Viongozi wetu wanatumia nafasi zao kuibia wananchi

NANCA

Member
Jun 23, 2023
92
100
-Mwaka fulani nlikutana na mtu akilalama kua mbunge kigwa anataka kuwadhurumu eneo lao huko kigamboni ambapo mbunge huyo alianza kwa kuchimba visima Kama hatua ya unyang'anya eneo hilo. Binafsi sikumjali, nkamuona Kama mwehu
-Mwaka 2021 nkiwa mwanza nakutana mzee mmoja ameishiwa, ananiomba nauli ili kurudi kwake ukerewe baada ya kufuatilia kesi ya ardhi huko mahakama kuu baada ya kutwaliwa kibabe ardhi yao na kiongozi mmoja
-Kwa zaidi ya miaka saba naisikia kesi ya familia fulani dhidi ya halmashauri fulani ambapo halmashauri inataka ichukue eneo ambalo familia hyo inadai ni yake. Kesi hyo imeisha juzi tu kwa makubaliano na familia lkn nyuma ya kesi hyo alikueko mbunge ambae aliichochea ili kutwaa ardhi ile kwa kisingizio maslah ya umma.
  • Juzi hapa nlipata habari juu ya kesi ya mama mmoja ambapo eneo lake walihamishiwa watu ambao maeneo yao yalivamiwa na maji ya ziwa hvyo mbunge kwa kushirikiana na mamlaka wakahamishia watu hapo bila mwenye eneo kuridhia, wakahamishia tena wauza magenge bila mwenye eneo kuridhia. Mwenye eneo akashtaki mahakamani na baada ya vuta ni kuvute mahakama ikaamua ushuru wote wa wafanyabiashara alipwe mwenye eneo.
  • Sasa hivi pira limenigeukia mm na ndipo naona maana halisi ya vilio vya walokua wakilia maeneo yao, ndo naona ubaya wa viongozi wa kiserikali na kisiasa ndio ninaona roho ya kishetani ya mbunge huyo, ndo naona jinsi watu wanavyotumia mamlaka na vyombo vya serikali kwa manufaa yao ndio ninaona jinsi wabunge wa nchi hii wanavyofanana na majangiri jinsi wanavyotumia watendaji halmashauri kunyang'anya maeneo ya watu. Mbunge anakuja na mpango wa mradi labda shule, kisha anawaambia nataka eneo fulani, fidia ntatoa mm ila muwaambie wananchi kua ni serikali(lenye fursa kwake) mkurugenzi anabariki ata Kama anajua kinachoendelea, kisha kwa kushirikiana na mbunge wanamwagiza mtendaji wa Kijiji kuitisha vikao uchwara na wenye maeneo ili kuwashawishi, wanaita ma surveyor na wathamini ili mbunge alipe hizo fidia uchwara, mtu anaegomea basi chawa wake wanampigia kwamba fulani amegoma, mbunge anamwambia kamishina wa ardhi kua nakuamini, kamishina nae anasema sintakuangusha mkuu.
-Kwahyo kiufupi ndio nipo ktk hali Kama hyo, sijashirikishwa ktk kuelewana fidia, sijapewa taarifa/barua au document yoyote kuhusu utwaaji huo ila nakuta tu wapo ktk eneo langu. Wabunge wanatumia ubunge tuliowapa wenyewe kutuadhibu, kila eneo zuri na lenye fursa wanataka liwe lao, watu mmekaa pakiwa vichaka hawakuleta mradi leo hii pamekua mjini eti ndo pyepyepye, wanatumia vibaya sheria ya utwaaji, pia wanatumia vibaya mstari kua ardhi ni mali ya rais, yaani wao ndo wenye haki ya kujenga maisha ya watoto wao ila sio sisi maskini. Kiufupi nchi hii ni yao, bora waseme hvyo tujue
-Ujumbe huu umfikie Rais. Samia Suluhu Hassan, waziri mkuu kasssim majaliwa, makamu wa rais Philip mpango, waziri tamisemi, waziri wa ardhi Jerry slaa na wabunge woooote, mseme Kama ardhi zote nzuri, zilizo pazuri, zilizo kaa vyema kibiashara Kama ni kwaajili yenu Basi semeni, mbunge anasema analeta maendeleo kumbe anajiletea maendeleo, barabara anajipitishia kwake kwanza, viwanja anajikusanyiaaaa wwwww, anannua wwww na vingine anatumia janja, mahala pakisha endelea mara unasikia serikali inataka kutwaa kuweka mradi ila mbaya husikiii maeneo ya watu hao vibopa yakipitiwa na miradi labda awamu iliyopita Tena kidogo.
-Mwisho, anaetaka eneo langu aje tuongee bei, kuja na gia ya mradi wa serikali haitosaidia kitu.
 
Bila kutaja eneo husika na kumtaja mbunge husika bandiko hili linakuwa kama riwaya ya kusadikika!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom