Nashauri waziri Pinda ajiuzulu

[h=2][/h]
quote_icon.png
By ......Mimi hapa ninacho kiona ni PM kutozijua kanuni na taratibu za Utumushi wa umma au kuwa mnafiki.​
Mwita nakubaliana na wewe mia kwa mia kwamba Pinda hajui taratibu za Utumishi wa Umma, hilo la Unafiki mie simo.
 
Sikubaliani na wazo lako. wajiuzuli wengine lakini sio huyo mtani wangu.
Kama kiongozi wa shughuli za kiserikali bungeni na kama kiongozi katika baraza la mawaziri na vilevile mtendaji mkuu wa serikali sioni sababu ya yeye kuendelea kuwepo katika hiyo nafasi wakati hakuna ata kimoja kipya alichokifanya. Mh Pinda hana maamuzi kama waziri mkuu,hajawahi kusema lolote ata pale inapobidi anasema ningekuwa na mamlaka ningefanya. Kama hana mamlaka anafanya nini basi? Ajiuzulu tujue Tanzania haina waziri mkuu. Wanatufanya wajinga, wanatukebehi bila hururma, wanakula jasho letu bure. Ifike mahali tuwatoe kwenye magari watembee kwa miguu maana hakuna wanachofanya.
 
.Hii tumu ya kutetea makengeza ya serikkali, nikiitizama kwa jicho la ndani kabisa naona ina ilmu ya chuo kikuu cha madrasa. Naipongeza kwa usomi wa ilmu ya juu kabisa na umakini wa kujibu kila hoja kwa mtizamo elekezi..
Mchango wa Great Thinker huo!! Ha ha ha haaa...!!!!
 
Nakubaliana na mtoa mada hii na nilitarajia Pinda ampe Rais 'live' kwamba; ama Jairo abakie kwenye serikali yake au yeye Pinda, lakini wote wawili hawawezi kubakia serikali. Haiwezekani. Ukitafakari kauli aliyotoa Pinda baada ya kikao cha CCM bungeni last week ni wazi kuwa alikuwa ameridhika Jairo amekiuka 'kanuni' za utawala bora na hivyo alihitaji tu kum-consult Rais ili hatua za kinidhamu zichukuliwe.

Lakini kama kuna mtu amesoma Tanzania Daima ya leo 22/07/11 kauli aliyotoa Katibu mkuu kiongozi Philemon Luhanjo ni kama yeye katibu mkuu ana mamlaka ya kumchukulia hatua Jairo. Luhanjo anasema amenukuliwa akisema hivi “Nimeona niwaambie hili ili tusiendelee kuwaambia wananchi tunamsubiri Rais, wakati mimi mwenye dhamana ya kusimamia nidhamu nipo hapa, nimeshachukua hatua".

Luhanjo anaendelea “Kutokana na uzito wa jambo hili, nimelazimika kumwamuru CAG, Ludovick Utuoh, kufanya uchunguzi ndani ya siku 10 na iwapo itabainika kuwa ana kosa, hatua nyingine za kisheria zitafuata” .

Sasa tujuilize:
1. Katibu mkuu kiongozi ana mamlaka kumshinda Waziri mkuu wa Nchi?
2. Katibu mkuu kiongozi ana mamlaka kumshinda makamu wa rais ambaye kikatiba ndiye aliyekuwa anakaimu kiti cha urais wakati rais yupo nje ya nchi?
3. Kama Katibu mkuu kiongozi ndiye mtu mwenye mamlaka kwa nini Pinda akapeleka mashauri kwa Rais na sio kwa Katibu mkuu kiongozi?

