Nasikia Harufu Kali na Mbaya ndani ya CHADEMA

Nasikia Harufu Kali na Mbaya ndani ya CHADEMA

Kubwa jinga;

KUNA tofauti ya mjinga na mpumbav.u Marehemu Mzee Jongo alipata kutamka; " Kusoma sio kuufuta ujinga, bali ni kuupunguza". Kila mwanadamu ana ujinga wa jambo moja au mia moja. Kuwa na ujinga wa jambo si kosa, hata Profesa anaweza asijue namna ya kuchochea kuni za kuchomea hindi bichi likachomeka. Kijana wa darasa la saba anaweza kuwa hodari wa jambo hilo kumshinda Profesa.

Lakini upumbavu ni ile hali ya mwanadamu kufanya jambo isivyotakiwa huku akiwa na uelewa wa namna ya kufanya inavyotakiwa. Huo ndio upumbavu. Na ndio maana binadamu kuitwa mpumbav.u ni tusi. Kuitwa mjinga si tusi, kila mmoja ana ujinga wake. Kuwa na ujinga wa jambo fulani ni kutoelewa jambo hilo. Ni nani anayeelewa kila jambo?
 
Watu wana mioyo! Wapo tayari kudandia gari lililochomoka tairi likiwa katika mwendo mkali kuliko kuona uozo uliopo cdm.
 
Chama cha ukanda hicho;
Ndiyo maana wakiamua kula pesa wanakula
Wakiamua kufukuza wa hawajali;

Kiacheni kijifilia pole pole tu. Utafanya nini
wakati chama ni chao viongozi ni watoto wao na wakwe
zao, wengine ni marafiki zao.
Dada, kitakufa tu hiki. Hakuna wa kukinusuru
 
Watu wana mioyo! Wapo tayari kudandia gari lililochomoka tairi likiwa katika mwendo mkali kuliko kuona uozo uliopo cdm.
Wapo tayari kupenda vitu visivyopendeka
 
Wadau,

Kwa siku za karibuni tumeshuhudia taarifa mbalimbali ndani ya CHADEMA ambazo kimsingi hazileti muonekano mzuri ndani ya chama hicho. Hizi ni dalili za wazi za chama kinachopoteza mvuto miongoni mwa jamii. Hizi ni dalili za chama kukosa internal mechanism ya kushughulikia mambo yake. Hizi ni dalili za chama kukosa viongozi wabunifu. Hizi ni dalili za chama kuwa na viongozi wasioruhusu challenge. Hizi ni dalili za chama kuongozwa na watu waoga. Hizi ni dalili za chama kuendeshwa kienyeji. Hizi ni dalili za chama kupoteza muelekeo. Sijui na wenzangu mmeliona hili?

Kuna taarifa ilipatikana humu JF kuwa kuna kikao cha Kamati Kuuu cha CHADEMA kiliketi huko Dodoma. Miongoni mwa mambo yaliyoazimiwa ni kuwafukuza uanachama baadhi ya viongozi wa mikoa na wilaya ambao kwa mtazamo wa uongozi ni mamluki wa CCM kupitia ACT Tanzania. Haijapita muda, taarifa hizo zilikanushwa na msemaji wa chama, Tumaini Makene.

Haijapita hata wiki, baadhi ya viongozi wa mikoa na Wilaya wamejitokeza hadharani na kutoa shutuma nzito kwa uongozi ikiwa ni pamoja na matumizi mabaya ya madaraka, ubadhilifu wa fedha za chama wanazopata kwa njia ya ruzuku na misaada pamoja na kukiukwa kwa katiba ya chama. Baada ya Taarifa hiyo, tumeshuhudia matamko mawili. Moja limetolewa na Michael Aweda na jingine limetolewa na Yeriko Nyerere ambaye amewalisha maneno baadhi ya viongozi ambao ni wa CHADEMA CHUMBANI. Katika matamko yote hayo, inaonekana dhahiri kuwa kuna vita kali baina ya wanaopigania chama dhidi ya wale wanaopigania matumbo yao. Pamoja na jitihada za akina Yeriko kuondoa harufu ya kinyesi kwa kupuliza pafyum, bado taarifa zao zimeshindwa kabisa kujibu hoja za akina Balozi.

Wadau, hii ni vita na ni vita kali kweli. Sote tunatambua madhara ya vita. Ama zako ama zangu. Ni kutokana na muktadha huo, ndipo nilipofikiria na nikabaini kuwa kuna jambo zito litatokea ndani ya CHADEMA na kuna watu watadhurika kutokana na hali hiyo. Uongozi uliopo madarakani haupo tayari kusikiliza hoja zinazotolewa na wapigania chama. Uongozi upo busy kupanga mikakati ya kuweza kuwanyamazisha wale wote wanaowapinga hata ikibidi kuwadhuru. Hii ni hatari sana. Kitengo chao cha Ujasusi kinahaha kutafuta mbinu za kunusuru jahazi lisizame. Mbinu moja inayotumiwa kwa sasa ni kuitupia mzigo wa lawama CCM kwa yote yanayoendelea ndani ya chama hicho as if wanachama wote wa CHADEMA ni misukule ambao hawana uwezo na utashi wa kuhoji mambo ndani ya chama.

Harufu mbaya iliyoanza kujitokeza inaweza kuenea zaidi ndani ya chama hicho na kadri siku zinavyoenda baadhi ya watu watapewa majina mengine bila ya ridhaa yao. Wenye akili wamenielewa. Tusubiri tuone. Ila nawasikitikia sana hawa viongozi walioamua kukipigania chama ambacho kinaongozwa na viongozi ambao ni sikio la kufa. Jitihada zao kama za akina Athumani Balozi hazitafua dafu mbele ya viongozi laghai akina Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa. Hata hivyo, nawapongeza kwa ujasiri waliouonesha ingawa wanajua kuwa mwisho wao utakuwa mbaya.

Jitizame Lizabon lazima utakua umejinyea pasipo kujua ndio mana unahisi harufu kali na mbaya.
 
Ya ngoswe mwachie ngoswe, ama kweli ukistaajabu ya Musa utayaona ya firauni, hii filamu ni km dentist kulilia kifo cha CDM mnafiki ni zaidi ya mchawi na muuaji combined.
 
Ya ngoswe mwachie ngoswe, ama kweli ukistaajabu ya Musa utayaona ya firauni, hii filamu ni km dentist kulilia kifo cha CDM mnafiki ni zaidi ya mchawi na muuaji combined.
Mkuu, hatutaacha kufuatilia masuala ya CDM kwa vile wao waiaifitinisha CCM kwa wananchi
 
Kazi kweli kweli.
Ninakubali kuwa Chadema kilikuwa na wahuni na wachumia tumbo pamoja na mamluki wengi.

Ninakipongeza na kukipa shavu kwa kukubali kwao kuyachekecha makundi haya yote bila hofu wala woga, huu ni uongozi shujaa kama wa Mandelela BIG UP SANA MBOWE,SLAA,LISSU NA WENGINE WENGI WAPIGANIA..............

Mandela na ANC walipambana na Inkata ya Butulezi na vingine vingi vya mlengo ule, unafuu wake wakorofi hawa na wahujumu wa juhudi zile za Waafrika wa Afrika ya Kusini chini ya ANC,ilikuwa waikuwa nje ya ANC.

Lakini kazi ya Chadema katika mapambano haya ni kuwa, vikaragosi hivi vilipenyezwa na kuingizwa ndani ya wapigania ukombizi, na wakafanikiwa kutumia hila mbalimbali kushika nyadhifa za juu katika Harakati hizi.
Niwapeni pole sana wapiganaji wa kweli Mungu awatieni nguvu.

Ahaa Kumbe ndiyo Maana CCM walitamka kwa kejeli na uhakika kifo cha Chadema kabla 2015, ilikuwa inatokana na uhakikisho wa Mamluki hawa wanatapikwa sasa kwa nguvu hivi!!,

Wahuni hawa, na Wachumia tumbo hawa wasiyo na huruma na watu sisi wanyonge tuliyofungwa kamba na kuburuzwa juani hivi, tukilazimishwa kuimba CCM ina wenyewe, Wenyewe ndiyo CCM huku jasho likitumiminika mwilini na kutoa jasho linalonuka, tukiwaimbia wakubwa akina Nape ambao mafuta ya kunukia yatiririka mwili mzima na wakitoka hapo kuku wetu afisa mtendaji anatunyang'anya na kuwachinjia wakubwa hawa! Laaa Mungu ATUKUMBUKE WAJE WAKE TUWAONE SIKU MOJA HAWA AKINA NAPE WAKONJA MACHUNGU HAYA WANAYOTUFANYIA SISI.

