Napewa talaka mie unlucky

sasa si amesema mpaka mwanao wa miezi mi nne afke miezi 10 ndo akupe talaka!sasa katka miez hyo cta muoneshe mahaba ya dhat na wala ucogope kum-bemenda mwanao...mwnyw atabdl maamuz
 
pole unlucky. hiari yashinda utumwa. utashangaa kujikuta unakuwa na furaha baada ya kuachana nae. sikumbuki kama unafanya kazi,lakini kama hufanyi kazi hebu kwanza tafuta kazi yoyote halali hata kama kipato ni kidogo.kazi itakuweka bize na kukuondolea mawazo,itakufanya kuwa na mtazamo mpya kuhusu maisha yako na itakupa ulinzi wa kiuchumi. hawezi kukunyang'anya mtoto wa miezi kumi. nenda tume ya haki za binadamu (ofisi nyuma ya chuo cha ustawi wa jamii ama kinondoni njia ya kutokea mwananyamala hosp), watakusaidia pia pamoja na tawlae ama tgnp.hawezi kukudhulumu chochote. achana na habari ya kumtoa mjini,unahitaji awepo ili aendelee kukupa challenge na akuone utakavyofanikiwa na kunawiri baada ya kutoka kwenye mateso yako. kila la kheri japo uko unlucky
 
Aisee pole sana!
Nafikiri umeshapata ushauri wa wapi uende; usisahau copies za RB, vyeti vya daktari na ushahidi mwingine! Tena waweza dai talaka wewe mwenyewe na yeye akapaswa kufuata masharti ya talaka, mf watoto wakae na nani etc; sidhani kama utakubali huyo unayemuita dancer wa club kukulelea watoto!
 
Pole unlucky, na majina mengine haya huwa mabaya sana , embu funga ID hii hili jina linakuchulia, kuna dada mmoja aliitwa taabu na aliteseka maisha yake yooote katika simulizi zake,kwa ulivosimulia hapo hakuna mapenzi hata kidogo, naona hakuna haja ya kung'ang'ania saaana, kuna maisha mazuri zaidi ya hayo, usitolee macho mali ambazo zinakutesa kisaikolojia, japo pia unaweza pigania ukapata haki yako kiasi, nina imani una kibalua chochote, jiweke bize sana jichanganye na marafiki mu ignore huyo jamaa kw muda
 
Pole sana,Usiwaze sana kuna hiyo miezi ya kumsubiri mtoto akue lolote linaweza kutokea ya Mungu ni mengi.Alafu mie nadhani anakutishia tu kama amefikia uamuzi wa kukupa talaka angetoa sasa.
Hata akija kukupa talaka utaweza tu kuishi bila yeye mtegemee sana Mungu na yote yatawezekana na unaweza kubarikiwa kuliko hapo ulipo sasa,nimeshaona wanawake wengi waliofukuzwa wakiwa hawana kitu lakini baadae Mungu aliwabariki na waliweza kulea na kuwasomesha vizuri sana watoto wao.
 
una bahati umejua hayo na una miezi ya kujiandaa kisaikolojia

BTW, hana uwezo wa kumchukua mtoto kwani sheria za nchi zipo wazi, mtoto huyo ni wako hadi afike at least 7 years na kuwe na ushahidi kwamba wewe huwezi kumtunza

SIMAMA IMARA PIGANIA MWANAO... HAYO YA YEYE KWNDA SHUKURU MUNGU, ATAWAUNGANISHA TU KAMA MISHKAKI NDANI YA NYUMBA
 
sasa si amesema mpaka mwanao wa miezi mi nne afke miezi 10 ndo akupe talaka!sasa katka miez hyo cta muoneshe mahaba ya dhat na wala ucogope kum-bemenda mwanao...mwnyw atabdl maamuz

Hapo nadhani unamshauri dada yetu awe 'mtumwa' sasa!
 
Maneno yanaumba. Badili jina lako kwanza. Unlucky? what a name? The only refuge iko kwa Mungu. Zoma Zaburi 23 na kisha usimamie hapo hapo na Mungu wetu asiyeshindwa kitu atakupitisha ktk bonde la uvuli wa mauti. Tena He will set the table before your enemies. Amen?
 
habari zenu wapendwa nadhani mlisoma story yangu yote na mume wangu haya sasa imefikia siku tena huyu bwana kanitafutia sababu eti hawezi kuishi na mimi kisa alinipiga wakati na mimba miezi nane nikaenda polisi lakini hakutiwa mbaroni leo ananitolea sababu hiyo kama umenivunja moyo sina mapenzi tena na wewe kisa hiyo sababu ya kwenda polisi watoto anataka kuwachukua anasubiri mtoto wangu wa miezi minne awe miezi 10 ndo anipe hiyo talaka,sasa jana binamu yake kaniambia kama huyu bwana anataka kuoa ndo mana wewe anakutafutia sababu dah roho inaniuma sana nimeteseka miaka sita hamna mapenzi nimechuma nae alikuwa maskini leo katajirika sasa anaenda kumuoa malaya anaedance clubs jamani naomba mnishauri niende wapi serekalini anipe jasho langu na hawa watoto pia nipate mimi na pia nataka huyu mtu atolewe kabisa hapa dar asiishi tena yani nimkomoe haswa kanitesa sana nimehangaika sana nae mpaka leo ana uwezo naomba mnisaidie dada judith upo
Pole sana shosti, huyo mwanamme sie kabisa na wala hastahili penzi lako,usipende usipopendwa kama anakuona wewe huna haki ya kula mali mlio chuma pamoja basi mwenyezi mungu atakulipia chamsingi nikuchukua watoto wako mali hutafutwa usikae kwenye mateso kisa mlichuma wote,
mwisho atakuletea maradhi.kumuamisha mji sio hakutokupa changamoto yakutafuta jiamini kua utaweza na nimini utafaulu,usikubali akakufanya mtumwa, nashindwa kuelewa why wanaume wengine wanakua na tabia mbaya yakupiga wanawake mwanamke hapigwa kwa ngumi na wala mateke anapigwa kwa ulimi. usijali dada yatakwisha na utasahau kua na moyo jasiri...
 
Wewe dada mshukuru sana mungu wako kwa kuwa anakuepusha na mengi japo wewe unaona kama ni bahati mbaya, i wish ningekuwa wewe, hakuna kitu kizuri kama kujua mtu hakupendi, mamii no matter umezaa watoto wangapi na yeye life goes on and we only live once kwa hiyo utilize vizuri hii opportunity ya maisha na kumbuka furaha yako ndio kitu muhimu kwa sasa, KATU USITHUBUTU KUFANYA VITU EXTRA ETI ILI KUMFANYA ASTAY, ALWAYS BE YOU. kikubwa mfute kadri uwezavyo katika akili yako anza moja, tafuta marafiki toka nao, toka na wanao hao ndio furaha yako. halafu jaribu pia kuwa unapata muda wa kutoka mwenyewe kwenda outting sehemu decent na huko jaribu kumake new friends ongea nao mambo tofauti ya maisha yani ukifanya hivi ndani ya miezi mitatu maisha yako yatabadilika completely na hautaamini. kikubwa look urself kwenye mirror and say this woman is sooo beatiful to be stressed, nenda saloon look beatiful and try as much as you can to love urself than anyone else. put in place plans from now ukiachana nae utaenda kuishi wapi, na kuhusu watoto asikutishe utaenda nao wewe until they are 14, mali mtagawana nusu kwa nusu, be ready for the devorce asikutishe hawa wanaume hawana lolote la kututisha kama mapenzi yameisha huna haja ya kukaa nae move on. WANAWAKE WANAWEZA. tena ndio utashangaa utapata mwanaume atakayekupenda mpaka utajiuliza ulikuwa unachelewa nini kutoka kwa hiyo ndoa.
 
Pole mwanadada, kwanza kabisa ingia kwenye maombi - I mean serious maombi nina imani Mungu atakupa jibu.
 
Suluhisho pekee ni MAOMBI kwa MUNGU.

Sheria inaweza kukurudisha kwake lakini ikawa imekosea

sheria inaweza kukutenganisha naye pia ikawa imekosea

lakini MAOMBI yenye IMANI chanya kwa MUNGU unayemtumaini kamwe hayakosei na mwisho wake uamuzi wowote utakaochukua wewe aua atakaochukua huyo mumoe utakuwa unakupa amani maisha yako yote na hutopungukiwa na kitu kamwe

USHAURI: Kwa wale ambao hawajaoa au kuolewa wajitahidi sana kumuomba MUNGU awape wake na waume bora kwakuwa ndoa yaweza kuwa mahali patakatifu kwako aua kuwa mahali pa huzuni kwako.
 
pole sana dada yangu kwa hayo matatizo.mimi nakushauri uchukue uamuzi wa kutoendelea kuishi naye kwakuwa huyo mtu sasa hivi hana mapenzi nawe tena na kama unavyojua huwezi lazimisha upendo.
jambo la msingi dai taraka na usiwe na huruma wala aibu yjuu yake mburuze mahakamani unaweza omba msaada kwenye chama cha kutetea haki za wanawake ili upate msaada wa kisheria ili taraka yako iambatane na ugawaji wa mali mlizo chuma mkiwa pamoja.
usikubari uondoke mikono mitupu ukahangaike kwa kuwa ashakutumia huyo kakuzalisha basi hunabudi mkiachana nawe upate pa kuanzia. nina imani mali ikishagawanywa ukapata haki yako kama huna kazi kile utakachopata waweza kukitumia kama mtaji ukatengeneza maisha mazuri kuliko kuendelea kuvumilia maisha ya utumwa na mateso kisa ndoa na watoto.
suala la watoto walioko chini ya umri wa miaka 7 lazma ukaish nao wewe na wale walioko juu ya umri huo basi itapangwa utaratibu wa kuwaona.
mimi nadhani ukifanya hivyo itakuwa bora zaidi na utaweza wasaidia wanao kwa kuwa kama ana mpango wa kuoa huwezi juamwanamke atakaye muoa atakuwa wa namna gani inawezekana akawa mwanamke ambaye huko mbeleni atakuja wanyanyasa wanao na kama wewe huna msingi wakateseka sana.
 
Mwanamke mwenye uwezo wa kuingia huku JF na kuchangia michango kupewa talaka si kuonewa lazima utakuwa umeshindikana. Wa kuonewa huruma ni wale wamama wa nyumbani wasiojua hili wala lile zaidi ya kuhudumia familia yake siku 365 bila kuchoka
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom