Nashauri Jen. Venance Mabeyo asome kitabu "Army of None" cha Paul Scharre ili atuondolee aibu ya kubebesha magunia makomandoo kwenye sherehe za uhuru

Mleta mada hajui vita
Kuna ebeo unahitaji physical presence sio teknolojia tu

Osama kuua kulitumika mbinu zote physical na technological

Kuteka hutumii teknolojia tu au kupambana na magaidi huhitaji teknolojia tu

Hata kupambana mijini na porini na kuteka mijasusi kunahitaji physical
Kubeba magunia tupu kunaisaidia nn Tanzania
 
Nanyi wote wawili mkasome:-

1. War is mainly a catalogue of blunders. ... The power of making war often prevents it, Lewis F. Korns.

2. War settles nothing, Herbert V. Prochnow.

3. Armies are not bad things in themselves; it’s war that’s evil, Dwight D. Eisenhower.

NB.
Duniani kote watu weupe wanaiheshimu Afrika pekee kwa vita aina ya guerrilla (vita vya msituni) . Hii ndiyo version ya vita iliyoleta ukombozi Afrika. US imejaribu kujifunza guerrilla lakini imewashinda, wamepoteza wapiganaji wengi kwenye mazoezi ya medani ya guerrilla. Guerrilla haihitaji teknolojia kubwa ya gharama na inahitaji mbinu kama hizo za ubebaji magunia mgongoni (uimara physically).

Aidha, Afrika haina uwezo wa kununua teknolojia hizo unazosema, labda baada ya miaka 50 ijayo, hivyo inabidi Afrika itegemee ilichonacho mkononi (guerrilla/ubebaji magunia).
What is ur opinion about King David. Jamaa hakuwahi kushindwa vita yoyote. What was his military techniques?
 
Hiyo teknolojia tunayo?
Idd Amin Dada tulimpiga kwa akili kwa silaha zake za msaada.

Tz imewekeza kwenye mafunzo zaidi (akili) wakati ikisubiri kupata uchumi wa kununua teknolojia.

Tz inajifunza silaha ambazo haina na haiwezi kuzinunua hata kwa miongo 4 mbele, ikitokea vita kama ilivyokuwa Kagera, TPDF inatumia akili kuteka na kuchukuwa silaha hizo za teknolojia ya juu na kuzitumia kushinda medani.

Ndyo maana ni jeshi bora Afrika ambalo UN inalitegemea sana kwasababu silaha nyingi ilizonazo UN, TPDF inajuwa kuzitumia bila kuhitaji mafunzo makubwa japo hainazo kwenye makambi yake.
 
Ndugu siku hizi ukiwa huwezi kubuni na kuitumia teknolojia kwenye vita wewe ni dhaifu sana, hayo mabavu wala hayakusaidii kitu. UTAPIGWA MA MISULI YAKO. NA HAKIKA NAKWAMBIA NDANI YA MIAKA 20 TU IJAYO HUTOONA WANAJESHI WAKIENDA VITANI BALI WANAKAA OFISINI LAKINI WANAFANYA MAMBO.
inaonesha hujui chochote kuhusu vita, marekani ndio wako juu kiteknolojia, umefuatilia mafunzo ya komandoo wao au uingereza? unademka dogo!
 
Unatazama in a narrow way

Kitabu kimoja kama reference ndio unaconculde in that way!?

Vita imehama focus but the threat still persists so challenging in that way you do means you lack basic knowledge ya mambo ya kijeshi
😍
 
Hawa Wamarekani vipi

images (9).jpeg


images (2).jpeg


images (3).jpeg
 
Na wewe nenda kasome " the art of war" by Sun Tzu.

"Pretend to be weak when ur stronger and stronger when ur weak so that u will make ur enemies to focus on the tree instead of the whole forest." Sun Tzu

Mabeyo yupo Sahihi kuliko unavyo weza kufikiri..


Huyo Paul Scharre ni kabulyage
Najibizano ya namna hii ndio majibizano bora zaidi duniani kwa mtazamo wangu mimi
 
Shalom from Jerusalem,

Imekuwa ni kawaida sasa kwenye kila sherehe za uhuru wa Tanganyika ama mapinduzi ya Zanzibar jeshi letu la ulinzi la wananchi wa Tanzania kutuonesha siraha na mbinu za kivita. Miongoni mwa mbinu hizo ni makomandoo wetu kubebeshwa mizigo na magunia mazito kuonesha maguvu na mabavu. Hii kwa wengi nadhani imepitwa na wakati kwa sababu vita ya sasa inahitaji teknolojia ya hali ya juu na wanajeshi wanaotumia akili zaidi kuliko mabavu.

Hatuhitaji tena mwanadamu mwenye mabavu kushinda vita bali matumizi ya technolojia ili kubaini mahali alipo adui, kumtageti na kumshambulia bila hata wewe mwenyewe kuwepo eneo la mashambulizi.

Kizazi hiki ni cha vita vya autonomous weapons hivyo sasa umefika wakati jeshi letu watuoneshe mbinu za aina hiyo na si kubeba magunia kama walivyozoea kufanya.

Namshauri Jen. Venance Mabeyo asome kitabu hiki "Army of None: Autonomous Weapons and the Future of War" cha Paul Scharre kitamsaidia kuja na mbinu mpya za kivita na kutuonesha ni namna gani wamejipanga kuzitumia.

Nawatakia siku njema.

View attachment 2079415

Mbeleni utashauri tufunge kambi za mazoezi. Maaake kwako mla chips anaweza kupigana vita akiwa na vijuice vya Mo au Azam mezani
 
Ndugu siku hizi ukiwa huwezi kubuni na kuitumia teknolojia kwenye vita wewe ni dhaifu sana, hayo mabavu wala hayakusaidii kitu. UTAPIGWA MA MISULI YAKO. NA HAKIKA NAKWAMBIA NDANI YA MIAKA 20 TU IJAYO HUTOONA WANAJESHI WAKIENDA VITANI BALI WANAKAA OFISINI LAKINI WANAFANYA MAMBO.
NA HAKIKA NAKWAMBIA NDANI YA MIAKA 20 TU IJAYO HUTOONA WANAJESHI WAKIENDA VITANI BALI WANAKAA OFISINI LAKINI WANAFANYA MAMBO.

Bongo kuna wajuaji hadi raha.
 
NA HAKIKA NAKWAMBIA NDANI YA MIAKA 20 TU IJAYO HUTOONA WANAJESHI WAKIENDA VITANI BALI WANAKAA OFISINI LAKINI WANAFANYA MAMBO.

Bongo kuna wajuaji hadi raha.
SIYO UJUAJI NDUGU NI KUSOMA NA KUFUATILIA MAMBO YANAVYOENDA DUNIANI. MBONA IKO WAZI. WEWE BADO UNATEGEMEA VITA YA MSITUNI KWA DUNIA YA LEO KWELI?
 
Back
Top Bottom