SoC04 Mambo ya kuboresha katika Jiji la Dodoma ili kuleta taswira ya makao makuu ya nchi

Tanzania Tuitakayo competition threads
Apr 20, 2024
25
23
UTANGULIZI.
Dodoma ulitangazwa kuwa mji mkuu wa Tanzania na mwasisi wa taifa hili mwalimu JK Nyerere mwaka 1973 na Rais JP Magufuli alitoa amri ya serikali kuhamia Dodoma mwezi Julai 2016 wakati alipopewa wadhifa wa mwenyekiti wa chama tawala, Chama Cha Mapinduzi/CCM.
Rais John Pombe Joseph Magufuli alitangaza na kuipandisha hadhi Manispaa ya Dodoma kuwa Jiji la Dodoma mnamo Aprili 26, 2018.
Kama tujuavyo, Dodoma ndio kitovu cha Taifa la Tanzania (Makao makuu ya nchi yetu, Tanzania).
Kwanza nitoe pongezi kwa Uongozi uliopita na uliyopo sasa, katika kuwekeza Jiji la Dodoma, Mfano.​
  • Mji wa Magufuli (Magufuli City)- Mtumba​
  • Uwanja wa Ndege wa Kimataifa- Msalato.​
  • Kituo cha Treni ya Mwendokasi (SGR)​
  • Kuhamishia Wizara zote Dodoma- Mtumba/Udom.​
  • Uboreshwaji wa Ikulu kuu- chamwino.​
images (1).jpg

Chanzo: Google

TASWIRA ya sasa katika Jiji la Dodoma.

Kwa sasa muonekano wa Jiji la Dodoma, hauhakisi taswira ya Nchi/Taifa. Mbali na juhudi zote bado kuna vipaumbele hatujaviweka/kuvifanyia kazi Ili kuleta taswira ya kitovu cha Taifa letu.

MAMBO YA KUFANYA ILI KUIFANYA DODOMA KUHAKISI TASWIRA YA MAKAO MAKUU YA NCHI.
Napendekeza Mambo yafuatayo yafanyike ili kuipa sifa na hadhi Dodoma kama Kitovu cha Taifa letu Tanzania;-

01. Matumizi ya maeneo yaliyo wazi (Idle lands)
Mfano. Hazina, Jamatini, Iringa road n.k, Maeneo haya na mengineyo yaliyo wazi yanaweza kutumika katika uzalishaji kama, Maeneo ya kufurahia/ Mapumziko (Refreshments & Recreation Centers). Hizi ni sehemu ambazo watu watalipia viingilio na kuweza kupumzika, Kufurahia, Michezo ya watoto na Maeneo ya kuogelea (Swimming Pools). Kwani kwa sasa Dodoma tuna upungufu wa maeneo ambayo watu wanaweza kukutana na kufurahia hasa siku za jioni, Mwisho wa wiki (weekends) na siku za mapumziko (Holidays). Hii itaongeza kipato na ajira kwa wananchi na kuboresha Taswira ya Dodoma.

02. Arena (Dodoma Arena).
Kwa sasa Dodoma hatuna uwanja wa hadhi ya kimataifa. Tunaweza kujifunza wazi kwa mfano wa ukuaji wa Jiji la kigali-Rwanda (Kigali Arena), Uwepo wa Arena ni makutaniko ya wanamichezo, Burudani, Mikutano mikubwa na Matamasha mbalimbali na hii inasaidia kukuza Jiji la Dodoma kwa kuleta Taswira na sifa ya kimataifa. Hii itapelekea ukuaji wa biashara na jiji kiujumla.
_ba00e6eb-7dfd-4179-ad37-4c8ba8bd34c2.jpeg

Chanzo: AI creation (Future View of Dodoma Arena)

03. Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa (International Conference/Convention Center).
Hadi sasa ukumbi mkubwa wa mikutano ni Jakaya Kikwete International Convention Center (JKICC), Tumekosa uwepo wa kumbi kubwa na za kisasa kama Arusha International Conference Center (AICC), hizi kumbi zinatambulisha na kuleta Taswira nzuri katika Jiji la Dodoma na Itapelekea watu kujumuika katika warsha/Mikutano na makongamano makubwa na kukuza Uchumi wa Jiji na nchi kiujumla.
Dodoma CC.jpg

Chanzo: Google (Future View of Dodoma International Conference Center/ DICC)

04. Makutano ya Kibiashara (International Business Centers).
• Tujiulize swali, kwanini wafanyabiashara wanatoka Kahama, Singida, Mwanza, Shinyamga, Tabora na kwenda kuchukua bidhaa Dar es salaam (Kariakoo)?? Kwanini wavuke Dodoma, wakati wanaweza kuishia hapa kuchukua bidhaa na kurudi mikoani kwao??, Tunaweza kujenga soko kuu la Biashara kimataifa Dodoma na kuwa Lango la Biashara kimataifa zaidi ya kutegemea Dar es salaam (Kariakoo).
• Kuboresha Soko la Mazao (Kibaigwa), Hadi sasa soko la Kibaigwa liko kizamani sana (Local market) mbali na kuwa na jina kubwa Lakini halivutii kabisa, vile sio viwango vyake. Uboreshaji katika miundombinu inahitajika, kama. -Magodown ya kisasa, -Wigo/Fences, -Parking za Magari/Malori, -Office/Vyoo, -Maeneo ya Chakula na Biashara.
• Kuboresha Chalinze nyama & Mbande. Haya ni maeneo maarufu sana kwa nyama na chakula hasa unapoingia Jiji la Dodoma ila sio masafi ni hatari kwa afya na usalama endapo moto ukitokea. Tunaweza kuboresha miundombinu na kuifanya ya kisasa -Parking, -Sehemu safi na salama ya Chakula/ Office/Vyoo, Hiii itasaidia.
• Kulinda afya za Walaji.
• Taswira na sifa ya Jiji la Dodoma.
• Mfumo wa ukusanyaji mapato.
• Ajira zitaongezeka zaidi.
BlendPhotoEditor_1717395183858.png

Chanzo: Google (Currently Chalinze Nyama & Mbande).

Sneo la chakula la kisasa.jpg

Chanzo: Google (Future View of Chalinze Nyama & Mbande).

5. Makumbusho & Makitaba ya kisasa.
Tunaweza kuwa na Maono ya kuweka sehemu ya Makumbusho ambayo inayoonyesha na kuielezea historia ya Tanzania, hii itaipa sifa na nguvu Dodoma ambayo ni kitovu na watu kujua historia kwa kuona na kusoma kumbukumbu za nchi yetu, huku ikiwa pamoja na makitaba ya kisasa. Makumbusho ya Dar es salaam, Ule muonekano na Picha inaweza kuhamishiwa hapa Ili ilete maana halisi ya Makao makuu.
_a096acd3-9bd9-4890-ab02-18b5ceea5ef6.jpeg

Chanzo: Ai Creation (Future View of Dodoma Historical Museum & Library).

6. Uboreshwaji wa Miundombinu na Mipango miji
Dodoma bado tuna upungufu wa Barabara nzuri kuzunguka mji, Ukosefu wa maji na umeme wa uhakika mbali na kuwa na chanzo cha umeme mtera. Mifumo ya utupaji taka ni mibovu tofauti na maeneo kama Moshi/Arusha, mji ni mchafu na haujapangiliwa vizuri kuendana na hadhi ya makao makuu. Chukulia mfano maeneo kama -Makole, -Majengo Sokoni na viunga vyake, -Bahi road, - Kizota. Napendekeza kuwa nyumba na Miundombinu za maeneo hayo viwekwe kisasa zaidi ili kuleta Taswira ya mji wa Dodoma.

HITIMISHO.
Kujengwa kwa mji bora na wakisasa Ili kuleta taswira ya makao makuu ya nchi ni jambo ambalo linagharimu muda na fedha, Lakini ni vizuri kama nchi kuwa na Mipango ya muda mrefu ili Kufanikiwa, Maono ya viongozi husika na utekelezaji wa maono hayo yanahitajika, bila viongozi bora wenye maono hatuwezi kufika kokote. Uboreshaji wa taswira ya Dodoma utaleta faida lukuki kama:-
• Miundombinu bora ya ukusanyaji mapato.
• Mji sana & Afya iliyozingatiwa.
• Ukuaji biashara & uchumi zaidi ya sasa.
• Taswira ya Taifa, kwani Dodoma ni Makao makuu ya nchi.​
 
Chanzo: AI creation (Future View of Dodoma Arena)
Ila AI nayo, ikatutengenezea myama 'Twembiago' kuwakilisha 😆😆

. Makutano ya Kibiashara (International Business Centers).
• Tujiulize swali, kwanini wafanyabiashara wanatoka Kahama, Singida, Mwanza, Shinyamga, Tabora na kwenda kuchukua bidhaa Dar es salaam (Kariakoo)?? Kwanini
Zijitahidi tu hizo ziwe ni biashara za nje na ndani.
 
UTANGULIZI.
Dodoma ulitangazwa kuwa mji mkuu wa Tanzania na mwasisi wa taifa hili mwalimu JK Nyerere mwaka 1973 na Rais JP Magufuli alitoa amri ya serikali kuhamia Dodoma mwezi Julai 2016 wakati alipopewa wadhifa wa mwenyekiti wa chama tawala, Chama Cha Mapinduzi/CCM.
Rais John Pombe Joseph Magufuli alitangaza na kuipandisha hadhi Manispaa ya Dodoma kuwa Jiji la Dodoma mnamo Aprili 26, 2018.
Kama tujuavyo, Dodoma ndio kitovu cha Taifa la Tanzania (Makao makuu ya nchi yetu, Tanzania).
Kwanza nitoe pongezi kwa Uongozi uliopita na uliyopo sasa, katika kuwekeza Jiji la Dodoma, Mfano.​
  • Mji wa Magufuli (Magufuli City)- Mtumba​
  • Uwanja wa Ndege wa Kimataifa- Msalato.​
  • Kituo cha Treni ya Mwendokasi (SGR)​
  • Kuhamishia Wizara zote Dodoma- Mtumba/Udom.​
  • Uboreshwaji wa Ikulu kuu- chamwino.​
View attachment 3007255
Chanzo: Google

TASWIRA ya sasa katika Jiji la Dodoma.

Kwa sasa muonekano wa Jiji la Dodoma, hauhakisi taswira ya Nchi/Taifa. Mbali na juhudi zote bado kuna vipaumbele hatujaviweka/kuvifanyia kazi Ili kuleta taswira ya kitovu cha Taifa letu.

MAMBO YA KUFANYA ILI KUIFANYA DODOMA KUHAKISI TASWIRA YA MAKAO MAKUU YA NCHI.
Napendekeza Mambo yafuatayo yafanyike ili kuipa sifa na hadhi Dodoma kama Kitovu cha Taifa letu Tanzania;-

01. Matumizi ya maeneo yaliyo wazi (Idle lands)
Mfano. Hazina, Jamatini, Iringa road n.k, Maeneo haya na mengineyo yaliyo wazi yanaweza kutumika katika uzalishaji kama, Maeneo ya kufurahia/ Mapumziko (Refreshments & Recreation Centers). Hizi ni sehemu ambazo watu watalipia viingilio na kuweza kupumzika, Kufurahia, Michezo ya watoto na Maeneo ya kuogelea (Swimming Pools). Kwani kwa sasa Dodoma tuna upungufu wa maeneo ambayo watu wanaweza kukutana na kufurahia hasa siku za jioni, Mwisho wa wiki (weekends) na siku za mapumziko (Holidays). Hii itaongeza kipato na ajira kwa wananchi na kuboresha Taswira ya Dodoma.

02. Arena (Dodoma Arena).
Kwa sasa Dodoma hatuna uwanja wa hadhi ya kimataifa. Tunaweza kujifunza wazi kwa mfano wa ukuaji wa Jiji la kigali-Rwanda (Kigali Arena), Uwepo wa Arena ni makutaniko ya wanamichezo, Burudani, Mikutano mikubwa na Matamasha mbalimbali na hii inasaidia kukuza Jiji la Dodoma kwa kuleta Taswira na sifa ya kimataifa. Hii itapelekea ukuaji wa biashara na jiji kiujumla.
View attachment 3007254
Chanzo: AI creation (Future View of Dodoma Arena)

03. Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa (International Conference/Convention Center).
Hadi sasa ukumbi mkubwa wa mikutano ni Jakaya Kikwete International Convention Center (JKICC), Tumekosa uwepo wa kumbi kubwa na za kisasa kama Arusha International Conference Center (AICC), hizi kumbi zinatambulisha na kuleta Taswira nzuri katika Jiji la Dodoma na Itapelekea watu kujumuika katika warsha/Mikutano na makongamano makubwa na kukuza Uchumi wa Jiji na nchi kiujumla.
View attachment 3007256
Chanzo: Google (Future View of Dodoma International Conference Center/ DICC)

04. Makutano ya Kibiashara (International Business Centers).
• Tujiulize swali, kwanini wafanyabiashara wanatoka Kahama, Singida, Mwanza, Shinyamga, Tabora na kwenda kuchukua bidhaa Dar es salaam (Kariakoo)?? Kwanini wavuke Dodoma, wakati wanaweza kuishia hapa kuchukua bidhaa na kurudi mikoani kwao??, Tunaweza kujenga soko kuu la Biashara kimataifa Dodoma na kuwa Lango la Biashara kimataifa zaidi ya kutegemea Dar es salaam (Kariakoo).
• Kuboresha Soko la Mazao (Kibaigwa), Hadi sasa soko la Kibaigwa liko kizamani sana (Local market) mbali na kuwa na jina kubwa Lakini halivutii kabisa, vile sio viwango vyake. Uboreshaji katika miundombinu inahitajika, kama. -Magodown ya kisasa, -Wigo/Fences, -Parking za Magari/Malori, -Office/Vyoo, -Maeneo ya Chakula na Biashara.
• Kuboresha Chalinze nyama & Mbande. Haya ni maeneo maarufu sana kwa nyama na chakula hasa unapoingia Jiji la Dodoma ila sio masafi ni hatari kwa afya na usalama endapo moto ukitokea. Tunaweza kuboresha miundombinu na kuifanya ya kisasa -Parking, -Sehemu safi na salama ya Chakula/ Office/Vyoo, Hiii itasaidia.
• Kulinda afya za Walaji.
• Taswira na sifa ya Jiji la Dodoma.
• Mfumo wa ukusanyaji mapato.
• Ajira zitaongezeka zaidi.
View attachment 3007257
Chanzo: Google (Currently Chalinze Nyama & Mbande).

View attachment 3007258
Chanzo: Google (Future View of Chalinze Nyama & Mbande).

5. Makumbusho & Makitaba ya kisasa.
Tunaweza kuwa na Maono ya kuweka sehemu ya Makumbusho ambayo inayoonyesha na kuielezea historia ya Tanzania, hii itaipa sifa na nguvu Dodoma ambayo ni kitovu na watu kujua historia kwa kuona na kusoma kumbukumbu za nchi yetu, huku ikiwa pamoja na makitaba ya kisasa. Makumbusho ya Dar es salaam, Ule muonekano na Picha inaweza kuhamishiwa hapa Ili ilete maana halisi ya Makao makuu.
View attachment 3007259
Chanzo: Ai Creation (Future View of Dodoma Historical Museum & Library).

6. Uboreshwaji wa Miundombinu na Mipango miji
Dodoma bado tuna upungufu wa Barabara nzuri kuzunguka mji, Ukosefu wa maji na umeme wa uhakika mbali na kuwa na chanzo cha umeme mtera. Mifumo ya utupaji taka ni mibovu tofauti na maeneo kama Moshi/Arusha, mji ni mchafu na haujapangiliwa vizuri kuendana na hadhi ya makao makuu. Chukulia mfano maeneo kama -Makole, -Majengo Sokoni na viunga vyake, -Bahi road, - Kizota. Napendekeza kuwa nyumba na Miundombinu za maeneo hayo viwekwe kisasa zaidi ili kuleta Taswira ya mji wa Dodoma.

HITIMISHO.
Kujengwa kwa mji bora na wakisasa Ili kuleta taswira ya makao makuu ya nchi ni jambo ambalo linagharimu muda na fedha, Lakini ni vizuri kama nchi kuwa na Mipango ya muda mrefu ili Kufanikiwa, Maono ya viongozi husika na utekelezaji wa maono hayo yanahitajika, bila viongozi bora wenye maono hatuwezi kufika kokote. Uboreshaji wa taswira ya Dodoma utaleta faida lukuki kama:-
• Miundombinu bora ya ukusanyaji mapato.
• Mji sana & Afya iliyozingatiwa.
• Ukuaji biashara & uchumi zaidi ya sasa.
• Taswira ya Taifa, kwani Dodoma ni Makao makuu ya nchi.​
Uko vizuri sana mkuu,pokea maua Yako🌾🌾🌾🌾🌾
 
Back
Top Bottom