KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,189
- 17,157
Kufikia hapa, unapiga propaganda tu hakuna lolote linalohusiana na kichwa cha mada yako; kwa hiyo tayari umekwishaififisha mada yenyewe.Nimpongeze Mhe. Rais kwa kuamua kukaa chini na kufanya kazi za ofisi ikiwemo kuhakikisha mambo nyeti yaliyokuwa yanasimamiwa na Marehemu Balozi Kijazi yanakabidhiwa kiutaratibu kwa mrithi wake.
Kuondoka ghafla kwa Mhe Kijazi si Jambo dogo kwenye utawala wa nchi, huyu alikuwa mshauri mkuu wa Rais na aliyahifadhi mengi ambayo hakuna mwingine aliyeweza kuyafahamu isipokuwa watu wawili labda na wasaidizi wao.
Basi ngoja nijibu kichwa cha mada, maanake nimechoka kupoteza muda kusoma hadi huko chini.
"Napingana na wanaosema afya ya rais si siri"
Ikiwa ni siri watu watajua kuwa huyo rais hawezi kuumwa?
Wewe umejuaje kuwa hayo uliyobuni ndiyo sababu rais haonekani hadharani!