Nashughulikia mambo mbalimbali Dodoma bila wewe kulazimika kufika hapa

Wewe mwenye mahitaji ya huduma ya site view na nyinginezo,waweza kufanya mawasiliano,uhudiwe pia Kwa gharama nafuu.Huna haja ya wewe kitembelea eneo husika ikiwa hakuna ulazima Kwa wakati huo.Tuwasiliane.
 
Hakikisha tu kua jambo lako halikulazimu wewe kuwepo eneo la kupatiwa huduma' husika.Fanya mawasiliano usaidiwe.
 
Hata wewe unayehitaji kufanyiwa SITE view,waweza kufanya mawasiliano na DODOMA MESSENGERS,anaglia tu kama Kuna tenda imetangazwa Kwa DODOMA, usaidiwe kupata taarifa sahihi kwa integrity kubwa,kama baadhi ya makampuni na watu binafsi wanavyohudumiwa.
 
Mdau mwenye shida Dodoma na uko mbali au upo Dodoma ila umetingwa na shughuli nyinginezo,usisite kuwasiliana na 'DODOMA MESSENGERS' kwa 0765920855 ili uweze kusaidiwa jambo lako lisilokulazimu wewe kuwepo eneo la kupatiwa huduma.
 
Miongoni mwa huduma ambazo zimekua zikitolewa ni kama;-
-Kufanya SITE VISITING na kumpa mrejesho mhusika.
-Kutafuta na kufanya booking ya vyumba kwa wageni kabla hawajafika Dodoma.
-Kufikisha jambo la mteja hasa kama anapiga simu haipokelewi mahala husika.
Hizo ni baadhi tu.
 
Epuka safari zisizokua za lazima kuja Dodoma,wasiliana na Dodoma messengers,uhudumiwe kwa weledi endapo shughuli yako haikulazimu wewe kuwepo eneo la kutolea huduma.
Mawasiliano yafanyike kupitia +255765920855,uokoe gharama mbalimbali zinazoweza kuepukika.
 
Mimi ni mkazi wa Dodoma, nimekuwa nikiagizwa sana na baadhi ya wadau hasahasa wale wa mbali na Dodoma na hata waliopo Dodoma,kuwatatulia matatizo mbalimbali ambayo hayawalazimu wao kufika huku (Dodoma) au sehemu husika kama wapo hapahapa Dodoma.

Kwa kufanya hivyo, huwa wanaokoa gharama za usafiri na malazi na badala yake, huchangia kiasi cha fedha, nikishamaliza kuwashughulikia hayo matatizo na kuridhika na huduma niliyoombwa kuifanya.

Mfano wa huduma ambazo mara kadhaa huambiwa niwashughulikie ni kama kwenda kwenye Wizara mbalimbali kama wizara ya mambo ya ndani, wizara ya mambo ya nje na uhusiano wa kimataifa,kupeleka barua za kuomba uanzishwaji wa viwanda vya vilipuzi, pia kwenda bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu kuomba statements za mikopo yao, kwa wale wanaokuwa na lengo la kumaliza madeni yao (loan liquidation), kufuatilia barua za wale walioachishwa kazi na wameomba kurudishwa kazini, kufuatilia kwa wale waliostaafu mafao yao kwa kupeleka viambatanisho husika kwenye mifuko waliokua wanachangia, kufuatilia hati za viwanja, kuwachukulia leseni za udaktari (practicing licenses) pale Medical Council of Tanganyika (MCT), kuwachukulia transcripts baadhi ya wadau wanaozihitaji pale NACTE VET n.k

Endapo wewe ni mmoja wa wale wanaohitaji huduma zenye kushabihiana na nilizotolea mfano hapo juu na hata kuuliza tu, karibu PM au hapahapa, kama utakuwa na la kuuliza.

Asanteni.
Mawasiliano: 0765920855
Mtaji wako ni UAMINIFU tu basi...Kula Tano Master👊
 
Asante mkuu,hapa tu tokea jana usiku,nimeshapata watu wanne,ambao natakiwa niendelee nao leo,naanza na mmoja ambaye kaniagiza pale Medical Council of Tanganyika(MCT),ambayo iko Kambarage Tower,nasubiria stationery zifunguliwe,nikaprint document yake,nimfikishie pale.
Sasa Mungu akiweka riziki ufungue stationery yako
 
Back
Top Bottom