kulipa bili za maji kweli?
 
Sio kwamba mkeo hajaoga siku tatu kwa sababu ya ubahili wako wa kulipa bili za maji kweli?
 
Hivi hawa vijana wa magamba wanasikitisha sana kazi yao ni kuota CHADEMA tu hata hawawezi kukishauri chama chao kupingana na ufisadi wa akina Werema na Muhongo kwenye EScrow account.mamilioni ya watanzania wanishi katika umaskini wa kutisha, ajira hakuna nchi vijana wanahangaika mitaani,lakini wao wamekazania CHADEMA tu! ni aibu kubwa!
 
Wadau,

Kwa siku za karibuni tumeshuhudia taarifa mbalimbali ndani ya CHADEMA ambazo kimsingi hazileti muonekano mzuri ndani ya chama hicho. Hizi ni dalili za wazi za chama kinachopoteza mvuto miongoni mwa jamii. Hizi ni dalili za chama kukosa internal mechanism ya kushughulikia mambo yake. Hizi ni dalili za chama kukosa viongozi wabunifu. Hizi ni dalili za chama kuwa na viongozi wasioruhusu challenge. Hizi ni dalili za chama kuongozwa na watu waoga. Hizi ni dalili za chama kuendeshwa kienyeji. Hizi ni dalili za chama kupoteza muelekeo. Sijui na wenzangu mmeliona hili?

Kuna taarifa ilipatikana humu JF kuwa kuna kikao cha Kamati Kuuu cha CHADEMA kiliketi huko Dodoma. Miongoni mwa mambo yaliyoazimiwa ni kuwafukuza uanachama baadhi ya viongozi wa mikoa na wilaya ambao kwa mtazamo wa uongozi ni mamluki wa CCM kupitia ACT Tanzania. Haijapita muda, taarifa hizo zilikanushwa na msemaji wa chama, Tumaini Makene.

Haijapita hata wiki, baadhi ya viongozi wa mikoa na Wilaya wamejitokeza hadharani na kutoa shutuma nzito kwa uongozi ikiwa ni pamoja na matumizi mabaya ya madaraka, ubadhilifu wa fedha za chama wanazopata kwa njia ya ruzuku na misaada pamoja na kukiukwa kwa katiba ya chama. Baada ya Taarifa hiyo, tumeshuhudia matamko mawili. Moja limetolewa na Michael Aweda na jingine limetolewa na Yeriko Nyerere ambaye amewalisha maneno baadhi ya viongozi ambao ni wa CHADEMA CHUMBANI. Katika matamko yote hayo, inaonekana dhahiri kuwa kuna vita kali baina ya wanaopigania chama dhidi ya wale wanaopigania matumbo yao. Pamoja na jitihada za akina Yeriko kuondoa harufu ya kinyesi kwa kupuliza pafyum, bado taarifa zao zimeshindwa kabisa kujibu hoja za akina Balozi.

Wadau, hii ni vita na ni vita kali kweli. Sote tunatambua madhara ya vita. Ama zako ama zangu. Ni kutokana na muktadha huo, ndipo nilipofikiria na nikabaini kuwa kuna jambo zito litatokea ndani ya CHADEMA na kuna watu watadhurika kutokana na hali hiyo. Uongozi uliopo madarakani haupo tayari kusikiliza hoja zinazotolewa na wapigania chama. Uongozi upo busy kupanga mikakati ya kuweza kuwanyamazisha wale wote wanaowapinga hata ikibidi kuwadhuru. Hii ni hatari sana. Kitengo chao cha Ujasusi kinahaha kutafuta mbinu za kunusuru jahazi lisizame. Mbinu moja inayotumiwa kwa sasa ni kuitupia mzigo wa lawama CCM kwa yote yanayoendelea ndani ya chama hicho as if wanachama wote wa CHADEMA ni misukule ambao hawana uwezo na utashi wa kuhoji mambo ndani ya chama.

Harufu mbaya iliyoanza kujitokeza inaweza kuenea zaidi ndani ya chama hicho na kadri siku zinavyoenda baadhi ya watu watapewa majina mengine bila ya ridhaa yao. Wenye akili wamenielewa. Tusubiri tuone. Ila nawasikitikia sana hawa viongozi walioamua kukipigania chama ambacho kinaongozwa na viongozi ambao ni sikio la kufa. Jitihada zao kama za akina Athumani Balozi hazitafua dafu mbele ya viongozi laghai akina Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa. Hata hivyo, nawapongeza kwa ujasiri waliouonesha ingawa wanajua kuwa mwisho wao utakuwa mbaya.
Kivuli cha Marehemu Chacha Wangwe kipo Ofisini kwa mbowe kinamlilia mbowe ni mwendo wa Majanga akina Deus malya na wenzako kaeni chonjo .
 
