Nashughulikia mambo mbalimbali Dodoma bila wewe kulazimika kufika hapa

Dodoma messengers

JF-Expert Member
Aug 28, 2019
485
776
Mimi ni mkazi wa Dodoma, nimekuwa nikiagizwa sana na baadhi ya wadau hasahasa wale wa mbali na Dodoma na hata waliopo Dodoma,kuwatatulia matatizo mbalimbali ambayo hayawalazimu wao kufika huku (Dodoma) au sehemu husika kama wapo hapahapa Dodoma.

Kwa kufanya hivyo, huwa wanaokoa gharama za usafiri na malazi na badala yake, huchangia kiasi cha fedha, nikishamaliza kuwashughulikia hayo matatizo na kuridhika na huduma niliyoombwa kuifanya.

Mfano wa huduma ambazo mara kadhaa huambiwa niwashughulikie ni kama kwenda kwenye Wizara mbalimbali kama wizara ya mambo ya ndani, wizara ya mambo ya nje na uhusiano wa kimataifa,kupeleka barua za kuomba uanzishwaji wa viwanda vya vilipuzi, pia kwenda bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu kuomba statements za mikopo yao, kwa wale wanaokuwa na lengo la kumaliza madeni yao (loan liquidation), kufuatilia barua za wale walioachishwa kazi na wameomba kurudishwa kazini, kufuatilia kwa wale waliostaafu mafao yao kwa kupeleka viambatanisho husika kwenye mifuko waliokua wanachangia, kufuatilia hati za viwanja, kuwachukulia leseni za udaktari (practicing licenses) pale Medical Council of Tanganyika (MCT), kuwachukulia transcripts baadhi ya wadau wanaozihitaji pale NACTE VET n.k

Endapo wewe ni mmoja wa wale wanaohitaji huduma zenye kushabihiana na nilizotolea mfano hapo juu na hata kuuliza tu, karibu PM au hapahapa, kama utakuwa na la kuuliza.

Asanteni.
Mawasiliano: 0765920855
 
Safi sana mkuu..kikubwa uaminifu.
Hakika, najitahidi sana kua mwaminifu, niliowafanyia hivyo wananijua, maana wamekua wakiambiana,hivyo kunitumia kuwarahisishia mambo. Mtu yupo Kigoma huko, haina haja ya kuja kulala loji, nauli za kuja na kurudi, kwahiyo ni bora nimshughulikie,nikimmalizia shughuli yake, aniwezeshe kiasi atakachowiwa nacho.
 
Hakika, najitahidi sana kua mwaminifu,niliowafanyia hivyo wananijua,maana wamekua wakiambiana,hivyo kunitumia kuwarahisishia mambo.Mtu yupo Kigoma huko,haina haja ya kuja kulala loji,nauli za kuja na kurudi,kwahiyo ni bora nimshughulikie,nikimmalizia shughuli yake,aniwezeshe kiasi atakachowiwa nacho.
Connection ya kazi je hutoi🤔
 
Messenger siyo bongo kama ulaya. Pambana, mi niliwahi tumwa hapo hazina.
Asante mkuu,hapa tu tokea jana usiku,nimeshapata watu wanne,ambao natakiwa niendelee nao leo,naanza na mmoja ambaye kaniagiza pale Medical Council of Tanganyika(MCT),ambayo iko Kambarage Tower,nasubiria stationery zifunguliwe,nikaprint document yake,nimfikishie pale.
 
Back
Top Bottom