Anajificha vipi wakati mwaka Jana tu alikua anapiga kampeni akishirikiana na polisi kuiweka CCM madarakani?
Yule ni Msomali.
Wasomali ni watu wasiopenda kudhulumiwa japo wao wanadhulumu.
Wanasimamia sana haki zao na Mali zao .
Kuna waziri Fulani ni msomali na ni mbunge pia hua Mara nyingi alikua anaongea kwa hisia sana akivituhumu vyombo vya dola kumtishia kwa silaha.
Nadhani wangethubutu kumdhulumu yule kada wa chama wangekutana na moto wake mana anaichukia dhulma kwa kiwango cha juu sana.
Sasa hili la Mhalifu na muuaji Hamza inabidi lifanyiwe kazi kimya kimya kupitia taasisi nyingine chini ya usimamiza wa TISS ili kuondoa kashfa ya CCM kuwekwa madarakani na magaidi hasa ukizingatia wameshahusishwa na ugaidi wa kidini kwa mujibu wa Wambura katika kubambika hukumu kwa marehemu Hamza. Nadhani kuna watu wanataka kuweka raisi wao 2025 kwa chuki za kidini hili halina ubishi.
Mama anahujumiwa sana lakini kwa hisia za mbali kuna kaudini kana tengenezwa ili watu waone kuwa watu wa dini Fulani wanashabihiana na ugaidi.
Kuna mawaziri sio wazuri kwa utawala wa awamu hii. Wanashirikiana na watu ndani ya dola kuvuruga utawala wa mama.
Jambo LA msingi ni Mama kutuma vyombo vyake kimya kimya.
Kwanza kwenda TCRA kupata mzunguko mzima wa miamala na mawasiliano wa Marehemu Hamza gaidi binafsi.
Pili kuchunguza kuwa Je, ni kweli kuwa Hamza hakuwa na uwezo wowote wa kifedha hata kwenye miamala ya simu.?
Kutumia TCRA watabaini kuwa je, Hamza hakuwa na mizunguko ya fedha kwenye simu zake kibiashara au kwa jamaa zake ? Mana tumeambiwa kuwa hakuwa na uwezo wowote na alikua ni mtu wa kujificha. Sasa tubaini kuwa je, ni kweli kuwa hakuwa na fedha wala uwezo hata wa kujenga Ofisi ya Chama ya Tawi ?
Na pia Mh. Mama SSH atume watu wake wanaomheshimu na kumthamini na kuuthamini Uongozi wake na kuwa tayari kupigania kiti chake kwa manufaa ya Taifa na utaifa wafuatilie kule kwenye migondi unayosemwa kuwa ni ya kwake wakawahoji watu kuwa Hamza kwa Mara ya mwisho alifika lini kule kufuatilia masuala ya madini ?
Lakini pia Watu waaminifu na watiifu kwa Rais wafuatilie kwenye benki zisizo na riba kama Hamza aliwahi kumiliki Akaunti huko mana wasomali hua hawali Riba na riba kwao ni Haramu sana.
Jambo lingine ni kuwa silaha yake aina ya Pistol aliilipia lini kwa Mara ya mwisho !!?
Kama mama atatumia wasiri wake na kubaini kwa wazi kuwa Wambura na tume ya polisi wamedanganya au wameficha ukweli au wamechunguza kinadharia kwa lengo la kujisafisha wakati vitendo hivyo vinafanywa sana na baadhi ya askari wasio waaminifu na wanapopiga pesa wanazitumia kuhongana ili kulindana basi mama achukue hatua haraka.
Lakini pia mbona kuna Mkubwa mmoja ndani ya polisi alisikika sana akiwakemea askari wanaotumia silaha kufanya ujambazi na kudhulumu Mali za watu?
Nadhani alikua ni RPC mwanamama mahiri sijui alikua ni mkoa gani ila alikemea sana na baadae nasikia alitolewa kuwa ameliaibisha jeshi kwa kusema hadharani uovu unaofanywa na polisi.
Ni juzi tu huko Handeni polisi wametuhumiwa kushika kwa nguvu wake za watu na mabinti za watu na kuwanyanyasa kingono. Hivi mtu anaona mtoto wake wa kike au binti ake wa kike anaingiliwa kwa nguvu na mtu aliyeshika bunduki ,anakua na hasira kiasi gani endapo atafanikiwa kuipata hiyo bunduki??
Hivi mtu akilipa kisasi kwa mtu aliyebaka binti yake utaita ni ugaidi au ni kisasi tu cha mambo binafsi.
Kwa nini watu wafanye mambo yao binafsi kwa tamaa zao kwa mgongo wa dola halafu ionekane kuwa ni masuala ya kazi?
Nani anaweza akaajiriwa ili akabake wake za watu na mabinti za watu ?
Ni vizuri sasa mama akateua IGP kutoka Jeshi la wananchi. Ili imani kwa jeshi la polisi irudi.
Hata jeshi la polisi halina imani na Jeshi la polisi. Ndio maana hakuna anayependa ndugu yake apelekwe polisi. Hawana imani na anakopelekwa !! Hata IGP hana imani na Jeshi la polisi. Hawezi akaacha ndugu yake akalazwa polisi mana hapaamini.!!
Kuondoa dhana mbaya kwa Jeshi la polisi ni vema IGP akateuliwa meja Jenerali kutoka JWTZ ,wasaidizi wake watatu wawe pia ni mabrigadia jenerali wengine wawe ni Polisi na Askari magereza wawili. Hii itavunja mtandao Fulani ndani ya polisi unaojali maslahi. Uhalifu na ugaidi unatokana na askari kuwa bize kutafuta madili ya pesa na rushwa za magendo huku vibaka ,waporaji na wauza bangi wakizidi na watu kukatana mapanga na wanafunzi kubakwa vikiwa vinaongezeka.
Kuna miji yenye uhalifu sana kama Arusha miaka nenda rudi ,lakini ukichunguza utagundua kuwa kuna ushirika wa kimaslahi na baadhi ya polisi wasio waadilifu na ndio inakua fursa ya kujitafutia Mali isivyo halali. Ukiona mahali kuna uhalifu sana ndipo unapokuta baadhi ya polisi wasio waaminifu wanageuka kuwa wabia wa uhalifu na kutafuta Mali isivyo halali.
Kuvunja mtandao huu ni vizuri kule ngazi za juu pawe na IGP asiye na mawakala ndani na nje ya mfumo. Ni vema akatoka JWTZ ambaye hata wauza magendo hawajawahi kukutana naye na kufahamiana naye.
Wananchi watarudisha imani kwa Jeshi la polisi kwa manufaa ya Polisi na Taifa kwa ujumla.
Mwisho kabisa ni kuwa Mama asimuogope mtu yeyote mana katiba ndiyo inayompa mamlaka aliyonayo na sio kikundi au genge la watu. Hii nchi ni kubwa kuliko mtu yeyote. Wapo watu wengi wanaokuunga mkono na wapo tayari kulinda kiti chako mpaka mwisho.
Mtu yeyote unayedhani au kuona kuwa haendani na zama zako basi usisite kumweka pembeni kabla hajaota pembe.
Sent from my TECNO L8 Lite using
JamiiForums mobile app