Nilikuwa ninapuuza sana upinzani kuwa ni wa ulaghai, lakini kilipofikia Chadema hapa, nimeanza kupata imani na matumaini ya kuona mabadiliko ya kweli ya ukombozi wa kutoka ukoloni mamboleo.

Hongera sana uongozi wa juu wa Chadema Hasa hawa wafuatao, Mbowe, Dr Slaa, Tundu Lissu, J.J. Mnyika, na Kamati kuu yao kijumla Big up sana.

Kumbukeni dhamana kubwa mliyobeba ya Watanzania, kumbuka wengi wenu milivyoteseka mnavyoteseka na kesi mbalimbali milizofunguliwa polisi mpaka mahakamani, kumbukeni mlivyosoteshwa mahabusu ya polisi magereza kwa kesi zisizo na kichwa wala miguu kwa ajili ya kujitoa kwenu muhanga kuwatetea Watanzania, Kumbukeni damu ya watu wasiyo nahatia iliyomwagika katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu wakiwaunga mkono katika kuwapigania Watanzania wanyonge, Kumbukeni Watu wamejitolea Muhanga na kuuwawa kwa mtutu wa Bunduki wakiwaunga mkono, Wakumbukeni wengi waliyoachwa vilema, wajane na yatima kwa sababu ya kuiunga mkono Chadema iwakombowe Watanzania.

Mkiwakumbuka hawa na mliyopatwa nayo basi damu hiyo iliyomwagika kwa kuwaunga mkono itawapeni ujasiri wa kuendelea kuwatapika wote waliyokuwa wamepandikizwa bila hofo wala woga na wanachama wa kweli mtawapata, hivi sasa endeleeni na uzi huo huo muingie mwakani na sura mpya damu mpya.

Katika Harakati zo zote za kuwapokonya tonge wafalme, wakati wote ni za hatari na ni kifo, Angalieni Syiria watu wanavyokufa. JIPENI MOYO.

CCM SIYO KUNDI DOGO NI KUBWA HASA UKIZINGATIA KUNDI LA VIONGOZI WANAODHULUMU WATU HAKI ZAO KWA NJIA MBALIMBALI WALIYOPO KUANZIA KATANI HADI TAIFA KAMA SIYO KUANZIA KITONGOJI NA KIJIJI, HALAFU JUMULISHA NA WANUFAIKA NDUGU, JAMAA WATOTO MASWAHIBA NA WAKE NA HAWALA ZAO WAUME ZAO NI HATARI SANA.

kUBWA JITAMBUAENI TU KUWA NINYI NI KAMA SISIMIZI MNAPAMBANA NA TEMBO. SASA JITAHIDI MUINGIE KWENYE MASIKIO NA MKONGA ATAJIPIGA SANA KWA NGUVU KWENYE MITI HADI KUFA.

ENDELEENI KUWATAPIKA HAO AKINA BAROZI, ZITTO NA MAKUNDI YAO YANAYOTEMBEA KWENYE VYAMA VYA UPINZANI NA VYA WANAHARAKATI KILA KUKICHA. MUNGU ATAKUWA NANYI.
 
Dah kama hao ndo chaguo lenu basi chama hakina watu kabisa. Labda mmevutiwa na uasherati wao

Naona lumumba mnataman mbowe na slaa waachie uongozi cdm kwasababu wamekua mwiba mkali sana kwenu. Tuacheni na cdm yetu mbowe na slaa wataendelea kuwepo sana tena sana nawatawabana kila kona.
 
Hiyo harufu ukute haitoki chadema bali kwenye sehemu zako za siri,jichunguze na ikibidi kafanye usafi!
 
unasikia harufu mbaya? mkeo yupo hapo pembeni? ni shida ya maji kwenu hajaoga jikakamue kamnunulie japo ya uhai aoge nakuapia harufu itapotea hapo ulipo!
 
Ukiwa chooni ukimaliza haja yako uwe unatumia maji kutawaza!, nakushauri uwe unafanya hivyo hutasikia tena hiyo harufu!
 
Wadau,

Kwa siku za karibuni tumeshuhudia taarifa mbalimbali ndani ya CHADEMA ambazo kimsingi hazileti muonekano mzuri ndani ya chama hicho. Hizi ni dalili za wazi za chama kinachopoteza mvuto miongoni mwa jamii. Hizi ni dalili za chama kukosa internal mechanism ya kushughulikia mambo yake. Hizi ni dalili za chama kukosa viongozi wabunifu. Hizi ni dalili za chama kuwa na viongozi wasioruhusu challenge. Hizi ni dalili za chama kuongozwa na watu waoga. Hizi ni dalili za chama kuendeshwa kienyeji. Hizi ni dalili za chama kupoteza muelekeo. Sijui na wenzangu mmeliona hili?

Kuna taarifa ilipatikana humu JF kuwa kuna kikao cha Kamati Kuuu cha CHADEMA kiliketi huko Dodoma. Miongoni mwa mambo yaliyoazimiwa ni kuwafukuza uanachama baadhi ya viongozi wa mikoa na wilaya ambao kwa mtazamo wa uongozi ni mamluki wa CCM kupitia ACT Tanzania. Haijapita muda, taarifa hizo zilikanushwa na msemaji wa chama, Tumaini Makene.

Haijapita hata wiki, baadhi ya viongozi wa mikoa na Wilaya wamejitokeza hadharani na kutoa shutuma nzito kwa uongozi ikiwa ni pamoja na matumizi mabaya ya madaraka, ubadhilifu wa fedha za chama wanazopata kwa njia ya ruzuku na misaada pamoja na kukiukwa kwa katiba ya chama. Baada ya Taarifa hiyo, tumeshuhudia matamko mawili. Moja limetolewa na Michael Aweda na jingine limetolewa na Yeriko Nyerere ambaye amewalisha maneno baadhi ya viongozi ambao ni wa CHADEMA CHUMBANI. Katika matamko yote hayo, inaonekana dhahiri kuwa kuna vita kali baina ya wanaopigania chama dhidi ya wale wanaopigania matumbo yao. Pamoja na jitihada za akina Yeriko kuondoa harufu ya kinyesi kwa kupuliza pafyum, bado taarifa zao zimeshindwa kabisa kujibu hoja za akina Balozi.

Wadau, hii ni vita na ni vita kali kweli. Sote tunatambua madhara ya vita. Ama zako ama zangu. Ni kutokana na muktadha huo, ndipo nilipofikiria na nikabaini kuwa kuna jambo zito litatokea ndani ya CHADEMA na kuna watu watadhurika kutokana na hali hiyo. Uongozi uliopo madarakani haupo tayari kusikiliza hoja zinazotolewa na wapigania chama. Uongozi upo busy kupanga mikakati ya kuweza kuwanyamazisha wale wote wanaowapinga hata ikibidi kuwadhuru. Hii ni hatari sana. Kitengo chao cha Ujasusi kinahaha kutafuta mbinu za kunusuru jahazi lisizame. Mbinu moja inayotumiwa kwa sasa ni kuitupia mzigo wa lawama CCM kwa yote yanayoendelea ndani ya chama hicho as if wanachama wote wa CHADEMA ni misukule ambao hawana uwezo na utashi wa kuhoji mambo ndani ya chama.

Harufu mbaya iliyoanza kujitokeza inaweza kuenea zaidi ndani ya chama hicho na kadri siku zinavyoenda baadhi ya watu watapewa majina mengine bila ya ridhaa yao. Wenye akili wamenielewa. Tusubiri tuone. Ila nawasikitikia sana hawa viongozi walioamua kukipigania chama ambacho kinaongozwa na viongozi ambao ni sikio la kufa. Jitihada zao kama za akina Athumani Balozi hazitafua dafu mbele ya viongozi laghai akina Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa. Hata hivyo, nawapongeza kwa ujasiri waliouonesha ingawa wanajua kuwa mwisho wao utakuwa mbaya.
maccm mmepotea sana, cdm mbele kwa mbele, ccm ndiyo majanga kabisa. Kama siyo polis na tume ya kikwete ccm ingekua imebaki historia.
 
We unataka taarifa zenye kuleta muonekano mzuri wa chama ili iweje?!
 
Back
Top Bottom