Cheo cha Unaibu Waziri Mkuu na uhusiano wake katika kukuza utendaji

Imma_Magira

Member
Jan 8, 2022
18
26
Na. Emmanuel Magira Werema

Ifahamike na ieleweke kuwa maamuzi yoyote yanayotakiwa kufanywa na serikali ya nchi yoyote ile duniani, ni lazima yawe yamefanyiwa uchambuzi wa kina kwasababu serikali inaendeshwa kwa kuzingatia uhalisia (facts) na sio nadharia.

Mfano serikali ikiamua kufikia maamuzi ya kufanya mabadiliko katika sekta mbalimbali kama Elimu na nyingnezo lazima itazingatia uwepo wa facts zinazolazimu mabadiliko hayo. Zaidi pia ita asssess data zilizopo kwa kulinganisha na utendaji wa nyuma( kabla ya ufikiaji wa utekelezaji wa maamuzi au sera mpya).

Baada ya kuangazia mchakato huo. Basi tuendelee na maamuzi ya uwepo wa nafasi ya Unaibu waziri mkuu. Kufuatia seeikali kufanya mabadiliko hivi karibuni katika wizara kadhaa, uliombatana uteuzi wa Mh. Dotto Biteko kushika wadhifa wa kuwa Naibu waziri mkuu, umezua chokochoko nyingi kwani kumekuwepo na baadhi ya watu kutilia shaka uteuzi huo, lakini hoja za utetezi wa uteuzi huo kama mbili (2) hivi ambayo ni Katiba (ingawa haionyeshi moja kwa moja) pamoja na kigezo cha uzoefu.

1. Kikatiba
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 haielezi moja kwa moja uwepo wa cheo hiki, pia hakuna kifungu kinachozungumzia moja kwa moja kuhusu cheo cha Naibu Waziri Mkuu. Ingawa, Ibara ya 36 ya Katiba hiyo inampa Rais Mamlaka ya kuanzisha na kuwateua watu wa kushika nafasi za madaraka.

Ibara ya 36
"(1) Bila ya kuathiri masharti mengineyo yaliyomo katika Katiba hii na ya sheria nyingine yoyote, Rais atakuwa na mamlaka ya kuanzisha na kufuta nafasi za madaraka ya namna mbalimbali katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano."

2. Kiuzoefu
Uteuzi huu unaonekana uko legitimate, kwasababu ya uwepo wa uteuzi wa nafasi kama hi, kipindi cha nyuma kumekuwepo na uteuzi wa baadhi ya viongozi waliowahi kushika wadhifa huo.
1. Salim Ahmed Salim (1985 aliteuliwa)
2. Augustino Lyatonga mrema (1993 alipandishwa cheo kutoka waziri wa mambo ya ndani)

Sasa basi, tumekwisha kuona uhalali unaothibitisha uwepo wa cheo hiki( Ingawa unaeza usiwe halali moja kwa moja). Hivyo kuna baadhi ya vitu vya kujiuliza na kutafakari ikiwa kama una uelewa wa kufanya hivyo. Mimi binafsi naweza kutumia uelewa wangu wa kawaida kuweza kureason juu ya swala hili kama ifuatavyo.

Tangu nchi hii ipate uhuru, ni mara 2 tu umuhimu wa cheo hiki ulionekana na hvyo watu wakateuliwa kushika nafasi hizo. Lakini swali la kujiuliza kama nafasi hii ilionekana ni nyeti na muhimu katika utendaji, kwanini serikali isingefanya mchakato wa cheo hiki kuwepo wazi na kifahamike kikatiba (na sio katiba kuwa silent kwenye cheo hiki)?

Kwasababu, serikali lazima ifanye evaluation ya facts kupima perfomance, na hii hufanyika kuassess facts zilizopo pamoja kuzingatia facts za kipindi cha nyuma ili kufahamu kuwa kama kuna uhitaji wa kutekeleza sera/maamuzi mapya.

Je, serikali ilipima facts za utendaji kazi wa kipindi cha akina Augustino Mrema na kuona utendaji kazi wao ulkuwa ni mkubwa kuliko sasa hadi kuona tunahitaji naibu waziri mkuu?

Lakini pia doubts niliyonayo ni kuwa naskia Augustino Lyatonga Mrema aliwahi kuomba mafao yake katika kutumikia cheo na akaliomba Bunge kuidhinisha walau asilimia kadhaa bado ikawa holaaa, na bado Bunge likamhitaji atoe kielelezo cha kikatiba kinachoidhinisha malipo ya cheo cha unaibu Waziri Mkuu (akuna kifungu chochote cha katiba kinachoeleza nafasi hii). Kama nafasi kubwa kama hyo ya utumishi inakuwa na contradictions katika mafao kuna uhalali gani hapa?

My take

1. Nia ya serikali yetu inaweza kuwa ni jema kabsa katika kukuza utendaji, lakini uwepo wa nafasi hii bado unaeza ukafeli kukuza utendaji na badala yake kusababisha chaos(vurugu) za kiutendaji kutokana na kuingiliana kimajukumu.

Kwanini nasema hivi? Nafasi ya waziri mkuu ni mtendaji na muangalizi wa shughuri zote za kiserikali, wakati huohuo Naibu waziri mkuu pia ata-act kama mtendaji wa shughuri zote za kiserikali. Je ni picha gani hapa unaipata?

Mbaya zaidi, Mh. Dotto Biteko pia anayo wizara anayosimamia tofauti na unaibu waziri mkuu. Sasa hapa ni nani atashuhurikia utendaji wa shughuri ya wizara yake? Ikiwa yeye binafsi ana mamlaka ya kushuhurkia utendaji wa wizara zote?

2. Cheo hiki ni muhimu katika kukuza utendaji, endapo tu kitapatia ufafanuzi mzuri kikatiba (Ndio maana katiba mpya ni muhimu). Hii itarahisisha mgawanyiko wa majukumu, pamoja na kuonesha limits baina ya Nafasi hii ya Naibu waziri mkuu na ile ya waziri mkuu.
 
Back
Top Bottom