Nashauri Jen. Venance Mabeyo asome kitabu "Army of None" cha Paul Scharre ili atuondolee aibu ya kubebesha magunia makomandoo kwenye sherehe za uhuru

Ndugu siku hizi ukiwa huwezi kubuni na kuitumia teknolojia kwenye vita wewe ni dhaifu sana, hayo mabavu wala hayakusaidii kitu. UTAPIGWA MA MISULI YAKO. NA HAKIKA NAKWAMBIA NDANI YA MIAKA 20 TU IJAYO HUTOONA WANAJESHI WAKIENDA VITANI BALI WANAKAA OFISINI LAKINI WANAFANYA MAMBO.
US siku hizi wanaajiri hadi walemavu kuwa Maaskari wakati Tz kuwa na tatoo tu ni disqualification.
 
Mleta mada hajui vita
Kuna ebeo unahitaji physical presence sio teknolojia tu

Osama kuua kulitumika mbinu zote physical na technological

Kuteka hutumii teknolojia tu au kupambana na magaidi huhitaji teknolojia tu

Hata kupambana mijini na porini na kuteka mijasusi kunahitaji physical
Mleta mada yupo sahihi sana...haya mambo ya mizigo,magogo hapana.Tunataka tuone drone zao,uwezo wa kuzuia majanga,ndege za kisasa nk...what they are doing its out of business
 
Ndugu siku hizi ukiwa huwezi kubuni na kuitumia teknolojia kwenye vita wewe ni dhaifu sana, hayo mabavu wala hayakusaidii kitu. UTAPIGWA MA MISULI YAKO. NA HAKIKA NAKWAMBIA NDANI YA MIAKA 20 TU IJAYO HUTOONA WANAJESHI WAKIENDA VITANI BALI WANAKAA OFISINI LAKINI WANAFANYA MAMBO.
Ni sawa lkn labda mwisho pamoja na kupiga kwa teknolojia UTEKE ENEO LA KUFIKIRIKA sio physical area on the earth.
Vyovyote physical inahitajika
 
Yaani unajua kuliko makamanda walioko vikosini siyo?

Unajua maana ya hiyo mizigo? Ina manufaa yapi kimedani na inamjenga nini askari?
 
Na wewe nenda kasome " the art of war" by Sun Tzu.

"Pretend to be weak when ur stronger and stronger when ur weak so that u will make ur enemies to focus on the tree instead of the whole forest." Sun Tzu

Mabeyo yupo Sahihi kuliko unavyo weza kufikiri..

Huyo Paul Scharre ni kabulyage
Nanyi wote wawili mkasome:-

1. War is mainly a catalogue of blunders. ... The power of making war often prevents it, Lewis F. Korns.

2. War settles nothing, Herbert V. Prochnow.

3. Armies are not bad things in themselves; it’s war that’s evil, Dwight D. Eisenhower.

NB.
Duniani kote watu weupe wanaiheshimu Afrika pekee kwa vita aina ya guerrilla (vita vya msituni) . Hii ndiyo version ya vita iliyoleta ukombozi Afrika. US imejaribu kujifunza guerrilla lakini imewashinda, wamepoteza wapiganaji wengi kwenye mazoezi ya medani ya guerrilla. Guerrilla haihitaji teknolojia kubwa ya gharama na inahitaji mbinu kama hizo za ubebaji magunia mgongoni (uimara physically).

Aidha, Afrika haina uwezo wa kununua teknolojia hizo unazosema, labda baada ya miaka 50 ijayo, hivyo inabidi Afrika itegemee ilichonacho mkononi (guerrilla/ubebaji magunia).
 
Ningeisoma hii post nisinge comment.
Mada closed
Wangeweza kutuonesha namna drone inavyoweza kwenda kariakoo ikiongozwa na mtu aliyeko Uhuru ikachagua mtu mmoja aliyeko kwenye kundi la watu na kumshambulia walau hata kwa kumwagia maji lakini siyo kutubebeshea vifurushi vya kilo 200 wanajeshi wetu.
 
Shalom from Jerusalem,

Imekuwa ni kawaida sasa kwenye kila sherehe za uhuru wa Tanganyika ama mapinduzi ya Zanzibar jeshi letu la ulinzi la wananchi wa Tanzania kutuonesha siraha na mbinu za kivita. Miongoni mwa mbinu hizo ni makomandoo wetu kubebeshwa mizigo na magunia mazito kuonesha maguvu na mabavu. Hii kwa wengi nadhani imepitwa na wakati kwa sababu vita ya sasa inahitaji teknolojia ya hali ya juu na wanajeshi wanaotumia akili zaidi kuliko mabavu.

