Napewa talaka mie unlucky

Pole sana Unlucky ila pls allow me nikuite Lucky,sababu umeshajua adui unayepambana naye anatumia silaha za namna gani,kama unapenda uendelee na ndoa yako liko tumaini nipm nikupe mistari na shuhuda za kwenye bible haitakuacha,na mumeo hajui ni kiasi gani anataka kujiharibia future yake kwa kwenda kuoa mtu mwingine Neno la Mungu linasema USIMTENDEE KWA HIYANA MKE WA UJANA WAKO,PIA - NINYI WAUME WAPENDENI WAKE ZENU MSIWE NA UCHUNGU NAO.Stay blessed

Wewe hiyo miezi ya maandalizi sijui ya kumsubiri mwanao akue ndo ifanyie kazi, kama unajua hati ya nyumba ilipo (kama mna nyumba) ichukue kafiche kokote unakijua, na jipange hata siku akitoka kazini akute ushaleta fuso na kumwachia nyumba nyeupe. Kaanze upya for the sake of your kids..wala usiogope. Ni maamuzi magumu lakini inabidi kuyafanya ili kutunza utu wako kama mwanamke na pia kwa ajili ya watoto wako, yeye hana cha kupoteza. pm for more information kama uko tayari kufanya maamuzi magumu. Its time wanawake tuache kulalamika na kujisimamia maana hapo ndoa yako ilipofikia haina cha kuomba Mungu wala kuvumilia, You need to live for your kids maana atakuja kukuua na wanao wakabaki hawana mzazi maana yeye akishaoa tena ndo kwisha habari yao. pole.

Wanawake ambao wanafikiria zaidi mambo ya kisheria kuolewa kwao kulivutwa na "material things" na hivyo anataka kugawia utajiri wa mumewe. Mimi nilifikiri kama kweli ulipenda kuolewa bila kusukumwa na kitu chochote linapotokea tatizo kwenye ndoa shauri litapelekwa kwa msimamizi wa ndoa, baadaye kwa wazazi. Huwezi kufikiria maswala ya kisheria wakati bado mnaishi nyumba moja.

sasa akionewa asitafte msaada wa sheria kisa atasemwa. haiwezekani mtu ageuke mtumwa kisa mfume dume.

Pole sana Unlucky ila pls allow me nikuite Lucky,sababu umeshajua adui unayepambana naye anatumia silaha za namna gani,kama unapenda uendelee na ndoa yako liko tumaini nipm nikupe mistari na shuhuda za kwenye bible haitakuacha,na mumeo hajui ni kiasi gani anataka kujiharibia future yake kwa kwenda kuoa mtu mwingine Neno la Mungu linasema USIMTENDEE KWA HIYANA MKE WA UJANA WAKO,PIA - NINYI WAUME WAPENDENI WAKE ZENU MSIWE NA UCHUNGU NAO.Stay blessed

mkuu mabandiko ya HOLLY BIBLE hayana talaka, huyu ni muislam ndo maana kwao kuna sheria ya talaka, bilashaka umpatie mistari ya kisheria zaidi. ila maneno mazuri haya kama atayafanyia kazi.

asanteni na hili jina nilijipa mda sana wakati yote yalinitokea nimevumilia mengi mpaka malaya zake wamnitukana lakini bado nimestahamili yote mpaka leo hii sina chochote kaniweka ndani tu ananipa hizo hela kidogo tu za mimi kununua vitu vyangu kama sabuni n.k pamoja na pampers za watoto mpaka leo hii sina akiba yoyote naomba mniambie hiyo talwa iko sehemu gani na je watanisaidia siyo kunizungusha ne je hawatataka pesa,huyu bwana ana pesa sana je nikifight nae na akaja kuwapa rushwa hao watu si watanigeuzia kibao ? Halafu huyu bwana ni foregner anaishi kwa permit hapa je nikienda imgration office itakuwa sawa?na talaka nataka nipate je niende wapi?

pole kwa matatizo yote yaliyojitokeza na hongera kwa kuweza kuvumilia
suala la talaka kabla ya kufika mahakamani inatakiwa ipitie sehemu 2 hadi 3 na sehemu zote hizo kuwepo na maandishi na mwafaka au kutokuwa na mwafaka
1. anzia serikali za mitaa (si lazima sana )
2. ustawi wa jamii baada ya hapa wataipeleka
3. baraza la usuluhishi wa ndoa then
4. mahakamani (ni vyema ukatumia mahakama ya wilaya ili uweze kuweka wakili wa kukusimamia sheria)
katika ufunguzi wa kesi hakikisha unaorodhesha asset mlizochuma kwa ajili ya mgao na kama kuna vitu vya kutoa kopi toa na hata picha ya vitu mbali mbali

Wewe hiyo miezi ya maandalizi sijui ya kumsubiri mwanao akue ndo ifanyie kazi, kama unajua hati ya nyumba ilipo (kama mna nyumba) ichukue kafiche kokote unakijua, na jipange hata siku akitoka kazini akute ushaleta fuso na kumwachia nyumba nyeupe. Kaanze upya for the sake of your kids..wala usiogope. Ni maamuzi magumu lakini inabidi kuyafanya ili kutunza utu wako kama mwanamke na pia kwa ajili ya watoto wako, yeye hana cha kupoteza. pm for more information kama uko tayari kufanya maamuzi magumu. Its time wanawake tuache kulalamika na kujisimamia maana hapo ndoa yako ilipofikia haina cha kuomba Mungu wala kuvumilia, You need to live for your kids maana atakuja kukuua na wanao wakabaki hawana mzazi maana yeye akishaoa tena ndo kwisha habari yao. pole.

Hili la kubeba vyombo mmmhh unataka akamshitaki ameiba?wewe ondoka na nguo zako Mungu si athumani Bwana,kama wewe ni mwenye haki Hakika hautakaa Huaibike.Mungu atajua jinsi ya kukusitiri

huna sababu ya kubeba vyombo wala kuondoka nyumbani anza taratibu za kisheria ... ni pm nikupe contact za mwanasheria kwa taarifa zaidi

jamani hata hizo nguo nimeshaambiwa nikikutoa hapa unaacha kila kitu mpaka chupi coz yote kabuy yeye siyo changu niondoke mtupu,hata mimi naona nisonge mbele wala nisihangaike uko kote ya nini yote mungu atanilipia mie nafikiria watoto niwachukue kimya niondoke coz mtu kama huyu ukishindana nae nita taabika sana dah

je huna akiba uliyojiwekea ???

habari zenu wapendwa nadhani mlisoma story yangu yote na mume wangu haya sasa imefikia siku tena huyu bwana kanitafutia sababu eti hawezi kuishi na mimi kisa alinipiga wakati na mimba miezi nane nikaenda polisi lakini hakutiwa mbaroni leo ananitolea sababu hiyo kama umenivunja moyo sina mapenzi tena na wewe kisa hiyo sababu ya kwenda polisi watoto anataka kuwachukua anasubiri mtoto wangu wa miezi minne awe miezi 10 ndo anipe hiyo talaka,sasa jana binamu yake kaniambia kama huyu bwana anataka kuoa ndo mana wewe anakutafutia sababu dah roho inaniuma sana nimeteseka miaka sita hamna mapenzi nimechuma nae alikuwa maskini leo katajirika sasa anaenda kumuoa malaya anaedance clubs jamani naomba mnishauri niende wapi serekalini anipe jasho langu na hawa watoto pia nipate mimi na pia nataka huyu mtu atolewe kabisa hapa dar asiishi tena yani nimkomoe haswa kanitesa sana nimehangaika sana nae mpaka leo ana uwezo naomba mnisaidie dada judith upo

Hilo jina la "UNLUCKY" ndio linalokuletea mikosi yote hiyo, japi najua sio jila lako halisi lakini kwa kuwa ndilo unalotumia humu, basi ndio jina linalokutambulisha.......... kwanza badili hilo jina na kisha mtazamio wako juu ya ndoa yako.
Pili, ni vyema ukaangalia usalama wako zaidi kuliko mali,..... hivi mali na usalama wako ni kipi chenye umuhimu, sasa uking'ang'ania kisha akakuua, hasara itakuwa ni ya nani? kama alikupiga ukiwa na ujauzito wa miezi nane, atashindwaje kukuua, mtu wa aina hii?
Niliwahi kuweka uzi hapa nikieleza namna ya kumpiga kibuti mume mkorofi, kama ulipata bahati ya kusoma uzi huo, basi akili ipo kichwani mwako.

Dada zangu mi nashindwa kuelewa mnachokuwa mkifikiri,
ndoa ni jambo la kushare raha na tabu,
zaidi kwa sasa kila mtu anapaswa kujituma ktk kazi za ujenzi wa taifa haya mambo ya mapenzi ni matokeo tu kama utampata anayekupenda sawa usipompata basi ipo sku lakin cku zote angalia kazi kwanza,
sasa wewe mtu kama unaona anakunyanyasa we upo tu ntafikir ukiondoka utakufa,
we kama hakutaki basi angalia maisha yako basi,zaid ukiendelea kulazimisha kuishi maisha ya majonzi ntafikiri umelazimishwa ni chukizo hat kwa bwana ,
pia we miaka yote hiyo unavumilia nini hali una nafac moja ya kuishi tu,

Mwanamke mwenye uwezo wa kuingia huku JF na kuchangia michango kupewa talaka si kuonewa lazima utakuwa umeshindikana. Wa kuonewa huruma ni wale wamama wa nyumbani wasiojua hili wala lile zaidi ya kuhudumia familia yake siku 365 bila kuchoka

huo ni mtazamo wake wewe mwanahizaya sema amen...

Come on, MOVE ON.
The man has no respect for you and your kids either. In the end he will fu#k-up your kids emotionally. This is mental abuse and you are better off without him. Stand for your right Sister, and God bless you.

sasa akionewa asitafte msaada wa sheria kisa atasemwa. haiwezekani mtu ageuke mtumwa kisa mfume dume.

Majibu yako yanawakilisha ulivyo. Utaendelea kuwa na boy friend maisha yako yote kama hutaki kutii maandiko "enyi wake Watiini waume zenu"

Ndachuwa.

Tangu mwanzo niliposoma post ya kwanza hadi ya tano nimegundua huyu Unlucky ndiye mwenye matatizo tena makubwa kuliko tunavyofikiri yamkini tunampa pole kwasababu hatujapata story upande wa pili.

Unlucky anadai alipigwa alipokuwa na mimba ya miezi minne lakini hajatuambia sababu za kupigwa zaidi ya kujitetea Bwana hakutiwa ndani na polisi hataki kutuambia kwanini polisi walikataa kumweka ndani mumewe.Napata hisia polisi waliona Unlucky ni mkorofi,mjinga kashindwa kumtii mumewe na nk.

Unlucky anadai Mumewe anataka malaya wa Club ?.Nakuuliza angetaka kuoa Nesi,Mwalimu au mwanamke mwingine mwenyekazi ya heshima ungeridhia ?.Again Unlucky nina kila sababu ya kukuita mkorofi na mdhalilisha wa mwanamke mwenzio unachoangalia ni mali alizochuma mumeo.Sheria ipo itakulinda utapata mgao wake lakini punguza makeke mpe mapenzi mumeo miezi mitatu au minne si michache unaweza kurejesha moyo wa upendo kwa mumeo kama utaacha makeke.

Mwanamke mwenye uwezo wa kuingia huku JF na kuchangia michango kupewa talaka si kuonewa lazima utakuwa umeshindikana. Wa kuonewa huruma ni wale wamama wa nyumbani wasiojua hili wala lile zaidi ya kuhudumia familia yake siku 365 bila kuchoka

pole kwa matatizo yote yaliyojitokeza na hongera kwa kuweza kuvumilia
suala la talaka kabla ya kufika mahakamani inatakiwa ipitie sehemu 2 hadi 3 na sehemu zote hizo kuwepo na maandishi na mwafaka au kutokuwa na mwafaka
1. anzia serikali za mitaa (si lazima sana )
2. ustawi wa jamii baada ya hapa wataipeleka
3. baraza la usuluhishi wa ndoa then
4. mahakamani (ni vyema ukatumia mahakama ya wilaya ili uweze kuweka wakili wa kukusimamia sheria)
katika ufunguzi wa kesi hakikisha unaorodhesha asset mlizochuma kwa ajili ya mgao na kama kuna vitu vya kutoa kopi toa na hata picha ya vitu mbali mbali
Mimi haya mambo ya sheria nilikuwa siyaelewi, nahisi umepewa ushauri mzuri.
Kitu ambacho ninsingekushauri, ni kukaa unapakata miguu na "kusubiri Mungu akuhukumie".
Changamka, chakarika, vinjari kutetea haki zako. Mungu yupo kwa nyinyi nyote, sio wewe unasubiri Mungu wakati mwenzako anakumaliza kiafya na kiakili (kwa kisago na vitisho).

Nimekumbuka kisa cha jamaa ambaye kuna mwizi alikuwa anamwibia mara kwa mara. Majirani wakamshauri amwachie Mungu atamlipia. Baada ya miaka 5 kupita bila kuona malipo ya Mungu, siku moja akaamua kumvizia mwizi wake, akampiga na kumjeruhi vibaya. Majirani walipomwuliza kwa nini aliamua vile akajibu aliona Mungu anachelewa na mwizi alikuwa anaendelea kuiba. Huyu jamaa kama angesubiri hukumu ya Mungu, pengine angesubiri na kulipwa ahera.

Cha kufanya dada, usisubiri mpakaakupeleke kaburini. Ya Mungu mwachie Mungu lakini yaliyoko katika uwezo wako yafanye mwenyewe, SASA, LEO KABLA YA KESHO:

Ndachuwa.

Tangu mwanzo niliposoma post ya kwanza hadi ya tano nimegundua huyu Unlucky ndiye mwenye matatizo tena makubwa kuliko tunavyofikiri yamkini tunampa pole kwasababu hatujapata story upande wa pili.

Unlucky anadai alipigwa alipokuwa na mimba ya miezi minne lakini hajatuambia sababu za kupigwa zaidi ya kujitetea Bwana hakutiwa ndani na polisi hataki kutuambia kwanini polisi walikataa kumweka ndani mumewe.Napata hisia polisi waliona Unlucky ni mkorofi,mjinga kashindwa kumtii mumewe na nk.
Mkuu, unataka kusema mwanamume ana haki ya kumpiga mke wake? Hivi tunaishi katika karne gani?
Hata kama Unlucky ana makosa na ukorofi, mume hana haki ya kumpiga, hana haki.

Similar Discussions

Back
Top Bottom