Bongolander
JF-Expert Member
- Jul 10, 2007
- 5,067
- 2,220
Nyote ongeeni siku 11 zijazo zitajulikana mbivu na mbichi.
Zimefika siku hizo ulizosema, hakuna lolote linalotokea na litakalotokea. Still ni kufanyana wajinga, kujivua gamba ni sawa na kusema iba iba iba halafu sema nimeacha wizi, huchukuliwi hatua zozote. Huu ni uswahili pia, ni kuwazuga watu.
Nape Nnauye can be as loud as he wants, lakini atakuwa NAPE kama kweli ataproduce results ambazo Tanzania inazitaka. Sio kuwavua magamba na kuwaonesha rangi zao, wafikishwe mahakamani waadhibiwe na kurudisha pesa walizotuibia.
nadhani imefika wakati wa vyama kufanya tathmini ya mambo waliyopanga kutekeleza na si yawe kwenye maandishi na midomo ya viongozi wa chama hiki bila ya utekelezaji wowote kwani watanzania wamechoka maneno matupu
Mkuu kama wewe ni mtanzania unaweza kufahamu wazi kuwa wanasiasa waliowengi wakisema hili hawamaanishi wanalolisema, so kujivua gamba ni kuwageresha tu wananchi. hakuna kitakachofanyika na kitakachobadilika.
Poor analysis. Nani hajui kwamba wengi wa wabunge wa CCM walikuwa-sponsored na Lowassa? Kushangiliwa hakumaanishi chochote zaidi ya wajibu wa wapambe kwa master wao. Mwisho wa yote maamuzi ya chama hayachukuliwi bungeni, ni kwenye vikao vya chama ambavyo tayari vimeshaamua kwamba yeye na wenzake wapotee. Wewe unashangaa yeye kutawala bunge, mbona alipomuondoa Sitta na kujigawia kamati za bunge wote tulijua kwamba vikaragosi wale walikuwa wake? In this contest, losser ni Lowassa na yeye anajua na ndiyo maana anahangaika hata kufikia kufanya outsourcing ya nguvu za giza kutoka Nigeria. Maji ya shingo!
NImeipenda hii. EL hana chake ndani ya CCM. KUna wabunge tena wengi walikuwa sponsored wakati wa kugombea ubunge kila mmoja sh. milioni tano. Sasa kazi wanayo. Watapiga makofi weeee lakini yataishia mjengoni.
Je nini matokeo ya mnyukano kati ya LOWASSA na NAPE katika chama cha magamba? je nani anaelekea kukimbizwa kwenye chama
Nadhani huu wakati mwafaka kwa NAPE kujiondoa katika chama cha CCM na kujichimbia kaburi,sijui ni nani alimdaganya apambane na CAPITALIST LOWASSA NA WENZAKE WAWILI,kwa tukio la jana LOWASSA kushangiliwa kwa nguvu wakati akichangia hotuba ya waziri mkuu ilionyesha ni jinsi gani mtandao wake ulivyo nanguvu ndani ya wabunge wa CCM na ndiyo ule usemi wa kuwa asilimia 90% ya wabunge wa CCM Anawamiliki yeye jana ulidhihirisha kwa uma,NAPE anawakati mngumu sana.
Chapa kazi Nape kamwe usiruri nyuma, kujiondoa kwenye chama ni dalili ya uoga endelea kuimarisha chama
Nionavyo mimi kutokana na analysis yake ni kuwa chama kimeshika hatamu hivyo maamuzi ya NEC yakiwa kinyume cha matakwa ya EL atakuwa amemalizika kisiasa ndani ya sisem labda atafute route mpya tha's NEC ina mamlaka ya kumvua mpaka uanachama .natambua wewe ni mtu makini ila nashangaa kusema lowassa analitawala BUNGE na wabunge wa CCM ndio wengi huoni kama mtu anauwezo wa kulitawala bunge anaweza kufanya lolote. au mkuu hutambui umuhimu wa bunge? je unatambua kuwa wabunge wengi wako ndani ya NEC?
Nionavyo mimi kutokana na analysis yake ni kuwa chama kimeshika hatamu hivyo maamuzi ya NEC yakiwa kinyume cha matakwa ya EL atakuwa amemalizika kisiasa ndani ya sisem labda atafute route mpya tha's NEC ina mamlaka ya kumvua mpaka uanachama .
NEC haina uwezo wa kumvua uanachama na chombo chenye uwezo wa kumvua uanachama ni CC(halmashauri kuu ya chama)
daima hakuna asiyejua nguvu za lowassa ndani ya NEC na ata mwenyekiti wa chama analitambua hili kwasababu NEC ni kundi kubla linatokana na wanamtandao ambao cordinator wake ni lowassa na kabla ya hapo lowassa alikuwa na nguvu kubwa kushinda mtu yeyote kwenye CC na NEC , ndio maana wakakurupuka kuvunja CC ili kupunguza nguvu za lowassa lakini kwa kadri siku zinavyoenda ndio washindani wake wanapungua nguvu na wote wanaendelea kulalamika majukwaani wakati wengine wanajipanga kwa 2015
muda ni mfupi na hakuna muda wa kupoteza kusikiliza polojo za mwenyekiti(JK) na katibu mwenezi(NAPE),
sasa ni mwendo mdundo kuelekea 2015
Nape jaribio dogo tu la mafuta serikali ya chama chako inalia .
je lowassa akianza si ndio mtakufa kabisa
Wanahitaji Anointing water toka kwa TB Joshua!