Napinga kwa michezo kuingizwa kwenye siasa

we hujui siasa ni mchezo mchafu hahahaaaaa mzee wa kimkono cha kangaroo alikuwa anahutubia viti tu hahahaaaa amechoma wese la chopper bureeeeee!huyu nchemba ni nomaaa.

Teh teh teeeh lazima wewe una makengeza,kubali ukweli Nchemba zote zinatoa harufu chafu.Pua zako zikoje wewe?jitambue
 
Hivi hao watu walioacha kwenda kwenye mkutano wakaenda kuangalia mpira kuna mtu aliwalazimisha? Mbona mnaanza kuleta lawama ambazo hazina maana.

Nakumbuka siku ya siku ya mechi ya Taifa star nadhan na Morocco TBC1 walikata matangazo ya mpira wakajiunga uwanja wa ndege kwenye mapokezi ya rais wa China watu walilaumu sana kwa nini TBC1 walifanya hivyo hii inaonyesha watu wanapenda mpira kuliko siasa, leo watu wengine wameacha mambo ya siasa wameenda mpirani mnaanza kuwalaumu, kwa nini sasa sio haki yao kuchagua wanachokipenda?
 
Mimi ni Simba damdam, ila nataka Simba ifungwe mpaka ishuke daraja, upuuzi huu Rage anapeleka timu kwenda kufanya siasa? Ushenzi mkubwa huu, hakuna timu ya Simba tena hiyo ni timu ya CCM
 
mimi sioni tofauti yeyote kati ya Rage na Mwigulu wote ni majangaa tu. Mimi ni Yanga damu na kuna wakati natamani ningekuwa mwenyekiti wa Yanga ningemvua uanachama Mwigulu kwasababu simpendi halafu anashabakia timu niipendayo ya Yanga. Taabu tuupu
 
Napata mashaka kidogo. Rage amewaudhi wana Simba wote au waliokereka ni wapenzi wa Simba wanaoshabikia Chadema? Huenda hilo wanalomlaumia (kuchanganya mpira na siasa) ndilo wanalolifanya hao washabiki wa Chadema walioko Simba: kuchanganya siasa na michezo. Ikumbukwe kwamba kila mtu ana uhuru wa kwenda anakotaka madhali havunji sheria. Waliotaka mpira wakafuata mpira, waliotaka mkutano wa katiba wakaufuata. Tatizo liko wapi?
 
Tafakari kwanza Simba siyo ya wasomali.Kwanza tumuondoe Rage.mambo mengine yatafuata.hata hivyo si tunajua Simba ni ya WEapenda mabadiliko?Hakuna kijani pale!

Mkuu mimi naipenda Simba, lakini kwa upuuzi niliouona sitataka niangalie tena mechi ya simba.
Mwenyekiti wa Simba ni Mbunge na kada wa CCM.
Labda sasa vilabu vyetu viwe na mfumo wa kuwa na viongozi wasiojihusisha na vyama vya siasa.
 
Napata mashaka kidogo. Rage amewaudhi wana Simba wote au waliokereka ni wapenzi wa Simba wanaoshabikia Chadema? Huenda hilo wanalomlaumia (kuchanganya mpira na siasa) ndilo wanalolifanya hao washabiki wa Chadema walioko Simba: kuchanganya siasa na michezo. Ikumbukwe kwamba kila mtu ana uhuru wa kwenda anakotaka madhali havunji sheria. Waliotaka mpira wakafuata mpira, waliotaka mkutano wa katiba wakaufuata. Tatizo liko wapi?
Mimi mwenyewe nashangaa kwa nini wanataka kuwapangia watu ni sehemu ya kwenda, hakuna atakayekujibu swali lako hilo, badala yake wanalalamika tu Simba imewaudhi na kama walitaka mkutano wa katiba ujaze watu si wangeenda hao wanaolalamika si taarifa za mkutano walikuwa nazo kwa nini mnawalalamikia watu ambao walitaka burudani ya soka.
 
Mkuu mimi naipenda Simba, lakini kwa upuuzi niliouona sitataka niangalie tena mechi ya simba.
Mwenyekiti wa Simba ni Mbunge na kada wa CCM.
Labda sasa vilabu vyetu viwe na mfumo wa kuwa na viongozi wasiojihusisha na vyama vya siasa.
Mkuu hivi tatizo la Simba ni nini? Na hao watu walilazimishwa kwenda mpirani?
 
Tatizo la simba ni kutumiwa na vigogo wa ccm kuwanyima fursa wananchi kushiriki katika mambo ya msingi. Vigogo wa CCM wanaona watanzania bado ni wajinga............
 
Mkuu wewe unajua ratiba ya Simba ilikuwaje, je ilibadilishwa ili igongane na ratiba ya mkutano wa katiba? Na kingine ambacho hujajibu hao watu walilazimishwa kwenda mpirani? Na kama hawakulazimishwa huoni kwamba waliamua kwenda kuangalia soka ili kupunguza stress za maisha pamoja na stress wanazoletewa na wanasiasa?
 
Mimi nadhani wewe ni mgeni na maisha ya vijijini. ndiyo maana unazungumzia habari ya stress. Kama unaipenda simba nakushauri uwaambie wasijihusishe na siasa watakuja kupoteza mashabiki. Uwe unaangalia mbali, ila kama uwezo wako wa kuona kimawazo ni sawa na urefu wa pua shauri yako......
 
Mkuu badala ya kujibu nilichokuuliza unakimbilia kunitukana, sawa tutabakia kushabikia Simba sisi wenye kuona sawa na urefu wa pua zetu.
 
Simba kwa heri sikutaki tena.kwanza team yenyewe pressure tu tunashabikia kigumu halafu unalainishwa na shabik wa yanga akubebe?kwa nn haikuchukuliwa yanga.we rageee mbulula kweli
 
Mkuu Crashwise upo wapi?
Nimekusoma mkuu Mchwechwele ila kwa hili nawasamehe bure waliohusika kama itajitokeza tena nitafanya maamzi magumu kwanini nimefanya hivyo Mwigulu aliuzwa kwanini umefanya hivyo kasema mwaka juzi aliwaleta polisi, mwaka jana Mtibwa na mwaka huu Simaba hivyo kilichotokea ni bahati mbaya tu na haikuwa makusudi tofauti kabisa na alicho kiongea JF jana, hivyo inawezekana hata viongozi wa simba hawakujua lengo la Mwigulu kuwaita siku hiyo, nakumbuka pia Mwigulu kama unavyo jua ni mhuni tu aliwahi kwendakwa mgombea wetu wa udiwani akapiga picha kisha kuileta hapa akisema mgombea huyo amehamia CCM lakini kufatilia ilikuwa ni habari tofauti kabisa, kuwa alimfata akimwambia ametumwa na kikwete aachane na Udiwani atapewa U-DC...
 
Last edited by a moderator:
Mimi mwenyewe nashangaa kwa nini wanataka kuwapangia watu ni sehemu ya kwenda, hakuna atakayekujibu swali lako hilo, badala yake wanalalamika tu Simba imewaudhi na kama walitaka mkutano wa katiba ujaze watu si wangeenda hao wanaolalamika si taarifa za mkutano walikuwa nazo kwa nini mnawalalamikia watu ambao walitaka burudani ya soka.
Masuke ukiliangalia swala hili namna lilivyopangiliwa hakika ilipangwa mkutano wa chadema/katiba ukose watu kwanini kwanza ulipangwa ufunguzi wa za vijiji vyote sikumbuki idadi yake mfano vijiji 100 zidi sha mara 22 kila timu unapata 2200 hao ni wachezaji tu bado viongozi wa timu husika halafu ujumlishe na uwepo wa timu kama simba ambayo sikumbuki kama ilisha wahi kucheza kijijini hapo halafu kiingilio bure nini unategemea? swala hapa ni je simba walijua kilichokuwa kinaendelea? je ratiba ya simba ilikuwaje...kingine cha kuzingatia mechi ya simba ni saa 11.00 jioni..na mkutano wa chadema ulikuwa saa nane na watu walijitokeza kwa wingi tu kinachoendelea ni siasa tu....
 
Hivi hao watu walioacha kwenda kwenye mkutano wakaenda kuangalia mpira kuna mtu aliwalazimisha? Mbona mnaanza kuleta lawama ambazo hazina maana.

Nakumbuka siku ya siku ya mechi ya Taifa star nadhan na Morocco TBC1 walikata matangazo ya mpira wakajiunga uwanja wa ndege kwenye mapokezi ya rais wa China watu walilaumu sana kwa nini TBC1 walifanya hivyo hii inaonyesha watu wanapenda mpira kuliko siasa, leo watu wengine wameacha mambo ya siasa wameenda mpirani mnaanza kuwalaumu, kwa nini sasa sio haki yao kuchagua wanachokipenda?
Ule ulikuwa zaidi ya mkutano wa siasa, ulikuwa ni mkutano wa katiba ambayo kimsingi inachangia hata soka letu kudoda...
 
Ndugu zangu wanajamvi,naomba nijitokeze kwenu kwa kuwaombeni tuungane kwa pamoja kupinga michezo kuhusishwa na mambo ya kisiasa.
Kwanza kabisa naomba niweke wazi mimi ni shabaki mkubwa wa simba.
Kwakitendo walicho kifanya mwenyekiti wetu bwana rage," kwa kuishusha thamani simba,kwenda kujipima ama kujifua dhidi ya timu ya kijiji yenye mkusanyiko wa wachezaji wanaotoka iramba ni kuikosea timu heshma pamoja na wachezaji waliocheza siku iyo pjamoja na mimi kama shabiki umenikosea na kutushusha thamani.
Binafsi nahisi kunahujuma imefanyika dhidi ya simba kwa manufaa ya kisiasa.
Binafsi nafahamu ndugu mwigulu yeye ni yanga damu. Sasa kwanini mwenyekiti wetu wa simba akubali kuingizwa mkenge kwa kubali kuishusha thamani timu kisa kuifanikisha malengo flani ya kisiasa!
Naombeni wanachama wenzangu tumpinge mwenyekiti wetu kwa kuishusha thamani timu yetu. Ikiwezekana kumfukuze kabisa kwenye chama kwa kuingiza siasa kwenye timu yetu,kwa kutotekeleza mambo aliyoahidi kipindi anaomba uenyekiti kama ifuatavyo
alituhaidi atajujengea uwanja matokeo yake juzi akapinga kama si yeye aliyekwisha wai kutuhaidi ataujenga kwa kipindi ambacho tutamchagua pia alituahidi angetulete mfadhili toka nje kwa ajili ya kuisaidia timu na kutujengea uwanja. Lakini mtokeo yake tumeyaona.
Rage anapaswa kuondolewa.

Jamani tafadhali sana tena sana. Mpira ubakie mpira na siasa zibakie kuwa siasa. Huko mnakotaka kutupeleka siko. Ndani ya Yanga na Simba, wamo CCM, CDM, CUF nk. Lakini kwenye timu zao ni kitu kimoja. Ndani ya Yanga na Simba wamo Waislamu, Wakristo nk lakini kwenye timu zao ni kitu kimoja. Ndani ya Yanga na Simba kuna makabila yote zaidi ya 120 Tanzania. Mpira ubakie kuwa mpira na hayo mengine yafuate mkondo, sehemu na wakati wake. Viongozi wa Yanga na Simba msikubali kutumiwa na wanasiasa. Kila mwana siasa ana timu yake. Uongozi kaupata si kwa sababu ya timu, dini au kabila lake. Tusilazimishe kuchanganya mafuta na maji sijui tutpata kitu gani. Mpira ubakie kuwa mpira. I have spoken!
 
Ndugu zangu wanajamvi,naomba nijitokeze kwenu kwa kuwaombeni tuungane kwa pamoja kupinga michezo kuhusishwa na mambo ya kisiasa.
Kwanza kabisa naomba niweke wazi mimi ni shabaki mkubwa wa simba.
Kwakitendo walicho kifanya mwenyekiti wetu bwana rage," kwa kuishusha thamani simba,kwenda kujipima ama kujifua dhidi ya timu ya kijiji yenye mkusanyiko wa wachezaji wanaotoka iramba ni kuikosea timu heshma pamoja na wachezaji waliocheza siku iyo pjamoja na mimi kama shabiki umenikosea na kutushusha thamani.
Binafsi nahisi kunahujuma imefanyika dhidi ya simba kwa manufaa ya kisiasa.
Binafsi nafahamu ndugu mwigulu yeye ni yanga damu. Sasa kwanini mwenyekiti wetu wa simba akubali kuingizwa mkenge kwa kubali kuishusha thamani timu kisa kuifanikisha malengo flani ya kisiasa!
Naombeni wanachama wenzangu tumpinge mwenyekiti wetu kwa kuishusha thamani timu yetu. Ikiwezekana kumfukuze kabisa kwenye chama kwa kuingiza siasa kwenye timu yetu,kwa kutotekeleza mambo aliyoahidi kipindi anaomba uenyekiti kama ifuatavyo
alituhaidi atajujengea uwanja matokeo yake juzi akapinga kama si yeye aliyekwisha wai kutuhaidi ataujenga kwa kipindi ambacho tutamchagua pia alituahidi angetulete mfadhili toka nje kwa ajili ya kuisaidia timu na kutujengea uwanja. Lakini mtokeo yake tumeyaona.
Rage anapaswa kuondolewa.

Mkuu, Wanasimba mtaacha kutoridhika hadi lini? Maharage mbona katimiza ahadi zake! 1). Uwanja wa Simba Arena pale Bunju umekamilika (Ili uuone, pitia Gamboshi) na TFF wameuidhinisha kutumika katika michezo ya Ligi Kuu huku Azam TV ikiwa na kibweta chake cha kuonesha mechi zote kutoka uwanjani hapo. 2) Mfadhili kapatikana kwa mkono wa Maharage, huyu si mwingine bali ni Malkia wa Nyuki. Jamani Maharage awafanyie nini zaidi watani zangu?
 
Back
Top Bottom