It is unbelieavable that Katibu mkuu kiongozi anaonekana kuendesha nchi wakati kikatiba Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Spika wa Bunge ndio wako kwenye safu ya kuongoza kama Rais hayupo. Kama Pinda atanyamazia hili (inaonekana kuwa hivyo) akae akijua mawili:
1. Mbele ya watanzania ataonekana mtua asiyekuwa na mamlaka yeyote, asiyejuwa nini kinaendelea na asiyesimamia chochote!
2. Kubwa zaidi, nafasi ya u-waziri mkuu kama kiongozi wa shughuli za serikali inakuwa -obsolete'. na watanzania watakuwa na kila sababu/haki ya kudai nafasi hii ifutwe ili kuondokana na gharama zisizo za lazima maana nafasi ya Katibu mkuu kiongozi inatosheleza! Afte all the person who took action ni Katibu mkuu kiongozi. Prime Minister's office can go.
Mkuu,nakubaliana na ww 100%,kwamba kupitia huyu Pinda nafasi ya Primier imeonekana kama haina maana yyte.Unaweza pia kurejea suala la spika wa bunge kujitwisha jukumu la kumjibia maswali katika vikao mbali mbali vya bunge hivi karibuni,pinda asijue kwamba an udhalilisha u PM,badala yake yye anafikiri anasaidiwa!.Au kwa vile meijaza nafasi ya aliye kuwa bosi wake(EL),anaona hayuko huru(he wasn't JK's first choice!)
 
Waziri mkuu mheshimiwa Pinda ni moungo aliyefuzu ktk hiyo fani, ningekuwa na uwezo ningempatia PHD ya uongo, nani kasema Pinda amekataa shangingi? Nenda Dodoma umwone anavyokula kiyoyozi kwenye mshangingi, tena zinafuatana mbili kwa taarifa yako na msafara mkubwa tu. Angekuwa kweli amefundwa na Mwl Nyerere akafundika angehakikisha ata wakurugenzi wa wilaya,miji na majiji hawapandi mashangingi. Kuna haja gani ya wakurugenzi kupewa mashangingi? Pinda anatudanganya Watanzania. Nchi hii haina wazalendo tene walikwisha kufa siku nyingi, watu wamevaa ngozi ya kondoo,wanakaa majukwaani wanaonyesha hisia za dhati lakin wakitoka wanakaa na hao wanaowaita mafisadi wanatucheka. Tusikubali kuwasikiliza watu kama kina pinda, hawana huruma na sisi wanajali matumbo yao. Pinda siyo mzalendo, hana uzalendo na wala hajawahi kuwa mzalendo alikosa nafasi ya kula akawa anajifanya mzalendo mbona leo hii hajiiti mtoto wa mkulima?
 
Ndugu yangu unakosea, sitashangaa kusikia au kuona kuwa nawe upo ktk kundi lililobebwa na serikali au kupewa vipau mbele bila vigezo, na mashaka na elimu yako, upeo wako na ata washauri wako
 
Ni hakika kama kweli ndio mwenendo huo wa KUOGOPANA naona MMOJA ambaye ni mdogo KUMPISHA mwingine aendelee na UTAWALA WAKE.Iweje unajua kuwa unajua unaambiwa ujui.Utajisikiaje umeambia umma kuwa maamuzi ambayo ungeyachukua kulingana na tukio ambalo Watanzania waliliona dhahili na jinsi wewe pia ulivyoliona kisha unakuwa sio bwana wakubwa wenzio wanavyotaka.

Kaa pembeni tuone tofauti,utakumbukwa kwa msimamo wa kujitoa kwa niaba ya Watanzani ana kuwapa picha kuwa CHUMBANI SIO SHWALI TENA.Walioko sebuleni wajitayarishe.
 
Tatizo la Mh. Pinda ni kwamba hajui mamlaka aliyopewa kupitia Uwaziri Mkuu.
This is absolute disqualification!
 
Mimi nadhani haya matukio yanatupa mwangaza wa kujua mema na mabaya ya katiba yetu. Hebu tujiulize kikatiba tumekwama wapi. Najua PM ni kiongozi wa shughuli za serikali bungeni na ni kiongozi wa Mawaziri wote. Je kinidhamu nafasi ya PM ikoje? Alikosea ama nini kifanyike. Nafikiri tulifikirie jambo hili kimapana ili liwe precedent katika katiba yetu tunayoipigania. Bila kujua utakuwa mjinga kwa muda
 
Back
Top Bottom