Napitia katika changamoto kubwa

Napitia katika changamoto kubwa

Madame mshukuru mungu kwa jinsi ulivyo na nilivyooona caption nitajua unashida kuuuubwa ,endelea kuomba endelea kua muaminifu kwa mungu wako,achana na huo mzigo wa mume wa mtu anakuzuia ktk baraka Zako,God time is the best time I belive hujachelewa na u shukuru unakazi jitunze
 
mimi niko silias niko bagamoyo natafuta mwanamke wa kuoa ila kama uko tayari tutafutane kwa mawasiliano 0767470332 au 0675918135 ila kama uko tayar bagamoyo niko kikazi nyumban mwanza

Sent from my TECNO M3 using JamiiForums mobile app
 
kuna 'online dating' ushajaribu hio?yaani una miaka 32 unasali novena mwaka mzima?? PM zitajaa kutokana na hii post yako..kumng'amua aliye mkweli ndio 'majaribu' utakayopitia..lol
 
Duh kumbe kuna wanawake wa disign yako aisee..!!! Ila ungekuwa near by ningekuchek ili kuyajenga
 
Acha kukosa uvumilivu. Uko desperate kiasi kwamba utafanya maamuzi ya kujuta baadae. Sometimes sio kuzaa tu sababu unataka mtoto, Endelea kumwomba Mungu.
 
mie sitaki mtoto wala sitaki ndoa nachohitaji ni kuitoa hiyo bikira tu. Maana hiyo ndio inakutia uchuro itoe utaona wanaume watakavyomiminika kutaka kukuoa
 
umeamua kumtegemea Mungu......ndio njia sahihi....Mungu hajaribiwi kwa kufunga au kusali sana......kamwe....Mungu husikiliza maombi yetu.....na hasa tukiwa wahitaji na unyenyekevu wa kweli.....kuwa makini sana dada yangu...usilazimishe mambo.....amekwambia....bisha hodi mpaka nikereke.....ntakufungulia.....bisha bidada.....bisha hodiiii tuu...Mungu yupo...
 
Mkumbushe Mungu wako kuwa ulijitunza kwa ajili ya kuingia kwenye ndoa kama alivyoamuru,kwamba sasa akupe mume aliyemkusudia,usiache kumuomba,usikate tamaa,kuzaa mradi upate watoto siliungi mkono,kumbuka muomba Mungu hachoki,nina hakika asilimia mia moja ndoa yako na aliyekuchagulia Mungu haiko mbali,nina hakika na Mungu ninayemzungumzia

Sent from my SM-G900F using JamiiForums mobile app
 
Jihusishe na makundi mazuri kama vile kwaya, vikundi vya sala kama viwawa, regio maria, nk. Huko huko wakati unasali uwe unachungulia chungulia nani anafaa kuwa mme wako. Ukiona anayefaa jiweke karibu taratibu taratibu wala husiwe na haraka kama unayoonesha hapa kwenye bandiko lako. Wewe vipi, wakatoliki wote hapo mwanza wanaotafuta wake wabichi na wacha Mungu kama wewe huwaoni hadi unakubali kubadili dini kabla hata ya kupata mpenzi mwenyewe wa kukubadilisha. Usikatie tamaa dini yako na msimamo wako. Ulichofanya ni kizuri kabisa kujiweka najifu mbele ya Mungu na kutunza (mwili) bikra yako ila sasa inaonekana umekata tamaa vibaya mno. Usijirahisishe kwa wanaume, utaharibikiwa mapema kabisa. Ebu jichanganye na vijana wa imani yako iliyokufikisha hapo utapata mme huko huko na haitakuchua muda. Dini zetu, mbali na kusali na kutufundisha mema ni sehemu sahihi ya watu kama wewe kuweka mawindo ya kupata wenza wao wa maisha.
 
Habari za Jumapili wanajamii.

Mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 32 kwa sasa. Napitia katika changamoto kubwa sana.

Hapo mwanzo kipindi ninasoma niliona si vyema kujiingiza katika mahusiano ya kufanya mapenzi kwani niliona yatanivuruga na ningejikuta napitia katika mahusiano mengi kitu ambacho sijawahi kukipanga maishani.

