Nashauri tupunguze idadi ya wabunge

Sasa hivi hakuna upinzani mjengoni, huwa ndio wakati mzuri wa kuwabana.
 
Tunaweza kuondoa wabunge wa vitu maalum. Hakuna uhitaji huo tena.
 

Tungependekeza wafute kabisa maana sioni kazi wanayofanya Subwoofer anakua kama rabastampu ya mapendekezo yote ya serikali.
 
Sasa hivi hakuna upinzani mjengoni, huwa ndio wakati mzuri wa kuwabana.
Ile team covid ipo kule mkuu!
Wanatuchezea akili, siyo wanachama wa chama cha siasa ila ni wabunge!

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Na mishahara ipunguzwe,walipwe laki 5 tu..hapa wazalendo tutawapata wa kuwatetea wananchi la sivyo wananchi wataona ubunge ni fursa.Mkuu naww UNADEMKA?😊😊
 
Huu Uzi nimeupenda.Yaani ingewezekana Uchaguzi wa 2025,hii Kitu ianze rasmi.Kila Wilaya kuwepo na mbunge mmoja TU wa kuchaguliwa bila kujali ukubwa wa Wilaya husika.Mbona KILA Wilaya tuna MKUU mmoja TU wa Wilaya(bila kujali ukubwa wa Wilaya) na Mambo yanaenda ? Hoja yako Nimeipenda mkuu.Ila kwa kuongezea hoja yako,Hata wabunge wa viti Maalum kwa KILA mkoa pia wangeondolewa,wabaki wabunge wa viti Maalum kwa baadhi TU ya makundi muhimu ya akina mama.Viti Maalum kwa KILA mkoa Ni Nafasi zimewekwa kupeana ulaji TU.
 
Viti Maalum ni upigaji mtupu wa pesa za walipa kodi
 
Nami naunga mkono. Hivi Nani huwa anatengeneza majimbo, je ana uwezo wa kuvunja na kukuunganisha Jimbo?
Isije ikawa mpaka suala license kuamuliwa bungeni na wabunge wenyewe, hapo mjadala utafeli
 
Serikali ndio inaamua idadi ya majimbo
Nami naunga mkono. Hivi Nani huwa anatengeneza majimbo, je ana uwezo wa kuvunja na kukuunganisha Jimbo?
Isije ikawa mpaka suala license kuamuliwa bungeni na wabunge wenyewe, hapo mjadala utafeli
 
Hata watumishi wa umma nao wapunguzwe wabaki wachache watakaoboreshewa maslahi yao na kupewa vitendea kazi ili utendaji wao uwe na tija
 
Wabunge wa Zanzibar wangepunguzwa.ila.idadinya kura zao zingehesabiwa kulingana.na uwiano wa sasa mfano kama sasa hivi idadi yao ni 113! Sawa na asilimia 40 wanaweza kupunguzwa hadi wabunge 40 lakini kwenye upigaji kura kila kura moja ikahesabika Ni kura 2.825 huku bara nqo wqkipunguza wabunge kwenye majimbo yenye idadi ndogo ya wqtu pamoja nq kupunguza viti maalumu
 
Tunaweza kuondoa wabunge wa vitu maalum. Hakuna uhitaji huo tena.
Viti maalum kazi yao kubwa ni kuongea visivyo na mashiko kama huyo aliyekuja na hoja za nguvu za kiume
 
Pia Bunge la Zanzibar sasa iwe lazima wabunge tokea Tanganyika waingie kule, siyo wao kuwa na Bunge lao binafsi kisha wao wanaingia Bungeni Dodoma pasipo wa wabunge wa Tanganyika kwenda Bungeni kwao, cha Zanzibar ni cha wazanzibar tu na cha Tanganyika ni cha wote hii dhana ifutwe sasa, wabunge wawe huru kuingia Bungeni kote kote, Zanzibar kuendelea kula posho Dodoma ni wizi lazima wabunge wa Tanganyika wale posho Zanzibar iwe ngoma sawa.
 
Hata watumishi wa umma nao wapunguzwe wabaki wachache watakaoboreshewa maslahi yao na kupewa vitendea kazi ili utendaji wao uwe na tija
Watumishi wakipunguzwa itakuwa tabu mitaani familia zitataabika mno, wa kupunguzwa ni wabunge pekee ndiyo wameonekana mzigo kwa kodi za watanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…