Gerald .M Magembe
JF-Expert Member
- Jul 17, 2013
- 2,495
- 1,802
Kumbe una muono wa mbali sana hongera, Chief Secretary, Chief of Public Service, Secretary to the Cabinet, Secretary to National Security Council, Secretary to National Projects Implementation Committee and Head of all Permanent Secretaries.Nimpongeze Mhe. Rais kwa kuamua kukaa chini na kufanya kazi za ofisi ikiwemo kuhakikisha mambo nyeti yaliyokuwa yanasimamiwa na Marehemu Balozi Kijazi yanakabidhiwa kiutaratibu kwa mrithi wake.
Kuondoka ghafla kwa Mhe Kijazi si Jambo dogo kwenye utawala wa nchi, huyu alikuwa mshauri mkuu wa Rais na aliyahifadhi mengi ambayo hakuna mwingine aliyeweza kuyafahamu isipokuwa watu wawili labda na wasaidizi wao.
Kwa kiongozi anayeliwazia mema na Taifa na kiongozi aliyefanya kazi kubwa ya mageuzi kwenye utumishi na mfumo wa serikali ikiwemo kupambana na ufisadi lazima akae ayapitie majalada yote nyeti nakutoa marlekezo kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
Lakini pia ipo hoja ya kuumwa, sidhani kama kukaa ofisini ukafanya kazi zako kumekatazwa kikatiba, hakuna sehemu katiba inamtaka Rais anatakiwa aonekane mara ngapi kwa wiki, mwezi au mwaka. Hivyo kukaa kwake kimya si kinyume Cha sheria.
Tatu Rais haendeshwi kwa matakwa ya watu flani wenye maslahi yao binafsi kwamba leo watamwambia ongea akaongea na kesho wakamwambia nyamaza akanyamaza. Rais ni mkuu wa nchi na hapaswi kuendeshwa na genge flani la watu. Hawa hawa mwaka jana walivumisha habari hizihizi lakini matokeo yalionekana. Tusipende kuibaka katiba kwa kuitumia vibaya au kuitafsiri tutakavyo.
Kama yupo mwenye ushahidi kwamba anaumwa aweke wazi na hapo ndipo zitaibuka hoja za kisheria na kikatiba na serikali itawajibika kujibu.
KUENDELEA KUMTAKA RAIS AJITOKEZE AACHE KAZI ALIZOKABIDHIWA NA SERIKALI NI UTOVU WA NIDHAMU DHIDI YA TAASISI HII NYETI. HATA AKIKAA MWAKA HAKUNA SEHEMU KATIBA INAMLAZIMU AJITOKEZE KUFANYA KAZI KWENYE MEDIA.
HONGERA SERIKALI KWA KUWEZA KUDHIBITI UPEPO WA WAHUNI WA MITANDAONI
Mtumishi mwenye nguvu mmno ambae hapigiwi kura. Roho ya kiutendaji ya Serikali.
Na Mtendaji mkuu wa hiyo ofisi akiondoka ghafla bila kuwa na matayarisho ya replacement, maana yake serikali inabidi uijenge upya.
Kiutendaji ndio Rais wa Utendaji wa Nchi. Viongozi wengine anapoondoka Chief Secretary bila matayarisho ya replacement, Marais huchanganyikiwa.
MSAHAFU AU BÍBLIA YA SERIKALI KWA WAKATI HUO.
Muda utatupa majibu. Hongera kumbe tuna watu humu JF.