Napenda kuishi sehemu yenye mji mdogo ila sio jiji kubwa au bush

We ni wale mnaopenda kujulikana na wengi, yaan unataka ukae sehem upatawale, uwajue watu wakujue.

Kwa wale busy na mambo yao hawawezi kuchagua size ya mji, yeye atajiangalia yeye anaishije na anafanya nini kwenye huo mji. Wengine siyo kazi yake. No kujuana juana kufuatiliana fuatiliana..
 
Napenda ishi mji mkubwa wowote wenye huduma muhimu ila sio mjini

niwe nnje ya mji kabisa kule ambapo Tanesco hawafikirii hata kupeleka umeme hivi karibuni

Solar Panel zitambae juu ya Bati za kutosha na Heavy duty Generator langu standby likiwa tyr pale

Uwanja usipungue 1heka Mbwa wasipungue 20 usiku,yani hizi ndoto kufika 2025 Hazijatmia itabd nihamie CUF.
 
Unajua kitu ambacho nimejua baada ya kuja hapa nilipo sasa hivi? Kuna nyoka wengi, milio ya ndege mpaka usiku ila nyoka.

Mara ya kwanza bafuni. Koboko.

Mara ya pili tunacheza drafti pembeni nyoka anapita.

Mara ya tatu nipo kwenye bodaboda ghafla akakatiza.

Mara ya nne nipo na wazee hivi tunaongea nyoka wa kijani akawa anapanda mti.

Mara ya tano kwenye bwawa tunalochota maji.

So pendeni kuishi hizi sehemu ila jiandaeni.
 
Yani hata nikiendaga Dar basi nakaa siku 3 tu, siku ya kwanza nafika, ya pili nafanya kilichonipeleka, ya tatu ndukii, kasoro labda kama kuna uhitaji wa kukaa zaidi.

Napenda kuishi miji midogo tu, Kwa sasa nnependa niishi hata Singida
True bro, nimekuliza Dar, nimesoma huko mpaka elimu ya chuo.Ila acheni bwana toka nilipokuja huku wilayani sijajuta kabisaaaa!!!.
 
Hiizi ni ndoto zangu baada ya kustaafu nikae kijijini sehemu isiyo kuwa na kelele za magari wala piki piki nifuge na kulima
 
Haupo peke yako mkuu! Mimi napenda kuishi sehemu ambayo nimezungukwa na mimea zaidi, tulivu ili mradi kuwe na umeme na internet na mahitaji mengineyo muhimu.

Sipendi kuishi kwenye makelele na msongamano, sijawahi kutamani kuishi miji mikubwa hasa dar, sipapendi mno japo nipo dar, siku nikifanya mizunguko ile mikelele na misongamano, naishia kuchoka akili na kuumwa kichwa.
 
Napenda ishi mji mkubwa wowote wenye huduma muhimu ila sio mjini

niwe nnje ya mji kabisa kule ambapo Tanesco hawafikirii hata kupeleka umeme hivi karibuni

Solar Panel zitambae juu ya Bati za kutosha na Heavy duty Generator langu standby likiwa tyr pale

Uwanja usipungue 1heka Mbwa wasipungue 20 usiku,yani hizi ndoto kufika 2025 Hazijatmia itabd nihamie CUF.
Mbwa wote hao wewe ni mhehe!?
 
Y
Yani hata nikiendaga Dar basi nakaa siku 3 tu, siku ya kwanza nafika, ya pili nafanya kilichonipeleka, ya tatu ndukii, kasoro labda kama kuna uhitaji wa kukaa zaidi.

Napenda kuishi miji midogo tu, Kwa sasa nnependa niishi hata Singida

ani hata nikiendaga Dar basi nakaa siku 3 tu, siku ya kwanza nafika, ya pili nafanya kilichonipeleka, ya tatu ndukii, kasoro labda kama kuna uhitaji wa kukaa zaidi.

Napenda kuishi miji midogo tu, Kwa sasa nnependa niishi hata Singida
Mi nilifikiri ni mshamba hivi, nimejenga Mwanza lakini nimeamua kuhamia katoro tena pembeni kabisa, hii inategemea na interest za shughuli za kiuchumi, napenda ufugaji sana, napenda biashara za mazao ya kilimo. Kama umetengeneza miundo mbinu huko unaisha bila shida, hutapata presha wala kisukali. Unaweka solar yako kubwa, trecter, unachimba borehole na unaweka irrigation system, haki ya Mungu we Dar kaa tu huko..
 
Nilikuwa na mawazo kama yako kipindi naishi katikati ya jiji,nikahamishiwa mji mmoja hivi kikazi aiseee,nashukuru Mungu nisharudi zangu mjini maisha yanaendelea na nimeapa nitakaa maisha yangu yote kwenye miji mikubwa tu!!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom