Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,901
- 20,417
Wadau,
Kwa siku za karibuni tumeshuhudia taarifa mbalimbali ndani ya CHADEMA ambazo kimsingi hazileti muonekano mzuri ndani ya chama hicho. Hizi ni dalili za wazi za chama kinachopoteza mvuto miongoni mwa jamii. Hizi ni dalili za chama kukosa internal mechanism ya kushughulikia mambo yake. Hizi ni dalili za chama kukosa viongozi wabunifu. Hizi ni dalili za chama kuwa na viongozi wasioruhusu challenge. Hizi ni dalili za chama kuongozwa na watu waoga. Hizi ni dalili za chama kuendeshwa kienyeji. Hizi ni dalili za chama kupoteza muelekeo. Sijui na wenzangu mmeliona hili?
Kuna taarifa ilipatikana humu JF kuwa kuna kikao cha Kamati Kuuu cha CHADEMA kiliketi huko Dodoma. Miongoni mwa mambo yaliyoazimiwa ni kuwafukuza uanachama baadhi ya viongozi wa mikoa na wilaya ambao kwa mtazamo wa uongozi ni mamluki wa CCM kupitia ACT Tanzania. Haijapita muda, taarifa hizo zilikanushwa na msemaji wa chama, Tumaini Makene.
Haijapita hata wiki, baadhi ya viongozi wa mikoa na Wilaya wamejitokeza hadharani na kutoa shutuma nzito kwa uongozi ikiwa ni pamoja na matumizi mabaya ya madaraka, ubadhilifu wa fedha za chama wanazopata kwa njia ya ruzuku na misaada pamoja na kukiukwa kwa katiba ya chama. Baada ya Taarifa hiyo, tumeshuhudia matamko mawili. Moja limetolewa na Michael Aweda na jingine limetolewa na Yeriko Nyerere ambaye amewalisha maneno baadhi ya viongozi ambao ni wa CHADEMA CHUMBANI. Katika matamko yote hayo, inaonekana dhahiri kuwa kuna vita kali baina ya wanaopigania chama dhidi ya wale wanaopigania matumbo yao. Pamoja na jitihada za akina Yeriko kuondoa harufu ya kinyesi kwa kupuliza pafyum, bado taarifa zao zimeshindwa kabisa kujibu hoja za akina Balozi.
Wadau, hii ni vita na ni vita kali kweli. Sote tunatambua madhara ya vita. Ama zako ama zangu. Ni kutokana na muktadha huo, ndipo nilipofikiria na nikabaini kuwa kuna jambo zito litatokea ndani ya CHADEMA na kuna watu watadhurika kutokana na hali hiyo. Uongozi uliopo madarakani haupo tayari kusikiliza hoja zinazotolewa na wapigania chama. Uongozi upo busy kupanga mikakati ya kuweza kuwanyamazisha wale wote wanaowapinga hata ikibidi kuwadhuru. Hii ni hatari sana. Kitengo chao cha Ujasusi kinahaha kutafuta mbinu za kunusuru jahazi lisizame. Mbinu moja inayotumiwa kwa sasa ni kuitupia mzigo wa lawama CCM kwa yote yanayoendelea ndani ya chama hicho as if wanachama wote wa CHADEMA ni misukule ambao hawana uwezo na utashi wa kuhoji mambo ndani ya chama.
Harufu mbaya iliyoanza kujitokeza inaweza kuenea zaidi ndani ya chama hicho na kadri siku zinavyoenda baadhi ya watu watapewa majina mengine bila ya ridhaa yao. Wenye akili wamenielewa. Tusubiri tuone. Ila nawasikitikia sana hawa viongozi walioamua kukipigania chama ambacho kinaongozwa na viongozi ambao ni sikio la kufa. Jitihada zao kama za akina Athumani Balozi hazitafua dafu mbele ya viongozi laghai akina Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa. Hata hivyo, nawapongeza kwa ujasiri waliouonesha ingawa wanajua kuwa mwisho wao utakuwa mbaya.