R.I.P chacha Wangwe : Dr Slaa japo ni Padri amekusahau kabsa amekariri ya Mbowe sasa Mziki unawanyemelea sijui Kama wana Pesa za Akiba za kuwanunua Wajumbe ili wapige kiimya . Mzee Sebodo ile pesa ya Msaada Mbowe anaitaka sasa ili imsaidie kuhonga wajumbe wa kupambana na wale Wasema Ukweli huku jitihada za kuwazima kwa Rushwa zikifanyika ikishindikana wata wa-chacha wangwe mmoja baada ya mwingine . Hivi sasa Deus Malya yupo kazini anawafuatilia nyendo zao.
 
Hivi hawa vijana wa magamba wanasikitisha sana kazi yao ni kuota CHADEMA tu hata hawawezi kukishauri chama chao kupingana na ufisadi wa akina Werema na Muhongo kwenye EScrow account.mamilioni ya watanzania wanishi katika umaskini wa kutisha, ajira hakuna nchi vijana wanahangaika mitaani,lakini wao wamekazania CHADEMA tu! ni aibu kubwa!

Vyote Vitafanyiwa Kazi Ufisadi wa CCM utafanyiwa kazi si kwamba utaachwa lakini sasa hivi tupo hapa kwa Mbowe kwanza inabidi kazi ifanyike haraka kabla Mbowe hajatembeza Rushwa Upepo ukageuka .
 
Chadema hawana sifa ya kitaifa wameshindwa kuwaunganisha watanzania wamewagawa watu kwa makabila yao.
 
Naona lumumba mnataman mbowe na slaa waachie uongozi cdm kwasababu wamekua mwiba mkali sana kwenu. Tuacheni na cdm yetu mbowe na slaa wataendelea kuwepo sana tena sana nawatawabana kila kona.
Kwa jinsi unavyowatetea nina imani Mgao wanakupatia lakini Ukumbuke Laana ya Chacha wangwe bado inasambaa Kama wewe unajilia pesa na mbowe laana lazima itakunasa tu.
 
Utaendelea kuckia harufu mpk unakufa unazikwa lkn CDM haifi!!!! Pole sana mtaalamu wa kunusa
 
Chadema hawana sifa ya kitaifa wameshindwa kuwaunganisha watanzania wamewagawa watu kwa makabila yao.

Vitengo vyote vya Pesa wamewekwa wachaga Mbowe washauri wake Wakuu ni Mnyika,Lema na Kileo wote ni Wachaga ni mwendo wa ukabla japokuwa huwa wanajitahidi kumix kimtindo Kama pale kwa Vijana yupo Heche akina Lisu,marando,safari,beregu nk lakini hao ni Sawa na Tone la Maji kwenye Bahari tu hawana nguvu ndani ya Chama wenye nguvu ni wana Ukanda wa Kasikazini tu.
 
Walisema Zitto Kabwe ndiye msaliti wa CHADEMA;
Wakamuundia zengwe wakamsaliti wakamtia pembeni;

Sasa ni nani anayewasaliti tena;

Hatupendi kife juu juu kabla ya hiyo aibu itakayowakuta 2015;
ni heri kiendelee kuwepo hadi wakati huo ufike.
Zitto ni mpuuzi sana
 
Last edited by a moderator:
Wewe wanawake wenzako wanavyoishi maisha ya tabu, wanajiuza, wengine wanakaa vibarazani wanauza karanga, wengine nenda pale temeke uuone wanavyojifungulia chini ..unakija hapa unaishangilia ccm..jinga kabisa..

Ni kweli CCM ina Mapungufu yake, lakini si Kigezo cha kuacha kuwamulika Mafisadi na Watawala wa kifalume hapo Chadema, hapo Kwenu sasa kumejaa mapungufu mengi yamalizeni kwanza ndipo muwe na Sifa ya kuwakosoa wengine : R.I.P chacha wangwe.
 
Ndio mwisho wa akili zako ndogo hapo. CDM ni chama cha kitaifa kisicho na mrengo wowote wa ukabila ndio mana wana wa bunge mpaka nyanda za juu kusi mikoa ya magharibi kama kigoma kanda ya ziwa yote nk.

Wewe lazima utakuwa umepewa Rushwa na Mbowe kwa Maana umeukana Ukweli kwa nguvu kubwa saana ! Ukipima kwa Mizani Uchaga (Ukanda) na makabila mengine ndani ya uongozi wa juu wa Chadema jawabu ni Uchaga upo juu Hilo halina Ubishi , ebu jaribu kuzinduka usikariri kila unachoambiwa na Mbowe kisa amekupa Pesa jitambue kataa ufisadi .
 
ili uwe na Sifa ya kuwakosoa wengine sharti na wewe uwe Saaafi , je? Chadema wapo saaafi ?
 
Back
Top Bottom