Hatuhitaji tena mwanadamu mwenye mabavu kushinda vita bali matumizi ya technolojia ili kubaini mahali alipo adui, kumtageti na kumshambulia bila hata wewe mwenyewe kuwepo eneo la mashambulizi.

Kizazi hiki ni cha vita vya autonomous weapons hivyo sasa umefika wakati jeshi letu watuoneshe mbinu za aina hiyo na si kubeba magunia kama walivyozoea kufanya.

Namshauri Jen. Venance Mabeyo asome kitabu hiki "Army of None: Autonomous Weapons and the Future of War" cha Paul Scharre kitamsaidia kuja na mbinu mpya za kivita na kutuonesha ni namna gani wamejipanga kuzitumia.

Nawatakia siku njema.

View attachment 2079415

Hayo ni maonesho tu
Hata nchi zilizoendelea wanafanya, haina maana ndio kinachotokea wakati wa vita
 
Nanyi wote wawili mkasome:-

1. War is mainly a catalogue of blunders. ... The power of making war often prevents it, Lewis F. Korns.

2. War settles nothing, Herbert V. Prochnow.

3. Armies are not bad things in themselves; it’s war that’s evil, Dwight D. Eisenhower.

NB.
Duniani kote watu weupe wanaiheshimu Afrika pekee kwa vita aina ya guerrilla (vita vya msituni) . Hii ndiyo version ya vita iliyoleta ukombozi Afrika. US imejaribu kujifunza guerrilla lakini imewashinda, wamepoteza wapiganaji wengi kwenye mazoezi ya medani ya guerrilla. Guerrilla haihitaji teknolojia kubwa ya gharama na inahitaji mbinu kama hizo za ubebaji magunia mgongoni (uimara physically).

Aidha, Afrika haina uwezo wa kununua teknolojia hizo unazosema, labda baada ya miaka 50 ijayo, hivyo inabidi Afrika itegemee ilichonacho mkononi (guerrilla/ubebaji magunia).
hiyo guerrilla war haina maisha marefu duniani ndugu yangu
 
Shalom from Jerusalem,

Imekuwa ni kawaida sasa kwenye kila sherehe za uhuru wa Tanganyika ama mapinduzi ya Zanzibar jeshi letu la ulinzi la wananchi wa Tanzania kutuonesha siraha na mbinu za kivita. Miongoni mwa mbinu hizo ni makomandoo wetu kubebeshwa mizigo na magunia mazito kuonesha maguvu na mabavu. Hii kwa wengi nadhani imepitwa na wakati kwa sababu vita ya sasa inahitaji teknolojia ya hali ya juu na wanajeshi wanaotumia akili zaidi kuliko mabavu.

Hatuhitaji tena mwanadamu mwenye mabavu kushinda vita bali matumizi ya technolojia ili kubaini mahali alipo adui, kumtageti na kumshambulia bila hata wewe mwenyewe kuwepo eneo la mashambulizi.

Kizazi hiki ni cha vita vya autonomous weapons hivyo sasa umefika wakati jeshi letu watuoneshe mbinu za aina hiyo na si kubeba magunia kama walivyozoea kufanya.

Namshauri Jen. Venance Mabeyo asome kitabu hiki "Army of None: Autonomous Weapons and the Future of War" cha Paul Scharre kitamsaidia kuja na mbinu mpya za kivita na kutuonesha ni namna gani wamejipanga kuzitumia.

Nawatakia siku njema.

View attachment 2079415

mwaka unaokuja kuna komando hatakuja kubeba kontena kwenye maonyesho.

Tatizo lilopo jeshi na nilishawahi kueleza mda mrefu hapa jf kuhusu swala la teknolojia na mbinu huwa zinaanzia jeshini kwanza.
ukitaka kujua jeshi ndio wakanza kuwa nateknolojia nyingi kabla ya kuanza kuingia mtaani.
anza kuangalia historia za vita na vipi viligunduliwa na kuongezwa ujuzi au kuvumbulia kama mawasiliano bila jeshi basi ingekuwa ngumu.
vifaa vya uchunguzi bila ussr na usa vita baridi tusingekuwa na setelite.

ila ningekuwa mwandishi mzuri ningeeleza vzuri na wangejifunza kwa nilicho jifunza kwa kutembea na kuona
 
Wangeweza kutuonesha namna drone inavyoweza kwenda kariakoo ikiongozwa na mtu aliyeko Uhuru ikachagua mtu mmoja aliyeko kwenye kundi la watu na kumshambulia walau hata kwa kumwagia maji lakini siyo kutubebeshea vifurushi vya kilo 200 wanajeshi wetu.
Hiyo teknolojia tunayo?
 
Back
Top Bottom