Nikamaliza chuo vizuri namshukuru Mungu.katika kutafuta ilikuwa ngumu kidogo nilitafuta mpaka nikakata tamaa nikaomba Mungu mpaka nikaona inatosha. Katikati ya kukata tamaa nikamuomba Mungu basi anipe kitu kimoja kwanza mme au kazi. Ila la kazi ndio nililoliwekea msisitizo kwani kwa kipindi hicho familia yangu ilikuwa inapitia changamoto nyingi kwa hiyo nikaona kazi itanisaidia kupunguza changamoto ama la basi niolewe ili nipunguze mzigo kwa familia yangu.

Siku isiyotarajiwa nikaitwa interview na nikapata kazi nzuri ambayo sikuwahi hata kufikiria wala kuiwaza. Nikashukuru Mungu na kuanza maisha mapya ya kazi na kusaidia familia yangu. Nikajikita kwenye kumuomba Mungu anijalie mme mwema atakayenifaa na kuongoza familia tutakayoipata katika misingi ya imani ta dini ya kikristo. Sikubagua kabila wala atakuwa mkirsto wa aina gani maadamu awe anaabudu jumapili maana mimi nilikuwa tiari kuhama katoliki ili tulee familia yetu tukiwa na muongozo wa dini moja.

Sikuwahi kudhani nitafikia huku maana mpaka sasa imekuwa ngumu kama ni Mungu hachelewi ama hawahi basi kwangu mimi kwa sasa imekuwa ni shida kubwa. Nimefunga novena nimesali sana mpaka naona nimeanza kuathirika na hili swala. Mwaka jana tarehe moja nikaona basi kama mme wangu hayupo nipate tu mwanamme nitakae zaa nae lakini awe mkirsto maana siko tiari kumtenga baba na mtoto wake hata kama hamhudumii, nikiamini kuwa uwezo wa kulea mwenyewe ninao hata kama watoto watakuwa zaidi ya mmoja niko tiari kupambana na maisha.

Nikaona kwa sababu nitakuwa pekeangu nikaanza kuwekeza ili watoto wangu wanikute nimejiandaa. Na penyewe Mungu akaona wakati wangu bado. Mwaka huu mwezi wa pili akatokea mme wa mtu kitu ambacho sijawahi hata fikiria kuwa kunasiku nitaangukia huko, Mwanzoni nilitaka tuzungumze mapema kabla hatujazoena sana matakwa yangu lakini akawa mtu wa kuona nampangia sheria mapema na kudai hizo mipango ninazotaka kupanga nae tukiwa hatujafika mbali ni mipango gani. Nikaona isiwe tabu.

Ikafika siku ya kukutana nikamwambia mimi sijawahi kabisa hakuamini na nikamwambia kama anajiamini aendelee ila ajue atakuwa na deni la kulipa, akatafakari akaona viatu ni vikubwa akaondoka.

Chenga zikaongezeka nikajiuliza ni nini shida, tukapanga tukutane ili tuone hatima ni nini kati yetu. Akaja na kudai yeye hayuko tiari kutoa bikira ya mtu asiye na mpango nae. nikamuelewa na nikaona yuko sahihi.Nikamuuliza wewe ulivyoanza ulitegemea mimi ni mti sina hisia za kufanya mapenzi akadai alijua anajihusisha na mapenzi ya kila mtu ana mtu wake hivyo wanakutana kulizishana tu. Akaniambia nahitaji nini hasa kwake nikamwambia kama ulishaona hisia zangu unadhani nahitaji nini? Niliona nisianze kutaja shida niliyonayo kwanza nimsikilize yeye ndio na mimi niseme ya kwangu. Yeye akadai aliona ni mahusiano ya kula na kuondoka. Akaniambia kama niko tiari ataweka sheria za kutuongoza za maandishi ili baadae tusijekupeana shida. Nikamwambia sheria zako utazoniwekea nitazifuata vilivyo japo najijua ninawivu lakini wewe ni mme wa mtu tiari nitavumilia.

Akaja na sheria na mipango mingi sana asee.sheria nyingi nilivyotafakari nikaona nyingi zinamlenga mtoto ambaye mimi ndio ninayemhitaji zaidi. na yeye akaona labda ni mmoja tu wakati mimi nishajipangia wakunitosha kabisa. Kwa maelezo yake nikaona hayuko tiari kuwa na mtoto nje ya familia na nikitokea kumpata basi nitoe mimba ama atamchukua. Nilichoka viungo vyote. Akaniuliza unalolote nikamwambia nizungumze nini wakati sheria zimekuwa ngumu.

Haki ya Mungu yaani natamani siku zirudi nyuma nizunguke na wanaume kama wafanyavyo wengine. Hukukujitunza kwangu kunanifanya nilie kila siku na kuomba Mungu usiku kucha kisa nilimtunzia mtu bikira. Jamii inayonizunguka itanitia wazimu maana swali la unaolewa lini limenichosha kabisa. Basi kama siolewi hata mtoto tu ni shida kumpata.

Kwasasa ninashida na mtoto kuliko maelezo na niendako nadhani nitawehuka. Msaada wenu tafadhalini sana.

NB. Hapo mwanzo nilifunga novena kwa muda wa mwaka mmoja na kuomba na kukabidhi mwili wangu uwe kwa ajili ya mtu mmoja tu ambaye ndio atakayekuwa mme au baba wa watoto wangu. Ndio maana inaniwia vigumu kuingia mahusiano mbalimbali.

Iyo Novena imeshakuangusha jaribu kwa Yesu....
 
Ulikosea sana kujitenga na wanaume kipindi upo unasoma..kwa miaka uliyo nayo na kwa dunia hii ya sasa ni kusali sana pasipo kukata tamaa... aidha upate mtu ambaye hana mtu au atakaye kuja kwako atakuwa ni mume wa mtu kama mwanaume wa kuzaa nae tu japo ni ngumu kupata pia ila...NI OMBI LANGU KWA MUNGU KWAKO katika kila uwombacho Mungu akitimize Mungu aliye wapa wengine hato shindwa kukupa na wewe haja ya moyo wako...MUNGU akupitishe njia salama Dada yangu amini nakwambi MUUJIZA WAKO UNAKUJA MBELENI Mungu yupo njiani kukujipu....NAKUTAKIA SIKU NJEMA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole.
Ila nikwambie kitu hakuna kitu kizuri kama subir(subra).
Vuta subra mpendwa God's timing is the best mwache Mungu atende kwa muda wake.

Sasa hivi point uliyofikia si nzuri kiwa makini maana waweza pata mwanaume akakuumiza maana waonekana unashida sana.

Endelea kumtegemea Mungu,kuwa na moyo wenye kusubiri.
Mleta mada fuata huu ushauri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaishi kwa ajili ya watu??usiombe kulea watoto mwenyewe dear..unaona ni rahisi kwa kuwa bado hujawapata.

1.unataka watoto wako waje kuishi bila baba yao kisa wti umri unaenda??tafakari.

2.unataka wasome katika mazingira magumu?

3.unaonekana unataka kuwafurahisha watu.ishi maisha yako.

4.inaonekana unafanya maombi yako kwa malalamiko.ni kama unamlaumu Mungu kwanini akupi unalolihitaji.kama unafanya hivyo acha mara moja.

5.Unataka kuolewa au kupata watoto kwa sababu marafiki uliomaliza nao chuo au unaofanya nao kazi wana watoto au wameolewa.nakusisitiza ishi maisha yako wewe hayo unayoyalazimisha yawe wakati muda wake bado,,utakuja kulia jua likiwa linawaka na usiamini.

6.usithubutu kuzaa na mume wa mtu mpendwa.kabisa usithubutu utakuja kulia machozi ya damu.bora uzae na mwanaume ambae hajaanza kuwa na familia,familia yako ndo iwe ya kwanza.

Mume wa mtu utazaa nae lkni ikifika jioni huyoooo kwa mke wake anakuacha bado unamuhitaji.atakuwa anakuona kwa kificho kwa sababu anaipenda familia yake ya kwenye ndoa.

Muda wako utafika tu usiishi kwa kufuata maishi ya watu kuwa wewe.punguza haraka.ulishawahi kujiuliza kwanini ulimuomba Mungu akupe mume na kazi lakini akaamua kukupa kazi na sio mume na vyote uliviomba kwake?????shukuru kwa kila nyakati unayopitia hutoamini majibu yatakayotoka hapo.

Naomba niishie hapa.uwe na wikend njema mpedwa.
Kuna watu mnaushauri mzuri mpaka mnakela

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom