Nashauri waziri Pinda ajiuzulu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nashauri waziri Pinda ajiuzulu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by hittler, Jul 22, 2011.

 1. h

  hittler Member

  #1
  Jul 22, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama kiongozi wa shughuli za kiserikali bungeni na kama kiongozi katika baraza la mawaziri na vilevile mtendaji mkuu wa serikali sioni sababu ya yeye kuendelea kuwepo katika hiyo nafasi wakati hakuna ata kimoja kipya alichokifanya. Mh Pinda hana maamuzi kama waziri mkuu,hajawahi kusema lolote ata pale inapobidi anasema ningekuwa na mamlaka ningefanya. Kama hana mamlaka anafanya nini basi? Ajiuzulu tujue Tanzania haina waziri mkuu. Wanatufanya wajinga, wanatukebehi bila hururma, wanakula jasho letu bure. Ifike mahali tuwatoe kwenye magari watembee kwa miguu maana hakuna wanachofanya.
   
 2. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #2
  Jul 22, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  bureee kabisa huyu MIZENGWE PINDA. mnyooongee hana analoamua yeye ni siasa tuuuuuuu ndo maana tupo hapa tulipo! mh!
   
 3. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #3
  Jul 22, 2011
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,423
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Sidhani kama yote uliyosema ni kweli lakini nina sababu kubwa ya kumtaka AJIUZULU! Hii kashfa ya Mh 50m- Bwana Jairo - yeye kama kiongozi wa shughuli za serikali bungeni, msemaji mkuu wa serikali, na akatoa hisia zake zote ambazo bila ubishi alichotaka kufanya ni KUMFUKUZA KAZI au KUMSHITAKI Jairo, na hata baada ya kuahidi tena kwa hisia kali kwamba angezungumza na Mh Raisi ili hatua stahili zichukuliwe, KUMBE, Katibu Mkuu Utumish ndiye ana mamlaka, na amempuuza alichokisema Bungeni, anampa Jairo likizo, eti apishe Uchunguzi! Uchunguzi gani? Fedha imekusanywa kutoka maidara ya wizara, zimewekwa kwenye Account ya mojawapo wa mawakala wa Wizara (nje ya ofisi ya KM Jairo), mgao umefanyika nje ya ofisi( hapa ninamaanisha chumba au jengo )- sasa anakaa nje ya ofisi, kwani uchunguzi ni ndani ya ofisi yake! Waongo wakubwa!

  Pinda angepasa kuona kejeli iliyofanyika, badala ya kumshikiza adabu Jairo anapewa ruhusa ya kwenda kutungua sehemu ya yale makusanyo, na Hosea anafaidishwa kwa kumegewa fedha ya walipa kodi achunguze! Ningekuwa Pinda Ningejiuzulu Mara Moja kwa Kudhalilishwa!

  Lingine ni Pinda kutojua ni nani anahusika katika kufukuza makatibu wakuu! KWANZA alifanya uma utambue kwamba URAISI husafiri na aliyeko madarakani, kwani JK alikuwa asubiriwe kutoka South Africa kana kwamba uraisi haukuwepo nchini na ukweli KM Mkuu wa Utumishi amemuumbua, JIUZULU PINDA
   
 4. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #4
  Jul 22, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  kila kitu kinachofanya na serikali hii WE UONE KAMA MAIGIZO TUU UTAISHI KWA RAHA SANA BUT UKIONGEZA AKILI YAKO KIDOGO UNAWEZA KWENDA IKULU NA BUNDUKI!
   
 5. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #5
  Jul 22, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Wewe ndio akili yako ijiuzulu kwa kutoijua katiba ya nchi na ukomo wa madaraka yake ! Soma katiba acha uvivu kama wa bata
   
 6. Mkiliman

  Mkiliman JF-Expert Member

  #6
  Jul 22, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 957
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  PINDA amepinda kweli kwani majibu na mambo anayoonekana kutenda ni kama gizani. Anaigiza huruma, hofu, upole, bidii na karama nyingine nyingi, hayo yote ni udhaifu usiofaa ktk kuongoza jamii yenye mitazamo, matukio na shida mbalimbali kama hapa tz. These psuedo leaders will never resign on their own unless they're topped by mass revolts.
   
 7. F

  FJM JF-Expert Member

  #7
  Jul 22, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Nakubaliana na mtoa mada hii na nilitarajia Pinda ampe Rais 'live' kwamba; ama Jairo abakie kwenye serikali yake au yeye Pinda, lakini wote wawili hawawezi kubakia serikali. Haiwezekani. Ukitafakari kauli aliyotoa Pinda baada ya kikao cha CCM bungeni last week ni wazi kuwa alikuwa ameridhika Jairo amekiuka 'kanuni' za utawala bora na hivyo alihitaji tu kum-consult Rais ili hatua za kinidhamu zichukuliwe.

  Lakini kama kuna mtu amesoma Tanzania Daima ya leo 22/07/11 kauli aliyotoa Katibu mkuu kiongozi Philemon Luhanjo ni kama yeye katibu mkuu ana mamlaka ya kumchukulia hatua Jairo. Luhanjo anasema amenukuliwa akisema hivi “Nimeona niwaambie hili ili tusiendelee kuwaambia wananchi tunamsubiri Rais, wakati mimi mwenye dhamana ya kusimamia nidhamu nipo hapa, nimeshachukua hatua".

  Luhanjo anaendelea “Kutokana na uzito wa jambo hili, nimelazimika kumwamuru CAG, Ludovick Utuoh, kufanya uchunguzi ndani ya siku 10 na iwapo itabainika kuwa ana kosa, hatua nyingine za kisheria zitafuata” .

  Sasa tujuilize:
  1. Katibu mkuu kiongozi ana mamlaka kumshinda Waziri mkuu wa Nchi?
  2. Katibu mkuu kiongozi ana mamlaka kumshinda makamu wa rais ambaye kikatiba ndiye aliyekuwa anakaimu kiti cha urais wakati rais yupo nje ya nchi?
  3. Kama Katibu mkuu kiongozi ndiye mtu mwenye mamlaka kwa nini Pinda akapeleka mashauri kwa Rais na sio kwa Katibu mkuu kiongozi?

  It is unbelieavable that Katibu mkuu kiongozi anaonekana kuendesha nchi wakati kikatiba Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Spika wa Bunge ndio wako kwenye safu ya kuongoza kama Rais hayupo. Kama Pinda atanyamazia hili (inaonekana kuwa hivyo) akae akijua mawili:
  1. Mbele ya watanzania ataonekana mtua asiyekuwa na mamlaka yeyote, asiyejuwa nini kinaendelea na asiyesimamia chochote!
  2. Kubwa zaidi, nafasi ya u-waziri mkuu kama kiongozi wa shughuli za serikali inakuwa -obsolete'. na watanzania watakuwa na kila sababu/haki ya kudai nafasi hii ifutwe ili kuondokana na gharama zisizo za lazima maana nafasi ya Katibu mkuu kiongozi inatosheleza! Afte all the person who took action ni Katibu mkuu kiongozi. Prime Minister's office can go.
   
 8. Donnie Charlie

  Donnie Charlie JF-Expert Member

  #8
  Jul 22, 2011
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 6,574
  Likes Received: 840
  Trophy Points: 280
  nakubaliana na wewe kabisa kuwa ukitathimini kwa kina kuhusu viongozi wetu utatamani ujitoe mhanga na ******
   
 9. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #9
  Jul 22, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Unahitaji dose ya kutosha ya Elimu ya Uraia. Hicho ulichoandika kina mapungufu mengi, hukupaswa hata kujiuliza hayo maswali kuhusu madaraka ya PM, VP na CS katika uendeshaji wa Nchi. Sakata la Jairo limekuwa Politicised bila sababu, amekosea kama Mtumishi wa Umma na anatakiwa kuchukuliwa hatua kwa utaratibu uliowekwa na Sheria ya Utumishi wa Umma 8/2002 pamoja na regulations zake ambayo haina nafasi kwa VP na PM. Aachwe CS achukue hatua na Rais atatoa uamuzi wa mwisho baada ya kupokea mapendekezo ya CS.
   
 10. F

  FJM JF-Expert Member

  #10
  Jul 22, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Read my comments again. Sijauliza kifungu cha sheria, nimeuliza nani ana mamlaka ya ku-implement hicho unachoita sheria ya utumishi wa umma 8/2002. Waziri mkuu yeye anasema anamsubiri Rais, Katibu mkuu kiongozi who according to our governance structure ni junior kwa Waziri anaonekana (with evedince) kuwa na mamlaka au uwezo kwa ku-implement kitu ambacho Waziri mkuu hawezi? What is so difficult for you to grasp this upside-down management/governance style? Nini maana ya kukaimu urais? Katiba inasemaje? Somo gani la uraia linasema kuwa Katibu mkuu atakuwa na mamlaka kushinda Vice President au Prime Minister?
   
 11. Manumbu

  Manumbu JF-Expert Member

  #11
  Jul 22, 2011
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 1,751
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  kama anaitakia mema hii nchi, naunga mkono hoja. Pinda ajiuzulu tena bila ya kusubiri bosi wake akubali. atangaze kujiuzulu akipinga utendaji kazi wa serikali... itatusaidia sana kama nchi
   
 12. delabuta

  delabuta Senior Member

  #12
  Jul 22, 2011
  Joined: May 23, 2011
  Messages: 179
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naunga mkono hoja ajiuzulu kwa sababu hajui anachokifanya
   
 13. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #13
  Jul 22, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,190
  Likes Received: 996
  Trophy Points: 280
  .Hii tumu ya kutetea makengeza ya serikkali, nikiitizama kwa jicho la ndani kabisa naona ina ilmu ya chuo kikuu cha madrasa. Naipongeza kwa usomi wa ilmu ya juu kabisa na umakini wa kujibu kila hoja kwa mtizamo elekezi..
   
 14. H

  Haki Yetu Senior Member

  #14
  Jul 22, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 162
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli hata mimi nashangaa sana. Kwani urais hua unasafiri? Nadhan JK aliposafiri alimkaimisha mtu mwingine madaraka ya urais. Kimantiki ni kwamba ofisi ya Raisi huwa inakaliwa na mtu wakati wote. Kama rais akiondoka hakaimishi mtu ofisi yake basi tumekwisha.

  Pinda ni mtu aliyefanya kazi Serikalini kwa muda mrefu sana. Taratibu za ofisi anazijua vizuri sana. Kwanini yeye alimkaimisha majukumu ya kiongozi wa shughuli za Serikali Bungeni Sitta wakati aliposafiri?

  Tabia hii aliyoionyesha na kutufanya watanzania tuamini kuwa sakata la Jairo mpaka JK awepo ndo liamuliwe ni unafiki mkubwa sana. Kwanini alishindwa kuwasiliana na kaimu rais ili hatua zichukuliwe? Pinda ni mtu ambaye watanzania wengi tulikua na imani naye, lakini anapoelekea atakuja kuijutisa nafsi yake.

  Naunga mkono hoja ya mwanajamvi kuwa, angempa taarifa JK kuwa amfute kazi Jairo au la yeye Pinda ajiuzulu. Kama si hivyo mambo yanayokuja ni makubwa zaidi.
   
 15. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #15
  Jul 22, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,041
  Likes Received: 6,479
  Trophy Points: 280
  sorry nina hasira, nitarudi.
   
 16. THE PERFECT

  THE PERFECT Member

  #16
  Jul 22, 2011
  Joined: Jun 22, 2011
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu mbona huyo hatufai kitambo ni mnafiki.... mwanzo alisema aliomba mungu asichaguliwe kuwa PM mara akasema ni mapenzi ya Mungu kuwatumikia wa-tz anyway ni PM wa kwanza kumfukuza kazi mtendaji wa kata huko kwao mpanda tokea hapo hajawahi kumfokea wala kumfukuza kazi mtendaji yoyote. alipewa report mtu hafai yeye anamhamisha kituo ofcoz naunga hoja mkono.
   
 17. H

  Heri JF-Expert Member

  #17
  Jul 22, 2011
  Joined: Aug 28, 2007
  Messages: 242
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Je Katibu Mkuu Kiongozi amewahi kumuadabisha katibu mkuu yeyote tangu hiyo sheria imetungwa?
  Luhanjo na Jairos wametoka mbali pamoja na JK. Walikuwa wote Foreign.
  Swali la kizushi ni Je waziri mkuu angekuwa Lowassa , hii scandal ingekwenda vipi?
   
 18. Mwita Matteo

  Mwita Matteo JF-Expert Member

  #18
  Jul 22, 2011
  Joined: May 16, 2010
  Messages: 216
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  [h=2][/h]
  [​IMG] By sikubaliki [​IMG]
  Unahitaji dose ya kutosha ya Elimu ya Uraia. Hicho ulichoandika kina mapungufu mengi, hukupaswa hata kujiuliza hayo maswali kuhusu madaraka ya PM, VP na CS katika uendeshaji wa Nchi. Sakata la Jairo limekuwa Politicised bila sababu, amekosea kama Mtumishi wa Umma na anatakiwa kuchukuliwa hatua kwa utaratibu uliowekwa na Sheria ya Utumishi wa Umma 8/2002 pamoja na regulations zake ambayo haina nafasi kwa VP na PM. Aachwe CS achukue hatua na Rais atatoa uamuzi wa mwisho baada ya kupokea mapendekezo ya CS.  Read my comments again. Sijauliza kifungu cha sheria, nimeuliza nani ana mamlaka ya ku-implement hicho unachoita sheria ya utumishi wa umma 8/2002. Waziri mkuu yeye anasema anamsubiri Rais, Katibu mkuu kiongozi who according to our governance structure ni junior kwa Waziri anaonekana (with evedince) kuwa na mamlaka au uwezo kwa ku-implement kitu ambacho Waziri mkuu hawezi? What is so difficult for you to grasp this upside-down management/governance style? Nini maana ya kukaimu urais? Katiba inasemaje? Somo gani la uraia linasema kuwa Katibu mkuu atakuwa na mamlaka kushinda Vice President au Prime Minister?.......

  Mimi hapa ninacho kiona ni PM kutozijua kanuni na taratibu za Utumushi wa umma au kuwa mnafiki.


   
 19. Nzowa Godat

  Nzowa Godat JF-Expert Member

  #19
  Jul 22, 2011
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 2,630
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Mtoto wa mkulima asijiuzuru ni kijana safi aliefundishwa kazi na Mwl. Nyerere na akafundishika. Alikuwa mbunge wa kwanza kukataa shangingi (gari la kifahari).
   
 20. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #20
  Jul 22, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Nikikurejesha kwenye comments zangu unaweza kuona nakukosea heshima. Mkuu kwa taarifa yako PM hana powers za kushughlikia Nidhamu za Watumishi wa Umma na hakupaswa kuonesha kuwa anazo siku ile Bungeni.
   
Loading...