Napingana na wanaosema Afya ya Rais si siri

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Nimpongeze Mhe. Rais kwa kuamua kukaa chini na kufanya kazi za ofisi ikiwemo kuhakikisha mambo nyeti yaliyokuwa yanasimamiwa na Marehemu Balozi Kijazi yanakabidhiwa kiutaratibu kwa mrithi wake.

Kuondoka ghafla kwa Mhe Kijazi si Jambo dogo kwenye utawala wa nchi, huyu alikuwa mshauri mkuu wa Rais na aliyahifadhi mengi ambayo hakuna mwingine aliyeweza kuyafahamu isipokuwa watu wawili labda na wasaidizi wao.

Kwa kiongozi anayeliwazia mema na Taifa na kiongozi aliyefanya kazi kubwa ya mageuzi kwenye utumishi na mfumo wa serikali ikiwemo kupambana na ufisadi lazima akae ayapitie majalada yote nyeti nakutoa marlekezo kwa Katibu Mkuu Kiongozi.

Lakini pia ipo hoja ya kuumwa, sidhani kama kukaa ofisini ukafanya kazi zako kumekatazwa kikatiba, hakuna sehemu katiba inamtaka Rais anatakiwa aonekane mara ngapi kwa wiki, mwezi au mwaka. Hivyo kukaa kwake kimya si kinyume Cha sheria.

Tatu Rais haendeshwi kwa matakwa ya watu flani wenye maslahi yao binafsi kwamba leo watamwambia ongea akaongea na kesho wakamwambia nyamaza akanyamaza. Rais ni mkuu wa nchi na hapaswi kuendeshwa na genge flani la watu. Hawa hawa mwaka jana walivumisha habari hizihizi lakini matokeo yalionekana. Tusipende kuibaka katiba kwa kuitumia vibaya au kuitafsiri tutakavyo.

Kama yupo mwenye ushahidi kwamba anaumwa aweke wazi na hapo ndipo zitaibuka hoja za kisheria na kikatiba na serikali itawajibika kujibu.

KUENDELEA KUMTAKA RAIS AJITOKEZE AACHE KAZI ALIZOKABIDHIWA NA SERIKALI NI UTOVU WA NIDHAMU DHIDI YA TAASISI HII NYETI. HATA AKIKAA MWAKA HAKUNA SEHEMU KATIBA INAMLAZIMU AJITOKEZE KUFANYA KAZI KWENYE MEDIA.

HONGERA SERIKALI KWA KUWEZA KUDHIBITI UPEPO WA WAHUNI WA MITANDAONI
 
Ila hii sio kawaida kwa Rais wetu mpenda maendeleo sio tumjuavyo aisee....
 
Hivi kwenye ule uzushi kuhusu Dr Mpango, mbona "hawakukaa" kimya?

Sasa kama baba unazushiwa kifo, halafu hutaki wanao wakuone kabisa.....si kwamba unawapa mateso makubwa zaidi wanao na sio hao wazushi?

Kuna watu wanampenda JPM kwa dhati kabisa, wapo wanaofaidika na uwepi wake na hivyo kumpenda kwa sababu hiyo tu, na wapo wanaomchukia (kwa sababu na hata bila sababu).....lakini wote hao bado wana mashaka juu ya ukweli ama la wa uzushi huu.

Kwa faida, ya wale wanaompenda (naamini ni wengi zaidi), JPM ajitokeze wamuone na pia wawape nguvu ya kuwananga wapinzani wao "waliozusha" haya yote. Kusema tu yupo bila kuonekana kunawatesa wafuasi wake zaidi kuliko maadaui zake.
 
Nimpongeze Mhe. Rais kwa kuamua kukaa chini na kufanya kazi za ofisi ikiwemo kuhakikisha mambo nyeti yaliyokuwa yanasimamiwa na Marehemu Balozi Kijazi yanakabidhiwa kiutaratibu kwa mrithi wake.

Kuondoka ghafla kwa Mhe Kijazi si Jambo dogo kwenye utawala wa nchi, huyu alikuwa mshauri mkuu wa Rais na aliyahifadhi mengi ambayo hakuna mwingine aliyeweza kuyafahamu isipokuwa watu wawili labda na wsaidizi wao. My

Kwa kiongozi anayeliwazia mema na Taifa na kiongozi aliyefanya kazi kubwa ya mageuzi kwenye utumishi na mfumo wa serikali ikiwemo kupambana na ufisadi lazima akae ayapitie majalada yote nyeti nakutoa marlekezo kwa Katibu Mkuu Kiongozi.

Lakini pia ipo hoja ya kuumwa, sidhani kama kukaa ofisini ukafanya kazi zako kumekatazwa kikatiba, hakuna sehemu katiba inamtaka Rais anatakiwa aonekane mara ngapi kwa wiki,mwezi au mwaka. Hivyo kukaa kwake kimya si kinyume Cha sheria.

Tatu Rais aendeshwi kwa matakwa ya watu flani wenye maslahi yao binafsi kwamba leo watamwambia ongea akaongea na kesho wakamwambia nyamaza akanyamaza. Rais ni mkuu wa nchi na apaswi kuendeshwa na genge flani la watu. Hawa hawa mwaka jana walivumisha habari hizihizi lakini matokeo yalionekana. Tusipende kuibaka katiba kwa kuitumia vibaya au kuitafsiri tutakavyo.

Kama yupo mwenye ushahidi kwamba anaumwa aweke wazi na hapo ndipo zitaibuka hoja za kisheria na kikatiba na serikali itawajibika kujibu.

KUENDELEA KUMTAKA RAIS AJITOKEZE AACHE KAZI ALIZOKABIDHIWA NA SERIKALI NI UTOVU WA NIDHAMU DHIDI YA TAASISI HII NYETI. HATA AKIKAA MWAKA HAKUNA SEHEMU KATIBA INAMLAZIMU AJITOKEZE KUFANYA KAZI KWENYE MEDIA.

HONGERA SERIKALI KWA KUWEZA KUDHIBITI UPEPO WA WAHUNI WA MITANDAONI
Bi. B.Kamugisha una fikra nzuri nyingi zisizo chakachuriwa na mihemuko. Hili uliloandika ni jema. Lingine ni ile ya ushetani wa siku ya wanawake. Hongera
 
Back
Top Bottom